MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amewaonya mashabiki wa timu hiyo kuwa matukio ya kuzomea wanayofanya wakiwa jukwaani yanaathiri kwa kiasi fulani hali ya wachezaji kujiamini katika mbio zao za ubingwa. Arsenal wamezidi kuachwa kwa pengo la alama nane dhidi ya vinara Leicester City na sasa timu hiyo haitakiwi kupoteza mechi nyingine huku kukiwa kumebaki michezo tisa ya Ligi Kuu. Akihojiwa Wenger amesema mashabiki wana mchango mkubwa haswa timu inapokuwa nyumbani lakini mashabiki wakianza kuzwazoemea wachezaji ile hali kujiamini inapotoea na kujikuta wakifanya makosa yasiyo ya lazima. Meneja huyo aliendelea kwa kuwapongeza wachezaji wake kwa kujitahidi kukabiliana na hali hiyo na kuwaomba mashabiki nao kuendelea kuwaunga mkono.
No comments:
Post a Comment