ROBERTO Martinez amefurahi kuteuliwa kama kocha mpya wa timu ya taifa ya Ubelgiji lakini ameonya ni lazima wabadilike kama wanataka kushinda chochote. Ubelgiji walikuwa wakipewa nafasi kubwa katika michuano ya Ulaya mwaka huu lakini waliondolewa katika hatua ya robo fainali kwa kuondolewa na Wales. Kutokana na kufanya vibaya katika michuano hiyo waliamua kuachana na kocha Marc Wilmots na badala yake sasa wamemteua Martinez. Akihojiwa mara baad ya uteuzi huo, Martinez amesema ni heshima kubwa amepewa lakini kuna kazi kubwa ya kufanya pamoja na nchi hiyo kuwa na kikosi kizuri. Martinez aliendelea kudai kuwa nchi hiyo imejaaliwa vipaji lakini maandalizi ni muhimu hivyo anatarajia kukutana na kila mchezaji ili kuzungumza nao na kuwakumbusha majukumu yao kwa taifa. Kibarua cha kwanza cha Martinez akiwa kocha wa nchi hiyo utakuwa ni mchezo dhidi ya Hispania Septemba mosi mwaka huu jijini Brussels.
No comments:
Post a Comment