Wednesday, February 29, 2012

England Vs Holland 2-3 - All Goals & Match Highlights - February 29 2012...

Germany Vs France 1-2 - All Goals & Match Highlights - February 29 2012 ...

Switzerland Vs Argentina 1-3 - All Goals & Match Highlights - February 2...

Brazil Vs Bosnia 2-1 - All Goals & Match Highlights - February 28 2012 -...

CORINTHIANS YAMNYAKUA NYOTA KUTOKA CHINA.

KLABU ya Corinthians ya Brazil imemsajili kiungo wa kimataifa kutoka China Chen Zhizhao wakiamini kuwa mchezaji huyo atawasaidia kuwatangaza katika nchi hiyo ya bara la Asia. Chen ameshawahikucheza katika klabu ya nchini kwao ya Nanchang Hengyuan na pia kabla ya kwenda Corinthians alikuwa nchini Ureno akikipiga katika klabu ya Trofense. Wazo la kumyakuwa mchezaji huyo lilitoka idara ya masoko ya klabu hiyo ambapo wanajaribu kuifanya klabu hiyo kujulikana zaidi nje ya nchi hiyo. Idara hiyo ya masoko ya klabu hiyo pia ndio iliyotoa wazo la kumsajili Ronaldo de Lima miaka michache iliyopita wakati nyota huyo wa zamani wa Brazil alipokuwa akiuguza majeraha ya mguu wakati akiicheza klabu ya Ac Milan ya Italia.

BARCA YALIPWA FIDIA.

KITUO kimoja cha radio nchini Hispania kimeondoa tangazo ambalo lilitumika mwaka jana likidai kuwa wachezaji wa Barcelona wanatumia madawa haramu yaliyopigwa marufuku michezoni na kukubali kulipa kiasi cha euro laki mbili kama fidia. Katika taarifa ya kituo hicho waliyoweka katika mtandao wake Jumanne imesema kuwa tuhuma hizo ambazo zilitoka Machi mwaka jana zimeonyesha kuwa hazina ukweli wowote kuhusu wachezaji hao kutumia madawa hayo. Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa kituo hicho kimegundua kuwa kitendo walichofanya ni kinyume na sheria na wamelichafua jina klabu hiyo kwa namna moja au nyingine na kwa hilo wanaomba radhi. Tuhuma hizo ambazo klabu ya Barcelona ilikanusha na kutaka ziondolewe zilileta mkanganyiko baada ya vyombo vya habari nchini humo kudai kuwa aliyetoa taarifa hizo ni mmoja wa maofisa wa mahasimu wakubwa wa klabu hiyo klabu ya Real Madrid ambaye hajajulikana

Tuesday, February 28, 2012

VAN DER VAART AACHWA KIKOSI CHA UHOLANZI.

KIUNGO wa kimataifa wa Uholanzi Rafael van der Vaart ameondolewa katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo ambacho kitacheza na Uingereza katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki Jumatano. Chama cha Soka nchini humo-KNVB kimesema katika taarifa yake kuwa kuingo huyo anayekipiga katika klabu ya Tottenham Hotspurs aliumia kifundo cha mguu mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akishuhudia kikosi chake kikipokea kipigo kutoka kwa mahasimu wao Arsenal chwa mabao 5-2. Mchezo baina ya timu hizo unatarajiwa kuchezwa nchini Uingereza katika Uwanja Wembley jijini London. Van der Vaart anakuwa mchezaji wa pili wa Uholanzi kuondolea katika kikosi hicho baada ya mlinda mlango wa kikosi hicho Michel Vorm nae kuondolewa kutoka kuugua.

PETR CECH MCHEZAJI BORA WA MWAKA NCHINI KWAO.

MILINDA mlango mkongwe wa kimataifa wa kutoka Jamhuri ya Czech Petr Cech ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa nchi hiyo na kufikia rekodi ya kushinda tuzo hiyo kwa mara ya tano. Cech ambaye ana umri wa miaka 29 ameichezea timu ya taifa ya nchi hiyo mara 88 akiwa kama mlinda mlango wa kutegemewa na amekuwa na mafanikio makubwa katika klabu yake ya Chelsea anayochezea. Mchezaji ambaye amewahi kushinda tuzo hiyo mwaka 2005, 2008, 2009, 2010 na sasa 2012 alifanikiwa kushinda tuzo hiyo baada ya kuwashinda wachezaji wenzie ambao ni kiungo anayekipiga katika klabu ya VfL Wolfsburg ya Ujerumani Petr Jiracek na Tomas Rosicky anayecheza Arsenal. Tuzo hizo ambazo hutolewa kila mwaka nchini humo hupigiwa kura na wachezaji, makocha, viongozi wa soka na waandishi wa habari za michezo.

Monday, February 27, 2012

WACHEZAJI WA BRAZIL WASHUTUMIWA KWA UNUNUZI WA NAGARI HARAMU.

Emerson
WAENDESHA Mshtaka nchini Brazil wanawatuhumu wachezaji wa Brazil Emerson na Diguinho kwa kuhusika na shughuli za magendo za kuingiza gari aina ya BMW nchini humo kutoka Marekani kinyume cha sheria. Waendesha mashtaka hao kutoka jiji la Rio de Janeiro wanataka kuwashitaki wachezaji hao kwa magendo pamoja na kutumia fedha chafu na majina yao yalionekana wakati wa uchunguzi wa tukio hilo kuhusu genge hilo ambalo huleta magari kutoka nje na kuuza nchini humo kinyume cha sheria. Kama wachezaji hao watakutwa na makosa hayo waatakabiliwa na kifungo cha miaka 14 jela ambapo hakimu anayesimamia kesi hiyo atapitia vilelezo kabla kuangalia uwezekano wa kuwafungulia mashtaka. Emerson ambaye ni mshambuliaji wa klabu ya Corinthians na Diguinho ambaye ni kiungo wa klabu ya Fluminense zote za nchini humo wamekana makosa hayo wakidai kuwa walinunua magaro hayo kwa kufuata taratibu zote za kisheria.

DONOVAN KUKOSA MCHEZO WA ITALIA.

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Marekani Landon Donovan atakosa mchezo wa timu yake hiyo dhidi ya Italia baada ya kujiondoa kutokana na maradhi yanayomsumbua. Donovan atakosa nafasi ya kucheza pamoja na Clint Dempsey kwa mara ya kwanza toka kocha Jurgen Klinsmann achukue mikoba ya kuinoa timu hiyo msimu uliopita. Mbali na Donovan mchezaji mwingine wa kikosi hicho ambaye atakosa mchezo huo utakaopigwa jijini Genoa, Italia ni Jermaine Jones ambapo ameumia kifundo cha mguu. Katika kuziba nafasi za wachezaji hao Klinsmann amewaita wachezaji Sasha Kljestan na Brek Shea ambao wanatoka katika kikosi timu ya vijana ya chini ya umri wa miaka 23 ya nchi hiyo.

MARADONA KUTEMBELEA KAMBI YA AL AHLY.

NGULI wa soka wa zamani Diego Armando Maradona anatarajiwa kutemebelea kambi ya timu ya Al Ahly ambayo wameweka huko Falme za Kiarabu-UAE ambapo vyombo vya habari nchini humo vimesema ziara hiyo itakuwa ni kuwapa moyo wachezaji wa timu kutokana na tukio liliwakuta hivi karibuni. Mjumbe mmoja wa bodi ya Al Ahly ambaye hakupenda jina lake litajwe amesema hawana uhakika sana kama Maradona atawatembelea lakini wanaamini kama atawatembelea na kuongea na wachezaji itasaidia kuwatia moyo wachezaji kutokana na tukio lilitokea nchini Misri. Maradona kwasasa ni kocha wa Al Wasel ya Dubai baada ya kuchukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo msimu uliopita. Wakiwa huko kambini Al Ahly wanatajiwa kucheza michezo kadhaa ya kirafiki na vilabu vya huko ikiwemo timu Al Ahly ya Dubai, Al Kuwait na nyingine ambazo zitatajwa hapo baadae.

RONALDO ASIFIA BAO LAKE LA KISIGINO.

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amesema bao lake la ushindi dhidi ya Rayo Vallecano aliloshinda kwa kisigino Jumapili kuwa ni la kukumbukwa lakini mchezaji huyo alikataa kulielezea bao hilo kama ni bora zaidi kufunga katika kipindi alichocheza soka. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno ameshafunga mabao 29 baada ya timu yake kuibuka kidedea kwa kushinda bao 1-0 dhidi ya majirani zao hao wanaotoka katika jiji la Madrid. Ronaldo alishinda bao hilo akiwa umbali wa mita 15 kutoka golini ambapo aliugonga mpira kwa kisigino na kuwapita mabeki wapatao wanne na kutinga wavuni. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Ronaldo amesema kuwa siku zote ni tofauti ukishinda bao la kisigino kwa kuwa linakuwa bao zuri lakini hadhani kuwa ndio bao bora toka aanze kusakata kabumbu.

MTUKUTU BALOTELLI AACHWA ITALIA.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa kutoka Italia Mario Balotelli ameachwa na kocha wa timu taifa ya nchi hiyo Cesar Prandelli kutokana na tabia za utovu wa nidhamu awapo uwanjani. Mshambuliaji huyo anayekipiga katika klabu Manchester City ya nchini Uingereza nafasi yake imechukuliwa na mshambuliaji anayecheza katika klabu ya AS Roma mwenye miaka 20 kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Marekani jijini Genoa. Balotelli amefungiwa kucheza michezo minne baada ya kumpga kofi kwa makusudi beki wa timu ya Tottenham Hotspurs Scott Parker Januari mwaka huu. Akihojiwa kuhusu uamuzi wa kumuacha mchezaji huyo Prandelli amesema kuwa katika kikosi chake hahitaji mchezaji ambaye anafanya makosa ambayo yanamsababisha atolewe nje hivyo kwake yeye haoni kama atakuwa na mchango katika kikosi chake. Mchezaji huyo ameshatolewa mara tatu toka ajiunge na City kwa ada ya paundi milioni 24 akitokea katika klabu Inter Milan Agosti mwaka 2010.

DALGLISH ATAMBA KULETA VIKOMBE ZAIDI ANFIELD.

MENEJA wa Liverpool Kenny Dalglish anaamini kuwa kikosi chake kitajijenga baada ya ushindi wa Kombe la Ligi dhidi ya Cardiff jana na kuleta vikombe vingi zaidi hapo Anfield. Liverpool walifanikiwa kuwashinda wapinzani wao kwa changamoto ya mikwaju ya penati mwishoni mwa mchezo huo na Dalglish anafikiria ushindi huo utaoneza hamasa kwa wachezaji ili kutafuta vikombe zaidi. Akihojiwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 60 ushindi huo ambao umemaliza ukame wa miaka sita ambayo klabu hiyo utakuwa ni chachu ya kupata mafanikio zaidi na vikombe vingi zaidi katika siku za mbeleni. Dalglish ambaye ni raia wa Scotland ni mmoja kati ya makocha saba wanaofundisha vilabu vya Ligi Kuu Uingereza ambaye ameshashinda mataji matatu makubwa ya Ligi Kuu nchini humo.

LAHM KUIKOSA UFARANSA.

NAHODHA wa timu ya taifa ya Ujerumani Philipp Lahm amelazimika kuijondoa katika kikosi cha timu hiyo ambacho kinatarajiwa kupambana na Ufaransa katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi timu ya taifa ya Ufaransa mchezo ambao utafanyika jijini Bremen, Ujerumani. Shirikisho la Soka nchini humo-DFB lilitoa taarifa katika mtandao wake kuwa kikosi hicho kitacheza bila nahodha wake huyo ambaye alikuwepo wakati klabu yake ya Bayern Munich ikipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Schalke Jumapili. Taarifa hiyo iliendelea kusema Lahm ambaye ameshaichezea Ujerumani mechi 85 mpaka sasa kwamba hatakuwepo katika kukosi hicho kutokana na majeruhi yanayomsumbua toka wiki iliyopita. Baada ya kupata ushauri wa daktari aliyemfanyia vipimo mchezaji huyo imeshauriwa kuwa abakie jijini Munich ili aweze kupata matibabu ya majeruhi yanayomsumbua. Mbali na Lahm mchezaji mwingine ambaye atakosa mchezo huo ni pamoja na Sven Bender anayekipiga katika klabu ya Borrusia Dortmund ambaye aliumia kifundi cha mguu wakati timu yake ilipopata ushidi wa mabao 3-1 dhidi ya Hannover mchezo ambao nao ulichezwa jana.

Atletico de Madrid Vs FC Barcelona 1-2 All Goals Full Match Highlights 2...

Cristiano Ronaldo AMAZING backheel GOAL! Rayo Vallecano Vs Real Madrid HD

Thursday, February 23, 2012

ROONEY KUIKOSA AJAX.

KLABU ya Manchester United imesema kuwa mshambuliaji wake Wayne Rooney atakosa mchezo wa Ligi ya Vilabu barani Ulaya dhidi ya Ajax Amsterdan ya Uholanzi leo kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya koo. Rooney alianza kuumwa baada ya timu yake hiyo kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ajax nchini Uholanzi katika mchezo wa kwanza wa michuano hiyo. Meneja wa United Sir Alex Ferguson amethibitisha kuwa mchezaji huyo anaumwa koo na kuongeza kuwa dalili za ugonjwa huo zilianza kuonekana toka katika mchezo waliocheza Amsterdam akapatiwa matibabu lakini hayakusaidia kwani hali iliendelea kuwa mbaya. Mbali na mchezo huo dhidi ya Ajax United pia inakabiliwa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Norwich na Ferguson amesema kuwa wanafanya kila wawezalo kuhakikisha anakuwa fiti kabla ya Jumapili.

GHANA KUMUANGUKIA BOATENG.

KOCHA wa timu ya taifa ya Ghana Goran Stevanovic amesema kuwa kiungo wa timu hiyo Kevin-Prince Boateng anatarajiwa kurejea katika kikosi hicho mapema. Kauli ya kocha huyo imekuja wakati akizungumza na waandishi wa habari waliomtaka kufafanua ni kitu gani kiliwatokea mpaka wakashindwa kufanya vyema katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika iliyofanyika Gabon na Guinea ya Ikweta. Kocha huyo aliendelea kusema kama ataendelea kukinoa kikosi hicho basi hana budi kuongeza damu change zaidi katika kikosi hicho akiwemo kiungo Boateng ambaye anakipiga katika timu ya AC Milan ya Italia. Stevanovic ambaye ni raia wa Serbia amesema kuwa jitihada za makusudi lazima zifanyike kumshawishi mchezaji huyo kurejea katika kikosi hicho maarufu kama Black Stars. Boateng aliandika barua kwa Shirikisho la Soka la Ghana-GFA kuomba kupumzika kuichezea Black Stars Novemba mwaka jana kwa kile alichodai matatizo ya kiafya yaliyokuwa yakimwandama.

NIGER NAYO YATIMUA KOCHA WAKE.

SHIRIKISHO la Soka nchini Niger-Fenifoot limemtimua kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Hamidou Doula na kumpitisha msaidizi wake Rolland Courbis ambaye ni raia wa Ufaransa kuchukua nafasi hiyo. Courbis alikuwa ameajiriwa kumsaidia Doula ambaye aliisaidia timu hiyo kukata tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika lakini makocha hao walipishana kauli wakati wa mchezo wa ufunguzi dhidi ya Gabon ambapo Courtis alimtuhumu Doula kwa kupanga kikosi kisicho sahihi. Fenifoot walikubaliana na Courtis ambaye pia aliwahi kuinoa klabu ya Marseille ya Ufaransa na kumpa kibarua hicho cha kukiongoza kikosi hicho katika michezo inayowakabili huko mbeleni. Niger ilishindwa kushinda hata mchezo mmoja kati ya mitatu waliyocheza katika hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Matifa ya Afrika na kuwa timu ya kwanza kung’olewa katika michuano hiyo.

MANCINI AMALIZA MGOGORO NA TEVEZ.

MENEJA wa Manchester City Roberto Mancini amemaliza mgogoro aliokuwa nao mwa muda mrefu na mshambuliaji wa klabu hiyo Carlos Tevez na kusisitiza kuwa sasa anaweza kumchagua mchezaji huyo katika kikosi chake. Lakini Mancini amesema baada ya timu hiyo kufika katika hatua ya timu 16 bora katika Kombe la Ligi la Vilabu vya Ulaya baada ya kuwafunga mabingwa watetezi Porto mabao 4-0 kuwa Tevez inabidi afanye mazoezi kwa bidii kuhakikisha anapata nafasi ya kucheza kama zamani. Mapema wiki hii Tevez aliomba msamaha kufuatia hatua yake ya kuondoka kikosini hapo bila kuaga na kuelekea kwao Argentina baada ya Mancini kumuondoa katika mipango yake baada ya kukataa kupasha misuli moto katika mchezo wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich Septemba mwaka jana. Mancini ambaye ni raia wa Italia amesema kuwa hana tatizo na mchezaji huyo kwakuwa ameshaomba msamaha na anatarajia anatarajia kukutana nae kabla ya mazoezi kesho na baada ya hapo anaweza kuendelea na mazoezi na wenzake.

Marseille vs Inter Milan - 1-0 - 22/02/2012 - ALL GOALS AND HIGHLIGHTS HD

FC Basel vs Bayern Munich 1-0 All Goals & Highlights Champions League 22...

Manchester City Vs Porto 4-0 All Highlights And Goals 2-22-2012

Wednesday, February 22, 2012

EUSEBIO AREJESHWA TENA HOSPITALI.

Mchezaji wa zamani wa Ureno Eusebio amerejea tena Hospitali kwa mara ya tatu ndani ya miezi miwili. Kwa mujibu wa Hospitali ya da Luz iliyopo Lisbon nyota huyo wa zamani wa Benfica alipelekwa Hospitalini hapo kutokana na kukabiliwa na shinikizo la damu. Madaktari wa Hospitali hiyo wamesema waliamua kubaki na Eusebio usiku baada ya kumfanyia vipimo vya mkojo siku ya Jumatatu na anatarajiwa kuruhusiwa ndani ya saa 48. Eusebio alishehereke sikukuu ya Christmas akiwa Hospitali kutokana na kukabiliwa na matatizo ya nimonia alirejeshwa tena Hospitali siku chache baadae kutokana na mamumivu ya shingo. Eusebio da Silva Ferreira ambaye amefikisha miaka 70 mwezi uliopita amekuwa nyota wa Ureno baada ya kuonyesha kiwango cha kuvutia katika miaka ya 1960 na alikuwa ni miongoni mwa wachezaji bora kumi wa muda wote mwaka 1998.

KESHI AMUACHA MIKEL OBI.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Nigeria Stephen Keshi ameamua kumuacha kiungo wa Chelsea John Mikel Obi katika kikosi cha timu hiyo kitakachocheza na tmu ya taifa ya Rwanda kutokana na majeruhi. Nigeria marufu kama Super Eagles inatarajia kucheza na Rwanda katika Uwanja wa Amavubi uliyopo Mjini Kigali February 29 kwa ajili ya kusaka nafasi ya kucheza fainali za Mataifa ya Mataifa mwaka 2013. Mikel amekuwa nje ya Uwanja katika Klabu yake baada ya kupata majeraha katika mchezo was re ya 1-1 dhidi ya Tottenham Hotspur Diemba mwaka jana huku Keshi akiamua kumuacha katika kikosi chake kwa ajili ya mchezo huo. Kiungo huyo amekuwa nje ya Uwanja kwa wiki saba kutokana na maumivu ya msuli na kuikosa michezo tisa lakini anatarajia kuanza katika kikosi cha kwanza katika mchezo wa FA dhidi ya Birmingham City utakaochezwa katika Uwanja wa Stamford Bridge Jumamosi. Keshi mwenye umri wa miaka 50 amesema yeye ni kama kwa Baba kwa Nyota huyo wa Chelsea mwenye umri wa miaka 24 hivyo hawezi kuhatarisha maisha yake . Wiki iliyopita Keshi aliwaita wachezaji 11 wanaocheza ndani ya nchi hiyo na kuwaacha wachezaji wenye majina makubwa akiwemo Kalu Uche, Brown Ideye, Chinedu Obasi na Mikel.

TEVEZ AOMBA RADHI.

Mshambuliaji wa Manchester United Carlos Tevez amewasilisha msamaha wake kwa Klabu hiyo na mashabiki wake kutokana na tabia alizozionyesha katika msimu huu. Tevez alitengeneza vichwa vya habari Octoba mwaka jana baada ya kukataa kupasha moto misuli alipotakiwa kufanya hivyo na Meneja Roberto Mancini wakati wa mchezo wa Klabu bingwa ulaya dhidi ya Bayern Munich uliofanyika katika Uwanja wa Allianz Arena. Muajentina huyo hajakichezea kikosi hicho cha Mancini tangu alipoamua kurejea kwao bila ruhusa kwa miezi mitatu huku akiwa katika jitihada za kuhamia AC Milan katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo mwezi Januari. Hata hivyo ameomba radhi kutokana na vitendo vyake na huenda akarejea katika kikosi cha kwanza cha City. Mshambuliaji huyo ametuma taarifa kupitia tovuti ya Klabu hiyo akiomba msamaha kwa wote aliowaangusha na kuathirika kutokana na vitendo alivyovifanya miezi iliyopita. Amesema kwasasa anataka kuelekeza mawazo yake kwa kucheza mpira katika Klabu ya Manchester City.

PRIMETIME PROMOTION KUSIMAMIA MCHEZO WA SIMBA NA KIYOVU.

Kampuni ya Primetime Promotion imeingia mkataba na klabu ya Simba kusimamia mchezo wa raundi ya pili ya kombe la shirikisho kati ya wekundu hao wa msimbazi na Kiyovu kutoka nchini Rwanda. Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Primetime kuandaa na kusimamia mechi za mashindano makubwa ya kimataifa baada ya kufanya kazi katika kuandaa na kusimamia na kuratibu mechi kati ya  Yanga na Zamalek.

Napoli Vs Chelsea 3-1 21-02-2012

CSKA Moscow Vs Real Madrid 1-1 All Goals & Match Highlights 21-2-12 HD

Tuesday, February 21, 2012

IVORY COAST YAIPONGEZA ZAMBIA.

SHIRIKISHO la Soka la Ivory Coast-FIF limetuma barua ya pongezi kwa maningwa wapya wa Kombe la Mataifa ya Afrika Zambia baada ya timu hizo kucheza hatua ya fainali ya michuano hiyo iliyofanyika Februari 12 mwaka huu. FIF walitoa pongezi zao kwa kiwango bora kilichoonyeshwa na timu hiyo maarufu kama Chipolopolo na kusifu kuwa ulikuwa ni mchezo mgumu na mzuri ambao Afrika na dunia nzima walifurahia. Katika barua hiyo ambayo rais wa FIF Augustine Sidy Diallo alimtumia rais wa Shirikisho la Soka la Zambia-ZFF Kalusha Bwalya aliwasifu Chipolopolo kwa kunyakuwa ubingwa huo kwa kudai kuwa walionyesha kiwango bora na walistahili ushindi katika mchezo huo. Diallo aliendelea kusema kuwa ushindi huo wa Zambia ulichochewa na umoja na ushirikiano waliokuwa nao wachezaji pamoja na uongozi mzima wa shirikisho la nchi hiyo pamoja na mashabiki kwa ujumla. Zambia walifanikiwa kuwafunga Ivory Coast kwa changamoto ya mikwaju ya penati 8-7 baada ya kushindwa kufungana katika muda wa kawaida na kutawadhwa kuwa mabingwa wapya wa michuano hiyo.

BERETTA APEWA MIKOBA YA KUINOA CESENA

MARIO Beretta ameteuliwa kuinoa klabu ya Cesena ya nchini Italia baada ya kuchuklua nafasi ya kocha aliyetimuliwa Daniele Arrigoni ambapo anakuwa kocha wa tatu kuinoa klabu hiyo toka msimu huu ulipoanza. Arrigoni alitimuliwa kuinoa klabu hiyo jana ikiwa ni siku moja baada ya timu hiyo kupokea kipigo cha mabao 3-1 wakiwa uwanja wao wa nyumbani dhidi ya AC Milan ambapo nae alichukua nafasi ya Marco Giampaolo aliyetimuliwa mapema Novemba mwaka jana. Hatahivyo klabu hiyo imeshinda mchezo wake mmoja tu kati ya michezo 10 iliyocheza hivi karibuni na kuifanya kushika mkia katika Ligi Kuu nchini Italia wakihitaji alama saba ili kujinasua katika hatari ya kushuka daraja. Kabla ya kutua Cesena Beretta aliwahi kuinoa klabu ya Brescia msimu uliopita lakini alitimuliwa ndani ya miezi miwili na klabu hiyo ambayo hatahivyo ilishuka daraja.

KESI YA BIN HAMMAM KUSIKILIZWA APRIL.

Rufani ya aliyekuwa mgombea urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Mohamed bin Hammam imetajwa kusikilizwa April 18 na 19 mwaka huu na Mahakama ya Michezo ya Usuluhishi-CAS akipinga kufungiwa maisha na shirikisho hilo kufuatia kashfa ya rushwa. Bin Hammam ambaye amekana makosa hayo hii inakuwa ni rufani yake ya pili ya kwanza ikiwa ni kusimamisha Shirikisho la Sola barani Asia-AFF kupinga kuondolewa nafasi yake kama rais wa Shirikisho hilo. FIFA ilimfungia Bin Hammam Julai mwaka jana baada ya Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo kumkuta na makosa ya kujaribu kununua wapiga kura wa Caribbean wakati wa uchaguzi wa ambapo alikuwa akipambana na Sepp Blatter. Bin Hammam ambaye ni raia wa Qatar alijitoa katika kinyang’anyiro hicho kufuatia kashfa hiyo Mei mwaka jana na sasa amekuwa akipambana na rufani yake aliyokata CAS ili kuzuia uchaguzi wa AFF unaotarajiwa kufanyika Mei mwaka huu.

LANDI ATIMULIWA LIBERIA.

SHIRIKISHO la Soka nchini Liberia-LFA limemfukuza kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Roberto Landi ikiwa ni wiki moja tu kabla timu hiyo haijaanza kampeni yake ya kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka ujao. Katika taarifa iliyotolewa na rais wa LFA Musa Bility alithibitisha kuondolewa kwa kocha huyo ambaye amekuwa akikinoa kikosi hicho kwa miezi 11. Sababu haswa za kumtimua kocha huyo hazikuwekwa wazi lakini timu hiyo imeshinda michezo miwili kati ya nane iliyocheza chini ya Landi na kipigo walichopata kutoka kwa timu ya Nigeria ambayo ilikuwa haina nyota wake wanaocheza ndizo zinatajwa kuwa sababu kubwa ya kutimuliwa na kocha huyo. Thomas Kojo ndio amepewa nafasi ya kushika nafasi ya Landi katika mchezo wa kwanza dhidi ya Namibia Jumatano wakati wakitafuta kocha atakayeziba nafasi hiyo.

FORLAN ATAMANI CHAMPIOS LEAGUE.

MSHAMBULIAJI wa Inter Milan Diego Forlan amedai kuwa ana hamu kubwa ya kucheza kwa mara ya kwanza michuano ya Klabu Bingwa ya Ulaya akiwa na kikosi hicho katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Olympique de Marseille utakaofanyika katika Uwanja wa Velodrome nchini Ufaransa Jumatano. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Atletico Madrid alishindwa kucheza michuano hiyo katika hatua za makundi kutokana na sheria za Shrikisho la Soka Barani Ulaya lakini sasa anaweza kurejea tena kwenye mashindano hayo. Akihojiwa na mtandao wa Shrikisho la Soka barani Ulaya-UEFA Forlan amesema kuwa alikuwa na hamu kubwa ya kucheza michuano hiyo ambayo ni muhimu duniani na sasa anaeza kucheza huku timu yake ikiwa imeingia katika hatua timu 16 bora. Forlan aliendelea kusema kuwa katika michuano hiyo kuna timu nyingi ngumu hivyo inatakiwa kuchukulia kila mchezo na umuhimu wake na kupunguza kuweka matumaini ya kushinda juu.

Monday, February 20, 2012

GATTUSO ADAI YUKO TAYARI KUCHEZA BURE MILAN.

KIUNGO wa AC Milan Gennaro Gattuso amesema kuwa yuko tayari kucheza bila kulipwa chochote pindi ataporejea uwanjani baada ya kuuguza jeraha la jicho linalomsumbua. Gattuso hajaichezea timu hiyo toka agongane na mchezaji mwenzie Alessandro Nesta katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu nchini Italia maarufu kama Serie A Septemba 9 mwaka jana. Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 unaisha mwishoni mwa msimu huu lakini mchezaji huyo alimwambia rais wa klabu hiyo Adriano Galliani kuwa yuko tayari kucheza bila malipo yoyote kwani anachikitaka yeye akirudi ni kufanya kile anachokipenda. Gattuso amekuwa na klabu hiyo toka mwaka 1999 na ameshinda kila kitu akiwa na klabu hiyo pamoja na Kombe la Dunia mwaka 2006 akiwa na timu ya taifa ya Italia. Mchezaji huyo amesema akiwa na umri wa miaka 34 hajafikiria chochote kuhusu kutundika daruga kwani anaishi kwa ajili ya soka.

QATAR YAPATA KOCHA MPYA.

Shirikisho la Soka nchini Qatar limeteua Paulo Autuori raia wa Brazil kuinoa timu ya taifa ya nchi hiyo kwa ajili ya mbio za kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil. Autuori ambaye alikuwa kocha wa timu ya Olimpiki ya nchi hiyo anakuwa kocha wa nne ndani ya mwaka mmoja kuinoa klabu hiyo ambayo imepania kupanda katika orodha za timu bora duniani ambapo kwasasa wanashika nafasi ya 96 kwasababu ndio watakaokuwa wenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022. Kocha huyo amewahi kuifundisha timu ya taifa ya Peru na klabu mbalimbali nchini Brazil ikiwemo klabu ya Sao Paulo ambayo aliiwezesha kunyakuwa Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia mwaka 2005 pia amefundisha baadhi ya vilabu nchini Qatar. Kazi ya kwanza ambayo itamkabili Autuori ni kukiongoza kikosi hicho katika mchezo wa mzunguko wa mwisho wa kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia ambapo katika kundi lao timu hiyo inashika nafasi ya pili huku ikikabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Iran Februari 29 mwaka huu.

GUARDIOLA MGUU NJE MGUU NDANI BARCA.

MENEJA wa klabu ya Barcelona Pep Guardiola amesema kuwa bado hajaamua kama ataendelea kuinoa kikosi cha timu hiyo baada ya msimu huu kumalizika. Akiwa na kikosi hicho Guardiola mwenye umri wa miaka 41 ameshinda mataji 13 katika ya 16 toka alichukua kibarua cha kuinoa klabu hiyo miaka minne iliyopita na kusema kuwa bado hajaamua kama atalendelea kuinoa klabu hiyo au atondoka. Meneja huyo amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo baada ya kukubali kuendelea kukaa klabuni hapo kwa miaka mingine miwili zaidi lakini akasema uongozi wa klabu hiyo haujampa masharti yoyote. Nafasi ya Guardiola imekuwa haieleweki kwa mabingwa hao wa Hispania kwasababu kocha huyo amekuwa akiongeza mkataba katikati ya msimu kwa miaka miwili iliyopita.

Barcelona Vs Valencia 5-1 All Highlights And Goals 2-19-2012

Saturday, February 18, 2012

WENGER AOMBA RADHI MASHABIKI WA KLABU HIYO.

MENEJA wa Klabu ya Arsenal Arsene Wenger amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kufuatia kipigi cha mabao 4-0 walichopata toka kwa AC Milan katikati ya wiki katika mchezo wa kwanza wa michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya. Akihojiwa kabla ya mchezo wa Kombe la Chama cha Soka cha Uingereza-FA dhidi ya Sunderland utakaopigwa leo Wenger amesema kuwa mashabiki walikuwa upande wao katika muda wote walipokuwa wanacheza na Milan ndio maana anaomba samahani kwa mashabiki hao kwa matokeo ambayo hayakuridhisha. Akizungumzia mchezo wa leo dhidi ya Sunderland Wenger amesema mchezo huo utakuwa ni vita nyingine ambayo wanahitajika kupambana hivyo aliwaomba mashabiki kushangilia timu yao hiyo ili waweze kufanya vizuri. Arsenal imeshindwa kushinda kikombe chochote kwa miaka saba huku wakiwa hawana matumaini ya kufanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kipigo walichopata kutoka Milan hivyo mchezo wa leo utakuwa muhimu ili kuweka matumaini ya kunyakuwa kombe la FA.

GHANA KUCHEZA NA CHILE.

TIMU ya taifa ya Ghana maarufu kama Black Stars wanatarajia kucheza mchezo wa kimataifa wa maonyesho wa kirafiki dhidi ya timu ya Chile Februari 29 mwaka huu jijini Philadelphia, Marekani. Mchezo baina ya timu hizo ulitangazwa jana na upo katika kalenda ya kimataifa ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA hivyo kuna uwezekano mkubwa vikosi vya timu zaote mbili vikaita nyota wao wanaocheza klabu mbalimbali Ulaya. Moja ya majina ya nyota wanaotarajiwa kuwepo katika timu ya Chile ni pamoja na mshambuliaji wa Barcelona Alexis Sanchez na Humberto Suazo anayekipiga Monterrey wakati Ghana wanatarajia kuwa na nyota wao kama Michael Essien anayekipiga Chelsea na Andre Ayew anayecheza Marseille ya Ufaransa. Ghana ambao walifika hatua ya nusu fainali katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika iliyoandaliwa kwa pamoja na Guinea ya Ikweta na Gabon waliifunga timu ya taifa ya Marekani kwa mabao 2-1 kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 na kufanikiwa kuingia mzunguko wa pili wa michuano hiyo.

DUARTE ATIMULIWA BURKINA FASO.

Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Burkina Faso Paulo Duarte ametimuliwa kibarua chake hicho kufuatia uamuzi ulifikiwa na Shirikisho la Soka la nchini hiyo-FBF. Uamuzi wa kumtimua kocha huyo raia wa Ureno ulifikiwa baada ya matokeo mabaya iliyopata timu hiyo katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kupoteza michezo yote mitatu katika kundi B walilopangwa hivyo kuwafanya kutolewa katika hatua za mwanzoni za michuano hiyo. Mwenyekiti wa FBF Zambede Theodore Sawadogo alithibisha suala la kusitisha mkataba na kocha kocha ambapo amesema kuwa aliyekuwa kocha msaidizi wa kikosi hicho ndiye atakayekinoa kikosi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Morocco Februari 29 mwaka huu wakati wanafanya mchakato wa kutafuta mbadala wa Duarte. Duarte mwenye umri wa miaka 42 ambaye alikuwa akifananishwa na kocha wa timu ya Real Madrid Jose Mourinho alikuwa akiinoa klabu hiyo toka mwaka 2008.

WARNER KUSHITAKIWA TRINIDAD & TOBAGO.

SHIRIKISHO la Soka la Trinidad na Tobago limesema liko katika mpango wa kumfungilia mashtaka aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Jack Warner kwa ajili ya kurudisha fedha za msaada zikiwemo zile za janga la tetemeko la ardhi nchini Haiti. Wakili wa Shirikisho hilo Derek Ali alimwambia Jaji kuwa wanampango wa kumfungulia mashtaka Warner kwa kushindwa kuachia fedha hizo zilizotolewa wakati ambao alikuwa kama mshauri maalumu wa shirikisho hilo kabla ya kujiuzulu mwaka uliopita kufuatia kashfa ya rushwa. Jaji wa mahakama kuu nchini humo Devindra Rampersad alimpa maagizo Ali kumpelekea barua Warner juu ya uamuzi wa shirikisho hilo. Akihojiwa juu ya suala hilo na waandishi wa habari Warner alijibu kwa kifupi kuwa hiyo ni haki yao ya msingi kufanya hivyo akawaomba waandishi kuwa na uvumilivu katika hili kuangalia nini kitatokea baadae.

Friday, February 17, 2012

SUNZU AZITAMANI CHELSEA NA BOLTON.

SHUJAA wa timu ya taifa ya Zambia Stoppila Sunzu anatamani kwenda Uingereza kucheza soka la kulipwa baada ya kufanikiwa kufunga penati ya mwisho dhidi ya Ivory Coast iliyoiwezesha timu yake kunyakuwa Kombe la Mataifa ya Afrika Jumapili iliyopita. Akihojiwa Sunzu ambaye ameshawahi kuichezea klabu ya Chateauroux ya nchini Ufaransa katika msimu wa mwaka 2008-2009 amesema kuwa anatamani kurudi kucheza soka ya kulipwa Ulaya. Sunzu aliendelea kusema kuwa ana ndoto za siku moja kucheza soka ya kulipwa nchini Uingereza haswa katika timu za Chelsea na Bolton Wanderers. Zambia ilifanikiwa kuwafunga Ivory Coast kwa changamoto ya mikwaju ya penati 8-7 jijini Libreville, Gabon baada ya kwenda sare ya bila kufungana katika muda wa kawaida na kufanikiwa kunyakuwa taji hilo kwa mara ya kwanza. Sunzu alishawahi kufanya majaribio nchini Uingereza katika klabu ya Reading baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika michuano ya Kombe la Dunia ya vijana chini ya miaka 20 iliyofanyika nchini Canada lakini alishindwa kupata kibali cha kufanya kazi nchini Uingereza.

MEZZARRI KUWAKOSA CHELSEA.

KOCHA wa klabu ya Napoli ya nchini Italia Walter Mezzarri atakosa michezo miwili ya timu yake katika michuano ya Kombe la Klabu Bingwa ya Ulaya hatua ya timu 16 bora dhidi ya Chelsea baada ya kushindwa rufani yake ya kufungiwa michezo miwili Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA. Mezzarri alifungiwa Januari baada ya kumsukuma mshambuliaji wa Villarreal Nilmar wakati wa mchezo wa Kundi A Desemba 7 mwaka jana ambapo timu yake ilishinda mabao 2-0 na kufanikiwa kuingia hatua hiyo. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 50 hatakuwepo katika benchi la ufundi la timu yake itapopambana na Chelsea Februari 21 pamoja na mchezo wa marudiano utakaochezwa Machi 14 mwaka huu. Pia kocha huyo amezuiliwa kuongea na wachezaji wake pamoja na benchi la ufundi kabla ya mchezo na wakati wa mchezo pamoja na kutumia simu kuwasiliana na benchi lake la ufundi.

VILLAR ACHAGULIWA TENA KUONGOZA RFEF.

Angel Maria Villar amechaguliwa tena bila kupingwa kwa mara ya saba kuongoza kwa miaka mingine minne kama rais wa Shirikisho la Soka nchini Hispania-RFEF huku kukiwa na madai ya kukiuka taratibu za uchaguzi. Villar mwenye umri wa miaka 62 ambaye ndiye Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA alikuwa ndiye mgombea pekee katika uchaguzi huo uliofanyika makao makuu ya RFEF jijini Madrid akiwa amepata kura 161 kati ya 167 ambapo kura tano ziliharibika na moja pekee ndio iliyompinga. Mahakama moja nchini Hispania ilitupilia mbali katika dakika za ombi la kusogeza uchaguzi huo mbele lililotolewa na Ignacio del Rio ambaye ni diwani wa zamani wa jiji la Madrid ambaye alikuwa akimtuhumu Villar na RFEF kukiuka taratibu za uchaguzi. Mshindi wa uchaguzi huo Villar pamoja na Rais wa UEFA Michel Platini walikuwa wkaifuatilia uchaguzi wakiwa katika msari wa mbele ambapo alishukuru wapiga kura wote pamoja na Kocha wa timu ya taifa ya Hispania Vicente del Bosque kwa ushirikiano walioonyesha na kusema kuwa uchaguzi huo unafaa kuigwa na vyama vya soka duniani kote.

BECKHAM AMKINGIA KIFUA CAPELLO.

NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza David Beckham yupo pamoja na Fabio Capello kufuatia uamuzi wake wa kujiuzulu wadhifa kama meneja wa timu hiyo. Beckham akihojiwa kwa mara ya kwanza toka kujiuzulu kwa kocha huyo amesema kuwa amesikitishwa na kitendo cha Capello kujiuzulu nafasi yake hiyo katika kipindi ambacho ni karibu na michuano ya Kombe la Ulaya lakini akasema kuwa anaheshimu uamuzi wake kwani anaamini kocha lazima apewe nafasi ya kuteua nahodha wake mwenyewe. Mchezaji huyo aliendelea kusema amefanya kazi na Capello kwa miaka michache hivyo inasikitisha kuona anaondoka katika kipindi hiki muhimu ambacho timu ya Uingereza inakabiliwa nacho. Capello aliachia wadhifa wake huo wiki iliyopita baada ya kufanya mkutano na Chama cha Soka cha Uingereza-FA ambapo walivua unahodha John Terry kufuatia kashfa ya kumtutolea maneno ya kibaguzi beki wa Queens Park Rangers Anton Ferdinand.

BEBETO ATEULIWA KATIKA KAMATI YA MAANDALIZI YA KOMBE LA DUNIA 2014.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Brazil Bebeto ambaye aliwahi kushinda michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1994 akiwa na timu ya taifa ya nchi hiyo ameteuliwa katika Kamati ya Maandalizi ya michuano hiyo ambayo itafanyika nchini humo 2014. Uteuzi wa Bebeto unakuwa ni wa pili kwa majina makubwa katika soka la Brazil akiungana na mshambuliaji wa zamani wa Barcelona, Inter Milan na Real Madrid Ronaldo ambaye nae pia aliiwezesha nchi yake kutwaa Kombela Dunia mwaka 2002. Akihojiwa mara baada ya uteuzi huo Bebeto amesema kuwa imekuwa ni heshima kubwa kwake kupata nafasi hiyo haswa katika siku hiyo muhimu ambayo alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa aitimiza miaka 48. Bebeto ambaye kwasasa ni mbunge jijini Rio de Jenairo amejiunga katika kamati hiyo huku kukiwa na changamoto nyingi zinazokabili maandalizi hayo ikiwemo miradi mingi kuvuka malengo ya kifedha huku viwanja vya ndege vikiwa havijafanyiwa matengenezo ya kuweza kupokea wageni zaidi ya 600,000 wanaotarajiwa kuhudhuria michuano hiyo. Bebeto ambaye aliunda safu kabambe ya ushambuliaji akiwa na Romario wakati Brazil iliponyakuwa Kombe la Dunia mwaka 1994 atakumbukwa zaidi kwa aina yake ya ushangiliaji akiwa kama amepakata mtoto aliyoifanya wakati wa mchezo wa robo fainali dhidi ya Uholanzi katika michuano hiyo.

Ajax vs Manchester United 0-2 - All Goals Highlights - (16-02-2012)

Wednesday, February 15, 2012

AMRI ZAKI AIHOFIA YANGA.

MSHAMBULIAJI wa Zamalek Amr Zaki ametoa tahadhari kufuatia mchezo wao Klabu Bingwa ya Afrika dhidi ya Yanga akidai kuwa utakuwa mchezo mgumu mchezo ambao utachezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Zaki amesema kuwa mchezo huo utakuwa mgumu hivyo inabidi wawe tayari kwa hilo na kama wakifanikiwa kushinda mchezo huo basi mchezo unaofuatia utakuwa rahisi kidogo kwao. Mshambuliaji huyo aliendelea kusema kuwa lazima waiheshimu Yanga kwasababu watakuwa wakicheza nyumbani mbele ya mashabiki wao hivyo kuwafanya wawe hatari kwa mchezo huo. Zaki ambaye ana umri wa miaka 28 ameshinda mabao mawili katika michezo miwili ya kirafiki Zamaleki iliyocheza dhidi ya timu ya Telcom ya nchini humo ambapo wanatarajiwa kusafiri kuja Tanzania kesho kwa ajili ya mchezo huo wa Jumamosi.

FIFA YASUBIRI MAELEZO YA TTFF.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA imethibitisha kuwa inasubiri maelezo kuhusu fedha za msaada kufuatia tetemeko la ardhi nchini Haiti ambazo zimeshindwa kufika huko baada ya kutumwa kupitia Shirikisho la Soka nchini Trinidad na Tobago-TTFF. FIFA imesema fedha hizo zilitumwa TTFF mwaka 2010 ambapo ziliombwa na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya FIFA Jack Warner ambaye katika kipindi hicho alikuwa kiongozi wa Vyama vya Soka vya Amerika ya Kaskazini, Kati na Caribbean-Concacaf. Katika taarifa yake FIFA imesema ilituma kiasi cha dola 250,000 kwenda TTFF lakini Shirikisho la Soka nchini Haiti limedai limepata dola 60,000 pekee. FIFA imesema bado haijapata maelezo yoyote kuhusu kilichotokea kwa kiasi dola 190,000 zilichobakia na tayari wamezuia misaada yote inayokwenda TTFF mpaka hapo watakapopata maelezo ya kina juu ya sula hilo. Haiti ilikumbwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa magnitude 7.0 ambalo liliua zaidi ya watu 300,000 na kuacha wengine zaidi ya milioni 1.5 wakiwa hawana makazi miaka miwili iliyopita.

(HD) Bayer Leverkusen Vs Barcelona 1-3 All Goals & Full Highlights *UCL*...

Monday, February 13, 2012

ZAMBIA YAPOKEWA KISHUJAA.

TIMU ya Taifa ya Zambia imewasili nchini mwao Jumatatu na kupata mapokezi ya hali ya juu kutoka kwa zaidi ya maelfu ya mashabiki waliojitokeza kuwalaki mashujaa wao baada ya kunyakuwa taji la kwanza la michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Wakiwa na kombe hilo walilopata baada ya kuifunga Ivory Coast kwa changamoto ya mikwaju ya penati Jumapili iliyopita mabingwa hao wapya wa Afrika waliwapungia mkono mashabiki walijitokeza kuwalaki katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka. Baadae kikosi hicho kilipanda basi kuelekea katika uwanja wa maonyesho wa Lusaka ambapo mashabiki wanaokadiriwa kufikia 200,000 wakiwa wamevaa jezi za timu ya taifa ya nchini hiyo walikuwa wamekusanyika kwa ajili sherehe maalumu iliyoandaliwa. Mashabiki hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali wakati wengine wakipuliza mavuvuzela na mara kikosi hicho kiliowasili polisi walipata wakati mgumu kuwatuliza mashabiki hao ambao kila mmoja alikuwa nataka kuwaona mashujaa wao hao.

RANGERS MBIONI KUFILISIKA.

Klabu ya soka ya Rangers imethibitisha kwamba imewasilisha ombi lake kisheria mahakamani ikiwa na nia ya kupata watu watakaosimamia shughuli za klabu huku ikijitayarisha kutangaza kufilisika. Klabu hiyo imetangaza kwamba itaendelea na shughuli zake kama kawaida, hadi itakapotangaza uamuzi wa mwisho kama itaendelea na hatua hiyo. Rangers sasa ina siku 10 kufanya uamuzi na wakati hayo yakiendelea klabu imetangaza kwamba mashabiki wenye tiketi za msimu mzima, na vile vile wenye hisa, wasiwe na wasiwasi wowote. Hatua hiyo imechukuliwa huku Rangers ikisubiri uamuzi kuhusiana na utata juu ya ushuru, pamoja na faini mbalimbali ambazo klabu hiyo inadaiwa na jumla ya deni likiwa ni pauni milioni 49. Katika taarifa iliyotilewa na klabu hiyo imeelezea kwamba ikiwa uamuzi huo utaamuliwa kwa idara ya forodha kushinda kesi basi itamaanisha malimbikizo ya deni hilo na faini huenda yakazidi hata pauni milioni 50 na klabu hakitakuwa na uwezo wa kulilipa deni hilo. Tajiri anayemiliki klabu hiyo Craig Whyte alinukuliwa baadaye akisema deni hili huenda likazidi na kufikia pauni milioni 75. Whyte, ambaye alinunua klabu kutoka kwa Sir David Murray mwaka jana, alisema suala la klabu kupata usimamizi mpya ni jambo la kufikiriwa iwapo klabu itashindwa katika kesi hiyo kuhusiana na ushuru.

"MANCINI TREAT ME LIKE A DOG", TEVEZ.

MSHAMBULIAJI wa Manchester City Carlos Tevez amerejea Uingereza akimtuhumu kocha wake Roberto Mancini kwa kumchukulia kama mbwa katika tukio lililopelekea kuondolewa katika kikosi cha timu hiyo ambao ni vinara wa Ligi Kuu nchini humo. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina amesema kuwa Mancini aliapa mbele yake wakati wa mchezo wa Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich ambao walipoteza Septemba mwaka jana ambapo mchezaji huyo alikataa kupasha misuli moto. Tevez hajaichezea City toka September 27 mwaka jana nchini Ujerumani lakini yuko tayari kurejea katika kikosi hicho baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda zaidi ya miezi mitatu. Mancini ameshaonyesha nia ya kumsamehe mchezaji huyo kama ataomba msamaha kwa kosa alilofanya na Tevez wakati akihojiwa na luninga moja nchini Uingereza amesema hadhani kama ana kosa lolote lakini kama klabu inafikiri hivyo anaomba msamaha.

ANZHI YAMTIMUA KOCHA WAKE.

KLABU ya Anzhi Makhachkala ua Urusi imemtimua kocha wake Yuri Krasnozhan baada ya kuinoa klabu hiyo kwa zaidi ya mwezi mmoja tu. Krasnozhan mwenye umri wa miaka 48 alijiunga na klabu hiyo mwishoni mwa mwaka uliopita baada ya kutimuliwa na klabu ya Lokomotiv Moscow mapema msimu huu pamoja na na kuyiwezesha klabu hiyo kuongoza katika kipindi hicho. Akihojiwa na mtandao wa klabu kocha huyo amesema kuwa sababu kubwa ya kuondoka kwake ni kushindwa kuelewana uongozi katika baadhi ya mambo ya klabu hiyo. Hatahivyo vyombo vya habari vya nchi hiyo vinasema kwamba sababu halisi ya kuondoka kwa kocha huyo ni kushindwa kuongoza wachezaji wenye majina makubwa katika timu hiyo kama mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon Samuel Eto’o na beki wa kimataifa wa zamani wa Brazil Roberto Carlos. Pia kuna taarifa nyingine kuwa Fabio Capello ndio anatarajiwa kuchukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo ambapo Muitaliano huyo ambaye ameachia kibarua cha kuinoa Uingereza wiki iliyopita alikuwepo nchini humo mwishoni mwa wiki hii kwa ajili ya mazungumzo ya kuinoa klabu hiyo.

African Cup of Nations 2012 - Top 10 Goals HD

Real Madrid Vs Levante 4-2 All Goals & Match Highlights 12-02-12 HQ

RENARD AJIFANANISHA NA MOURINHO.

KOCHA wa timu ya taifa ya Zambia Herve Renard amejifananisha mwenyewe na kocha wa Real Madrid Jose Mourinho akijiita mteule. Kocha huyo raia wa Ufaransa ana kila sababu ya kuwa na furaha baada ya kuiongoza kikosi Zambia wanaojulikana zaidi kama Chipolopolo kunyakuwa taji lao la kwanza la michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2012. Timu hiyo ambayo inatoka katika ukanda wa Kusini mwa Afrika walifanikiwa kuifunga timu ambayo ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kunyakuwa taji hilo kutokana na nyota iliyosheheni ya Ivory Coast kwa changamoto ya mikwaju ya penati 8-7 jijini Libreville. Renard alichukua mikoba ya kuinoa Chipolopolo mwaka 2010 baada ya aliyekuwa kocha wa kikosi hicho Dario Bennetti kubwaga manyaga ikiwa ni siku kabla ya michuano ya 28 ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huo.

ROONEY AMPIGIA DEBE GERRARD KUWA NAHODHA UINGEREZA.

MSHAMBULIAJI wa Manchester United Wayne Rooney amesema nyota wa Liverpool Steven Gerrard ndiye anafaa kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza. Kwasasa Uingereza hawana nahodha wala kocha baada ya aliyekuwa kocha wa nchi hiyo Fabio Capello kujiuzulu Jumatano iliyopita kufuatia John Terry kuvuliwa unahodha na Chama cha Soka cha nchi hiyo-FA. Hatua hiyo ya FA ilifikiwa kutokana na mchezaji huyo kusubiri kusikilizwa kwa kesi yake iliyotokana na kutoa kauli ya kibaguzi lakini mchezaji huyo ataweza kuitumikia nchi yake katika michuano ya Kombe la Ulaya itakayochezwa baadae mwaka huu. Rooney aliandika katika ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa kama akiteuliwa kuwa nahodha wa Uingereza atafurahia lakini akasema suala hilo ni juu ya kocha mpya atayeteuliwa ingawa kwa muono wake yeye anaona Gerrard anafaa zaidi kwa nafsi hiyo.

WOLVES YAMTIMUA KOCHA WAKE.

KLABU ya Wolverhampton Wanderers ya Uingereza imemtimua meneja wake Mick McCarthy kutokana na timu hiyo kusuasua kubakia katika Ligi Kuu nchini humo. Mchezo wa mwisho wa kikosi hicho chini McCarthy ulikuwa ni mchezo wa Jumapili dhidi ya mahasimu wao West Bromwich Albion ambapo walipoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 5-1 na kuifanya timu hiyo kutupwa katika mstari wa kusguka daraja. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo Jumatatu ilisema kwamba klabu hiyo imechukua uamuzi huo kutokana na matokeo mwenendo mbovu wa timu hiyo ambapo katika michezo 22 ya ligi iliyocheza imefanikiwa kupata alama 14 tu. Kocha Msaidizi wa Wolves Terry Connor ndiye atayrchukua majukumu ya kukinoa kikosi hicho wakati wakitafuta kocha mwingine atakayeziba nafasi ya MacCarthy.

CAF YATOA RAMBIRAMBI KWA WAATHIRIKA MISRI.

SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF limetoa kiasi cha dola 150,000 kwa familia za waathirika ya watu ambao walikumbwa katika vurugu zilizotokea uwanjani nchini Misri. Rambirambi hizo kutoka CAF zilipitishwa katika kikao ilichokaa Jumamosi katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon huku Shirikisho la Soka Duniani-FIFA nalo limesema litatoa kiasi cha dola 250,000 kwa ajili ya familia za waathirika. Bendera zimekuwa zikipepea nusu mlingoti latika michuano hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya Gabon na Guinea ya Ikweta na pia kumekuwepo na dakika moja za maombolezo katika kila mchezo. Vurugu hizo zilitokea baada ya mchezo wa Ligi Kuu nchini Misri ulifanyika jijini Port Said Februari 1 mwaka huu ambapo zaidi ya watu 70 walipoteza maisha katika vurugu hizo.

Zambia vs Ivory Coast (8-7) PENALTY SERIES (CAN2012 - Final)

Sunday, February 12, 2012

SENEGAL YAMWINDA HERVE RENARD.

SHIRIKISHO la Soka nchini Senegal-FSF limesema liko katika mipango ya kujaribu kuzungumza na kocha wa Zambia Herve Renard mwenye miaka 43 ili aibe pengo la Amara Traore ambaye alifukuzwa wiki iliyopita baada ya timu hiyo kutolewa mapema katika michuano ya Kombe la Matifa ya Afrika. Rais wa FSF Augustin Senghor aliwasili Gabon Alhamisi iliyopita kwa ajili ya mkutano mkuu wa Shrikisho la Soka barani Afrika-CAF ambapo alitarajia kuanzisha mawasiliano na kocha huyo. Maofisa wa Senegal wanahitaji kocha ambaye ana uzoefu na soka la Afrika ili kuendelea pale alipoishia Traore. Renard ambaye alishawahi kuinoa klabu ya USM Alger ya Algeria ndio anayepewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba ya Traore lakini haijafahamika kama kocha huyo ataacha kukinoa kikosi cha Zambia baada ya michuano hiyo.

ROMARIO AIKOSOA NCHINI KUTOKANA NA MAANDALIZI MABOVU YA KOMBE LA DUNIA.

NYOTA wa zamani wa Brazil Romario kwa mara nyingine ameikosoa nchi yake katika maandalizi ya Kombe la Dunia mwaka 2014 kwa kusema kuwa anahofia aibu kufuatia ujenzi wa kusuasua katika viwanja vya ndege. Romario ambaye kwasasa ni mbunge amesema kuwa kutakuwa na matumizi yaliyozidi katika viwanja 12 vitavyotumika kwa ajili ya Kombe la Dunia na itawabidi wachukue fedha za umma na kuitumia michuano hiyo kama sababu. Katika mahojiano yake na mtandao mmoja nchini humo Romario amesema kutakuwa na vurugu katika viwanja vya ndege nchini humo katika kipindi cha michuano hiyo kama ujenzi wa kuvikarabati viwanja hivyo hautaanza mapema. Nyota huyo amesema kuwa kama hatua za makusudi za ukarabati wa viwanja vya ndege hautafanyika haraka ni wazi kwamba nchi hiyo itatia aibu kutokana na ubovu wa viwanja hivyo akitolea mfano jinsi zinavyokuwepo vurugu katika kipindi cha mapumziko ambapo wageni wengi huingia nchini humo. Mbali na Romario nyota mwingine wa zamani wa nchi hiyo Pele naye alikuwa na mawazo kama hayo akidai kuwa viwanja vya ndege nchini humo vinahitaji ukarabati ili viweze kupokea wageni wengi katika kipindi cha michuano ya Kombe la Dunia.