KLABU ya Manchester City imepata ahueni kufuatia taarifa za kiungo wake Yaya Toure kuanza mazoezi kuelekea katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Dynamo Kiev kesho. Toure alifunga bao la mwisho katika ushindi wa mabao 3-1 waliopata dhidi ya klabu hiyo ya Ukraine mwezi uliopita lakini alikosa mechi mbili za Ligi Kuu dhidi ya Liverpool na Norwich City kutokana na matatizo ya kisigino. Kukosekana kwake kunaonekana kuleta pengo kwenye timu hiyo baada ya kufungwa mabao 3-0 katika mchezo dhidi ya Liverpool huku wakitoa sare ya bila kufungana katika mchezo dhidi ya Norwich. Baada ya kucheza mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya City watawakaribisha mahasimu wao jiji Manchester United katika Uwanja wa Etihad Jumapili ijayo.
No comments:
Post a Comment