Wednesday, December 21, 2011

SPAIN LEAD RANKINGS FOR FOURTH YEAR, TANZANIA YAPOROMOKA NAFASI MOJA.ZAIDI.

Fifa rankings for December (November position in parentheses):

1. Spain (1).
2. Netherlands (2).
3. Germany (3).
4. Uruguay (4).
5. England (5).
6. Brazil (6).
7. Portugal (7).
8. Croatia (8).
9. Italy (9).
10. Argentina (10).
11. Denmark (11).
12. Russia (12).
13. Chile (13).
14. Greece (14).
15. France (15).
16. Ivory Coast (16).
17. Switzerland (17).
18. Sweden (18).
19. Japan (19).
20. Bosnia-Herzegovina (23).

CAF RANKINGS

(Africa ranking, world ranking)

Ivory Coast 1, 16
Ghana 2, 29
Algeria 3, 30
Egypt 4, 31
Nigeria 5, 43
Senegal 6, 44
Cameroon 7, 50
South Africa 8, 52
Cape Verde Islands 9, 58
Tunisia 10, 59
Sierra Leone 11, 60
Morocco 12, 61
Burkina Faso 13, 62
Libya 14, 63
Mali 15, 67
Gabon 16, 77
Zambia 17, 79
Guinea 18, 80
Angola 19, 83
Uganda 20, 89
Malawi 21, 94
Botswana 22, 95
Niger 23, 97
Zimbabwe 24, 98
Togo 25, 101
Mozambique 26, 105
Rwanda 27, 106
Sudan 28, 113
Gambia 29, 116
Kenya 30, 120
Namibia 31, 121
Liberia 32, 123
Benin 33, 124
Democratic Republic of Congo 34, 125
Central African Republic 35, 129
Congo Brazzaville 36, 133
Ethiopia 37, 135
Tanzania 38, 137
Burundi 39, 140
Chad 40, 143
Lesotho 41, 147
Equatorial Guinea 42, 150
Madagascar 43, 160
Guinea Bissau 44, 163
Swaziland 45, 180
Comoros Islands 46, 187
Seychelles 47, 188
Somalia 48, 189
Eritrea 49, 190
Mauritius 50, 194
Sao Tome e Príncipe 51, 196
Djibouti 52, 198
Mauritania 53, 204

Monday, December 19, 2011

NADAL AUZA HISA ZAKE ZA MALLORCA.

MCHEZA tenisi anayeshika namba mbili dunia katika orodha ya viwango vya ubora Rafael Nadal pamoja na mjomba wake Miguel Angel Nadal wameuza asilimia 10 za hisa zao walizokuwa wakimiliki katika klabu ya Real Mallorca. Katika taarifa iliyotumwa na mtandao wa klabu hiyo hisa hizo zimenunuliwa mfanyabiashara wa Ujerumani Utz Claassen ambaye ameongoza hisa zake na kufikia asilimia 20. Nadal shabiki wa kutupwa wa klabu ya Real Madrid ambaye anaishi katika visiwa vya Mediterranean alijiunga katika kinyang’anyiro cha kununua hisa hizo mwaka 2010 wakati timu hiyo ilipokuwa katika wakati mgumu kiuchumi. Sababu kubwa ya Nadal na mjomba wake ambaye aliwahi kuwa beki wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania ni kutofurahishwa na uongozi wa klabu ya Mallorca unavyofanya maamuzi yake.

ETO'O AGOMA KUKATA RUFANI KUPINGA ADHABU YAKE.

Nahodha wa timu ya taifa ya Cameroon Samuel Eto’o amesema hatarajii kukata rufani juu ya adhabu aliyopewa na Shirikisho la Soka la nchi hiyo-Fecafoot la kumfungia kucheza mechi 15 za timu hiyo. Mwanasheria wa Eto’o Barrister Gabriel ambaye pia anamwakilisha mchezaji mwenzie Eyong Enoh katika kesi hiyo ya Kamati ya Nidhamu ya Fecafoot amesema kwa niaba ya mteja wake kuwa alipewa maelekezo na Eto’o kuwa asikate rufani juu ya adhabu hiyo aliyopewa. Gabriel aliendelea kusema kuwa Fecafoot walitakiwa wafikirie kwanza kabla ya kutoa adhabu hiyo kwani haikuwa na maana yoyote kumpa adhabu kubwa kama hiyo wakati mchezaji mwenyewe alikuwa akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake. Kabla ya kusikilizwa kwa kesi hiyo Eto’o alitishia kumshitaki Makamu wa Rais wa Fecafoot Francis Mveng na pia alipokea kauli zisizo za kiungwana kutoka kwa viongozi wa shirikisho hilo ambapo toka aongoze mgomo huo amekuwa na maelewano yasio mazuri.

RAIS WA SEVILLA KWENDA JELA MIAKA SABA.

RAIS wa klabu ya Sevilla Jose Maria del Nido amehukumiwa miaka saba na nusu jela kufuatia kukutwa na hatia ya makosa ya rushwa katika mahakama ya Malaga nchini Hispania. Kesi hiyo ambayo haihusiana na klabu Sevilla imemkumba Del Nido akiwa kama mshauri wa kisheria wa Baraza katika mji wa Marbela akiwa na wenzake 16 katika kesi hiyo. Del Nido mweye miaka 54 aliteuliwa kushika wadhifa huo wa kuwa mshauri wa kisheria wa baraza hilo na aliyekuwa Rais wa klabu Atletico Madrid ambaye pia alikuwa meya wa mji wa Marbella. Del Nido ameiongoza klabu ya Sevilla kwa mafanikio toka mwaka 2002 ambapo amefanikiwa kushinda Kombe la Uefa mwaka 2006 na 2007, kombe la mfalme mwaka 2007 na 2010 pamoja na kuwa washiriki wa michuano ya Ligi ya Ulaya katika kipindi chote cha uongozi wake.

ANZHI YASAKA KOCHA MPYA.

KLABU ya Anzhi Makhachkala ya Urusi inatarajia kuteua kocha mpya atakayeinoa klabu hiyo ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Akizungumza na mtandao wa klabu hiyo Mkurugenzi Mkuu aliyeteuliwa hivi karibuni Alan Soziyev amesema anawaomba mashabiki wa klabu hiyo kuwa wavumilivu kwani wako katika mchakato wa kuteua kocha mpya. Uteuzi wa Soziyev ni sehemu ya mabadiliko ya klabu hiyo ambayo inataka kupanga upya safu ya uongozi itakayoipa mafanikio klabu hiyo. Klabu hiyo hiyo inayomilikiwa na bilionea wa Urusi Suleman Kerimov imekuwa ikitajwa kuwanyemelea makocha wakubwa barani Ulaya wakiwemo Fabio Capello anayeinoa Uingereza kwasasa, meneja wa Real Madrid Jose Mourinho na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Urusi Guus Hiddink.

Friday, December 16, 2011

UEFA CHAMPIONS LEAGUE DRAW.

Lyon v APOEL
Napoli v Chelsea
AC Milan v Arsenal
FC Basle v Bayern Munich
Bayer Leverkusen v Barcelona
CSKA Moscow v Real Madrid
Zenit St Petersburg v Benfica
Marseille v Inter Milan

Group stage runners-up listed first and will play first legs at home.

First legs to be played February 14/15 and 21/22, second legs March 6/7 and 13/14.

EUROPA LEAGUE DRAW.

FC Porto v Manchester City
Ajax Amsterdam v Manchester United
Lokomotiv Moscow v Athletic Bilbao
FC Salzburg v Metalist Kharkiv
Stoke City v Valencia
Rubin Kazan v Olympiacos
AZ Alkmaar v Anderlecht
Lazio v Atletico Madrid
Steaua Bucuresti v FC Twente
Viktoria Plzen v Schalke
Wisla Krakow v Standard Liege
SC Braga v Besiktas
Udinese v PAOK
Trabzonspor v PSV Eindhoven
Hannover 96 v Brugge
Legia Warszawa v Sporting Club

LAST 16 DRAW

FC Salzburg/Metalist Kharkiv v Rubin Kazan v Olympiacos
Legia Warszawa/Sporting Club v FC Porto/Manchester City
Steaua Bucuresti/FC Twente v Viktoria Plzen/Schalke
AZ Alkmaar/Anderlecht v Udinese/PAOK
Stoke City/Valencia v Trabzonspor/PSV Eindhoven
Ajax Amsterdam/Manchester United v Lokomotiv Moscow/Athletic Bilbao
Steaua Bucuresti /FC Twente v Viktoria Plzen/Schalke
Wisla Krakow/Standard Liege v Hannover 96/Brugge

SENEGAL KUJIPIMA NGUVU NA SUDAN NA TUNISIA.

TIMU ya Taifa ya Senegal inatarajiwa kucheza michezo yake ya kimataifa kirafiki na timu za Sudan na Tunisia ikiwa ni maandalizi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayotarajiwa kufanyika mapema mwakani. Senegal ambao mwezi Agosti mwaka huu ililala mabao 2-0 dhidi ya Morocco katika mchezo wa kirafiki itakuwa imepania kulipiza kisasi wakati watakapokutana na Tunisia ambao wanatoka ukanda mmoja wa Afrika ya Kaskazini na Morocco wakati timu zitapokutana jijini Dakar Januari 14. Kabla ya kumenyana na Tunisia timu hiyo kwanza itacheza na Sudan Januari 12 hapohapo jijini Dakar ambapo kocha wa timu hiyo Amara Traore amedai michezo hiyo itakuwa ni kipimo tosha kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Afrika Januari 22. Hata hivyo kikosi hicho kinaweza kuingia matatizoni baada ya Traore kukataa kuongeza mkataba ambao unakaribia kuisha akidai nyongeza ya mshahara ya Dola 24,000 kwa mwezi.

DONOVAN KUREJEA EVERTON JANUARI.

Timu ya Everton imefikia makubaliano ya kumchukua kwa mkopo mshambuliaji wa Los Angeles Galaxy London Donovan na kumrudisha tena Goodison Park mkopo ambao utakuwa wa muda mfupi. Meneja wa Everton David Moyes amesema amefurahishwa kuweza kumpata mchezaji huyo kwani atawasaidia katika kipindi cha mwezi Januari na Februari mwakani kwani alifanya vizuri wakati alipoichezea timu hiyo miaka miwili iliyopita. Donovan anatarajiwa kuwemo katika kikosi cha Everton kitakachoivaa Bolton katika mchezo wa ligi utakaochezwa Januari 4 mwakani ambapo mkataba wake unatarajiwa kuisha baada ya mchezo wa baina ya timu hiyo na mahasimu wao Liverpool Februari 25. Akihojiwa na tovuti ya klabu hiyo Donovan mwenye umri wa miaka 29 amesema ni nafasi ya kipekee kwake kurudi tena na kuichezea klabu hiyo inayoheshimika na yenye meneja ambaye amenisaidia kwa namna moja au nyingine kunifanya niwe mchezaji niliyekamilika.

Thursday, December 15, 2011

BARCELONA YAIADHIBU AL SADD 4-0.

TIMU ya Barcelona imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya Klabu bingwa ya Dunia baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya Al Sadd ya Qatar kwa mabao 4-0 katika mchezo uliofanyika jijini Tokyo, Japan. Mabao mawili ya Barcelona yalifungwa na mchezaji Adriano katika dakika ya 25 akimalizia mpira baada ya kipa wa Al Sadd kushindwa kuondoa hatari langoni mwao huku la pili akifunga kwa shuti kali nje kidogo ya eneo la hatari dakika ya 43 na kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza. Mabao mengine ya Barcelona yalifungwa na Seydou Keita dakika ya 64 akimalizia pasi murua iliyopigwa na Lionel Messi na bao la mwisho la Barcelona lilifungwa na Maxwell Cabelino dakika ya 81 na kuipeleka Barcelona fainali. Kilele cha michuano hiyo kitafikia Jumapili kwa mchezo wa fainali utakaozikutanisha timu za Barcelona na Santos ya Brazil mchezo ambao utafanyika jijini Yokohama, Japan

TEVEZ ATAKA KUHAMIA BOCA JUNIORS.

MSHAMBULIAJI wa Manchester City Carlos Tevez amedai kuwa hahitaji kurejea katika Ligi Kuu nchini Uingereza na anachotaka yeye ni kujiunga na klabu yake ya utotoni ya Boca Juniors. Tevez mwenye umri wa miaka 27 amekuwa nje ya mipango ya meneja wa City Roberto Mancini msimu huu na hajajumuishwa katika kikosi cha timu hiyo toka akatae kuingia kama mchezaji wa akiba katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich mwezi Septemba. Timu za AC Milan, Paris Saint-Germain na Corinthians ya Brazil zimekuwa zikimnyemelea mshambuliaji huyo lakini mwenyewe amesema hana mpango wa kujiunga na klabu yoyote zaidi ya Boca Juniors. Tevez amesema kuwa hajali kama atakatwa mshahara wake na kwamba amechoka kusafiri mara kwa mara hivyo hatarudi tena Uingereza na anahitaji kuanza msimu na kucheza michuano ya Klabu Bingwa ya Amerika Kusini maarufu kama Copa Libertadores akiwa na Boca Juniors.

COLOMBIA YAMTIMUA KOCHA WAKE.

SHIRIKISHO la Soka la Colombia-FCF limesitisha mkataba wa aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Lionel Alvarez. Taarifa ya FCF iliyotolewa na rais wake Luis Bedoya imefafanua kuwa wajumbe wa kamati ya shirikisho hilo hawakuwa na imani na kocha huyo kwamba ana uwezo wa kuiwezesha timu hiyo kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014. Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa wajumbe wa kamati hiyo wameamua kusitisha mkataba wa Alvarez na sasa wanahitaji kuchukua hatua za haraka ili kuziba pengo la kocha huyo ili timu hiyo iweze kushiriki vyema michezo ya kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil 2014. Toka Alvarez achukue mikoba ya kukinoa kikosi hicho Septemba mwaka huu timu hiyo imeshinda mchezo mmoja dhidi ya Bolivia, imetoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Venezuela na kufungwa na Argentina mabao 2-1.

KESI YA SUAREZ KUMALIZWA KISIKILIZWA IJUMAA.

KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka la Uingereza-FA imeanza kusikiliza mashitaka ya kibaguzi yanayomkabili mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez dhidi ya beki wa Manchester United Patrice Evra. Evra alifikisha mashtaka hayo akidai Suarez kumtolea kauli za kibaguzi mwezi Octoba mwaka wakati timu hizo zilipokutana na kutoa sare ya bao 1-1. Baada ya uchunguzi wa tukio hilo kufanyika FA imeamua kumshtaki Suarez kwa kutumia lugha ya kudhalilisha na kibaguzi dhidi ya beki huyo tegemeo wa Manchester United. Suarez mwenye umri wa miaka 24 amekana tuhuma hizo na amekuwa akisaidiwa na timu yake ya Liverpool muda wote wa uchunguzi huku mwisho wa kusikilizwa mashtaka hayo unatarajiwa kuwa mwishoni mwa wiki hii.

Wednesday, December 14, 2011

SANTOS YATINGA FAINALI MICHUANO YA KLABU BINGWA YA DUNIA.

BECKENBAUER AUKANDIA MFUMO WA GOAL-LINE TECHNOLOGY.

MCHEZAJI nguli wa zamani wa Ujerumani Franz Beckenbauer amesema hafurahishwi na utumiaji wa mfumo wa teknologia ya kompyuta katika mstari wa goli. Kauli wa nyota huyo wa zamani imekuja kufuatia Rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kudai kuwa mfumo huo umeonyesha mafanikio katika majaribio yake na unaweza kuanza kutumika katika Kombe la Dunia mwaka 2014 litalofanyika nchini Brazil. Beckenbauer mwenye umri wa miaka 66 hivi sasa amesema kuwa mchezo wa mpira ni mchezo wa kawaida wenye sheria nyepesi na unatakiwa ubaki hivyo. Mchezaji huyo wa zamani ambaye sasa ni rais wa klabu ya Bayern Munich amesema ni bora kutumika waamuzi wa nyongeza kuliko mfumo huo wa kompyuta. Beckenbauer ambaye amewahi kushinda Kombe la Dunia akiwa kama mchezaji na pia kama kocha amefafanua kuwa waamuzi wa ziada wanaweza kufanya kazi zaidi ya mfumo huo wa kompyuta ambao utakuwa ukifanya kazi moja tu kuangalia mpira kama umevuka goli wa la.

AS MONACO YANUNULIWA NA BILIONEA WA URUSI.

Rais wa klabu ya AS Monaco ya Ufaransa Etienne Franzi amedai kuwa klabu hiyo itamilikiwa na mfanyabiashara wa Urusi Dmitry Rybolovlev mwishoni mwa mwaka huu. Franzi amesema kila kitu kuhusu umilikishwaji wa klabu hiyo kitajulikana mwishoni mwa mwaka huu na kudai kuwa hizo ni habari njema kwa klabu hiyo na soka la Ufaransa kwa ujumla. Bilionea huyo ambaye kwa mujibu wa orodha ya mabilionea inayotolewa na gazeti maarufu la Forbes anashika namba 93 kwa utajiri duniani mwaka 2010 aliuza hisa zake kwa kampuni ya uzalishaji wa mbolea zinafikia kiasi cha dola bilioni 6.5. Monaco ambao ni mabingwa mara saba wa Ligi Kuu ya Ufaransa huku wakiwa wamefika hatua ya fainali katika michuano ya Klabu ya Bingwa ya Ulaya mwaka 2004 waliteremka daraja mwishoni mwa msimu uliopita na hivi sasa bado wanasuasua katika ligi daraja pili baada ya kucheza michezo 16 na kushinda mmoja tu.

ETO'O NA WENZIE KUFUNGIWA MECHI SABA NA FECAFOOT.

KAMATI ya nidhamu ya Shirikisho la Soka la Cameroon-Fecafoot huenda ikawafungia michezo saba wachezaji wake Samuel Eto’o, Eyong Enoh na Benoit Assou kwa makosa tofauti yanayowakabili. Eto’o na Enoh wao wanaweza kupewa adhabu hiyo kwa kuchochea mgomo katika kikosi cha timu ya taifa cha nchi hiyo wakati Assou yeye anaweza kufungiwa kwa kukataa mara kadhaa kukitumikia kikosi cha nchi yake. Kamati hiyo ilitarajiwa kufanya kikao chake Jumatatu jijini Younde ambacho kilihudhuriwa na Eto’o Makamu wa Rais wa Fecafoot Francis Mveng kocha wa kikosi hicho Denis Lavagne na msaidizi wake Ntoungou Mpile. Eyong hakuwepo wakati wa usikilizaji wa kesi hiyo lakini aliwakilishwa na wakili wake huku Assou pamoja na barua waliyompa kuhudhuria kesi yake yeye hakuwepo kabisa na hakutuma mwakilishi yoyote.

KOCHA WA AL SADD AOMBA KUCHEZESHA WACHEZAJI 16 DHIDI YA BARCA.

KLABU ya Al Sadd ya Qatar imelitaka Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA kuwaruhusu kuchezesha wachezaji 16 wakati watakapokutana na mabingwa wa Ulaya Barcelona Alhamisi hii katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia. Akihojiwa kuhusiana na mchezo huo kocha wa timu hiyo raia wa Uruguay Jorge Fossati amesema mikakati yake kama watakubaliwa kuchezesha wachezaji 15 au 16 uwanjani anafikiri wanaweza kuwa na nafasi ya kuwafunga Barcelona. Nae Nahodha wa Al Sadd Abdulla Koni amesema kama Real Madrid ambao nao wanawachezaji nyota duniani wameshindwa kuwafunga Barcelona haoni kama wao wanaweza kufanya hivyo. Fainali ya ,michuano hiyo ambayo timu za Barcelona na Santos zinatabiriwa kukutana inatarajiwa kuchezwa Jumapili jijini Yokohama.

Tuesday, December 13, 2011

CECAFA YAINGIZA MILIONI 267 KATIKA MICHUANO YA CHALLENGE 2011.

Mechi 26 za michuano ya 35 ya CECAFA Tusker Challenge Cup iliyofanyika Dar es Salaam kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10 mwaka huu zimeingiza sh. 267,066,000. Michuano hiyo iliyoandaliwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ilishirikisha timu za mataifa 12. Hatua ya makundi ya michuano hiyo iliingiza sh. 145,613,000, robo fainali (sh. 58,470,000), nusu fainali (sh. 55,787,000) wakati fainali iliingiza sh. 17,196,000. Kila siku zilichezwa mechi mbili isipokuwa Novemba 26 mwaka huu ambapo ilikuwa siku rasmi ya ufunguzi na Novemba 28 mwaka huu zilichezwa mechi tatu. Mechi iliyoingiza fedha nyingi kuliko zote ilikuwa ya ufunguzi hatua ya makundi kati ya Tanzania na Rwanda ambapo zilipatikana sh. 64,178,000 wakati fedha kidogo (sh. 446,000) zilipatikana kwenye mechi kati ya Uganda na Somalia iliyochezwa Novemba 28 mwaka huu Uwanja wa Azam. Jumla ya washabiki walioshuhudia michuano hiyo walikuwa 103,312. Washabiki walioshuhudia hatua ya makundi walikuwa 65,617, robo fainali (17,844), nusu fainali (16,014) wakati fainali walikuwa 4,837. Mechi iliyokuwa na washabiki wengi zaidi ni kati ya Tanzania na Rwanda ambapo waliingia 23,946 wakati iliyoingiza wachache ni 446 walioshuhudia mechi kati ya Somalia na Uganda. Tunawashukuru wadhamini wakuu Tusker na washabiki waliojitokeza kushuhudia michuano hiyo. Vilevile Kampuni ya mafuta ya Gapco, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na PSPF, na pia wadau wengine waliofanikisha mashindano hayo kwa njia mbalimbali akiwemo Zacharia Hanspope.

MTUKUTU DIOUF AWINDWA NA ANZHI MAKHACHKALA.

MSHINDI mara mbili wa tuzo za Mchezaji bora wa Afrika na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Senegal El Hadji Diouf ametajwa kama mmoja wa wachezaji wanaowindwa na klabu tajiri ya Anzhi Makhachkala. Diouf ambaye kwasasa anakipiga katika klabu ya daraja la kwanza nchini Uingereza ya Doncaster Rovers mkataba ambao utaisha Januari mwakani amesema mazungumzo kuhusu uhamisho wake yameshaanza ingawa hakuna makubaliano yoyote waliyofikia. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amesema kuwa kucheza pamoja na Samuel Eto’o itakuwa ni heshima kubwa kwake lakini akasema kuwa hilo ni suala la kushauriana na familia yake kwanza kabla ya kufanya uamuzi wowote. Diouf ambaye alifungiwa kuichezea timu ya taifa ya Senegal kwa miaka mitano anaweza kupunguziwa adhabu hiyo baada ya kukubali kuhudhuria kesi yake itakayosikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka nchini Senegal amedai pia kuwindwa na klabu nyingine nchini Urusi pamoja na Los Angeles Galaxy.

IVORY COAST KUWEKA KAMBI DUBAI.

TIMU ya Taifa ya Ivory Coast inatarajiwa kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika jijini Dubai. Kikosi hicho ambacho kinajulikana kwa jina la utani la Tembo kimepania kujiandaa vyema kwa ajili ya kunyakuwa taji la michuano hiyo ambalo litakuwa la pili kwao, kitaelekea katika jiji hilo mwishoni mwa mwezi Desemba. Tembo hao wakiwa Dubai kwa ajili ya maandalizi kikosi hicho kinatarajiwa kucheza michezo ya kirafiki na timu kubwa za taifa ingawa kocha wa timu hiyo Francois Zahoui hakutaja ni timu gani kwasababu taratibu za kutafuta timu hizo bado zinaendelea. Ivory Coast imepangwa kundi B katika michuano hiyo ikiwa na timu za Sudan, Burkina Faso na Angola ambapo katika mchezo wake wa kwanza itacheza na Sudan Januari 22 katika Uwanja wa Nuevo ulipo jijini Malabo nchini Equatorial Guinea.

VAN PERSIE KUINGOZA ARSENAL KATIKA ZIARA YA KIHISTORIA NCHINI NIGERIA.

NAHODHA wa timu ya Arsenal Robin Van Persie anatarajiwa kukiongoza kikosi hicho katika ziara ya kimichezo nchini Nigeria mara baada ya kumalizika kwa msimu huu wa Ligi Kuu nchini Uingereza. Wachezaji wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo wanatarajiwa kufanya ziara nchini humo mwaka ujao ambapo mbali ya Van Persie pia watakuwa na nyota wao kama Theo Walcott, Alex Song, Gervinho, Thomas Vermaelen, Per Mertesacker, Mikel Arteta na Andre Arshavin.
Arsenal ilithibitisha ziara yake hiyo kupitia kwa Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Angus Kinnear kuwa timu hiyo itafanya ziara jijini Abuja baada ya kukagua na kuridhishwa na Uwanja wa Taifa uliopo katika mji huo mkuu. Kinnear ambaye alifunga safari hiyo akiwa na ofisa mwenzake Paul Johnson amesema amefurahishwa na mapokezi aliyopata na anaamini kuwa nyota wake watapata mapokezi kama hayo ambapo pia alifurahishwa na idadi ya mashabiki wa klabu aliyoiona ambayo inakadiriwa kufikia milioni mbili.

CELTIC YATOZWA FAINI KWA USHANGILIAJI HARAMU.

SHIRIKISHO la Soka la Ulaya-UEFA limeitoza klabu ya Celtic faini ya Euro 15,000 kufuatia ushangiliaji haramu uliofanywa na mashabiki wa timu hiyo mwezi uliopita katika mchezo wa Ligi ya Ulaya dhidi ya Rennes. Klabu hiyo ilithibitisha kupokea barua ya faini ikiwa haina maelezo mengine ambapo wamesema kwasasa wanajipanga kuangalia kama walipe faini hiyo au wakate rufani kupunguziwa adhabu hiyo. Jopo la maofisa wa Kamati ya Nidhamu ya UEFA ilifikia maamuzi hayo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mapolisi waliokuwa wakisimamia mchezo huo uliochezwa Novemba 3. Tabia hiyo ya ushangiliaji uliokatazwa wa mashabiki wa Celtic umeonekana kuwa sugu ambapo mapema mwezi huu timu hiyo iliepuka kupewa adhabu kwa matatizo kama hayo katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Scotland ambao uliisha kwa sare ya bila ya kufungana dhidi ya timu ya Hibernian.

ARSENAL KUKOSA HUDUMA YA SANTOS MWA MIEZI 3.

BEKI wa Arsenal Andre Santos anatarajiwa kukaa nje uwanja kwa muda wa miezi mitatu kwasababu ya kuumia kifundo cha mguu. Santos anayecheza kama beki wa kushoto alipata majeraha hayo wiki iliyopita katika mchezo dhidi ya Olympiakos uliochezwa nchini Ugiriki ambapo Arsenal walipoteza mchezo huo na sasa beki huyo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji nchini Brazil baadae wiki hii. Katika taarifa iliyotolewa katika tovuti ya klabu hiyo imethibitisha kuwa ni kweli mchezaji huyo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wiki hii na atakuwa nje ya uwanja katika kipindi kinachokadiriwa kuwa cha miezi tatu ambapo kila mmoja katika klabu hiyo anamtakia mchezaji huyo kupona haraka. Santos mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na klabu hiyo mwezi Agosti mwaka huu akiwa ameichezea timu hiyo michezo 14 na kufunga mabao mawili.

Monday, December 12, 2011

CHELSEA YAKATA NGEBE ZA MAN CITY.

Wachezaji wa Chelsea wakishangilia bao la kusawazisha dhidi ya Manchester City.
TIMU ya Chelsea imefanikiwa kumaliza ubabe wa Manchester City wa kutofungwa katika Ligi Kuu nchini Uingereza baada ya kufanikiwa kuifunga timu hiyo mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Stamford Bridge. Chelsea ambao sasa wamerudi katika mbio za kusaka ubingwa wa ligi hiyo ilibidi wafanye kazi ya ziada baada ya mshambuliaji wa City Mario Balotelli kuipatia timu yake bao la kuongaza ikiwa ni dakika mbili toka mpira uanze. Bao halikuonyesha kuwakatisha tamaa Chelsea ambao walionyesha kutulia katika mchezo huo kusaka bao la kusawazisha na juhudi zao hizo zilizaa matunda dakika ya 34 ambapo mchezaji Raul Meireles aliisawazishia bao timu yake akimalizia pasi murua iliyopigwa na Bosingwa na kuzifanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu. 
Kadi nyekundu aliyopewa Gael Clichy.
Kipindi cha pili hakikwenda vizuri kwa upande wa City baada ya beki wake Gael Clichy kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi ya pili ya njano na kulazimika kucheza karibu dakika 30 zilizobakia wakiwa pungufu. Chelsea walitumia vyema mapungufu hayo na kuongeza kasi ya mashambulizi katika lango la City na juhudi zao hizo zilizaa matunda dakika nane kabla ya mpira kumalizika kwa kuzawadiwa penati iliyofungwa na Frank Lampard kufuatia beki wa City Joleon Lescott kuunawa mpira katika eneo la hatari.

Sunday, December 11, 2011

GABON YATWAA TAJI LA VIJANA CHINI YA MIAKA 23.

TIMU ya taifa chini ya miaka 23 ya Gabon imeshinda taji lake la kwanza barani Afrika baada ya kufanikiwa kuifunga Morocco katika mchezo wa fainali ya michuano ya vijana ya umri huo uliofanyika jijini Marrakech, Morocco. Timu zote mbili zilishakata tiketi ya kucheza michuano ya Olimpiki itakayofanyika mwakani jijini London hivyo mchezo huo ulikuwa kwa ajili ya taji hilo la ubingwa wa vijana chini ya miaka 23. Misri nao walikata tiketi ya kucheza michuano ya Olimpiki baada ya kufanikiwa kuifunga Senegal kwa mabao 2-0 katika mchezo wa mtoano wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo. Pamoja na kupoteza mchezo huo Senegal ambao wanashika nafasi ya nne watalazimika kucheza hatua ya mtoano na mshindi wanne wa michuano kama hiyo kutoka bara ya Asia ili waweze kufuzu michuano ya Olimpiki.

GHANA KUANDAA GLO-CAF AWARDS.

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limethibitisha nchi ya Ghana kuandaa tuzo za Mwanasoka Bora wa Afrika kwa mwaka huu. Jiji la Accra ndio watakuwa wenyeji wa shughuli hiyo inayotarajiwa kufanyika Desemba 22 mwaka huu ambapo mbali na tuzo ya mwanasoka bora pia zitatolewa tuzo mbalimbali kwa wanamichezo waliofanya vizuri kwa mwaka huu. Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa nchi hiyo kuandaa tafrija hiyo ambapo kwa mara ya kwanza walikuwa wenyeji wa sherehe hizo mwaka 2007 na 2009. Shirikisho la Soka nchini Ghana-GFA limefurahishwa na uteuzi huo na kdai ni heshima kubwa kwao kuandaa tafrija hiyo ambayo inatoa heshima kwa wanasoka waliofanya vizuri katika ligi mbalimbali Afrika na Duniani kwa ujumla.

SAFARI YA CHINA YANUKIA KWA ANELKA.

KLABU ya Shanghai Shenhua inayoshiriki Ligi Kuu nchini China imethibitisha Jumapili kuwa wamefikia makubaliano kuhusu mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Nicolas Anelka. Msemaji wa timu ya Shanghai Ma Yue amesema kuwa wamefikiwa makubaliano juu ya mkataba wa mchezaji huyo na wanachosubiri ni yeye kutia saini na kuwa mchezaji rasmi wa klabu hiyo. Meneja wa Chelsea Andre-Villas Boas amekuwa katika katika mkakati mzito wa kukitengeneza upya kikosi cha Chelsea na tayari kuna baadhi ya nyota wa timu hiyo amewaweka sokoni ili aweze pata fedha za kukiimarisha kikosi hicho. Anelka katika kipindi cha hivi karibuni amekuwa akisumbuliwa na majeruhi kwa muda mrefu hivyo kusababisha kutokuwemo katika mipango ya kocha huyo ambaye anaonekana kuhitaji damu changa zaidi.

Friday, December 9, 2011

EL CLASICO: HAPATOSHI LA LIGA LEO.

Timu ya Real Madrid leo itawakaribisha mahasimu wao Barcelona katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania unaotarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Santiago Bernabeu. Madrid ambao wanaongoza ligi hiyo kwasasa wakiwa na tofauti ya alama tatu nyuma ya Barcelona wataingia uwanjani huku wakiwa na kiu kubwa ya ushindi ili kuzidi kujizatiti kileleni na kuweka matumaini hai ya kunyakuwa ubingwa wa ligi hiyo ambao wameukosa kwa muda wa miaka mitatu sasa. Barcelona ambao msimu huu wamekuwa na rekodi isiyo ya kuridhisha katika michezo yao ya ugenini itakuwa na kibarua kigumu katika mchezo huo na Madrid ambayo wameonyesha kuwa katika kiwango bora msimu huu. Pamoja na rekodi hiyo Barcelona toka kuwasili meneja wake Pep Guardiola mwaka 2008 timu hiyo hiyo imekuwa mwiba mchungu kwa mahasimu wao Madrid kwa kuibuka kidedea katika michezo yao ilizozikutanisha timu hizo.

MSENEGAL N'DOAYE AWA MCHEZAJI BORA DENMARK.

MCHEZAJI wa Kimataifa kutoka Senegal Dame N’Doye ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Denmark na Shirikisho la Soka la nchi hiyo. Mshambuliaji mwenye miaka 26 anayekipiga katika klabu ya FC Copenhagen amekuwa katika kiwango bora msimu wa 2010-2011 baada ya kufunga mabao 25 katika michezo 31 aliyocheza na kuiwezesha timu yake kunyakuwa ubingwa tisa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo. Mchezaji huyo ambaye amezaliwa katika mji wa Thie ambao ni wa tatu kwa ukubwa nchini Senegal alianza kucheza soka katika klabu ya nchini kwao ya Jeanne d’Arc kabla ya kuhamia Qatar kuichezea klabu ya Al-Saad mwaka 1996. Baadae alihamia klabu ya Academica de Coimbra ya Ureno na Panathinaikos ya Ugiriki kabla ya kujiunga na Copenhagen anayochezea`mpaka hivi sasa.

"MESSI NI BORA DUNIANI": NEYMAR.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Brazil Neymar da Silva amekiri kuwa mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi ndiye mchezaji bora duniani kwasasa. Kauli ya mchezaji huyo anayekipiga katika klabu ya Santos imekuja kufuatia nguli wa soka wa zamani wa nchi hiyo Pele kudai kuwa mchezaji huyo kinda anafuata nyendo zake na kwasasa ndiye mchezaji bora bora duniani ukimlinganisha na Messi. Neymar wakati akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kikosi chake kuwasili nchini Japani kwa ajili ya michuano ya Kombe la Klabu Bingwa la Dunia amesema ni heshima kubwa kwa gwiji huyo kumfananisha na yeye ingawa akakiri kuwa hadhani kama atafikia kiwango chake. Mchezaji huyo mwenye miaka 19 pia alipingana na kauli ya Pele aliyoitoa akidai kuwa Messi siyo bora kama alivyokuwa yeye kwa kufafanua kuwa yeye anadhani mshambuliaji huyo wa Barcelona ndiye bora duniani kwasasa.

VILLAS-BOAS AMNYEMELEA AYEW.

MENEJA wa timu ya Chelsea Andre Villas-Boas yuko katika harakati za kumnasa kiungo wa kimataifa wa Ghana Andre Ayew ambaye anaichezea klabu ya Marseille ya Ufaransa katika msimu ujao wa usajili. Meneja huyo raia wa Ureno kwasasa yuko katika mkakati mzito wa kukisuka kikosi cha Chelsea ambacho kimeonekana kusuasua msimu huu hivyo kuamua kuongeza damu changa nyingi katika msimu ujao. Mpango wa kocha huyo unatarajiwa kuanza kufanya kazi mapema katika kipindi cha dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa Januari mwakani na moja ya dhamira yake ni kumsajili mshambuliaji huyo Marseille. Ayew mwenye umri wa miaka 21 amekuwa akiwindwa pia na klabu ya Arsenal katika kipindi cha miezi ya karibuni lakini Chelsea wameonyesha nia ya dhati ya kumnyakuwa mchezaji huyo kwa kitita cha Euro milioni 10.

Thursday, December 8, 2011

CECAFA CHALLENGE CUP: KILI STARS YAVULIWA UBINGWA.

TIMU ya taifa ya Uganda-The Cranes imetinga katika hatua ya fainali baada ya kuifunga Kilimanjaro Stars mabao 3-1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mabao yaliyofungwa na nahodha wa Cranes Andrew Mwesigwa, Emmanuel Okwi pamoja na moja la penati yalitosha kabisa kuizamisha Stars na kufuta ndoto zao za kutetea ubingwa huo. Bao la kufutia machozi la Stars lilifungwa na Mrisho Ngassa katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo. Kwa matokeo hayo sasa Uganda itapambana na Rwanda ambao katika mchezo wao waliocheza mapema leo walifanikiwa kuifunga Sudan bao 1-0 na kuingia fainali huku Stars wao wakicheza na Sudan katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu siku ya Jumamosi.

ROONEY APUNGUZIWA ADHABU.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza Wayne Rooney amepunguziwa adhabu yake ya kufungiwa michezo mitatu baada ya kukata rufani katika Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA nchini Switzerland. Adhabu hiyo ya Rooney ilipunguzwa kutoka michezo mitatu mpaka miwili ambapo adhabu ya mchezo wa tatu sasa atatakiwa kuitumikia ndani ya miaka minne hivyo kumwezesha kucheza mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi Ukraine katika michuano ya Kombe la Ulaya mwakani. Meneja wa Uingereza Fabio Capello aliungana na Rooney kusikiliza rufani hilo iliyokuwa ikisikilizwa na jopo la maofisa watatu wa UEFA leo asubuhi. Rooney ambaye ameichezea Uingereza mara 73 na kufunga mabao 28 alifungiwa na shirikisho hilo kufuatia kumchezea vibaya mchezaji timu ya Montenegro katika mchezo wa mwisho wa kutafuta tiketi ya michuano hiyo.

Wednesday, December 7, 2011

GABON YAFUZU KUCHEZA OLIMPIKI.

Timu ya Taifa ya Gabon kwa mara kwanza imefanikiwa kufuzu kucheza michuano ya Olimpiki kwa mara ya kwanza baada ya kuifunga Senegal bao 1-0 katika mchezo wa vijana chini ya miaka 23 uliofanyika jijini Marakech, Morocco. Shujaa katika mchezo mchezo huo alikuwa ni mchezaji Andre Biyogo Poko baada ya kuunganisha kwa mpira wa kona dakika za mwisho za muda wa nyongeza baada ya timu hizo kwenda suluhu katika muda wa kawaida. Senegal itakuwa na nafasi nyingine ya kufuzu michuano hiyo itrayofanyika jijini London mwakani itakapocheza na hatua ya mtoano Jumamosi wakati katika mchezo mwingine wa nusu fainali utakaochezwa leo Misri itacheza na mwenyeji wa mashindano hayo Morocco. Timu tatu kati ya nne zilizoingia hatua ya nusu fainali ndizo zitakazopata nafasi ya kufuzu kucheza michuano hiyo ambapo timu itakayokamata nafasi ya tatu itabidi icheze hatua ya mtoano na kutoka bara la Asia mwakani.

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: CHELSEA, MARSEILLE ZATINGA HATUA YA MTOANO.

TIMU ya Chelsea jana usiku ilikata tiketi ya kucheza hatua ya mtoano ya timu 16 ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kufanikiwa kuigaragaza Valencia mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Stamford Bridge. Mabao mawili yaliyofungwa na mshambuliaji wake Didier Drogba na moja la Ramires yaliiwezesha timu hiyo kumaliza wakiwa vinara wa kundi E ikifuatiwa na Bayer Leverkusen ambao wamemaliza wakiwa wa pili baada ya kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Genk. Katika mchezo mwingine uliokuwa mkali na wa kusisimua timu ya Marseille ilifanikiwa kuibanjua Borussia Dortmund kwa mabao 3-2 katika mchezo wa kundi F hivyo kupelekea timu hiyo kuungana na Arsenal ambao walifungwa na Olympicos mabao 3-1 katika hatua mtoano. Michezo mingine ya michuano hiyo inatarajiwa kupigwa tena leo ambapo vinara wanaoongoza Ligi Kuu nchini Uingereza Manchester City ina kibarua kizito cha kuhakikisha inaifunga Bayern Munich ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele huku mahasimu wao Manchester United nao wakihitaji ushindi wowote dhidi ya Basle ili nao waweze kusonga mbele.

NEYMAR MCHEZAJI BORA LIGI YA BRAZIL.

MSHAMBULIAJI wa Santos Neymar da Silva amepigiwa kura kuwa mchezaji bora wa mwaka katika Ligi Kuu ya Brazil. Neymar mwenye umri wa miaka 19 amefunga mabao 13 katika michezo 21 aliyochezwa hivyo kupelekea kushinda tuzo hiyo akiwazidi wachezaji wenzake ambao ni beki wa Vasco da Gama Dede na mshambualiaji wa Corinthians Liedson. Mshambuliaji huyo anayewaniwa na klabu mbalimbali za Ulaya hakuwepo kupokea tuzo yake hiyo kwasababu timu ilikuwa tayari imesafiri kuelekea Japan kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Klabu Bingwa la Dunia. Corinthians ndio wamenyakuwa ubingwa wa Brazil msimu huu ukiwa ni ubingwa wao wa tano wakifuatiwa na Vasco da Gama wakiwa na alama mbili nyuma yao wakati Santos na Palmeiras ambazo zimemaliza katika nafasi ya sita na saba zikiwa ndio klabu zenye mafanikio zaidi katika ligi hiyo baada ya kunyakua taji hilo mara nane kila mmoja.

MILAN YAAFIKIANA NA TEVEZ.

KLABU ya AC Milan imefikia makubaliano ya kumchukua kwa mkopo mshambuliaji wa Manchester City Carlos Tevez. Ofisa Mkuu wa klabu hiyo Adriano Galliani amesema City wameonyesha nia ya kumuuza mshambuliaji huyo moja kwa moja kutokana na maelewano mabovu aliyonayo na kocha Roberto Mancini wao wako tayari kumchukua kwanza kwa mkopo. Gilliani amesema kwasasa wanamhitaji kwa mkopo kutokana na kutokuwa na uwezo wa kumlipa mshahara mkubwa kama anaolipwa na City hivyo ni matumaini yao wanaweza kumshawishi huko mbeleni kupunguza kiwango hicho ili wamchukue moja kwa moja. Milan wanasaka mshambuliaji kwa udi na uvumba katika kipindi cha dirisha dogo la usajili baada ya mshambuliaji wake Antonio Cassano kuwa nje kwa miezi kadhaa kufuatia upasuaji wa moyo aliofanyiwa.

SPEED KUZIKWA WIKI HII.

Chama cha Makocha nchini Uingereza-LMA kumetoa taarifa kuwa mazishi ya aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa ya Wales yatafanyika wiki hii. Katika taarifa yake hiyo chama hicho kilifafanua kuwa mazishi ya kocha huyo yatakuwa ni ya kifamilia, marafiki wa karibu na familia hiyo pamoja na wageni maalumu ambao watapewa mwaliko. Speed alikutwa amejinyonga nyumbani kwake Novemba 27 mwaka huu ambapo uchunguzi dhidi ya kifo chake kusogezwa mbele mpaka januari 30 mwakani. Taarifa ya LMA iliendelea kusema kuwa mjane na familia ya Speed ambaye pia aliwahi kuwa mchezaji akichezea timu za Leeds United, Newcastle na Everton inashukuru wote wakiwemo mashabiki wake walioguswa na kifo cha mchezaji huyo.

Tuesday, December 6, 2011

CECAFA CHALLENGE CUP: KILI STARS YATINGA NUSU FAINALI.

TIMU taifa ya Tanzania Bara-Kilimanjaro Stars imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Challenge baada ya kuifunga Malawi kwa bao 1-0 katika mchezo wa robo fainali uliofanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na kiungo wa Kilimanjaro Nurdin Bakari katika ya 16 ya mchezo ambapo sasa timu hiyo itapambana na Uganda ambao wameshinda kombe hilo mara 11 siku ya Alhamisi.

Monday, December 5, 2011

CECAFA CHALLENGE CUP: BOBAN ATIMULIWA KILI STARS.

KIUNGO Haruna Moshi-Boban ametimuliwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Bara-Kilimanjaro Stars kutokana na sababu za utovu wa nidhamu alizozionyesha katika mchezo wa wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Zimbabwe wiki iliyopita. Akizungumza Dar es Salaam, Kocha wa Kilimanjaro Charles Mkwasa amesema kuwa wamemuondoa Boban katika kikosi hicho kutokana na kitendo chake cha kuondoka katika benchi ya wachezaji wa akiba kabla mchezo kumalizika ambapo timu hiyo ililala bao 2-0. Mkwasa amesema hakuna kocha yoyote anayeweza kuvumilia kitendo kilichofanywa na mchezaji huyo hivyo wameona ni bora kumuondoa katika kikosi hicho ingawa alikiri kuwa kuondoka kwake kutaacha pengo katika kikosi hicho. Kocha aliendelea kusema kuwa kikosi chake hakikuanza vyema michuano hiyo kwa mwaka huu hivyo kwasasa anahitaji wachezaji wenye nidhamu na wanaojituma ili kufanikiwa kutetea taji hilo ambalo walilichukua mwaka jana.

MAS YANYAKUWA KOMBE LA SHIRIKISHO.

Kikosi kamili cha MAS
TIMU ya MAS ya Morocco jana ilifanikiwa kunyakuwa ushindi katika michuano Kombe la Shirikisho baada ya kuibanjua timu ya Africain ya Tunisia kwa changamoto ya mikwaju ya penati 6-5 baada ya timu hizo kwenda sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida. Golikipa wa MAS Anas Zniti ndio alikuwa shujaa wa mchezo huo baada ya kuzuia mkwaju wa penati wa mchezaji Zied Ziadi kabla ya yeye mwenyewe kupiga penati ya mwisho na kuipa ushindi wa kwanza wa kihistoria timu yake hiyo. 
Anas Zniti, golikipa wa MAS
Ushindi huo umekuwa ni kama historia ikijirudia baada ya klabu nyingine kutoka Morocco ya FUS Rabat kuifunga Etoile du Sahel ya Tunisia katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo msimu uliopita. MAS ambaye ndio bingwa wa michuano hiyo imekunja kitita cha dola 660,000 ambapo mapema mwaka ujao watapambana na bingwa wa michuano ya Klabu Bingwa ya Afrika timu ya Esperance katika kombe lililoandaliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF.

NAHODHA WA ZAMANI WA BRAZIL AFARIKI DUNIA.

MCHEZAJI soka wa zamani ambaye pia aliwahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Brazil Socrates amefariki dunia akiwa na miaka 57. Nahodha huyo alijulikana zaidi mwaka 1982 wakati alipokiongoza kikosi cha Brazil katika michuano ya Kombe la Dunia kwa mwaka huo kikosi ambacho kinasifika kwa kuonyesha kandanda safi kuliko kikosi chochote cha timu hiyo kilichopata kutokea. Lakini mbali na uchezaji soka mchezaji pia alikuwa akijulikana kwa unywaji wa pombe uliopitiliza kitu ambacho aliwahi kukiri kimemsababishia matatizo ya afya mpaka kupelekea kifo chake kilichotokea jana. Mbali na kuwa mcheza soka Socrates alikuwa na shahada ya udaktari aliohitimu akiwa na miaka 23 na pia alikuwa mwandishi na mchambuzi wa masuala mbalimbali yahusuyo michezo pamoja na siasa na ameacha mke na watoto sita.

BLATTER APANIA KUISAFISHA FIFA.

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter amesema Jumapili hii kuwa anataka kubadilisha taswira ya shirikisho hilo ambalo kwasasa limekumbwa na kashfa mbalimbali zikiwemo za rushwa. Blatter ambaye ni raia wa Switzerland alikataa mapema mwaka huu kwamba hana mpango wa kuachia ngazi kwani kuna mambo mengi ya kufanya ili kurudisha heshima ya shirikisho hilo ambayo inataka kutoweka. Kiongozi huyo wa FIFA ambaye hivi karibuni alijikuta katika vita nzito baada ya kauli yake kuhusiana na ubaguzi amesema yapo mambo ya kufanya ili kuhakikisha wanasafisha jina la FIFA. FIFA katika kipindi cha karibuni limekumbwa na matukio kadhaa ikiwemo lile la kuzipa nchi za Russia na Qatar uenyeji michuano ya kombe la Dunia 2018 na 2022 kuwa liligubikwa na rushwa huku tukio lingine likiwa la aliyekuwa mpinzani wake katika uchaguzi wa rais wa shirikisho hilo Mohamed bin Hammam kufungiwa kufuatia kashfa ya kununua wapiga kura.