Friday, June 26, 2015

LIVERPOOL YAONGEZA OFA KWA CLYNE.

KLABU ya Liverpool imeboresha ofa yake kufikia paundi milioni 12.5 kwa ajili ya kutaka kumsajili beki wa kulia wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Southampton Nathaniel Clyne. Mwezi uliopita Southampton walikataa ofa ya paundi milioni 10 iliyotolewa na Liverpool kwa ajili ya beki huyo mwenye umri wa miaka 24. Klabu hizo mbili zimeendelea na mazungumzo huku Southampton wo wakitaka paundi milioni 15 kwa ajili ya mchezaji huyo ambaye amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake. Liverpool wamekuwa wakimuwinda Clyne baada ya kuondoka kwa Glen Johnson mwenye umri wa miaka 30 mwishoni mwa msimu huu. Klabu hiyo inampa ofa Clyne ambaye alijiunga na Southampton akitokea Crystal Palace Julai mwaka 2012, mkataba wa miaka mitano. Kama wakifanikiwa, huo utakuwa usajili wa sita kwa Liverpool katika kipindi cha usajili wa kiangazi baada ya kuwa tayari wameshwasajili beki Joe Gomez, kiungo James Milner, washambuliaji Danny Ings na Roberto Firmino pamoja na golikipa Adam Bogdan.

No comments:

Post a Comment