Friday, February 17, 2012

BEBETO ATEULIWA KATIKA KAMATI YA MAANDALIZI YA KOMBE LA DUNIA 2014.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Brazil Bebeto ambaye aliwahi kushinda michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1994 akiwa na timu ya taifa ya nchi hiyo ameteuliwa katika Kamati ya Maandalizi ya michuano hiyo ambayo itafanyika nchini humo 2014. Uteuzi wa Bebeto unakuwa ni wa pili kwa majina makubwa katika soka la Brazil akiungana na mshambuliaji wa zamani wa Barcelona, Inter Milan na Real Madrid Ronaldo ambaye nae pia aliiwezesha nchi yake kutwaa Kombela Dunia mwaka 2002. Akihojiwa mara baada ya uteuzi huo Bebeto amesema kuwa imekuwa ni heshima kubwa kwake kupata nafasi hiyo haswa katika siku hiyo muhimu ambayo alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa aitimiza miaka 48. Bebeto ambaye kwasasa ni mbunge jijini Rio de Jenairo amejiunga katika kamati hiyo huku kukiwa na changamoto nyingi zinazokabili maandalizi hayo ikiwemo miradi mingi kuvuka malengo ya kifedha huku viwanja vya ndege vikiwa havijafanyiwa matengenezo ya kuweza kupokea wageni zaidi ya 600,000 wanaotarajiwa kuhudhuria michuano hiyo. Bebeto ambaye aliunda safu kabambe ya ushambuliaji akiwa na Romario wakati Brazil iliponyakuwa Kombe la Dunia mwaka 1994 atakumbukwa zaidi kwa aina yake ya ushangiliaji akiwa kama amepakata mtoto aliyoifanya wakati wa mchezo wa robo fainali dhidi ya Uholanzi katika michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment