Friday, December 16, 2011

SENEGAL KUJIPIMA NGUVU NA SUDAN NA TUNISIA.

TIMU ya Taifa ya Senegal inatarajiwa kucheza michezo yake ya kimataifa kirafiki na timu za Sudan na Tunisia ikiwa ni maandalizi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayotarajiwa kufanyika mapema mwakani. Senegal ambao mwezi Agosti mwaka huu ililala mabao 2-0 dhidi ya Morocco katika mchezo wa kirafiki itakuwa imepania kulipiza kisasi wakati watakapokutana na Tunisia ambao wanatoka ukanda mmoja wa Afrika ya Kaskazini na Morocco wakati timu zitapokutana jijini Dakar Januari 14. Kabla ya kumenyana na Tunisia timu hiyo kwanza itacheza na Sudan Januari 12 hapohapo jijini Dakar ambapo kocha wa timu hiyo Amara Traore amedai michezo hiyo itakuwa ni kipimo tosha kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Afrika Januari 22. Hata hivyo kikosi hicho kinaweza kuingia matatizoni baada ya Traore kukataa kuongeza mkataba ambao unakaribia kuisha akidai nyongeza ya mshahara ya Dola 24,000 kwa mwezi.

No comments:

Post a Comment