NGULI wa soka wa Arsenal, Ian Wright amesema inamuumiza kuona Arsene Wenger akiwa chini ya shinikizo kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo. Wenger amekuwa akizidi kukosolewa na baadhi ya mashabiki wenye hasira kutokana na kiwango duni cha timu hiyo huku wengine wakibeba mabango ya kumtaka kuondoka baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 19. Arsenal kwasasa wako katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu huku wakitolewa katika michuano ya Kombe la FA jana. Akihojiwa Wright amesema hajisikii vyema kuona jinsi Wenger anavyotendewa kwasababu alicheza chini yake na ana muheshimu kwa kiasi kikubwa.
No comments:
Post a Comment