KLABU ya Manchester City imefanikiwa kumsajili winga chipukizi wa Brazil Gabriel Jesus kutoka klabu ya Palmeiras kwa ada ya paundi milioni 27. Jesus mwenye umri wa miaka 19 amekubali mkataba wa miaka mitano lakini ataendelea kubakia Palmeiras mpaka msimu wa soka wa Brazil utakapomalizika Desemba mwaka huu. Chipukizi huyo ambaye pia alikuwa akiwindwa na Barcelona, alipigiwa kura ya kuwa mchezaji bora anayechipukia nchini Brazil msimu uliopita na yupo katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kinachoshiriki michuano ya Olimpiki. Jesus amefunga mabao 26 katika mechi 67 za kikosi cha alizocheza akiwa na Palmeiras na ndio anaongoza kwa ufungaji katika Ligi Kuu ya nchi hiyo kwasasa. City chini ya meneja mpya Pep Guardiola sasa wanakuwa wametumia kiasi cha paundi milioni 100 katika kipindi hiki cha kiangazi kwa kusajili wachezaji sita ambapo mbali na Jesus tayari wameshwasajili Leroy Sane, Ilkay Gundogan, Nolito, Oleksandr Zinchenko na Aaron Mooy.
No comments:
Post a Comment