Friday, June 26, 2015

DE JONG AONGEZA MIAKA MITATU MILAN.

KLABU ya AC Milan imetangaza kuwa Nigel de Jong amesaini mkataba mpya ambao utamuweka katika klabu hiyo mpaka majira ya kiangazi mwka 2018. Kiungo huyo mzoefu mkataba wake wa sasa ulikuwa unamalizika wiki ijayo na hivyo kuzua tetesi juu ya mustakabali wake wa kubakia San Siro huku kukiwa na minong’ono ya kutakiwa na Schalke pamoja na klabu yake ya utotoni ya Ajax Amsterdam. Hata hivyo, De Jong mwenye umri wa miaka 30 ameamua kubakia Milan na kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu. Kiungo huyo alijiunga na Milan akitokea Manchester City majira ya kiangazi mwaka 2012 na toka wakati huo ameimarika na kuwa mchezaji muhimu wa timu hiyo.

No comments:

Post a Comment