Friday, June 26, 2015

JORDI ALBA ATAKA KUZEEKEA BARCELONA.

BEKI mahiri wa Barcelona, Jordi Alba amesisitiza kuwa anafurahia maisha katika timu hiyo na amepanga kubakia hapo mpaka atakapoamua kutundika daruga zake. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 ambaye ametokea katika shule ya klabu hiyo, alirejea Camp Nou majira ya kiangazi mwaka 2012 baada ya kuzitumikia klabu za Cornella, Valencia na Gimnastic ambapo toka wakati huo ameimarika na kuwa mchezaji muhimu. Alba pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Barcelona ambacho kilinyakuwa mataji mataji msimu uliopita na bado anaonyesha kuwa na njaa ya kunyakuwa matji zaidi. Akihojiwa nyota huyo wa kimataifa wa Hispania amesema anataka kuichezea Barcelona kwa miaka mingi ijayo kwani amejifunza mengi katika kipindi cha miaka mitatu. Alba ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2020 amesema pamoja na kuwa hajui itakavyokuwa huko mbele lakini kama itawezekana angependa kutundika daruga zake akiwa Barcelona.

No comments:

Post a Comment