Monday, September 5, 2016

GRIEZMANN ADAI ATAONDOKA ATLETICO PINDI SIMEONE AKIONDOKA.

MSHAMBULIAJI Atletico Madrid, Antoine Griezmann amedai kuwa amejitoa kuitumikia klabu hiyo chini ya meneja wake Diego Simeone pamoja na taarifa zilizozagaa kuwa Manchester United imepania kumsajili kiangazi mwakani. Taarifa kutoka nchini Uingereza zimedai kuwa mshambuliaji huyo nyota wa kimataifa wa Ufaransa anatarajiwa kuwa chaguo namba moja la United mwaka 2017. Hata hivyo, Griezmann ambaye amesaini mkataba mpya Juni ambao utamuweka Atletico mpaka waka 2021, amesema ataondoka Atletico kama Simeone ataondoka. Kabla ya kusaini mkataba mpya mapema kiangazi hiki, Griezmann alizungumza na Simeone ili kufahamu mipango yake ya baadae.

No comments:

Post a Comment