Wednesday, September 14, 2011

WACHEZAJI WATANO WA AFRIKA USAJILI WAO ULISTUSHA WATU.

UHAMISHO katika Ligi kubwa barani Ulaya lina umuhimu kwa mashabiki wa Afrika wanaofuatilia ligi hizo kama ilivyo kwa wachezaji wa kiafrika wanaocheza huko.
Katika orodha inayofuata utaona uhamisho wa wachezaji watano ambao umewashtua watu wengi.


5) DOMINIC ADIYIAH, AC MILAN TO KARSIYAKA

Mfungaji wa bao la ushindi katika Kombe la Dunia la Under-20 alitengeneza vichwa vya habari kwa kiwango kikubwa alichokionyesha mpaka kupelekea kusajiliwa katika kikosi cha AC Milan baada ya mashindano hayo. Hatahivyo bado anapigania nafasi katika soka la Italia ambapo uhamisho wa mkopo mara mbili katika klabu ya Serie B Reggina na Partizan ya Serbia haukusaidia kumrudisha katika kiwango chake.

Adiyian (21) aliwasononesha mashabiki wake wengi wa Ghana baada ya kukubali kwenda kwa mkopo kwa mara ya tatu katika klabu ya daraja la pili Karsiyaka ya Uturuki.

4) SAMSON KAYODE, DONG THAP TO ATLETICO MADRID

Uhamisho wake wa kutoka katika ligi ambayo haijulikani ya Vietnam mpaka Spanish La liga lilikuwa ni suala zuri. Wanigeria walishtushwa lakini na wakati huohuo walijivunia mchezaji wao ambaye alikuwa akicheza V-League kwa muda sasa.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 22 alisajiliwa kutoka Dong Thap kwenda Atletico Madrid Agosti mwaka huu na toka kipindi hicho amepelekwa kwa mkopo katika klabu ya Braga ya Ureno. suala hilo ni hatua kubwa mchezaji huyo kama akiongeza bidii.

3) BENNI MCCARTHY, WEST HAM TO ORLANDO PIRATES

 Ni mshambuliaji anayeongoza kwa ufungaji mabao katika timu ya ya Taifa ya Afrika Kusini katika kipindi chote alichochezea ambaye amerudi nyumbani baada ya miaka 13 akiwa katika vilabu vya Ulaya. kama uamuzi ungekuwa ni wa mashabiki wake basi wangependa abakie hukohuko Ulaya.

Hata hivyo mchezaji pekee kutoka Afrika Kusini kushinda medali Uefa Champions League amesema kikubwa ambacho kimechangia kurudi nyumbani ni kuachana na mke wake mpendwa ambaye ni Mhispania na kifo cha baba yake.

2) ASAMOAH GYAN, SUNDERLAND TO AL AIN

Katika jambo lililostusha sio mashabiki wa soka Ghana pekee lakini mashabiki duniani kote ni uhamisho wa mshambuliaji wa Sunderland Gyan kutoka Ulaya mpaka Asia. Mashabiki wa nyumbani bado hawakubaliani na taarifa hiyo na wanajaribu kuelewa sababu za mshambuliaji huyo kama alifurahia kupelekwa kwa mkopo eneo ambalo ni wachezaji wanaokaribia kutundika daruga ndio kimbilio lao. Gyan amewavunja mashabiki wengi moyo hata kama ndio atakuwa mchezaji wa Ghana anayelipwa zaidi inawezakuwatuliza.

1) SAMUEL ETO'O, INTER TO ANZHI MAKHACHKALA

Wakati ilipothibitika kwamba mshambualiji huyu wa Cameroon amehamia Russia mashabiki wengi walishtushwa na kuonekana kutokubaliana na uamuzi wa mchezaji huyo. Mashabiki wengi Afrika walikuwa bado wanataka kumuona kijana wao akiendelea kutesa katika ligi za Ulaya na sio hiyo timu aliyohamia ya Makhachkala mji ambao una watu wasiozidi 600,000.

Pamoja na mkanganyiko huo, wengi wanakubaliana na ukweli kwamba mchezaji huyo ameshashinda kila kitu katika umri wake alionao na hana cha kupoteza kwakuwa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi kwasasa.

No comments:

Post a Comment