Monday, March 7, 2016

CITY KUTENGA PAUNDI MILIONI 80 KWA AJILI YA LAPORTE NA STONES.

KLABU ya Manchester City inadaiwa kuwa tayari kutumia zaidi ya paundi milioni 80 kwa ajili ya Aymeric Laporte na John Stones katika harakati zao za kujenga kikosi chao chini ya Pep Guardiola. Laporte ambaye ni beki wa Athletic Bilbao anathaminishwa kwa kitita cha paundi milioni 40, wakati Everton wao walikataa ofa ya paundi milioni 38 waliyotoa Chelsea kiangazi mwaka jana kwa ajili ya kumuwania Stones. Inadaiwa kuwa Guardiola anataka kujenga upya safu yake ya ushambuliaji pindi atakapotua City haswa kutokana na tatizo la majeruhi kuzidi kwa nahodha wa timu hiyo Vincent Kompany. Laporte pia amekuwa akizivutia Barcelona na Real Madrid katika miezi ya karibuni, wakati kuna hatihati ya Everton kutokubali kumuuza Stones kirahisi.

No comments:

Post a Comment