Monday, July 2, 2012
INIESTA MCHEZAJI BORA EURO 2012.
KIUNGO wa kimataifa wa Hispania, Andres Iniesta ambaye ameisaidia timu yake hiyo kunyakuwa taji la pili mfululizo la michuano ya Ulaya iliyofanyika nchini Poland na Ukraine ametajwa kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo. Iniesta ambaye alitoa msaada mkubwa kwa timu yake ya Hispania katika nafasi ya katikati na kupelekea kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa ya kwanza kutetea taji lake kwenye michuano hiyo. Ofisa Mkuu wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Andy Roxburgh amesema kuwa kuna wachezaji wengi kama Andrea Pirlo wa Italia Xavi ambaye alishinda tuzo hiyo mwaka uliopita na Xabi Alonso walionyesha viwango vizuri katika michuano hiyo. Lakini Iniesta alionyesha uwezo wa hali ya juu zaidi ya wenzake hao kutokana na kuwa mbunifu, kasi na uwezo binafsi pale timu yake inapokuwa katika wakati mgumu. UEFA pia iliteua timu ya nyota wa Ulaya ambayo itaundwa na wachezaji kutoka nchi mbalimbali zilizoshiriki michuano hiyo ambao ni makipa: Gianluigi Buffon-Italia, Iker Casillas-Hispania, Manuel Neuer-Ujerumani, mabeki: Gerard Pique-Spain, Fabio Coentrao-Ureno, Philipp Lahm-Germany, Pepe-Ureno, Sergio Ramos-Hispania, Jordi Alba-Hispania. Wengine ni viungo Daniele De Rossi-Italia, Steven Gerrard-Uingereza, Xavi-Hispania, Andres Iniesta-Hispania, Sami Khedira-Ujerumani, Sergio Busquets-Hispania, Mesut Ozil-Ujerumani, Andrea Pirlo-Italia, Xabi Alonso-Hispania wakati washambuliaji ni Mario Balotelli-Italia, Cesc Fabregas-Hispania, Cristiano Ronaldo-Ureno, Zlatan Ibrahimovoic-Sweden, David Silva-Hispania.
MTANANGE WA AL AHLY NA MAZEMBE KUPIGWA BILA YA MASHABIKI.
WIZARA ya Mambo ya Ndani nchini Misri imeamuru timu ya Al Ahly kucheza bila ya mashabiki katika mchezo wao wa Ligi ya Klabu Bingwa barani Afrika dhidi ya timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Al Ahly itakuwa mwenyeji wa Mazembe katika mchezo wa kwanza katika hatua ya makundi ya michuano hiyo ambao utafanyika Julai 8 mwaka huu. Mkurugenzi wa Michezo wa Al Ahly, Mahmoud Alaam alithibisha klabu hiyo kupokea taarifa rasmi kutoka wizarani jana ikiwahitaji kucheza mchezo huo bila uwepo wa mashabiki wake. Wachezaji wengi wa Al Ahly walikuwa wakitegemea mashabiki wao kuwashangilia katika mchezo huo lakini hilo halitawezekana baada ya mameneja wa Uwanja wa Kijeshi ambao utatumika kwa ajili ya mchezo huo kukataa kwa sababu za kuisalama. Mwanzoni TP Mazembe waliliandikia barua Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF kutaka mchezo huo uchezwe nje ya nchi hiyo kwasababu za kiusalama.
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.
PONGEZI KWA RAIS MPYA WA ZFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linampongeza Amani Ibrahim Makungu kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) katika uchaguzi uliofanyika juzi (Juni 30 mwaka huu) kwenye hoteli ya Bwawani, mjini Zanzibar. Ushindi wa asilimia 94 alioupata Makungu ambaye hakuwa na mpinzani katika uchaguzi huo mdogo unaonesha imani ambayo wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ZFA wanayo kwake katika kukiongoza chama hicho. Ni matarajio ya TFF kuwa ushindi huo utatafsiriwa kwa vitendo na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ZFA na wadau wa mpira wa miguu Zanzibar kwa kumpa Makungu ushirikiano wa asilimia 100 ili kuhakikisha Kamati yake ya utendaji inafanya kile kinachotarajiwa na wengi. Makungu si mgeni katika mpira wa miguu, na mchango aliotoa kwa mchezo huo visiwani kabla ya kuwania nafasi hiyo unatambuliwa na kila anayefuatilia maendeleo ya mpira wa miguu katika Zanzibar. TFF tunaahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa ZFA chini ya Makungu kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Ali Ferej Tamim ili kuhakikisha ustawi wa mpira wa miguu visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
MISRI YAAHIRISHA MECHI DHIDI YA NGORONGORO HEROES
Mechi mbili za kirafiki kati ya timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) na Misri zilizokuwa zichezwe mwezi huu zimefutwa. Chama cha Mpira wa Miguu Misri (EFA) kimetuma taarifa jana (Julai 1 mwaka huu) kikiomba kusogezwa mbele hadi mwishoni mwa Agosti baada ya kushindwa kupata usafiri wa ndege kuwahi tarehe ambazo ilikubaliana na TFF kwa ajili ya mechi hizo. Ngorongoro Heroes ambayo tayari iko kambini ilikuwa icheze mechi hizo Julai 3 na 5 mwaka huu jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi kabla ya kuikabili Nigeria katika mechi ya michuano ya Afrika, Julai 29 mwaka huu. Mechi nyingine za kirafiki kwa Ngorongoro Heroes inayofundishwa na Jakob Michelsen zitachezwa Julai 14 na 16 mwaka huu dhidi ya Rwanda.
RUVUMA YAIFANYIA MAUAJI LINDI 7-2
Timu ya Ruvuma imethibitisha kuwa mwiba mkali katika michuano ya Copa Coca-Cola mwaka huu baada ya leo asubuhi (Julai 2 mwaka huu) kuishushia Lindi kipigo cha mabao 7-2. Hadi mapumziko kwenye mechi hiyo ya kundi A iliyochezwa Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani, washindi ambao kwa matokeo hayo wamejiweka katika nafasi nzuri ya kucheza 16 bora walikuwa mbele kwa mabao 3-0. Waliotikisa nyavu ni Anthony Christian dakika ya 23 na 50, Edward Songo dakika ya 27, 75 na 86 na Sunday Leonard dakika ya 32 na 60. Mabao ya Lindi yalifungwa na Salum Mnyamwile dakika ya 18 kwa njia ya penalti na lingine dakika ya 48 kupitia kwa Mwarami Maundu. Nayo Tanga imepata ushindi wake wa kwanza katika michuano hiyo baada ya kuifunga Manyara mabao 2-0 katika mechi ya kundi B iliyochezwa Uwanja wa Tamco mkoani Pwani. Mabao ya washindi yalifungwa na Mbwana Musa dakika ya 47 na Issa Mwanga dakika ya 60. Katika mechi tatu zilizotangulia Tanga ilitoka sare ya mabao 3-3 na Morogoro, ikapata sare nyingine ya 1-1 dhidi ya Mwanza, na baadaye 1-1 na Tanga. Kagera imeendelea kujitutumua katika michuano hiyo baada ya kupata ushindi wake wa pili katika kundi D kwa kuilaza Kusini Unguja bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe jijini Dar es Salaam. Bao lake lilifungwa dakika ya 76 na Novati Sebastian. Mechi iliyopita Kagera iliifunga Tabora mabao 2-0 baada ya kuteleza katika mechi mbili za kwanza kwa kufungwa na Kilimanjaro na Singida. Mechi nyingine ilichezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam ambapo Kinondoni iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mara.
UONGOZI TWIGA STARS WATOA TAMKO
Uongozi wa Twiga Stars umekana kuwepo vitendo vyovyote vya kinyume na maadili kwa wachezaji wa timu hiyo ambayo hivi karibuni ilitolewa kwenye mechi za mchujo za michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC). Wakizungumza na waandishi wa habari leo (Julai 2 mwaka huu), Meneja wa Twiga Stars, Furaha Francis na aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa wamesema hakuna vitendo vya aina hiyo. Mkwasa amesema alikaririwa vibaya kuhusu suala hilo wakati akiwa kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha Star Tv kutokana na swali alilokuwa ameulizwa kuhusiana na vitendo hivyo. “Ukifuatilia mahojiano yangu na Star Tv mimi sikusema kuwa kuna vitendo hivyo. Tatizo nadhani lilianzia kwa magazeti yaliyonukuu kupitia Star Tv, na wala kujiuzulu kwangu hakukuhusiana na hilo, nimewajibika kama kocha kutokana na kutolewa na Ethiopia,” amesema Mkwasa. Naye Furaha Francis amesisitiza kuwa hakuna vitu vya aina hiyo katika timu hiyo, na kama kuna mtu ana ushahidi na hilo ni bora akauonesha badala ya kuzungumzia uvumi kuliko ukweli. “Ukweli ni kwamba si sisi na wachezaji tu ambao hatukufurahishwa kutolewa na Ethiopia, wapo Watanzania wengi ambao hawakufurahishwa na matokeo yale. Twiga Stars si timu ya kudumu, haikai na wachezaji kwa muda wote, kila mchezaji ana timu yake. “Madai yanayoenezwa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu vitendo hivyo yametuchafua sana. Tunaomba kama kuna mtu ana ushahidi na hilo atueleze kuliko kuendelea kutuchafua,” amesema.

TORRES ANYAKUWA KIATU CHA DHAHABU EURO 2012.
BOLT ACHEMSHA TENA MBELE YA BLAKE.
MWANARIADHA nyota wa Jamaica Usain Bolt ameshindwa kutamba tena mbele ya mwanariadha mwenzake Yohan Blake baada ya kushika nafasi ya pili katika mbio za mita 200 ambazo ni mahsusi kwa ajili ya maandalizi ya michuano Olimpiki. Bolt ambaye anashikilia rekodi ya dunia kwa kukimbia kwa kasi zaidi, hiyo ni mara ya pili kushindwa mbele ya Blake ndani ya saa 48. Blake alimshinda Bolt katika mbio za mita 100 zilizofanyika Ijumaa na kufanya hivyo tena katika mbio za mita 200 ambazo alimaliza akitumia muda wa sekunde 19.80 wakitofautiana kwa sekunde 0.03. Akihojiwa mara baada ya mbio hizo Bolt amesema kuwa kushindwa kwake katika mbio hizo ni changamoto ya kuona wapi ambapo alikosea na kufanyia kazi eneo hilo tayari kwajili ya michuano ya Olimpiki itakayoanza kutimua vumbi Julai 27 mwaka huu jijini London, Uingereza. Naye kocha wa Bolt, Glen Mills amesema ana imani na mwanariadha wake huyo kwamba atarejea katika kiwango chake kutokana na uzoefu alionao kabla ya kuanza kwa michuano ya olimpiki.
Sunday, July 1, 2012
SHEHATA AMKINGIA KIFUA BRADLEY.
| Hassan Shehata. |
KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya Misri, Hassan Shehata amesema pamoja na kusikitishwa kwa kusindwa kufuzu kwa kikosi hicho katika michuao ya Mataifa ya Afrika mwakani lakini suala hilo lilitegemewa kutokea. Shehata amesema kuwa kinachotakiwa sasa hivi timu hiyo ni kujipanga na kuangalia changamoto zinazowakabili huko mbele ili kuhakikisha wanarudisha heshima yao kama mabingwa soka Afrika. Kocha huyo aliendelea kusema kuwa Misri imeshinda mataji matatu ya Afrika mfululizo hivyo ni kawaida kushika kiwango lakini anaomba wazinduke mapema ili kurejea makali yao kama zamani. Shehata pia alimkingia kifua kocha wa timu hiyo Bob Bradley na kusema kuwa amesaidia kujenga kikosi kizuri na wanatakiwa waendelee kumpa ushirikiano kwani anafanya vizuri katika michezo ya kufuzu Kombe la Dunia ambapo anaamini ataweza kukipeleka kikosi hicho nchini Brazil mwaka 2014. Hata hivyo taarifa kutoka kwa msemaji wa Chama cha Soka cha nchi hiyo-EFA, Azmey Megahed amesema kuwa kutakuwa na kikao cha bodi ili kujadili mustakabali wa Bradley.
Subscribe to:
Posts (Atom)