Monday, September 5, 2016

WAKALA WA YAYA TOURE AMJIA JUU GUARDIOLA.

WAKALA wa Yaya Toure, Dimitri Seluk amedai kuwa meneja wa Manchester City Pep Guardiola amemdhalilisha mteja wake kwa kumuacha katika kikosi chake kitakachoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Toure mwenye umri wa miaka 33, hataruhusiwa kuichezea City katika hatua ya makundi ya michuano hiyo kwasababu Guardiola amelazimika kuacha baadhi ya wachezaji wanaotoka nje ya bara la Ulaya kama sheria za Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA linavyotaka. Akihojiwa kuhusiana na hilo, Seluk amesema kama City wakishinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu atasafiri kwenda Uingereza na kutangaza mbele ya wanahabari kuwa Guardiola ndio meneja bora duniani. Wakala huyo aliendelea kudai kuwa lakini kama City hawatashinda taji la michuano hiyo basi anadhani Guardiola atakuwa na ujasiri wa kukiri kumdhalilisha mchezaji mkubwa kama Yaya Toure. Seluk amesema huo ni uamuzi wa Guardiola na wanauheshimu na mteja wake ana taaluma ya kutosha na kazi yake hivyo atafanya kila anachoambiwa.

No comments:

Post a Comment