Wednesday, September 28, 2011

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: ARSENAL YASHINDA, CHELSEA YANG'ANG'ANIWA.

Mshambuliaji wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain akishangilia pamoja na Arshavin mara baada ya kuipatia timu yake bao la kwanza dhidi ya Olympiakos katika Uwanja wa Emirates ambapo Arsenal ilishinda 2-1.

Chamberlain akifunga bao la kwanza.

Adre Santos akiweka kimiani bao la pili la Arsenal katika mchezo huo.

Santos na Thomas Rosicky wakishangilia mara baada ya kufunga bao la pili.

Mshambuliaji wa olympiakos David Fuster akipiga kichwa kufunga bao la kufutia machozi la timu yake.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger akizungumza na CEO wa  timu hiyo upande wa jukwaani ikiwa ni hatua ya kumalizia adhabu yake ya kufungiwa mechi mbili kutokukaa katika benchi la ufundi katika mchezo huo.

MATOKEO YA MICHEZO YA LEO.

Arsenal 2-1 Olympiakos
AC Milan 2-0 Plzen
BATE Borisov 0-5 Barcelona
Bayer Leverkusen 2-0 Genk
Marseille 3-0 Borussia Dortmund
Shakhtar Donetsk 1-1 Apoel Nicosia
Valencia 1-1 Chelsea

Bate Vs Fc Barcelona all goals and all highlights ( 28 09 2011 )

YANGA 5 COASTAL UNION 0.

Mshambuliaji wa Yanga Davis Mwape akijaribu kumtoka beki wa Coastal Union katika mchezo uliozikutanisha timu hizo jioni hii katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo Yanga ilishinda kwa mabao 5-0.

CHAMPIONS LEAGUE: MADRID YAENDELEA KUTAKATA, MAN UNITED CHUPUCHUPU.

MATOKEO YA MECHI ZA JANA CHAMPIONS LEAGUE.
Luzhniki, Moscow
CSKA Moscow 2 - 3 Internazionale 


Allianz-Arena, Munich
Bayern Munich 2 - 0 Manchester City 


Stadio San Paolo, Naples
Napoli 2 - 0 Villarreal CF 


Hüseyin Avni Aker, Trabzon
Trabzonspor 1 - 1 Lille OSC 


Old Trafford, Manchester
Manchester United 3 - 3 FC Basel 


Stadionul National Arena, Bucharest
Otelul Galati 0 - 1 Benfica 


Stade Gerland, Lyon
Olympique Lyon 2 - 0 Dinamo Zagreb 


Bernabéu, Madrid
Real Madrid 3 - 0 Ajax


MECHI ZA LEO JUMATANO.
Petrovskiy, St. Petersburg
Zenit St. Petersburg v FC Porto 


BayArena, Leverkusen
Bayer Leverkusen v Racing Genk 


Mestalla, Valencia
Valencia CF v Chelsea 


Stade Vélodrome, Marseille
Olympique Marseille v Borussia Dortmund


Emirates Stadium, London
Arsenal v Olympiacos 


Donbass Arena, Donetsk
Shakhtar Donetsk v APOEL Nicosia 


Stadio Giuseppe Meazza, Milan
AC Milan v Viktoria Plzen 


Dynamo Stadium, Minsk
BATE Borisov v FC Barcelona

Tuesday, September 27, 2011

Bayern Munich vs. Man City Press Conference [Dzeko & Mancini]

POULSEN ATAJA 23 WATAOIVAA MOROCCO.

MAKIPA: Shabani Dihile (JKT Ruvu Stars), Juma Kaseja (Simba) na Shabani Kado (Yanga)

MABEKI: Nahodha Shadrack Nsajigwa (Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya), Amir Maftah (Simba), Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso na Victor Costa (Simba).

VIUNGO: ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Jabir Aziz (Azam), Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam) na Ramadhan Chombo ‘Redondo’ (Azam).

WASHAMBULIAJI: Abdi Kassim ‘Babbi’ (DT Long An, Vietnam), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Danny Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden), John Bocco (Azam) na Hussein Javu (Mtibwa Sugar).

Wednesday, September 21, 2011

KIKOSI CHA STARS KITAKACHOPAMBANA NA MOROCCO KUTAJWA.

DAR ES SALAAM, Tanzania
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen anatarajia Septemba 26 mwaka huu kutaja wachezaji watakaoingia kambini kwa ajili ya mechi dhidi ya Morocco itakayochezwa Oktoba 9 mwaka huu jijini Casablanca.

Akizungumza Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura alisema kikosi hicho kinatarajiwa kujitupa kambini Septemba 28 kwa ajili ya kujjiwinda na mchezo huo ambapo inatarajiwa kuondoka Octoba 6 kwenda Casablanca.

Alisema mchezo huo ni wa mwisho wa hatua ya makundi wa kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zinazotarajiwa kufanyika kwa pamoja Equatorial Guinea na Gabon, ambapo Stars inatakiwa kushinda mchezo huo ili kujihakikishia nafasi ya kucheza michuano hiyo.

Alisema kwa sasa Poulsen ambaye pia ni mkufunzi wa makocha wa Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA) yuko Gambia ambapo anaendesha kozi ya wakufunzi na anatarajiwa kurejea nchini Septemba 24 kwa ajili ya maandalizi ya kikosi chake.

Wakati huohuo Wambura alisema Ligi Daraja la Kwanza inayoshirikisha timu 18 inatarajia kuanza mwezi ujao.

Alisema Kamati ya Mashindano inayoongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa TFF, Ramadhan Nassib inatarajia kukutana Septemba 24 mwaka huu kuangalia mambo mbalimbali ya ligi hiyo.

Alisema moja ya mambo ambayo kamati hiyo itafanya ni kupitisha tarehe ya kuanza ligi hiyo pamoja na vituo.

Sunday, September 18, 2011

BARCLAYS PREMIER LEAGUE: MAN UNITED 3 CHELSEA 1, LIVERPOOL YACHAPWA 4-0 NA TOTTENHAM.











MATOKEO YA MECHI ZA LEO:

Tottenham 4-0 Liverpool
Fulham   2-2 Manchester City
Sunderland 4-0 Stoke City
Man Utd 3-1 Chelsea


MATOKEO YA MECHI ZA JANA;

Blackburn 4-3 Arsenal
Aston Villa 1-1 Newcastle
Bolton        1-2 Norwich City
Everton        3-1 Wigan Athletic
Swansea City 3-0 WBA
Wolves         0-3 QPR

LIGI KUU BARA: YANGA YASHINDWA KUFURUKUTA KWA AZAM, SIMBA YAIFUNGA KAGERA SUGAR 1-0.


Timu ya Yanga imeshindwa kufurukuta mbele ya Azam fc baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0, ambalo lilifungwa na mshambuliaji John Boco dakika 20, katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wan Taifa, Dar es Salaam jioni hii.

BARCELONA YAFANYA KUFURU LA LIGA.

Wednesday, September 14, 2011

CHAMPIONS LEAGUE: MATOKEO YA MECHI ZA JUMATANO.

Manchester City 1-1 Napoli
Villarreal 0-2 Bayern Munich


Lille 2-2 CSKA Moscow
Inter 0-1 Trabzonspor


Basel 2-1 Otelul Galati
Benfica 1-1 Manchester United


Dinamo Zagreb 0-1 Real Madrid
Ajax 0-0 Lyon

Benfica vs Manchester United 1-1 [All goals & Highlight] 14-09-2011 HD

Dinamo Zagreb 0-1 Real Madrid All Goals & Highlights 14.09.11

Manchester City Vs Napoli All Goals And Highlights 14-9-2011

Inter Milan vs Trabzonspor 0-1 Celustka Goal 14.9.2011 UEFA Champions Le...

SIMBA YAENDELEZA USHINDI CHAMAZI.

Wachezaji wa Polisi Dodoma wakisalimiana na wachezaji wa Simba kabla ya kuanza kwa mchezo wao ambao Simba walishinda kwa bao 1-0 (Picha kwa hisani ya Michuzi.)


WACHEZAJI WATANO WA AFRIKA USAJILI WAO ULISTUSHA WATU.

UHAMISHO katika Ligi kubwa barani Ulaya lina umuhimu kwa mashabiki wa Afrika wanaofuatilia ligi hizo kama ilivyo kwa wachezaji wa kiafrika wanaocheza huko.
Katika orodha inayofuata utaona uhamisho wa wachezaji watano ambao umewashtua watu wengi.


5) DOMINIC ADIYIAH, AC MILAN TO KARSIYAKA

Mfungaji wa bao la ushindi katika Kombe la Dunia la Under-20 alitengeneza vichwa vya habari kwa kiwango kikubwa alichokionyesha mpaka kupelekea kusajiliwa katika kikosi cha AC Milan baada ya mashindano hayo. Hatahivyo bado anapigania nafasi katika soka la Italia ambapo uhamisho wa mkopo mara mbili katika klabu ya Serie B Reggina na Partizan ya Serbia haukusaidia kumrudisha katika kiwango chake.

Adiyian (21) aliwasononesha mashabiki wake wengi wa Ghana baada ya kukubali kwenda kwa mkopo kwa mara ya tatu katika klabu ya daraja la pili Karsiyaka ya Uturuki.

4) SAMSON KAYODE, DONG THAP TO ATLETICO MADRID

Uhamisho wake wa kutoka katika ligi ambayo haijulikani ya Vietnam mpaka Spanish La liga lilikuwa ni suala zuri. Wanigeria walishtushwa lakini na wakati huohuo walijivunia mchezaji wao ambaye alikuwa akicheza V-League kwa muda sasa.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 22 alisajiliwa kutoka Dong Thap kwenda Atletico Madrid Agosti mwaka huu na toka kipindi hicho amepelekwa kwa mkopo katika klabu ya Braga ya Ureno. suala hilo ni hatua kubwa mchezaji huyo kama akiongeza bidii.

3) BENNI MCCARTHY, WEST HAM TO ORLANDO PIRATES

 Ni mshambuliaji anayeongoza kwa ufungaji mabao katika timu ya ya Taifa ya Afrika Kusini katika kipindi chote alichochezea ambaye amerudi nyumbani baada ya miaka 13 akiwa katika vilabu vya Ulaya. kama uamuzi ungekuwa ni wa mashabiki wake basi wangependa abakie hukohuko Ulaya.

Hata hivyo mchezaji pekee kutoka Afrika Kusini kushinda medali Uefa Champions League amesema kikubwa ambacho kimechangia kurudi nyumbani ni kuachana na mke wake mpendwa ambaye ni Mhispania na kifo cha baba yake.

2) ASAMOAH GYAN, SUNDERLAND TO AL AIN

Katika jambo lililostusha sio mashabiki wa soka Ghana pekee lakini mashabiki duniani kote ni uhamisho wa mshambuliaji wa Sunderland Gyan kutoka Ulaya mpaka Asia. Mashabiki wa nyumbani bado hawakubaliani na taarifa hiyo na wanajaribu kuelewa sababu za mshambuliaji huyo kama alifurahia kupelekwa kwa mkopo eneo ambalo ni wachezaji wanaokaribia kutundika daruga ndio kimbilio lao. Gyan amewavunja mashabiki wengi moyo hata kama ndio atakuwa mchezaji wa Ghana anayelipwa zaidi inawezakuwatuliza.

1) SAMUEL ETO'O, INTER TO ANZHI MAKHACHKALA

Wakati ilipothibitika kwamba mshambualiji huyu wa Cameroon amehamia Russia mashabiki wengi walishtushwa na kuonekana kutokubaliana na uamuzi wa mchezaji huyo. Mashabiki wengi Afrika walikuwa bado wanataka kumuona kijana wao akiendelea kutesa katika ligi za Ulaya na sio hiyo timu aliyohamia ya Makhachkala mji ambao una watu wasiozidi 600,000.

Pamoja na mkanganyiko huo, wengi wanakubaliana na ukweli kwamba mchezaji huyo ameshashinda kila kitu katika umri wake alionao na hana cha kupoteza kwakuwa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi kwasasa.

13-09-2011 - Borussia Dortmund 1-1 Arsenal All Goals And Highlights (Cha...

Chelsea vs Bayer Leverkusen 2-0 All Goals Full Highlights 13.9.2011 UEFA...

Barcelona 2-2 AC Milan All Goals & Highlights HD 13/09/2011

Tuesday, September 13, 2011

CHAMPIONS LEAGUE: ARSENAL, BARCA ZABANWA CHELSEA MWENDO MDUNDO.











MATOKEO YA MICHEZO ILIYOCHEZWA JUMANNE.



Chelsea 2-0 Leverkusen
Porto 2-1 Shakhtar Donetsk
Genk 0-0 Valencia
Dortmund   1-1 Arsenal
Barcelona    2-2  Milan
Plzeň 1-1 BATE
Olympiacos     0-1 Marseille
APOEL 2-1 Zenit

Sunday, September 11, 2011

HATIMAYE AZAM WAZIACHIA SIMBA NA YANGA KUTUMIA UWANJA WAKE.

DAR ES SALAAM, Tanzania
KWA kutekeleza maagizo ya Serikali kucheza mechi mbili tu za Ligi Kuu ya Vodacom kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam tumefanya marekebisho kwa baadhi ya mechi zilizokuwa zichezwe kwenye uwanja huo.

Sasa mechi zitakazochezwa Uwanja wa Taifa ni mechi namba 39- Azam vs Yanga (Septemba 18), mechi namba 50-Simba vs Mtibwa Sugar (Septemba 25), mechi namba 52-Yanga vs Coastal Union (Septemba 28) na mechi namba 58- Yanga vs Kagera Sugar (Oktoba 13).

Nyingine ni mechi namba 62- Simba vs African Lyon (Oktoba 16), mechi namba 65- Yanga vs Toto Africans (Oktoba 20), mechi namba 72- Simba vs JKT Ruvu (Oktoba 22), mechi namba 78-Yanga vs Simba (Oktoba 29) na mechi namba 86- Moro United vs Simba (Novemba 2).

Mechi zifuatazo zitachezwa Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam; mechi namba 35- Simba vs Polisi Dodoma (Septemba 14), mechi namba 29-African Lyon v Yanga (Septemba 15), mechi namba 45- Yanga vs Villa Squad (Septemba 21), mechi namba 66- Simba vs Ruvu Shooting (Oktoba 19) na mechi namba 71- Yanga vs Oljoro JKT (Oktoba 23).

Uongozi wa Azam unaomiliki uwanja wa Chamazi tayari umekubali timu za Simba na Yanga kutumia uwanja huo kwa mechi hizo.

Saturday, September 10, 2011

MATOKEO YA MECHI ZA JANA LIGI KUU UINGEREZA.

Arsenal 1-0 Swansea City
Everton 2-2 Aston Villa
Manchester City 3-0 Wigan Athletic
Stoke City 1-0 Liverpool
Sunderland 1-2 Chelsea
Wolves 0-2 Tottenham
Bolton 0-5 Man Utd

JULIO AITA 24 UNDER 17.

DAR ES SALAAM, Tanzania
KOCHA msaidizi wa timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, Jamhuri Kihwelo, ameita wachezaji 24 ambao wataingia kambini jumapili kujiandaa na mashindano ya Copa cocacola yatakayo fanyika nchini Brazil hapo baadae.

Julio kabla ya kuwataja wachezaji hao 24 alisema safari ya kwenda Brazil ipo lakini itakuja kuthibitishwa na Cocacola ambao ni wadhamini wa safari hiyo ya mafunzo na mashindano nchini Brazil. Msafara huo utakuwa na watu 18 huku wachezaji wakiwa 16 na viongozi wawili.

Kikosi hicho kinatarajiwa kuanza mazoezi Jumatatu na hapo baadae watachujwa na kubakia 16 watakao safiri. Wachezaji hao ni pamoja na Paulo John (Morogoro), Hamad Hamad (kinondoni), Mohamed H. Mohamed (kinondoni), Peter Manyika (Temeke), Ismail Gambo (Kigoma), Miraji Adam (Morogoro).

Wengine ni Basil Seif (Morogoro), Huseni Twaha (Tanga), James Ambros (Morogoro), Aishi Salum (Morogoro), Hashim Mwalo (kigoma), Mohamed Salum (Zanzibar), Mohamed Kapeta (Dar es salaam), Mbwana Hasani (kinondoni), Salvatory Rafael (kigoma), Paulo James (Shinyanga), Huseni Ibrahim (Morogoro), Gabson Nyamtema (kigoma), Mohamed kapeta (temeke), Joseph Kimwaga (kinondoni).

Thursday, September 8, 2011

YANGA YAKOMALIA JEZI ZA VODACOM MPAKA KIMEELEWEKA LAKINI YAENDELEA KUBURUTA MKIA KATIKA LIGI.

Kikosi kamili cha Yanga wakiwa wamevaa jezi za mdhamini ambazo hazina rangi nyekundu ya kidoti kama ilivyo nembo ya Vodacom ambaye ndiye mdhamini, kikosi hicho jana jioni kilimenyana na Mtibwa Sugar na kutoka 0-0 katika Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro, matokeo hayo inaifanya Yanga iendelee kuburuza mkia wakiwa wameshacheza michezo mitatu na kuambulia pointi mbili na bao moja.

Wednesday, September 7, 2011

BAADA YA MGOMO SASA SERIE A KUANZA KUTIMUA VUMBI IJUMAA.

MILAN, Italia
RAIS wa kamati ya usimamizi wa ligi ya nchini Italia Maurizio Beretta amewaambia waandishi wa habari kwamba ni furaha kubwa sana kwao kumaliza matatizo yaliyokua yanawakabili na sasa wanachosubiri ni kuona ligi inaanza kuchezwa katika viwanja mbali mbali.

Kiongozi huyo amedai kwamba mkataba walioingia na chama cha wachezaji upo wazi kwa kila mmoja wao, na hadhani kama kutakua na malalamiko tena mpaka mwezi June mwaka 2012 ambapo itakua mwisho wa mkataba huo.

Nae Rais wa chama cha wachezaji nchini Italia Damiano Tommasi amesema kama uongozi wa kamati ya kusimamia ligi umedhihirisha wazi makubaliano waliyofikia hakuna haja ya kuzungumza kwa kina zaidi ya kushukuru kwa kila jambo lilivyokua likipangwa katika mikutano yao.

Kumalizika kwa mgomo huo, kunaifanya ligi ya nchini Italia kuanza kuunguruma siku ya ijumaa ambapo mabingwa watetezi AC Milan watafungua kwa kucheza na SS Lazio katika uwanja wa San siro.

Monday, September 5, 2011

GHANA PUNGUFU YALALA KWA BRAZIL 1-0.

TFF YATANGAZA MAPATO KIDUCHU MECHI YA STARS.

DAR ES SALAAM, Tanzania
PAMBANO la mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Algeria (Desert Warriors) limeingiza sh.148,220,000. Mechi hiyo ilichezwa Septemba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mashabiki waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo ni 29,892. Viti vya kijani ambavyo kiingilio kilikuwa sh. 3,000 ndivyo vilivyovutia mashabiki wengi ambapo 17,650 ikiwa ni zaidi ya nusu ya mashabiki wote walinunua tiketi kwa ajili ya viti hivyo.

VIP A ambapo ndipo kulikokuwa na kiingilio cha juu cha sh. 30,000, jumla ya mashabiki 394 walinunua tiketi kwa ajili ya eneo hilo. Viti vya bluu ambapo kiingilio kilikuwa sh. 5,000, mashabiki walionunua tiketi walikuwa ni 8,166.

Viingilio vingine katika pambano hilo vilikuwa sh. 7,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 VIP C na sh. 20,000 VIP B.

TWIGA STARS YAANZA VIBAYA ALL AFRICA GAMES.

MAPUTO, Msumbiji
TIMU ya wanawake ya Taifa ya Tanzania (Twiga Stars) imepoteza mechi yake ya kwanza ya michezo ya All Africa Games (AAG) baada ya leo kufungwa mabao 2-1 na Ghana katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Machava, jijini Maputo.

Kwa mujibu wa Meneja wa Twiga Stars, Furaha Francis hadi mapumziko timu hiyo ilikuwa nyuma kwa bao 1-0. Mwanahamisi Shuruwa aliisawazishia Twiga Stars dakika ya 85, lakini Ghana ikapata bao la pili dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho.

Twiga Stars itacheza mechi yake ya pili Septemba 8 mwaka huu dhidi Afrika Kusini. Mechi ya mwisho katika hatua hiyo ya makundi itakuwa Septemba 11 mwaka huu dhidi ya Zimbabwe.

RONALDO AMVULIA KOFIA MESSI.

MADRID, Hispania
MSHAMBULIAJI wa Real Madrid Cristiano Ronaldo anafikiri kuwa mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi kuwa ndiye mchezaji bora duniani.

Ronaldo (26) aliulizwa kuhusu mawzo yake anamuonaje Muargentina huyo ndivyo akajibu hivyo, lakini aliendelea kusema kuwa mchezaji huyo ni wa aina ya peke yake.

"Ndiye mchezaji bora kwa sasa," alikaririwa Ronaldo kwa mujibu wa gazeti la Sport.

"Ana tabia zake nami nnazo zangu pia. Ana aina ya mchezo wake nami nnao wangu. Pia nacheza klabu kubwa kama yeye. Tuko tofauti kwa kila kitu." alimalizia Ronaldo.

Maelezo yake hayo yamekuja siku chache baada ya mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United kudai kuwa klabu yake ya sasa ya Madrid ndiyo bora duniani kwa sasa.

Lionel Messi - Skills and Goals 2011 - HD

Cristiano Ronaldo - Impossible 2011

MISRI WAVULIWA UBINGWA.

MABINGWA watetezi Misri "The Pharaos" wameutema ubingwa huo baada ya kuchapwa 2-1 ugenini na Sierra Leone, lakini walishaonyesha kukata tamaa kwa sababu ya kuwatumia kikosi cha wachezaji wa umri wa miaka 23 kwenye mchezo huo uliofanyika Freetown.

Cameroon ilitoa namachungu yake kwa kuinyuka Mauritius 6-0, nayo Ivory Coast walitoa salamu za pole kwa majeruhi Didier Drogba baada ya chipukizi Gervinho kuongoza mauaji ya mabao 5-0 dhidi Rwanda.

Mali ikiwa na kiungo wa Barcelona, Seydou Keita wamejiweka vizuri baada ya kushinda 3-0 nyumbani dhidi ya Cape Verde jijini Bamako huku Tunisia ikiweka njia panda baada ya kutoka suruhu na Malawi.

Timu ya Senegal imefuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani shukrani kwa mabao mawili ya Moussa Sow na kuisaidia nchi yake kushinda 2-0 dhidi ya DR Congo, huku Misri ikiaga rasmini baada ya kufungwa 2-1 na Sierra Leone.

Mfungaji bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Ufaransa Ligue 1 alionyesha thamani yake kwenye ardhi ya nyumbani baada ya kupachika mabao hayo mawili katika kipindi cha kwanza na kuamsha shangwe kwenye jiji la Dakar na kuifanya Senegal kuongoza Kundi E.

Wanaungana na Botswana, Burkina Faso na Ivory Coast kuunda timu 16 zitazocheza michuano hiyo pamoja na wenyeji wawili Equatorial Guinea na Gabon.

Burkina Faso ilifuzu hata kabla ya kuanza kwa mpira baada ya Namibia kuichapa Gambia 1-0 jijini Windhoek kwenye mechi iliyochezwa mapema.

Mafanikio ya Burkina Faso na Senegal yalifunika kwa ushindi wa Libya, ikicheza timu mpya chini ya bendera mpya ya taifa walifanikiwa kufufua matumaini yao.

Libya ilifanikiwa kuichapa Msumbiji kwa bao1-0 jijini Cairo katika mechi Kundi C iliyochezwa huku milango ya uwanja ikiwa imefungwa.

MATOKEO YA MICHEZO YA JUMAPILI SEPT 4 2011

Guinea 1–0 Ethiopia
Togo 1–0 Botswana
Angola 2–0 Uganda
Congo 0–1 Sudan
Central African Republic 0–0 Morocco
Burundi 1–1 Benin
Zimbabwe 2–0 Liberia
Comoros 1–2 Zambia

Saturday, September 3, 2011

STARS YATOKA SARE YA 1-1 NA ALGERIA.

Kikosi cha Taifa Stars.

Kikosi cha Algeria.

Mshambuliaji Mbwana Samata akishangilia bao na Dani Mrwanda na Shaaban Nditi mara baada ya kuifungia Stars bao la kuongoza dakika ya 22.

Abdi Kassim akikabiliana na  beki wa Algeria Kassim Zian katika mchezo huo.