Tuesday, June 30, 2015

HIDDINK AACHIA NGAZI UHOLANZI.

KOCHA wa timu ya taifa ya Uholanzi, Guus Hiddink ametangaza kuachia nafasi hiyo kufuatia kusuasua kwa kikosi cha nchi hiyo katika michuano ya kufuzu michuano ya Ulaya mwakani. Katika taarifa yake Shirikisho la Soka nchi hiyo-KNVB ilithibitisha taarifa hizo huku mkurugenzi wake Bert van Oostveen akidai kuwa pamoja na kuwa kazi ya kocha huyo ilikuwa bado haijaonekana machoni kwa wengi lakini anashukuru kwa muda wote waliokuwa naye. Hiddink ambaye mkataba wake ulikuwa unamalizika baada ya michuano Ulaya mwaka 2016 amesema ilikuwa ni heshima kubwa kwake kuinoa timu hiyo kwa mara ya pili na kuongeza kuwa anamtakia kila la heri kocha atakayechukua nafasi yake. KNVB kwasasa itakutana kuangalia jinsi ya kuziba nafasi hiyo huku msaidizi wa Hiddink, Danny Blind alitajwa kuwa ndiye atakayechukua nafasi hiyo.

WOLFSBURG YADAI HAWANA MPANGO WA KUMUUZA DE BRUYNE.

MKURUGENZI wa michezo wa Wolfsburg, Klaus Allofs amesisitiza kuwa klabu hiyo haina mpango wowote wa kumuuza Kevin De Bruyne katika usajili wa majira haya ya kiangazi. Manchester City ndio wanaoenekana kumuwinda nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji huku mwenyewe akithibitisha amepama mwezi huu kuwa wakala ameshafanya mazungumzo na klabu hiyo. Hata hivyo, Wolfsburg bado wameendelea na msimamo wao wa kutotaka kumuacha De Bruyne na Allofs amebainisha kuwa klabu hiyo inatarajia kuangalia uwezekano wa kumboreshea maslahi katika mkataba wake nyota huyo mwenye umri wa miaka 24. Allofs amesema De Bruyne ana mkataba na Wolfsburg unaomalizika mwaka 2019 na tayari wameshatuma ujumbe kuwa hawana mpango wa kumuuza. Mkurugenzi huyo aliendelea kudai kuwa kikubwa wanachotizama hivi sasa ni kupitia upya mkataba wake na kuangalia jinsi ya kuuboresha zaidi.

FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA 2017 KUCHEZWA UWANJA WA MILLENNIUM, CARDIFF.

SHIRIKISHO la Soka la Ulaya-UEFA limethibitisha kuwa Uwanja wa Millennium uliopo jijini Cardiff ndio utakuwa mwenyeji wa mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2017. Mara ya mwisho Cardiff kuandaa mechi ya UEFA ilikuwa ni mwaka jana wakati Real Madrid walipoitandika Sevilla kwa mabao 2-0 katika mchezo wa Super Cup ambao hukutanisha bingwa Ligi ya Mabingwa na Europa League. Taarifa hizo zimeonyeha kufurahisha wachezaji nyota wa kimataifa wa Wales Gareth Bale na Aaron Ramsey ambao hawakusita kusifia hatua hiyo. Akihojiwa Bale amesema hilo ni jambo muhimu kwa soka la Wales kwani inaonekana nchi nzima iko nyuma yao wakati wakijaribu kufuzu fainali za michuano ya Ulaya zitakazochezwa mwakani nchini Ufaransa. Naye Ramsey mwenye umri wa miaka 24 alisifia hatua hiyo akidai ni muhimu kwa maendeleo ya soka la nchi hiyo. UEFA pia ilitangaza Uwanja wa Friends Arena uliopo jijini Solna, Sweden kuwa ndio utakaochezwa fainali ya michuano ya Europa League mwaka huohuo huku Uwanja wa Taifa wa Filip II uliopo huko Skopje, Macedonia wenyewe ukitumika kwa ajili ya mchezo wa Super Cup.

LAPORTA AJINADI KUIREJESHA TENA NEMBO YA UNICEF KATIKA FULANA ZA BARCELONA.

RAIS wa zamani wa Barcelona, Joan Laporta amejinadi kuwa atafanya kila awezalo kuhakikisha analirejesha jina la UNICEF au shirika lolote la misaada ya kibinadamu katika fulana za timu hiyo kama akirejea tena madarakani katika uchaguzi wa mwezi ujao. Laporta ndiye aliyetengeneza dili la UNICEF miaka 10 iliyopita wakati akiwa rais kuanzia mwaka 2003 mpaka 2010 ambapo ilishuhudia nembo ya shirika hilo ikiwekwa katika fulana za timu hiyo kwa mara ya kwanza katika historia. Chini ya uongozi uliopita, ulioongozwa na Sandro Rosell na baadae Josep Maria Bartomeu umeshuhudia nembo ya wadhamini ya shirika la ndege la Qatar ikionekana mbele ya fulana huku nembo ya UNICEF ikiwekwa nyuma. Akijinadi katika kampeni za uchaguzi, Laporta amesema atafanya kila awealo kuhakikisha anatafuta wadhamini ambao wataweza kufanikisha hilo na kurejesha nembo ya UNICEF katika fulana za timu hiyo tena. Laporta anakabiliwa na upinnzani mkali kutoka kwa rais aliyepita Bartomeu katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Julai 18 mwaka huu.

MALDINI AITABIRIA MAKUBWA BARCELONA.

NGULI wa soka wa Italia, Paolo Maldini ametabiri kuwa Lionel Messi na wachezaji wa sasa wa Barcelona watakuja kuvunja rekodi zote. Katika msimu wake wa kwanza Camp Nou meneja Luis Enrique, Barcelona imefanikiwa kunyakuwa taji la La Liga, Kombe la Mfalme na Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa ni mara ya pili katika historia klabu hiyo kunyakuwa mataji matatu mfululizo. Wakiwa wamefikia mafanikio waliyopata mwaka 2009 chini Pep Guardiola, Maldini anafikiri Messi, Neymar na Luis Suarez wanaweza kuisaidia Barcelona kuendelea kutengeneza historia zaidi katika kipindi kinachokuja. Maldini amesema Messi, Neymar na Suarez wameonyesha kiwango kikubwa msimu uliopita na anadhani wakiendelea hivyo wataiwwezesha klabu hiyo kuvunja rekodi zote zilizopo mbele yao.

IVORY COAST YAKARIBIA KUPATA MRITHI WA RENARD.

SHIRIKISHO la Soka la Ivory Coast limetoa majina ya makocha watano waliopenya katika kinyang’anyiro cha kutafuta kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo kufuatia kuondoka kwa Herve Renard. Maofisa wa shirikisho hilo wamesema vigezo vikubwa vinavyohitajika kwa kocha wanayemuhitaji ni uzoefu wa soka la Afrika na awe anazungumza kifaransa ili kumuwezesha kuwasiliana kirahisi sio tu na wachezaji wanaocheza soka nje bali hata wale waliopo ndani. Mojawapo ya majina yaliyotajwa katika orodha hiyo ni pamoja na Henyk Kasperczak (Pichani) ambaye amewahi kuinoa timu hiyo kati ya mwaka 1993 na 1994. Kocha huyo raia wa Poland mwenye umri wa miaka 68 pia amewahi kuzinoa timu za taifa za mali, Tunisia na Senegal. Wengine ni kocha wa zamani wa Guinea, Dr Congo na Mauritania Patrice Neveu, Michel Dusseyer ambaye naye amewahi kuinoa Guinea, Mreno Paulo Duarte na Frederic Antonetti akiwa kocha pekee ambaye hajawahi kufundisha soka Afrika. Ivory Coast imekuwa bila kocha toka alipoondoka Renard ambaye aliiwezesha nchi hiyo kunyakuwa taji la michuano ya Mataifa ya Afrika mapema mwaka huu.

SANCHEZ TEGEMEO KUBWA KWA CHILE.

KOCHA wa timu ya taifa ya Chile, Jorge Sampaoli amedai kuwa Alexis Sanchez anahitaji kucheza kwa ubora wake wakati wakijaribu kukata kiu ya karibu karne moja kunyakuwa taji la kwanza la michuano ya Copa America. Chile walifanikiwa kutinga hatua ya fainali jana baada ya kuichapa Peru kwa mabao 2-1 na sasa wanasubiri mshindi katika mchezo wa leo kati ya Argentina wanaopewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo na Paraguay. Akihojiwa Sampaoli amesema Sanchez ni mchezaji muhimu katika kikosi chao ndio maana wanafanya kila wanaloweza kujaribu kumrejesha katika kiwango chake kabla ya mchezo wa fainali. Kocha huyo amedai kikosi chake kiko katika shinikizo kubwa kutoka kwa mashabiki wao kutokana na kuwa wenyeji hivyo ni muhimu kwa kila mchezaji kuwa fiti kwa asilimia 100 katika mchezo huo. Fainali ya michuano hiyo ambayo ilianzishwa miaka 99 iliyopita inatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Taifa uliopo jijini Santiago Jumamosi hii.

ARSENAL WAMPOKEA CECH KWA SHANGWE.

WACHEZAJI wa mbalimbali wa Arsenal wameungana na meneja wao Arsene Wenger kumkaribisha golikipa Petr Cech aliyetua Emirates akitokea kwa mabingwa wa Ligi Kuu Chelsea. Arsenal ilithibitisha jana kumsajili Cech kwa kitita ambacho kinaaminika kufikia paundi milioni 11. Nyota huyo anaondoka Chelsea baada ya kuitumikia kwa muda wa miaka 11 na kufanikiwa kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu na Kombe la FA pamoja na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Wenger alimuelezea Cech kama mmoja wa magolikipa mahiri duniani na kuungwa mkono na wachezaji kadhaa wa timu hiyo ambao walitumia mitandao yao ya kijamii kumkaribisha. Miongoni mwa nyota walituma ujumbe wa kumkaribisha golikipa huyo katika kurasa zao za mitandao ya kijamii ni pamoja na Theo Walcott, Jack Wilshere, Aaron Ramsey, Olivier Giroud pamoja na golikipaWojciech Szczesny,

MAN UNITED YATOA OFA YA PAUNDI MILIONI 28.6 KWA AJILI YA KUMSAJILI RAMOS.

KLABU ya Manchester United imetuma ofa ya paundi milioni 28.6 kwenda Real Madrid kwa ajili ya kumsajili beki wake Sergio Ramos. United inaamini nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 anataka kuondoka Madrid baada ya kushindwa kupewa ofa ya kuongezwa mkataba wake ambao unamalizika mwaka 2017. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania amecheza mechi 445 toka ajiunge na Madrid mwaka 2005 akitokea Sevilla. Meneja wa United Louis van Gaal anataka kuimarisha safu yake ya ulinzi katika kikosi chake tayari kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu.

COPA AMERICA: VARGAS AIBUKA SHUJAA CHILE IKITINGA FAINALI.

WENYEJI Chile Alfajiri ya leo wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Copa America baada ya kuigaragaza Peru kwa mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fanali uliofanyika huko Santiago. Shujaa wa Chile katika mchezo huo alikuwa Eduardo Vargas ambaye alifinga mabao yote mawili katika dakika ya 42 na 64 na kumfanya kufikisha mabao 22 kwa nchi yake. Akihojiwa mara baada ya mchezo, Vargas ambaye anakipiga katika klabu ya Napoli ya Italia amesema alihisi mapema kuwa atafunga mabao katika mchezo huo kwani wakati wakifanya mazoezi Jumamosi alifunga karibu kila mpira aliopiga langoni. Chile sasa wanasubiri mshindi katika mchezo mwingine wa nusu fainali utakaochezwa baadae leo ambapo Argentina watakwaana na Paraguay.

Monday, June 29, 2015

RAIA MMOJA WA ARGENTINA ADAI MESSI KAOKOA MAISHA YAKE.

RAIA mmoja wa Argentina aliyetekwa nchini Nigeria, amedai kuwa jina la mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi ndio lililookoa maisha yake. Santiago Lopez Menendez mwenye umri wa miaka 28 ambaye kitaaluma ni injinia wa kilimo, alikuwa akifanya kazi Nigeria toka mwaka jana akisaidia upandaji wa mazao ya soya na nafaka katika mji wa Kontagora. Lakini mapema wiki iliyopita alitekwa na kupigwa na watu wasiojulikana ambao walikuwa hawawezi hata kuzungumza lugha ya kiingereza na kudhani alikuwa raia wa Marekani. Katika hekaheka za kujaribu kuwafafanulia kuwa yeye sio raia wa Marekani, alifanikiwa kuwatuliza watekaji wake kwa kulitaja jina la Messi mara kadhaa huku akilia. Watekaji hao walimshikilia kwa siku tatu kabla ya kumuachia baada ya kampuni ambayo ilimuajiri kuwalipa kiasi cha fedha ambacho hakikuwekwa wazi. Mara baada ya kuachiwa Menendez amesema anamshukuru Messi kwani kitendo cha kutaja jina lake ndio kilichookoa maisha yake mikononi mwa watekaji hao.

STUTTGART YASAJILI GOLIKIPA WA DORTMUND.

KLABU ya Stuttgart imefanikiwa kumsajili golikipa Mitchell Langerak kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka kwa mahasimu wao Bundesliga Borussia Dortmund. Nyota huyo wa kimataifa wa Australia mwenye umri wa miaka 26, alijiunga na Dortmund akitokea Melbourne Victory mwaka 2010 na kufanikiwa kucheza mechi yake ya kwanza Februari mwaka uliofuata wakati Dortmund walipotandikwa mabao 3-1 na Bayern Munich. Msimu uliopita Langerak ambaye alikuwa golikipa namba mbili wa Dortmund alicheza mechi tisa za Bundesliga. Langerak amelazimika kuondoka baada ya meneja mpya wa Dortmund Thomas Tuchel kumleta Roman Burki kutoka klabu ya Freiburg mapema mwezi huu.

CITY YAMUWINDA FABINHO.

KLABU ya Manchester City inajipanga kumuwania beki wa kulia wa klabu ya AS Monaco ya Ufaransa Fabinho. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 alikuwepo katika kikosi cha Brazil chini ya kocha Dunga kwenye michuano ya Copa America nchini Chile ingawa hakucheza katika mechi yeyote. Pamoja na kuwa hakuna mazungumzo yeyote yaliyoanza mpaka sasa, inaaminika City wamekuwa wakifuatilia nyendo za beki huyo katika wiki za karibuni. Beki huyo ambaye pia amekuwa akidaiwa kuwindwa na klabu za Chelsea na Manchester City, Monaco wamepanga kumuuza kwa kitita cha euro milioni 25.4 kwa timu itakayomuhitaji.

RONALDO APANIA KUJITANGAZA ZAIDI BARANI ASIA.

MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amebanisha kuuza sehemu ya haki ya kutumia picha zake kwa mmiliki wa klabu ya Valencia Peter Lim ili kukuza jina lake barani Asia. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 30, hivi karibuni alitajwa kuwa wa tatyu katika orodha ya wanamichezo matajiri duniani na sasa anajipanga kuongeza utajiri wake zaidi. Ronaldo mwenyewe ambaye ana urafiki wa karibu na bilionea huyo wa Valencia, alithibitisha taarifa hizo kupiti mtandao wake wa kijamii wa facebook akidai kuwa hatua hiyo ni muhimu kwake kwa kulikuza jina lake kimataifa. Kampuni ya Mint Media yenye makao yake huko Hong Kong na kumilikiwa na Lim, ilidai katika taarifa yake kuwa mkataba wa miaka sita waliosaini na Ronaldo utasaidia kukuza jina la nyota huyo barani humo.

SCHWEINSTEIGER AIZODOA MAN UNITED.

KIUNGO wa Bayern Munich, Bastian Schweinsteiger amesema anataka kushinda taji la nne mfululizo ya Bundesliga akiwa na timu hiyo, pamoja na tetesi zinazomhusisha na kwenda klabu ya Manchester United. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 anamaliza mkataba wake kiangazi mwakani na alicheza katika mechi 20 za Bundesliga msimu uliopita na 28 katika mashindano yote wakati Bayern walipofanikiwa kunyakuwa taji la tatu la ligi mfululizo. Ingawa bado hajakubali kusaini mkataba mpya na Bayern, Schweinsteiger amesema anataka kushinda taji lingine la Bundesliga akiwa na Bayern msimu ujao. Kiungo huyo amekuwa akihusishwa na tetesi za kujiunga na United katika majira haya ya kiangazi hatua ambayo ingemuwezesha kuungana na kocha wake wa zamani Louis van Gaal ambaye amemfundisha wakati akiwa Bayern. Hata hivyo kauli yake ya kutaka kunyakuwa taji la nne la Bundesliga akiwa na Bayern inafifisha tetesi hizo za kwenda United kiangazi hiki.

COSTA ATHIBITISHA KUTAKIWA NA BAYERN.

KIUNGO wa kimataifa wa Brazil, Douglas Costa leo amethibitisha nia ya mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich kutaka kumsajili lakini amedai hakuna dili lolote lililoafikiwa mpaka sasa. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye anakipiga katika klabu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine amesema mazungumzo yanaendelea kufanyika kati ya klabu hizo mbili. Bayern wanataka kumsajili kiungo huyo ambaye pia anaweza kucheza kama winga kutokana na wasiwasi wa majeruhi ya muda mrefu wa mawinga wake Franck Ribery na Arjen Robben. Akihojiwa Costa amesema anafahamu kuwa mazungumzo kati ya klabu yake na Bayern yamefanyika lakini hajui kinachoendelea zaidi kufahamu Bayern wanataka kumsajili.

CLYNE KUFANYIWA VIPIMO VYA AFYA LIVERPOOL.

BEKI wa Southampton Nathaniel Clyne anatarajiwa kujiunga na Liverpool muda wowote wakati meneja Brendan Rodgers akiendelea kukisuka kikosi chake kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu. Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24, tayari amesharejea kutoka mapumzikoni na atafanyiwa vipimo vya afya kabla ya kukamilisha usajili wake ambao umegharimu kiasi cha paundi milioni 12.5. Kila kitu kikikamilika, Clyne atakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Liverpool katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi. Mipango pia imeshaandaliwa kukamilisha usajili wa nyota wa kimataifa wa Brazil Roberto Firmino bada ya kumaliza majukumu yake ya kimataifa kwa kutolewa katika michuano ya Copa America na Paraguay Jumamosi iliyopita. Wengine ambao tayari wameshaanguka saini zao mpaka sasa ni kiungo wa Manchester City james Milner, mshambuliaji wa Burnley Danny Ings na golikipa wa Bolton Wanderers Adam Bogdan.

LIGI YA MABINGWA AFRIKA: MAZEMBE YAVUTWA SHATI NA AL HILAL.

KLABU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC jana imeshindwa kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kung’ang’aniwa sare ya bila kufungana na Al Hilal ya Sudan katika mchezo wa makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Katika mchezo huo Mazembe walionyesha soka safi lakini walishindwa kuipenya ngome ya Al Hilal mbele ya mashabiki wao waliojazana katika Uwanja wa Kamalondo uliopo jijini Lubumbashi. Katika mchezo mwingine wa kundi A uliochezwa jana timu ya Smouha ya Misri walifanikiwa kuitandika Moghreb Athletic Tetouan ya Morocco kwa mabao 3-2. Sasa Tetouan ambao wanashiriki hatua hiyo kwa mara ya kwanza watavaana Mazembe katika mchezo wao utakaofanyika Julai 10 mwaka huu. Kwa upande wa Al Hilal wao wataivaa Smouha wikiendi hiyohiyo.

COPA AMERICA: JARA FUNGIWA MECHI TATU KWA KOSA LA "KUMNAWA" CAVANI.

BEKI wa timu ya taifa ya Chile, Gonzalo Jara anatarajiwa kukosa michezo inayoendelea ya Copa America baada ya kunyukwa adhabu ya kutocheza mechi tatu kwa kosa la kumshika makalio mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani. Shirikisho la Soka la Amerika Kusini-Conmebol limedai kuwa wamefikia uamuzi kutokana na beki huyo kuonyesha tabia isiyokuwa ya kiuanamichezo. Mbali na adhabu hiyo lakini Jara ametundikwa faini ya dola 7,500. Tukio hilo lilitokea wakati Chile waliposhinda bao 1-0 katika mchezo wa robo fainali uliofanyika Alhamisi iliyopita. Cavani alimtundika kibao Jara baada ya kufanyiwa kitendo hicho hatua ambayo ilipelekea mwamuzi kumlima kadi ya pili njano na hivyo kutolewa nje. Adhabu hiyo inamaanisha Jara ataukosa mchezo wa leo wa nusu fainali dhidi ya Peru pamoja na mechi nyingine ya aidha fainali au kutafuta mshindi wa tatu kutegemeana na matokeo watakayopata leo.

Friday, June 26, 2015

PETR CECH HUYOOO ARSENAL.

GOLIKIPA wa Chelsea Petr Cech anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya katika klabu ya Arsenal leo ili kukamilisha taratibu za mwisho za uhamisho wake Emirates. Klabu hizo mbili tayari wameonekana kufikia muafaka wa ada ya uhamisho huku Cech mwenye umri wa miaka 33 akiwa tayari ameshakubali mambo yake binafsi. Golikipa huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech anatarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na timu hiyo majira haya ya kiangazi. Cech ameamua kuondoka Arsenal baada ya kunyang’anywa namba katika kikosi cha kwanza cha Chelsea na golikipa wa kimataifa wa Ubelgiji Thibaut Courtois mwenye umri wa miaka 23. Cech ambaye ameichezea Chelsea zaidi ya mechi 300 katika kipindi cha miaka 11, alifanikiwa kushinda mataji manne ya Ligi Kuu, manne ya Kombe la FA, matatu ya Kombe la Ligi, moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya na moja la Europa League.

BLATTER ADAI HAJAJIUZULU.

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter amesema hajajiuzulu nafasi yake hiyo katika shirikisho hilo. Blatter mwenye umri wa miaka 79 alikuwa akifikiriwa kuwa amejiuzulu nafasi hiyo ambayo ameiongoza kwa kipindi cha miaka 17 kufuatia madai ya ufisadi yaliyoikumba shirikisho hilo. Lakini kwa mujibu wa gazeti la Blick, Blatter alikaririwa akidai kuwa hajajizulu bali ameacha mustakabali wake uamuliwe katika Mkutano Mkuu wa FIFA. Kauli hiyo imezusha hofu kuwa Blatter anafikiria kugombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mwingine.

MECHI ZA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO KUANZA KUTIMUA VUMBI LEO.

MICHUANO ya Kombe la Shirikisho ya Afrika hatua ya makundi inatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo kwa mchezo mmoja wa kundi A. Katika mchezo huo klabu kongwe ya Tunisia Etoile du Sahel wanatarajiwa kuikaribisha timu ya Stade Malien ya Mali katika uwanja wao nyumbani wa Seydou Tiama. Mchezo mwingine wa kundi hilo unatarajiwa kuchezwa Jumapili hii ambapo mabingwa watetezi wa kombe hilo Al Ahly ya Misri itavaana na mahasimu wao wa siku nyingi Esperance ya Tunisia katika Uwanja wa Suez Army. Katika michezo ya kundi B ambayo itachezwa kesho AC Leopards ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC wataikaribisha Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika uwanja wao wa Denis Sassou Nguesso uliopo huko Dolisie. Mchezo mwingine wa kundi hilo klabu kongwe ya Zamalek ya Misri watawakaribisha mabingwa mara tatu wa michuano hiyo CS Sfaxien ya Tunisia katika mchezo utakaofanyika katika Uwanjwa wa Michezo Petro jijini Cairo.

BECKERNBAUER AMFUNDA GUARDIOLA.

NGULI wa soka wa Ujerumani, Franz Beckernbauer amemwambia meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola kuwa anapaswa kushinda mataji kama anataka kuonyeshwa upendo. Mapema wiki hii Guardiola alibainisha kuwa moja na malengo yake makubwa katika maisha ni watu kumhusudu ya kutambua kazi yake na Beckernbauer amesisitiza kuwa mafanikio ni njia rahisi ya kukufanya upendwe na mashabiki. Nguli huyo amesema upendo ni jambo kubwa kwa mtu kupata na iwapo Guardiola anahitaji hilo njia rahisi ya kufanikisha in kuhakikisha anashinda mataji. Bayern imetawala Bundesliga chini ya Guardiola katika misimu miwili iliyopita kwa kushinda taji hilo kwa vipindi vyote hivyo lakini Beckernbauer anadhani kocha huyo atakabiliwa na wakati mgumu kuhakikisha anatetea taji hilo msimu ujao.

JORDI ALBA ATAKA KUZEEKEA BARCELONA.

BEKI mahiri wa Barcelona, Jordi Alba amesisitiza kuwa anafurahia maisha katika timu hiyo na amepanga kubakia hapo mpaka atakapoamua kutundika daruga zake. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 ambaye ametokea katika shule ya klabu hiyo, alirejea Camp Nou majira ya kiangazi mwaka 2012 baada ya kuzitumikia klabu za Cornella, Valencia na Gimnastic ambapo toka wakati huo ameimarika na kuwa mchezaji muhimu. Alba pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Barcelona ambacho kilinyakuwa mataji mataji msimu uliopita na bado anaonyesha kuwa na njaa ya kunyakuwa matji zaidi. Akihojiwa nyota huyo wa kimataifa wa Hispania amesema anataka kuichezea Barcelona kwa miaka mingi ijayo kwani amejifunza mengi katika kipindi cha miaka mitatu. Alba ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2020 amesema pamoja na kuwa hajui itakavyokuwa huko mbele lakini kama itawezekana angependa kutundika daruga zake akiwa Barcelona.

DE JONG AONGEZA MIAKA MITATU MILAN.

KLABU ya AC Milan imetangaza kuwa Nigel de Jong amesaini mkataba mpya ambao utamuweka katika klabu hiyo mpaka majira ya kiangazi mwka 2018. Kiungo huyo mzoefu mkataba wake wa sasa ulikuwa unamalizika wiki ijayo na hivyo kuzua tetesi juu ya mustakabali wake wa kubakia San Siro huku kukiwa na minong’ono ya kutakiwa na Schalke pamoja na klabu yake ya utotoni ya Ajax Amsterdam. Hata hivyo, De Jong mwenye umri wa miaka 30 ameamua kubakia Milan na kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu. Kiungo huyo alijiunga na Milan akitokea Manchester City majira ya kiangazi mwaka 2012 na toka wakati huo ameimarika na kuwa mchezaji muhimu wa timu hiyo.

LIVERPOOL YAONGEZA OFA KWA CLYNE.

KLABU ya Liverpool imeboresha ofa yake kufikia paundi milioni 12.5 kwa ajili ya kutaka kumsajili beki wa kulia wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Southampton Nathaniel Clyne. Mwezi uliopita Southampton walikataa ofa ya paundi milioni 10 iliyotolewa na Liverpool kwa ajili ya beki huyo mwenye umri wa miaka 24. Klabu hizo mbili zimeendelea na mazungumzo huku Southampton wo wakitaka paundi milioni 15 kwa ajili ya mchezaji huyo ambaye amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake. Liverpool wamekuwa wakimuwinda Clyne baada ya kuondoka kwa Glen Johnson mwenye umri wa miaka 30 mwishoni mwa msimu huu. Klabu hiyo inampa ofa Clyne ambaye alijiunga na Southampton akitokea Crystal Palace Julai mwaka 2012, mkataba wa miaka mitano. Kama wakifanikiwa, huo utakuwa usajili wa sita kwa Liverpool katika kipindi cha usajili wa kiangazi baada ya kuwa tayari wameshwasajili beki Joe Gomez, kiungo James Milner, washambuliaji Danny Ings na Roberto Firmino pamoja na golikipa Adam Bogdan.

UCHAGUZI BARCELONA MOTO.

KAMPENI za urais katika klabu ya Barcelona zimezidi kushika kasi baada ya mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo Jordi Majo kuwaonya wapiga kura kuwa mgombea mwenzake Josep Maria Bartomeu anaweza kuhukumiwa na kwenda jela. Bartomeu ambaye alichukua nafasi ya Sandro Rosell aliyejiuzulu Januari mwaka 2014, kwasasa anakabiliwa na kesi ya ukwepaji kodi inayohusu uhamisho wa Neymar uliofanyika miaka miwili iliyopita. Kumekuwa na masuala kadhaa ya kisheria yanayomkabili Bartomeu ambayo yametajwa na Majo anayedhani mpinzani wake huyo hakuchukua hatua stahiki kukabiliana nayo. Kutokana na hayo, Majo anadhani si vyema kwa Bartomeu kuchaguliwa tena kushika wadhifa huo kwani anaweza hata kwenda jela kama akikutwa na hatia. Uchaguzi rasmi wa klabu hiyo unatarajiwa kufanyika Julai 18 mwaka huu, wiki nne kabla ya msimu ujao wa La Liga haujaanza ambapo Barcelona chini meneja Luis Enrique watakuwa wakitetea taji lao.

COPA AMERICA: PERU KUKWAANA NA WENYEJI CHILE NUSU FAINALI.

MABAO matatu yaliyofungwa na mshambuliaji Paulo Guerrero yalitosha kuipa Peru ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Bolivia na kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Copa America. Guerrero alifunga mabao mawili ndani ya dakika tatu katikati ya kipindi cha pili na kuipa Peru uongozi katika mchezo huo wa robo fainali uliofanyika huko Temuco. Peru ambao pia walitinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mwaka 2011 sasa watakwaana na wenyeji Chile mchezo ambao utafanyika huko Santiago Jumatatu ijayo. Mechi zingine za robo fainali zitawakutanisha Argentina dhidi ya Colombia Jumamosi na Brazil dhidi ya Paraguay Jumapili hii.

FA YATETEA UAMUZI WAKE WA KUWAACHA BAADHI YA WACHEZAJI WA LIGI KUU KATIKA KIKOSI CHA UNDER21.

MKURUGENZI wa maendeleo wa Chama cha Soka cha Uingereza-FA Dan Ashworth amedai kuwa walifanya uamuzi sahihi wa kuwaondoa baadhi ya wachezaji wa Ligi Kuu katika kikosi cha timu ya taifa kilichoshiriki michuano ya Ulaya kwa vijana chini ya umri wa 21. Kikosi cha Uingereza kilichokuwa chini ya kocha Gareth Southgate kilishindwa kuvuka hatua ya makundi ya michuano hiyo inayoendelea huko Jamhuri ya Czech. Akihojiwa Ashworth alitetea uamuzi wao huo akidai kuwa timu za vijana zipo kusaidia kuwakuza wachezaji na kuwapa uzoefu kuingia katika timu ya wakubwa. Mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling, kiungo wa Everton Ross Barkley, viungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain na Jack Wilshere na mlinzi wa Manchester United Phil Jones ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakihitajika katika timu hiyo, lakini hawakuitwa. Baadhi ya wachezaji wa Ligi Kuu waliochukuliwa kwa ajili ya michuano hiyo ni pamoja na mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, mlinzi wa Everton John Stones na mshambuliaji mpya wa Liverpool Danny Ings. Katika michuano hiyo Uingereza, ilipoteza kwa Ureno kwa kufungwa 1-0, lakini wakazinduka na kuifunga Sweden kwa idadi kama hiyo huku wakipoteza mchezo wao mwisho kwa kuchapwa mabao 3-1 na Italia.

Thursday, June 25, 2015

ADRIANO MGUU NDANI MGUU NJE BARCELONA.

WAKALA wa mshambuliaji nyota wa Barcelona, Adriano amedai kuwa mteja wake huyo anaweza kuondoka katika klabu hiyo kutokana na kukosa namba katika kikosi cha kwanza. Adriano mwenye umri wa miaka 30 amecheza mechi 16 pekee msimu uliopita akiwa ameanza katika kikosi cha kwanza mechi 10 kati ya hizo. Toka Jordi Alba atue Barcelona Adriano amekuwa akipata muda mchache wa kucheza katika kikosi timu hiyo. Wakala wa mchezaji huyo Paulo Affonso Neves amesema Adriano amekuwa akifanya kazi kwa bidii lakini hapewi nafasi ya kutosha ya kucheza ndio maana anataka kuondoka kutafuta timu itakayoweza kumpa nafasi hiyo. Neves aliendelea kudai kuwa kama Adriano ataendelea kubakia chaguo la tatu Barcelona itakuwa vyema kutafuta mahali pengine lakini hawna haraka katika hilo. Beki huyo wa zamani wa Sevilla ana mkataba na Barcelona unaomalizika mwaka 2017.

MAN CITY WANASA KINDA MATATA KUTOKA UTURUKI.

KLABU ya Manchester City imefanikiwa kumsajili mshambuliaji kinda mwenye umri wa miaka 19 Enes Unal kutoka klabu ya Bursaspor. Nyota huyo amefunga mabao manne katika mechi 35 za Ligi Kuu ya Uturuki alizoichezea timu hiyo lakini anaonekana atakuja kuwa moto baadae baada ya kuweka rekodi ya kufunga mabao 170 katika mechi 102 alizocheza katika timu za vijana. Kabla ya kuchagua kujiunga na City, Unal alikuwa akiwindwa pia na klabu za Arsenal, Chelsea na Manchester United. Rais wa Bursaspor, Recep Bolukbasi alithibitisha taarifa hizo na kudai kuwa Unal anatarajiwa kwenda Uingereza mwishoni mwa wiki hii kukamilisha usajili huo.

WENGER AANZA USAJILI KATIKA MAFUNGU, BAADA YA KUMSAJILI KINDA WA ROMANIA KWA EURO 100,000.

KLABU ya Arsenal imekamilisha usajili wa Vlad Dragomir kutoka klabu ya ACS Poli Timisoara kwa ada ya euro 100,000 huku kiungo huyo chipukizi akiepwa mkataba wa miaka mitatu. Usajili wa Dragomir mwenye umri wa miaka 16 unakuwa wa kwanza kufanyika katika kipindi hiki cha kiangazi na anatarajiwa kujiunga na akademi ya klabu hiyo. Chipukizi huyo ambaye alikuwa nahodha wa kikosi cha timu ya taifa ya Romania kea vijana chini ya umri wa miaka 16, alikuwa akihusishwa na tetesi za kwenda Inter Milan lakini mwenyewe amekiri nafasi ya kujiunga na Arsenal waliyopata ilikuwa ngumu kuikataa. Akihojiwa Dragomir amesema ofa aliyopewa na Arsenal ilionekana kuwa bora kwake na amefurahi kukamilisha usajili huo.

MARSEILLE YAKUBALI OFA YA WEST HAM KWA SHINGO UPANDE.

KLABU ya Marseille imekubali ofa kutoka kwa West Ham United kwa ajili ya nyota wao wa kimataifa wa Ufaransa Dimitri Payet lakini wamemtaka mchezaji kuendelea kubakia hapo. Katika siku za karibuni mshambuliaji huyo alikutana na viongozi wa klabu hiyo kuzungumzia mustakabali wake na kumuhakikishia rais wa Marseille Vincente Labrune kuwa ataendelea kuitumikia timu hiyo. Hata hivyo, Payet sasa ameamua kuwa anataka kuondoka kufuatia fungu kubwa la pesa lililotolewa na West Ham. Katika taarifa yake iliyotumwa katika mtandao, klabu hiyo imedai kuwa makubaliano yalishafikiwa Juni na Payet pamoja na wakala wake kuwa mchezaji huyo ataheshimu mkataba wake mpaka utakapomalizika mwaka 2017. Taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa siku tatu zilizopita wakala wa mchezaji huyo aliomba mkutano mwingine na Labrune na baada ya kukutana alimtaarifu juu ya ofa hiyo kubwa ya euro milioni 30 waliyopata kutoka West Ham. Rais huyo alishtushwa na taarifa hizo na kwakuwa wakala huyo alikutana na West Ham bila kuwa taarifa ombi lake la kutaka mkataba wa mteja wake kuangaliwa upya lilikataliwa kwa kipindi ambacho wakala huyo alitaka.

TABAREZ AMTETEA CAVANI BAADA YA BEKI LA CHILE 'KUMNAWA'.

KOCHA wa timu ya taifa ya Uruguay, Oscar Tabarez amemkingia kifua Edinsoni Cavani aliyetolewa nje jana katika mchezo war obo fainali ya michuano ya Copa America dhidi ya wenyeji Chile. Katika mchezo huo Uruguay walivuliwa ubingwa na wenyeji hao kea kufungwa bao 1-0 huku Cavani akionekana kuchangia bao hilo kutokana na kadi nyekundu aliyopewa kea kumpiga kibao beki wa Chile Gonzalo Jara. Picha za video zinaonyesha kabla ya Cavani kutenda kosa hilo Jara alimfuata kwa karibu na kuingiza mkono wake katika makalio ya mshambuliaji huyo ambaye alihamaki kea hasira. Akihojiwa Tabarez amesema alimtetea Cavani akidai mwamuzi msaidizi alipaswa kuliona tukio hilo kwani ndiye aliyekuwa karibu zaidi kuliko mwamuzi wa kati. Hiyo sio mara ya kwanza kwa Jara kuwafanyia wachezaji wenzake uhuni pindi wanapokutana na timu hiyo kwani mwaka 2013 mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez alimpiga ngumi beki huyo baada ya kushinda uume wake wakati wa mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia.

BRAZIL BADO HAWAJASAHAU KIPIGO CHA UJERUMANI - TAFFAREL.

GOLIKIPA wa zamani wa Brazil, Claudio Taffarel anaamini kovu la kutolewa katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana bado lipo ndani ya kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo wakati wakijiandaa na mchezo wao wa robo fainali ya michuano ya Copa America dhidi ya Paraguay. Brazil imefanikiwa kushinda mechi 12 kati ya 13 walizocheza toka wamalize katika nafasi ya nne katika Kombe la Dunia ambapo walishuhudia wakitandikwa mabao 10 katika mechi mbili kikiwepo kipigo cha mabao 7-1 kutoka kea Ujerumani katika mchezo nusu fainali. Pamoja na ujio wa kocha mpya Dunga kubadilisha mwelekeo wa kikosi hicho, Taffarel amedai wachezaji bado hawajapona sawasawa aibu waliyoipata kutoka katika michuano hiyo. Taffarel amesema itachukua muda wachezaji hao kusahau kipigo hicho lakini anaamini itafikia wakati watarejesha hali yao ya kujiamini na kuwaletea tena furaha mashabiki wa soka nchini Brazil na duniani kea ujumla.

BOCA JUNIORS YATHIBITISHA KUAFIKIANA NA JUVENTUS KUHUSU TEVEZ.

KLABU ya Boca Juniors imetangaza kuwa Carlos Tevez anatarajiwa kurejea katika timu hiyo ambayo ndio aliyoanza kucheza soka lake baada ya kufikiwa makubaliano na mabingwa wa Italia Juventus. Katibu Mkuu wa Boca, Cesar Martucci alikaririwa na redio moja nchini Argentina akidai kuwa usajili wa Tevez umeshakamilika, ingawa hakuna taarifa zozote rasmi kutoka Buenos Aires au Turin. Martucci amesema wana furaha kubwa baada ya kufanya kazi kubwa hatimaye wameweza kumshawishi Tevez kurejea tena nyumbani. Ingawa Martucci hakutoa taarifa za ndani zaidi kuhusiana na dili hilo lakini amesema Tevez anatarajiwa kutambulishwa mbele ya mashabiki wa Boca katika Uwanja wa Bombonera Julai 7 mwaka huu. Tevez mwenye umri wa miaka 31, aliwahi kuichezea Boca kuanzia mwaka 2001 mpaka 2004 kabla ya kutimkia Corinthians ya Brazil na baadae kutimkia Ligi Kuu katika klabu ya West Ham United mwaka 2006. Nyota huyo baadae alihamia Manchester United kabla ya kuhamia kea majirani zao Manchester City kea kitita cha paundi milioni 40 mwaka 2009 na kukaa hapo kwa misimu kisha kwenda Juventus mwaka 2013 mpaka sasa.

LAPORTA AAHIDI KUMSAJILI POGBA AKICHAGULIWA KUIONGOZA TENA BARCELONA.

MGOMBEA urais wa klabu ya Barcelona, Joan Laporta ana uhakika kiungo wa Juventus Paul Pogba atakuwa radhi kutua Camp Nou. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22, amekuwa akitajwa kama mmoja wachezaji bora kabisa katika soka kipindi hiki na amekuwa kihusishwa na tetesi za kuondoka jijini Turin zaidi ya mara moja pamoja na kuwa na mkataba na mabingwa hao wa Serie A mpaka mwaka 2019. Barcelona in moja wapo ya timu zilizoonyesha in ya kumsajili Pogba na Laporta amedokeza yuko tayari kumsajili kiungo huyo kama akichaguliwa kuwa rais wa klabu hiyo tena. Laporta alijinadi kuwa amekuwa na mahusiano ya karibu na wakala wa mchezaji huyo Mino Raiola hivyo anaamini haitamuwia vigumu kumsajili mchezaji huyo kama kichaguliwa tena kuiongoa timu hiyo. Laporta ambaye amewahi kuingoza Barcelona kuanzia mwaka 2003 mpaka 2010 anakabiliwa na upinzani kutoka kwa rais wa sasa Josep Maria Bartomeu, Jordi Majo na Agusto Benedito katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.V

SOUTHGATE AKOMAA PAMOJA NA KUTOLEWA EURO U21.

KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza kwa vijana chini ya umri wa miaka 21, Gareth Southgate amedai kuwa bado anataka kuendelea kuinoa timu hiyo pamoja na kuenguliwa katika michuano ya Ulaya kwa vijana wa umri huo inayoendelea huko Jamhuri ya Czech. Uingereza jana ilishindwa kufua dafu mbele ya Italia baada ya kukubali kucharangwa mabao 3-1 katika mchezo huo. Southgate ambaye mkataba wake unafikia kikomo mwaka 2017 amesema anataka kuendelea mpaka hapo atakapomaliza mkataba huo. Southgate alikwenda katika michuano hiyo ya nyota Saido Berahino aliyekua majeruhi, huku akiwakosa Raheem Sterling, Jack Wilshere na Ross Barkley ambao wangeweza kukisaidia kikosi hicho lakini waliachwa kutokana na majukumu yao katika timu ya wakubwa.

ETO'O NJIANI KWENDA UTURUKI.

MCHEZAJI bora wa zamani wa Afrika, Samuel Eto’o ameripotiwa kukubali kusajiliwa na klabu ya Antalyaspor ambaye imepanda katika Ligi Kuu ya Uturuki msimu huu. Klabu hiyo ilithibitisha kuwa wamefikia makubaliano na Eto’o lakini bado hawajasaini dili lolote rasmi. Katika taarifa yake, klabu hiyo imedai dili hilo limekwama kutokana na Eto’o kuwa na matatizo kuhusiana na haki za matangazo nchini Italia na pindi atakapomaliza ataelekea nchini humo kusaini mkataba. Mapema mwezi huu vyombo vya habari nchini Italia vilimkariri rais wa klabu ya Sampdoria Massimo Ferrro akidai kuwa anaamini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 ataondoka ikiwa in miezi sita imepita toka atue Italia. Nahodha huyo wa zamani wa Cameroon amewahi kucheza katika klabu za Barcelona, Inter Milan, Chelsea na Everton huku akifanikiwa kunyakuwa tuzo mbili za mchezaji bora wa mwaka wa Afrika.

Wednesday, June 24, 2015

Zinedine Zidane & his Son vs F2 Freestylers - adidas The Base

ROBO FAINALI COPA AMERICA.

B

ROMA YAMNASA BERTOLACCI.

KLABU ya AS Roma imetangaza rasmi katika mtandao wake kuwa imemnyakuwa moja kwa moja Andrea Bertolacci kwa kitita cha euro milioni 8.5. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 alikuwa akimilikiwa nusu na Roma pamoja na timu ya Genoa ambayo ameitumikia katika misimu mitatu iliyopita. Hata hivyo, nyota huyo sasa amepata nafasi ya kurejea tena Roma kufuatia kuonyesha kiwango bora akiwa na Genoa. Katika taarifa yake Roma ilithibitisha taarifa hizo za kumsajili moja kwa moja Bertolacci ambaye ameanzia soka lake katika shule ya michezo ya klabu hiyo.

RENARD AMTAKA JORDAN AYEW LILLE.

MENEJA wa klabu ya Lille, Herve Renard amedai kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana Jordan Ayew anataka kuikacha klabu ya Loriente na kujiunga na timu yake. Renard amewahi kufanya kazi na Ayew wakati akiinoa klabu ya Sochaux ambako kinda huyo alikuwa akicheza kwa mkopo akitokea Olimpique Marseille. Wawili hao walitengeneza mahusiano ya karibu kati yao na sasa baada ya Renard kuchukua kibarua Lille anataka kumsajili nyota huyo. Akihojiwa Renard amesema ana uhakika Ayew anataka kujiunga na kikosi chake lakini ana viongozi wake ambao ndio wataamua mustakabali wake.

NFF YARIDHISHWA NA UTETEZI WA KESHI.

SHIRIKISHO la Soka la Nigeria-NFF limesisitiza kuwa Stephen Keshi ataendelea kubakiwa kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo pamoja na taarifa zinazomhusisha na kuomba kibarua katika timu ya Ivory Coast. Keshi aliorodheshwa miongoni mwa majina 60 ya makocha walioomba kibarua cha kuinoa nchi hiyo na Shirikisho la Soka la Ivory Coast. Taarifa hizo zilileta mkanganyiko na kufanya kamati ya nidhamu na sheria kukutana kwa dharura kujadili suala hilo huku Keshi mwenyewe akiitwa kujieleza na kukanusha taarifa hizo. Mwenyekiti wa kamati hiyo Christopher Green amebainisha kuwa uchunguzi zaidi utaendelea baada ya kusikiliza utetezi wa Keshi katika kikao chao kilichoketi jijini Abuja. Green aliendelea kudai kuwa wakati uchunguzi huo ukiendelea Keshi ataendelea na kibarua chake kama kawaida. Mbali na kuinoa Nigeria, Keshi pia amewahi kuzifundisha timu za taifa za Mali na Togo.

CAVANI MGUU NDANI MGUU NJE COPA AMERICA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Uruguay, Oscar Tabarez ameonyesha matumaini yake kuwa Edinson Cavani atabakia katika kikosi chake baada ya baba wa mshambuliaji huyo kukamatwa kufuatia kupata ajali ya barabarani. Nyota huyo wa Paris Saint-Germain ameripotiwa kutojua la kufanya kama abakie au arudi nyumbani Uruguay kuwa na baba yake kufuatia ajali hiyo aliyopata juzi. Hata hivyo, Cavani alionekana akifanya mazoezi na wenzake jana wakati wakijiandaa na mchezo wao robo fainali ya michuano ya Copa America dhidi ya wenyeji Chile baadae leo. Tabarez aliwaambia wanahabari kuwa Cavani atapewa muda wa kuamua mwenyewe kuhusiana na suala hilo. Vyombo vya habari nchini Uruguay vimeripoti kuwa kijana mwenye umri wa miaka 19 aliyekuwa akiendesha pikipiki alifariki kwa kugongwa na gari ambalo lilikuwa likiendeshwa na baba yake Cavani. Mzee huyo alikamatwa baada ya ajali hiyo huku uchunguzi ukiendelea kujua chanzo chake.

LIVERPOOL YAKAMILISHA USAJILI WA FIRMINO.

KLABU ya Liverpool, imefanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji Roberto Firmino kutoka timu ya Hoffenheim kwa kitita cha paundi milioni 29. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya baada ya kurejea kutoka Chile ambako anaitumikia Brazil katika michuano ya Copa America. Firmino ambaye amefunga mabao 49 katika mechi 153 alizoichezea Hoffenheim anakuwa mchezaji wa pili ghali kuwahi kusajiliwa na Liverpool. Liverpool iliwahi kuweka rekodi yake ya usajili kwa Andy Carroll ambaye alijiunga nao kwa kitita cha paundi milioni 35 akitokea klabu ya Newcastle United mwaka 2011.

PELLEGRINI AMPONDA MOURINHO.

MENEJA wa Manchester City, Manuel Pellegrini amemponda hasimu wake Jose Mourinho akidai meneja huyo wa Chelsea anapenda kusifiwa kea kila kitu. Mourinho ameingoza Chelsea kunyakuwa taji la Ligi Kuu msimu uliopita, wakimaliza kea alama nane mbele ya City walioshika nafasi ya pili. Lakini Pellegrini anaamini tabia ya jinsi wao wawili wanavyosheherekea ubingwa unaonyesha kea kiasi walivyo tofauti huku kocha huyo raia wa Chile akimtuhumu Mourinho kutotambua mchango wa wachezaji wake. Akihojiwa kuhusiana na hilo Pellegrini amesema wakati Mourinho akishinda anataka sifa zote apewe yeye hali ambayo in tofauti kwake kwani aliposhinda taji hilo hakusema lolote. Hata hivyo kocvha huyo aliongeza kuwa hana tatizo lolote na Mourinho na pia sio adui yake lakini anaamini wanatofautiana kea kiasi kikubwa.

MKWASA AITA 26 TAIFA STARS.

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine leo amemtambulisha kocha mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Charles Boniface Mkwasa mbele ya waandishi wa habari. Akiongea na waandishi wa habari, Mwesigwa amewaomba wadau wa mpira wa miguu nchini kuwapa sapoti makocha hao wazawa wanaoanza kazi kesho kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda julai 4, 2015 jijini Kampala. Mara baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari, Mkwasa amesema anashukuru kwa TFF kumpatia nafasi hiyo ya kuingoza Taifa Stars na msaidizi wake Hemed Morocco, na kuomba watanzania kuwapa sapoti. Mkwasa amesema cha kwanza atakachokifanya na msaidizi wake Morocco ni kurudisha imani ya watanzania juu ya timu yao ya Taifa, kisha watajitahidi kadri ya uwezo wao kuhakikisha kuwa timu inafanya vizuri katika michezo inayowakabili. Aidha Mkwasa ametangaza kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kesho alhamisi katika hoteli ya Tansoma tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda. Wachezaji walioitwa ni makipa: Mudathir Khamis (KMKM), Mwadini Ally (Azam), Ally Mustafa “Barthez” (Yanga). Walinzi: Shomari Kapombe (Azam), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Mohamed Hussein “Tshabalala” (Simba), Haji Mwinyi (KMKM), Nadir Haroub “Cannavaro” (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Hassan Isihaka (Simba), Aggrey Morris (Azam).
Viungo: Jonas Mkude (Simba), Abdi Banda (Simba), Salum Telela (Yanga), Frank Domayo (Azam). Viungo wa pembeni: Saimon Msuva (Yanga), Said Ndemla (Simba), Deus Kaseke (Mbeya City), Ramadhan Singano “Messi” (Simba). Washambuliaji: John Bocco (Azam), Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar) na Ame Ally (Mtibwa Sugar). Wachezaji Juma Abdul (Yanga), Mudathir Yahya (Azam) na Samwel Kamuntu (JKT Ruvu) wameitwa kama wachezaji wa akiba katika kikosi cha timu ya Taifa kinachoingia kambini kesho. Katika hatua nyingine Mkwasa ametangaza benchi la ufundi la Taifa Stars, kocha msaidizi Hemed Morocco, kocha wa magolikipa Peter Manyika, Mshauri wa timu Abdallah Kibadeni, mtunza vifaa Hussein Swedi Gaga huku mratibu wa timu akiwa ni Alhaj Ahemd Mgoyi. Kamati ya tiba ya TFF itapendekeza majina ya daktari wa timu na mchua misuli watakaoungana na kambi ya Taifa Stars.

Tuesday, June 23, 2015

NOOIJ AWAAGA WATANZANIA, MKWASA KUINOA STARS.

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania - TFF, Jamal Malinzi leo ameagana rasmi na aliyekua kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, mholanzi Mart Nooij. Akiongea na waandishi wa habari leo katika hoteli ya Tansoma, Malinzi amesema wameamua kuagana nae mbele ya vyombo ya habari kama iliyofanyika pia wakati wa utambulisho wake wakati wa kuanza kazi. “Mpira wa miguu unachangamoto nyingi, watanzania tunasafari ndefu katika mafanikio ndio maana TFF imeanza kuwekeza katika soka la vijana, sababu ndio msingi wa kuwa na timu bora ya Taifa” alisema Malinzi. Duniani kote chimbuko la timu bora ni soka la vijana na watoto, tukiwa na vijana wengi walioanza kucheza mpira katika umri mdogo wanapofikia umri wa kuchezea timu ya Taifa tutakua na kikosi bora. Nchi za wenzetu inapofikia kocha kuita wachezaji wa timu ya Taifa anakuwa na wigo mpana, kwetu sisi wachezaji wanocheza soka nje ya nchi wanahesabika, hivyo ni lazima tuanze kuwekeza kwenye soka la vijana TFF ilishaanza mkakati huo ndio maana kuna timu za U13, U15 ambazo zitakua zikiingia kambini na kucheza michezo ya kirafiki ndani ya nje kwa lengo la kupata uzoefu kabla ya kushiriki kuwania kufuzu kwa fainali za vijana mwaka 2016. Kikosi cha U15 kinatarajiwa kufanya ziara mwezi Disemba mwaka huu katika nchi za Malawi, Zambia, Zimbambwe, Botswana na Afrika Kusini, kisha mwakani mwezi April 2016 kitaenda Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya kucheza michezo ya kirafiki. Naye Mart Nooij aliyekua kocha wa Taifa Stars, akiongea na waaandishi wa habari alisema anawashukuru watanzania wote, serikali, wadau wa mpira wa miguu nchini na TFF kwa sapoti waliyompatia wakati akiwa kocha mkuu wa timu ya Taifa. Nooij alisema alifurahia maisha yake akiwa Tanzania kwa kipindi chote alichokua akifundisha timu ya Taifa, lakini kwa sababu imefikia mwisho wa ajira yake hana jinsi anaondoka, lakini ataendelea kuikumbuka Tanzania na watanzania wote kila siku kwa ukarimu wao. Wakati huo huo Rais wa TFF. Jamal Malinzi amemtangaza Charles Mkwasa kuwa kocha mpya wa Taifa Stars akisaidiwa na kocha Hemed Morocco, Mkwasa ambaye ni kocha wa Yanga na Morocco kocha wa Mafunzo watafanya kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo timu ya taifa itakua na michezo ya kuwania kufuzu kwa CHAN na AFCON. Malinzi amesema uteuzi wa makocha hao wazawa umezingatia vigezo vya makocha wa timu ya Taifa kuwa na leseni A ya ukocha kutoka CAF au zinazofanana kutoka mashiriksho mengine duniani wanaozifanyia kazi, jambo ambalo makocha hao wazawa wamekizi. Kocha Mkwasa atakua akipewa hudumu zote na masilahi (zikiwemo posho) alizokuwa anapewa kocha aliyeondoka, pia amepewa nafasi ya kuchagua benchi lake la ufundi la kufanya nalo kazi, hivyo nawaomba wadau wa mpira wa miguu na watanzania kwa ujumla tuwape sapoti makocha hao wazawa” aliongeza Malinzi” Aidha Kamati ya utendaji ya TFF Iimemteua Alhaj Ahmed Mgoyi kuwa mratibu wa timu ya Taifa, lengo la uteuzi huo wa Mgoyi ni kuwa kiunganishi kati ya kamati ya Utendaji na timu ya Taifa.

MANDZUKIC AMWAGA WINO WA MIAKA MINNE JUVENTUS.

KLABU ya Juventus imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Croatia, Mario Mandzukic kutoka Atletico Madrid kwa ada ya paundi Milioni 13.6. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amekamilisha vipimo vya afya jana jijini Turin kabla ya kusaini mkataba wa miaka minne na mabingwa hao wa Italia. Mandzukic anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa Juventus kuelekea msimu mpya, baada ya awali kusajiliwa mshambuliaji wa Argentina, Paulo Dybala kutoka Palermo na Sami Khedira kutoka Real Madrid mapema mwezi huu. Akihojiwa Mandzukic amesema anafuraha kubwa kutua katika klabu kubwa kama Juventus na ana matumaini makubwa ya kuisaidia timu hiyo kushinda mataji zaidi.

KINDA LA CHELSEA KUTOKA BURKINABE LAPATA KIBALI.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Burkina Faso, Bertrand Traore sasa anatarajiwa kucheza katika kikosi cha kwanza cha Chelsea baada ya kupata kibali cha kazi. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 19 alisajiliwa na Chelsea Januari mwaka 2014 lakini alikuwa hajafuzu kupata kibali hivyo kumfanya kupelekwa kea mkopo katika klabu ya Vitesse Arnhem ya Uholanzi. Chelsea iliomba tena kibali kipindi hiki cha kiangazi na kufanikiwa kupata chini ya mfumo mpya wa Chama cha Soka cha Uingereza. Traore sasa anatarajiwa kuwepo katika ziara ya Chelsea watakayoifanyika nchini Marekani ambapo watacheza na timu za New York Red Bulls, Paris Saint-Germain na Barcelona kama sehemu ya maandalizi kea ajili ya msimu ujao.