Thursday, April 30, 2015

TAMBWE AISHITAKI SIMBA.

MCHEZAJI Amissi Tambwe aliwasilisha malalamiko dhidi ya Simba ya kutolipwa dola 7,000 za Marekani zilizotokana na klabu hiyo kuvunja mkataba wake Desemba 15, 2014. Uamuzi wa kuvunja mkataba ulikuwa ni wa makubaliano ya pande zote ambapo Simba ilitakiwa iwe imemlipa fedha hizo mlalamikaji kufikia Desemba 17, 2014. Katibu Mkuu wa Simba SC , Steven Ally alikiri klabu yake kudaiwa na mchezaji huyo na kuwa wameshafanya mawasiliano na wakili wake aliyepo Ureno, Felix Majani na kupanga utaratibu wa kulipa isipokuwa kinachosubiriwa ni kusaini hati ya makubaliano ya malipo (Deed of Settlement). Kamati imesikitishwa na klabu ya Simba kushindwa kumlipa mchezaji huyo kama ilivyokuwa katika makubaliano ya kuvunja mkataba yaliyofikiwa na pande zote mbili Desemba 15, 2014. Klabu ya Simba inatakiwa kumlipa Amissi Tambwe fedha hizo kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ya dola 5,000 malipo yawe yamefanyika kufikia Aprili 30, 2015. Salio la dola 2,000 ili kukamilisha jumla ya dola 7,000 liwe limelipwa kufikia Mei 10, 2015, uamuzi ambao upande wa Simba ulikubaliana nao.

SIMBA WATAKIWA KUMLIPA CHANONGO MIL 11.

KLABU ya Simba SC inatakiwa kumlipa mchezaji Haruni Chanongo sh. 11,400,000, kufikia Aprili 30, 2015 vinginevyo Sekretarieti ya TFF itaanza kukata mapato ya Simba ili kumlipa mchezaji huyo. Iwapo Simba itakuwa na vielelezo vingine katika kikao kinachofuata cha Kamati kitakachofanyika Mei 3, 2015 itafanywa hesabu na Simba kurejeshewa fedha itakayokuwa imezidi. Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF imeagiza kwa klabu ya Simba na klabu nyingine zote kuwa kwa wachezaji wa mkopo, maslahi yao (mishahara na posho) yote yailipwe na klabu husika kwa klabu ambayo mchezaji anakwenda kwa mkopo ili malipo yake yawe yanafanyika kutoka kwenye klabu moja badala ya kufuatilia malipo yake katika klabu mbili tofauti, hali hii inaweza msabababishia usumbufu mchezaji aliye kwenye mkopo.

JUVENTUS YAKUBALI KUMUUZA POGBA KWENDA PSG KWA EURO MILIONI 80.

KLABU za Paris Saint-Germain-PSG na Juventus zimekubaliana ada ya euro milioni 80 kea ajili ya uhamisho wa kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Paul Pogba. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mtandao wa Goal, zimedai kuwa ofa ya PSG imekubaliwa na Juventus kea ajili ya usajili wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye amekuwa mchezaji muhimu toka aondoke Manchester United mwaka 2012. Lakini pamoja na mabingwa hao wa Ufaransa kuonekana kukaribia kumnasa nyota huyo bado hakuna uhakika kama mwenyewe atakuwa kurejea jijini Paris. Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi alikutana na Pogba na wawakilishi wake huko Monte Carlo mapema wiki hii lakini hawakufikia makubaliano ya masuala binafsi ikiwemo mshahara atakaolipwa. Inaaminika kuwa Pogba yuko tayari kusubiria ili kuona ofa nyingine ambazo anaamini zitakuja katika kipindi cha majira ya kiangazi.

ASTON VILLA KUMUUZA BENTEKE KWA EURO MILIONI 42.

KLABU ya Aston Villa itahitaji kitita cha euro milioni 42 kwa ajili ya mshambuliaji wake Christian Benteke ambaye anawindwa na Liverpool katika majira ya kiangazi. Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amekuwa akimhusudu mshambuliaji huyo huku akiwa amepania kuimarisha safu yake ya ushambuliaji pindi dirisha la usajili litakapofunguliwa. Wakala wa Benteke alidai mapema wiki hii kuwa hakuna timu iliyojitokeza kumtaka mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji lakini Villa wenyewe wameamua kujitayarisha kama litatokea lolote. Meneja wa Villa Tim Sherwood anatarajia kuitaka klabu hiyo kuzuia ofa yeyote itakayotolewa kea ajili ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha timu hiyo msimu huu huku akiwasaidia kutinga fainali ya Kombe la FA. Klabu za Manchester United na Tottenham Hotspurs nazo pia zinahusishwa na tetesi za kumtaka Benteke lakini Liverpool ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kumchukua nyota huyo.

HATMA YA DROGBA ITAAMULIWA NA ABRAMOVIC - MOURINHO.

MENEJA wa Chelsea, Jose Mourinho amebanisha kuwa hatma ya mshambuliaji wake Didier Drogba iko mikononi mwa mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovic. Drogba alijiunga tena na Chelsea katika majira ya kiangazi mwaka jana kea uhamisho huru akitokea Galatasaray baada ya kuitumikia klabu hiyo miaka nane mara ya kwanza. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 37 amecheza mechi 27 msimu huu wakati Chelsea ikikaribia kunyakuwa taji lake la kwanza la Ligi Kuu katika kipindi cha miaka mitano lakini anatarajia kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu. Inaripotiwa kuwa Mourinho sasa anataka kuleta washambuliaji wapya vijana Stamford Bridge huku Charlie Austin wa QPR na Paulo Dybala wa Inter Milan wakipewa nafasi ya kuziba pengo la Drogba. Hata hivyo, Mourinho amefafanua kuwa mustakabali wa Drogba utaamuliwa na Abramovic na kuongeza kuwa nyota huyo amekuwa sehemu ya historia ya klabu hiyo.

SPURS YAJIHAKIKISHIA KUNYAKUWA SCHNEIDERLIN.

KLABU ya Tottenham Hotspurs ina uhakika wa kushinda mbio za kumuwania nyota wa Southampton Morgan Schneiderlin katika kipindi hiki cha kiangazi huku wakiwa tayari kuwatoa nyota wake Andros Townsend au Benjamin Stambouli ili kusaidia kukamilisha azma hiyo. Klabu za Arsenal na Chelsea pia zimekuwa zikimuwinda nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa lakini Spurs sasa wanaamini lazima atatua White Hart Lane. Spurs walishajaribu kumsajili Schneiderlin majira ya kiangazi mwaka jana lakini ofa yao ilizuiwa na Southampton.Hata hivyo inaaminika kuwa sasa nyota huyo anataka kuondoka majira ya kiangazi huku Southampton wakiripotiwa kutaka kitita cha paundi milioni 20.

PAMOJA NA MAN UNITED KUCHOMOA, PSG YAZIDI KUMKOMALIA DI MARIA.

WINGA wa Manchester United, Angel Di Maria bado anawindwa na klabu ya Paris Saint-Germain-PSG ambao wamepania kumsajili majira ya kiangazi. United wao imesisitiza kuwa hawana mpango wa kumuuza winga huyo ambaye alivunja rekodi ya usajili wa paundi milioni 59.7 mwaka jana. Lakini hata hivyo, nyota huyo wa zamani wa Real Madrid amekuwa akisugua benchi katika mechi tano za United zilizopita huku akishindwa kung’aa katika timu hiyo kama ilivyotegemewa. PSG walijaribu kumsajili Di Maria majira ya kiangazi mwaka jana lakini mipango yao ilishindwa kutokana na kubanwa na sheria za matumizi ya fedha za Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA.

MAMA WA MCHEZAJI KINGA ARSENAL ATIMULIWA KWA VURUGU.

KLABU ya Arsenal imemfungia mama wa mmoja wa wachezaji wao nyota chipukizi Ainsley Maitland-Niles baada ya mama huyo kumpiga mmoja ya wasaidizi wa meneja Arsene Wenger, Dick Law na kutishia kumtoa mwane uwanjani wakati wa mechi ya vijana chini ya umri wa miaka 21. Polisi waliitwa katika uwanja wa mazoezi wa Arsenal mwezi uliopita na kumkamata mama huyo kwa tuhuma za kufanya vurugu ingawa hakuna hatua yeyote zaidi iliyochukuliwa. Maitland-Niles msimu huu amekuwa mchezaji wa pili mdogo kuiwakilisha Arsenal katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wakati alipochukua nafasi ya Aaron Ramsey katika mchezo dhidi ya Galatasaray Desemba mwaka jana akiwa na umri wa miaka 17 na siku 102. Siku nne baadae chipukizi huyo anayecheza nafasi ya kiungo alicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu katika mchezo dhidi ya Newcastle United ambao Arsenal walishinda mabao 4-1 huku pia akicheza kama mchezaji wa akiba katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Hull City.

TORRES ANG'ARA ATLETICO IKIPATA USHINDI MWEMBAMBA.

MSHAMBULIAJI nyota wa Atletico Madrid, Fernando Torres anaamini ameisogeza timu hiyo karibu na michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufunga bao la ushindi katika mchezo wa La Liga dhidi ya Villarreal jana. Nyota huyo wa zamani wa Liverpool alitumia vyema makosa ya Eric Bailly na kufunga bao hilo pekee katika dakika ya 74 akiwa ameingia akitokea benchi. Mabingwa hao wakiwa alama saba juu ya Valencia waliopo nafasi ya tano katika msimamo wa ligi, Torres ana uhakika kuwa watafuzu tena kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa. Akihojiwa Torres amesema katika mchezo huo walikaa na mpira kea kipindi kirefu lakini walishindwa kutengeneza nafasi ingawa hata hivyo wanashukuru kea ushindi huo mwembamba waliopata. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa bao lake hilo lina maana kubwa kwani wamejiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa mwakani.

PARMA YASHUKA DARAJA RASMI.

KLABU ya Parma imeshuka rasmi kutoka katika Serie A baada ya msimu wa misukosuko ambao umewafanya kutangazwa mufilizi na kupokonywa alama tisa kutoka na makosa ya kifedha. Kipigo walichopata kutoka kea Lazio na sare ya mabao 2-2 dhidi ya Atalanta kinaifanya timu hiyo inayonolewa na Roberto Donadoni kukaa mkiani mwa msimamo wa ligi. Parma ilitangazwa mufilisi Machi mwaka huu wakiwa na deni linalofikia paundi milioni 54. Wachezaji wa timu hiyo hawajalipwa msimu huu na wamekuwa wakifua nguo zao wenyewe na kuendesha basi la timu. Parma ambao wamebadilisha wamiliki mara mbili msimu huu walikuwa washindi wa pili wa Serie A mwaka 1997 huku wakiwa wamewahi kushinda taji la Uefa Cup mwaka 1995 na 1999.

INZAGHI ADAI BADO HAJAKATA TAMAA.

MENEJA wa AC Milan, Filipo Inzaghi amesisitiza hataki kukata tamaa pamoja nay a kuzuka kwa mjadala kuhusiana na mustakabali wake. Milan ilitandikwa mabao 3-1 nyumbani na Genoa jana na kuendelea matokeo mabovu kea timu hiyo katika mechi nne zilizopita hivyo kuwafanya kubakia katika nafasi ya 10 katika msimamo wa Serie A wakipitwa alama tano na mahasimu wao Inter Milan. Kumekuwa na tetesi kuwa Inzaghi atatimuliwa mwishoni mwa msimu huu huku kocha Primavera Christian Brocchi akiripotiwa kuchukua mikoba yake. Hata hivyo, Inzaghi amepuuza tetesi hizo na kuwataka wachezaji kumaliza msimu wakiwa imara kea ajili ya heshima ya timu hiyo kongwe. Akihojiwa Inzaghi aliwapongeza wapinzani wao na kuomba radhi mashabiki wachache waliojitokeza katika Uwanja wa San Siro na kuahidi kuwa ataendelea kupambana kuhakikisha timu hiyo inarejesha heshima yake.

CHELSEA KUTANGAZA UBINGWA MBELE YA CRYSTAL PALACE?

KLABU ya Chelsea imebakisha mchezo mmoja wa ushindi ili waweze kutawadhwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu baada ya kutoka nyuma na kuichapa Leicester City jana katika Uwanja wa King Power. Kikosi hicho cha Jose Mourinho kililazimika kutumia mbinu zake zote kuhakikisha wanashinda katika mchezo huo mgumu dhidi ya Lecister. Ushindi huo sasa unaifanya Chelsea kukabikiwa na mechi moja ya ushindi na kama wakifanikiwa kuifunga Crystal palace katika mchezo wao utakaofanyika katika Uwanja wa Samford Bridge Jumapili hii watakuwa mabingwa rasmi wa Uingereza. Chelsea ilikuwa watangazwe mabingwa jana lakini sare ya bila kufungana dhidi ya Arsenal katika Uwanja wa Emirates Jumapili iliyopita ilikwamisha sherehe zao hizo.

WOLFSBURG YATAMBA KUICHAPA DORTMUND DFB POKAL.

MENEJA wa klabu ya Wolfsburg Dieter Hecking amesema kikosi chake kitafanya kila iwezalo kuhakikisha wanaichapa Borussia Dortmund katika mchezo wa fainali ya Kombe la Ujerumani baada ya kuichapa Arminia Bielefeld. Wolfsburg wanaoshika nafasi ya pili walitinga katika hatua hiyo jana baada ya kushinda mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya timu hiyo ya daraja la tatu kwa mabao 4-0. Heckin ana uhakika kikosi chake kiko tayari kukabiliana na Dortmund ambao waliwang’oa Bayern Munich kwa changamoto ya mikwaju ya penati katika nusu fainali nyingine iliyochezwa juzi. Kocha huyo amesema kwasasa wako imara na kikosi kipo katika kiwango ambacho walikuwa wakikihitaji. Heckin aliendelea kudai kuwa hajali timu gani watakayokutana nayo katika fainali kwani anachojua yeye wana uwezo wa kupambana na yeyote.

Tuesday, April 28, 2015

BAADA YA KUKOSA WALICHOHITAJI KWA BALOTELLI, LIVERPOOL SASA YAMNYEMELEA JOVETIC.

KLABU ya Liverpool imeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Stevan Jovetic katika kipindi cha majira ya kiangazi. Kikosi hicho cha Brendan Rodgers kimekuwa na mapungufu katika safu ya ushambuliaji msimu huu hivyo kuamua kuongeza ngumu katika upande mapema pindi dirisha la usajili litakapofunguliwa. Mshambuliaji alitegemewa kuokoa jahazi Mario balotelli ambaye alisajiliwa katika dakika za mwisho katika saujili wa mwaka jana ameshindwa kuonyesha cheche zake akiwa amefunga bao moja pekee katika Ligi Kuu toka atue Anfield. City wanadaiwa kuwa tayari kumuuza Jovetic katika majira ya kiangazi lakini wangependelea zaidi mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kwenda Serie A huku Sampdoria wakitajwa kuweza kumchukua.

WAKALA WA DE BRUYNE ADAI NYOTA HUYO ANA THAMANI YA EURO MILIONI 60.

WAKALA wa kiungo wa Wolfsburg Kevin De Bruyne amedai kuwa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG imeonyesha nia ya kutaka kumsajili mteja wake huyo lakini amesema anaweza kuwagharimu kitita cha euro milioni 50 hadi 60. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 ameimarika na kuja kuwa mchezaji muhimu katika klabu hiyo toka alipojiunga nao akitokea Chelsea Januari mwaka jana. Katika kipindi cha karibuni De Bruyne amekuwa akihusishwa na tetesi za kutakiwa Manchester City na Bayern Munich lakini wakala wake Patric De Koster amesisitia PSG ndio wako katika nafasi nzuri ya kunyakuwa kiungo huyo. Akihojiwa De Koster amesema PSG in klabu inayovutia na anadhani itakuwa sahihi kea mteja huyo kuitumikia. Hata hivyo De Koster aliendelea kudai kuwa mchezaji kama De Bruyne ana thamani ya kati ya euro milioni 50 hadi 60 kea soko la sasa na klabu zinazodai kuwa ziko tayari kutoa euro milioni 30 haziko karibu na ukweli.

KOCHA WA BARCELONA CHUKUA TAHADHARI KWA KUWAPUMZISHA NYOTA WAKE.

MENEJA wa Barcelona, Luis Enrique ameamua kuwaacha Gerard Pique na Thomas Vermaelen katika kikosi chake kea ajili ya mchezo wa La Liga dhidi ya Getafe. Pique amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Barcelona msimu huu lakini hatakuwepo katika mchezo huo baada ya Enrique kuamua kumpumzisha. Wakiwa bado na nafasi ya kupigania taji la La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Mfalme, kocha huyo amemua kutomuharakisha Vermaelen kurejea baada ya kupona majeruhi yaliyokuwa yakimkabili. Beki huyo wa kimataifa wa Ubelgiji hajacheza mechi yeyote ya mashindano kea Barcelona toka ajiunge nao akitokea Arsenal katika majira ya kiangazi mwaka jana baada ya kusumbuliwa na majeruhi ya misuli kwa kipindi kirefu. Wachezaji wengien walioachwa katika kikosi hicho in pamoja na Jordi Masip na Douglas, wakati Jordi Alba yeye ahatakuwepo kwasababu ya kutumikia adhabu.

ZABALETA ADAI WACHEZAJI WA CITY WANAPASWA KULAUMIWA KWA MSIMU MBAYA.

MCHEZAJI nyota wa Manchester City, Pablo Zabaleta amesisitiza kuwa yeye pamoja na wenzake wanapaswa kubeba baadhi ya lawama kea matokeo mabaya ya timu hiyo badala ya kumuachia meneja Manuel Pellegrini kubeba lawama zote. City wanatarajia kukabidhi taji lao la ubingwa wa Ligi Kuu kea Chelsea msimu huu, kutokana na vijana hao wa Jose Mourinho kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi kea tofauti ya alama 10 huku zikiwa zimebaki wiki chache kabla ya msimu kumalizika. Kuporomoka kea City kumezusha mjadala juu ya mustakabali wa Pellegrini huku meneja wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp na meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti wakitajwa kuja kuziba nafasi yake. Hata hivyo Zabaleta amesisitiza kuwa Pellegrini hapaswi kutimuliwa kwa matokeo yaliyotokana na kiwango kisichoridhisha kutoka kea wachezaji wake. Zabaleta amesema Pellegrini anastahili heshima kutoka kea kila mtu kwani alikuja kuanza kuinoa timu hiyo msimu uliopita na kunyakuwa taji la Ligi Kuu na Kombe la Ligi. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa baadhi ya wachezaji pia wanapaswa kubebeshwa lawama kutokana na kutokuwa katika kiwango chao kwa msimu wotehuu.

FERGUSON AVUNJA UKIMYA NA KUDAI RONALDO NI BORA MESSI.

MENEJA wa zamani wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson anaamini Cristiano Ronaldo in mchezaji bora wa jumla kuliko Lionel Messi. Ronaldo na Messi wameshakubalika kea kipindi kirefu kuwa wachezaji bora duniani wakiwa wamepokezana tuzo ya Ballon d’Or katika kipindi cha miaka saba iliyopita. Ferguson amewahi kumfundisha Ronaldo wakati wakiwa wote United na kocha huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 73 anafafanua kwanini anaona Ronaldo in bora kuliko Messi. Ferguson amesema watu wanadai Messi ndio bora kuliko Ronaldo lakini hilo kea maoni yake sio kweli kwani Ronaldo anaweza kucheza kea kiwango cha hata ukimpeleka timu za daraja la chini jambo ambalo anadhani kea Messi halitawezekana. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa Ronaldo anatumia miguu miwili, ana kasi, mzuri kea mipira ya juu na jasiri lakini Messi anadhani in mchezaji wa Barcelona pekee na sio timu zingine.

BEKI WA UBELGIJI AANGUKA NA KUZIRAI AKIWA MAZOEZINI.

MCHEZAJI wa kimataifa wa Ubelgiji, Gregory Mertens amelazwa hospitali baada ya kuanguka wakati wa mchezo wa wachezaji wa akiba katika klabu yake. Beki huyo wa timu ya Sporting Lokeren mwenye umri wa miaka 24 alipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuanguka katika kipindi cha kwanza na baadae kukimbizwa hospitali. Taarifa za klabu hiyo zinadai kuwa hali ya mchezaji huyo in mbaya na amewekwa katika hali ya kutojitambua huku akisaidia kupumua kea mashine katika hospitali ya Genk. Klabu hiyo pia ilituma salamu za pole kea familia yake huku wakimuombea mchezaji kuvuka kikwazo hicho kigumu katika maisha yake. Wachezaji wa kimataifa wa Ubelgiji Thibaut Courtois anayecheza Chelsea na mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku wote walituma salamu zao pole kea mchezaji huyo kupitia ukurasa wa mitandao yao ya twitter.

BOURNEMOUTH, WATFORD ZAKWEA LIGI KUU UINGEREZA.

MWENYEKITI wa klabu ya Bournemouth, Jeff Mostyn amedai kuwa timu hiyo imepata mafanikio yasiwezekana baada ya kujihakikishia nafasi ya kucheza katika Ligi Kuu Uingereza msimu ujao. Mwaka 2008 klabu hiyo ilibakiza dakika tano kufilisiwa kabla ya Mostyn kutoa kitita cha paundi 100,000 kuikoa klabu hiyo. Akihojiwa Mostyn amesema klabu hiyo imepitia mambo mengi ambayo mengine yalikuwa kama hayawezekani lakini wamefanikiwa. Mwenyekiti huyo aliendelea kudai kuwa kutokana uzoefu huo anaamini wataweza kuhimili mikikimikiki ya Ligi Kuu.

BAADA YA KAMPUNI YA SIMU, ETO'O SASA AHAMIA KWENYE MAVAZI.

BAADA ya kuanzisha kampuni ya siku za mkononi inayojulikana kama Eto’o Telecom nyumbani kwao, nyota wa zamani wa Cameroon Samuel Eto’o sasa anatarajia kuhamia katika ulimwengu wa mavazi kwa kuzindua nguo mbalimbali zenye nembo yake. Mojawapo ya mavazi yanayotarajiwa kutolewa kea nembo yake mpya ya Samuel Eto’o 9 ikimaanisha jezi ambayo amekuwa akivaa uwanjani, in pamoja na mashati, kofia na viatu. Kwa mujibu wa mbunifu kutoka Cameroon ambaye amebuni mpango huo, Gabriel Pascal Nyemeg Nlend amesema lengo kuu in kutambulisha mafanikio ya Samuel Eto’o katika soka la Afrika. Nlend aliendelea kudai kuwa baada ya kumaliza kazi yake uwanjani sasa wanataka Eto’o kuwasindikiza majumbani, mijini na vijijini kea kuvaa nguo zenye nembo yake. Eto’o na Nlend wanatarajia kukutana nchini Ureno baadae mwezi huu ili kukamilisha mpango huo kwabla ya kuanza kuzindua rasmi nembo hiyo katika nchi za Hispania, Urusi, Ureno na Uingereza.

GOLIKIPA WA ZAMANI MAN UNITED KUHUKUMIWA BAADA YA KUKIRI KUMGONGA MWENDESHA BAISKELI.

GOLIKIPA wa zamani wa klabu ya Manchester United, Mark Bosnich amekiri kosa la kuendesha hovyo baada ya kumgonga na kumuumiza mwendesha baiskeli kea gari lake jijini Sydney. Bosnich mwenye umri wa miaka 43 alikwenda katika mahakama wa mji huo kusikiliza kesi yake kuhusiana na tukio hilo lililotokea Mei 21 mwaka jana. Golikipa huyo wa kimataifa wa zamani wa Australia anatarajiwa kuhukumiwa Juni 9 mwaka huu baada ya kumalizika kesi yake. Taarifa ya polisi inadai kuwa Bosnich ambaye pia amewahi kuzidakia timu za Aston Villa na Chelsea alimgonga mwendesha baiskeli huyo kwa upande na kumfanya kuanguka. Mwendesha baiskeli huyo alikimbizwa hospitali akiwa na majeruhi madogo katika sehemu za mbavu na kiwiko.

YANGA KUKABIDHIWA NDOO YAO YA UBINGWA MEI 6 BAADA YA KUKIPIGA NA AZAM.

WAZIRI wa Habari, Vijana Utamuduni na Michezo, Dr. Fennela Mkangara anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kukabidhi Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Soka nchini-TFF, Mkangara anatarajiwa kukabidhi kombe hilo kwa Yanga Mei 6, mwaka huu katika mchezo kati ya mabingwa hao dhidi ya Azam FC. Wakati huohuo rais wa TFF Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kea mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji kufuatia timu huyo kutawadhwa mabingw wapya wa ligi hiyo. Katika salamu zake za pongezi, Malinzi amesema kutwaa Ubingwa wa VPL ni jambo muhimu na sasa wanapaswa kuanza maaandalizi kwa ajili ya michuano ya kimataifa barani Afrika mwakani . Yanga imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu nchini kwa mara ya 25 jana, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya timu ya Polisi Morogoro katika uwanja wa Taifa huku ikiwa na michezo miwili mikononi kabla ya ligi kumalizika.
RAIS WA PSG AMKOMALIA CAVANI.

RAIS wa klabu ya Paris Saint-Germain, Nasser Al Khelaifi amasisitiza kuwa hataitazama ofa ya paundi milioni 50 kwa ajili ya Edinson Cavani kufuatia taarifa kuwa Manchester United itatoa kitita hicho kea ajili ya kuwania kumsajili. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay amekuwa akihusishwa na tetesi za kwenda Old Trafford mara kadhaa lakini mabingwa hao wa Ufaransa wanaonekana kutokuwa na mpango wa kumuuza nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 hivi karibuni. Akihojiwa Al Khelaifi amesema ameshafanya mazungumzo na Cavani kuhusiana na mustakabali wake hivyo ana uhakika kuwa ataendelea kuwa nao. Rais huyo alipoulizwa kuhusu ofa ya paundi milioni 50 iliyotolewa na United, alieleza kuwa hatataka hata kuitazama ofa kama hiyo.

Friday, April 24, 2015

CHAMPIONS LEAGUE: BARCELONA KUKWAANA NA BAYERN.

KLABU ya Barcelona imepangwa kucheza dhidi ya Bayern Munich katika ratiba ya nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopangwa leo. Katika mechi nyingine ya nusu fainali itawakutanisha Juventus ya Italia dhidi ya mabingwa watetezi wa taji hilo Real Madrid. Mechi za mkondo wa kwanza za michuano hiyo zinatarajiwa kuchezwa Mei 5 na 6 mwaka huu huku zile za marudiano zikichezwa wiki moja baadae. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa meneja wa Bayern Pep Guardiola kukutana kwa mara ya kwanza na timu yake ya zamani ya Barcelona ambayo aliiwezesha kunyakuwa mataji 13 akiwa kocha kwa kipindi cha miaka minne. 
Kwa upande wa michuano ya Europa League, Sevilla wao watakwaana na Fiorentina wakati Napoli wakipepetana na Dnipro ya Ukraine. Fainali ya Ligi ya Mabingwa inatarajiwa kuchezwa Juni 6 katika Uwanja wa Olimpiki jijini Berlin Ujerumani wakati ile ya Europa League itachezwa Mei 27 katika Uwanja wa Taifa jijini Warsaw, Poland.

Thursday, April 23, 2015

WANYAMA AKANUSHA KUFANYA MAZUNGUMZO NA ARSENAL.

KIUNGO mahiri wa klabu ya Southampton, Victor Wanyama amekanusha taarifa kuwa amefanya mazungumzo na klabu ya Arsenal kwa ajili ya uhamisho majira ya kiangazi. Vyombo vya habari nchini Uingereza jana viliripoti kuwa Wanyama amefanya mazungumzo na meneja wa Arsenal, Arsene Wenger na kuwa ana nia ya kujiunga nao mwishoni mwa msimu. Nyota huyo wa kimataifa wa Kenya aliadika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akikanusha taarifa hizo akidai kuwa hajawahi kuzungumza na Wenger kuhusiana na suala lolote kama inavyodaiwa. Wanyama aliendelea kudai kuwa anawaheshimu sana mashabiki wa Southampton ambao wamekuwa wakimuunga mkono toka alipowasili akitokea Celtic na angependa kuendelea kuitumikia timu hiyo.

WENGER AKIRI KUCHEMKA KUMUUZA FABREGAS.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amekiri kujuta kumruhusu Cesc Fabregas kuondoka lakini amewataka mashabiki wa timu hiyo kumuheshimu kiungo huyo wa Chelsea pindi watakapocheza nao katika Uwanja wa Emirates Jumapili hii. Fabregas mwenye umri wa miaka 27 aliondoka Arsenal mwaka 2011 na kwenda Barcelona lakini baada ya kushindwa kupata nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza alirejea katika Ligi Kuu kiangazi mwaka jana chini Jose Mourinho. Akihojiwa Wenger amesema kitu pekee anachojutia in kumuacha kiungo huyo aondoke lakini anachoataka yeye in kila mchezaji aheshimiwe. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa anampongeza Fabregas kwa jinsi alivyoimarika na kuwa mchezaji tegemeo kwa Chelsea msimu huu.

JAPANA KUWA MWENYEJI WA MICHUANO YA KLABU BINGWA YA DUNIA.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limetangaza Japan kuwa mwenyeji wa michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia kea kipindi cha miaka miwili ijayo. Baada ya kuandaa michuano hiyo mara ya mwisho mwaka 2012, Japana inatarajiwa kuwa mwenyeji tena mwaka 2015 na 2016, huku kwa mwaka huu ikitarajiwa kufanyika Desemba 10 mpaka 20. Katibu mkuu wa FIFA, Jerome Valcke alithibitisha taarifa hizo na kudai kuwa Japan imeonyesha weledi mkubwa katika kuandaa michuano ya FIFA, zikiwemo fainali sita za Klabu Bingwa ya Dunia ambazo zimekuwa na mafanikio. Naye rais wa Chama cha Soka cha Japan-JFA, Kuniya Daini amesema nafasi hiyo ni nyingine ya kipekee kea wachezaji na mashabiki kushuhudia michuano mikubwa ya soka ya vilabu. JFA inatarajia kutangaza miji itakayotumika kwa ajili ya michuano hiyo ya siku 10 baadae ambapo bingwa mtetezi in mabingwa wa Ulaya Real Madrid.

FULANA YAMPONZA GUARDIOLA.

SHIRIKISHO la Soka la Ulaya-UEFA limemfungulia mashitaka meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola kea kuvaa fulana yenye maandishi ya kudai haki ya mwandishi wa habari za michezo aliyeuawa katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana. Mwanahabari huyo Jorge Lopez alifariki baada ya teksi aliyokuwa amepanda akielekea hotelini kwake kugongwa na gari linalodaiwa kuwa lilikuwa limeibwa katikati ya jiji la Sao Paulo nchini Brazil mwaka jana. Guardiola alikuwa amevaa fulana yenye maandishi ya kudai haki ya uchunguzi wa kifo cha mwandishi huyo wakati wa mkutano wake na wanahabari kabla ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Porto juzi. UEFA imesema kwamba Guardiola amechukuliwa hatua za kinidhamu kwa sababu kitendo alichofanya hakihusiani na masuala ya michezo. Kanuni za shirikisho hilo zinapiga marufuku kea mtu yeyote kutumia matukio ya kimichezo kwa shughuli zisizohusiana na suala hilo.

KUSHUHUDIA PAMBANO LA MAYWEATHER NA PAQUIAO MILIONI 18.

TIKETI kwa ajili ya pambano langumi la wiki ijayo kati ya bondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao hatimaye zinatarajiwa kuingia sokoni leo huku zikitegemwa kugharimu kiasi cha paundi 60,000. Ukumbi wa MGM Grand uliopo jijini Las Vegas, Nevada una uwezo wa kuingoza watazamaji 16,500 lakini in tiketi 1,000 pekee ndio zitakwenda sokoni. Tiketi zilizobakia zitakakwenda kwa mabondia wenyewe, casino, wadhamini na mapromota wa pambano hilo. Tiketi rahisi zaidi katika pambano hilo la Mei 2 mwaka huu zinatarajiwa kugharimu kiasi cha paundi 1,000 kwa pesa za madafu shilingi 2,903,000 na kupanda mpaka paundi 6,700 sawa na shilingi 18,869,500. Mayweather raia wa marekani ataingia katika pambano hilo akiwa na rekodi ya kushinda mapambano yake yote 47 ya kulipwa aliyocheza 26 kati ya hayo akishinda kea knockout wakati Pacquiao raia wa Filipino akiwa na rekodi ya kushinda mapambano 57, kupoteza matano na sare mawili.

JUVENTUS YAKIRI KUANZA MAZUNGUMZO YA KUMSAJILI DYBALA.

OFISA mkuu wa Juventus Giuseppe Marotta amethibitisha kuwa klabu hiyo iko katika mazungumzo na Palermo kea ajili ya kumsajili mshambuliaji Paulo Dybala lakini akaongeza kuwa dili hilo bado in gumu kufanikiwa. Dybala amekuwa katika kiwango bora msimu huu akiwa amefunga mabao 13 katika michezo 30 aliyoichezea Palermo jambo ambalo limemfanya kuzivutia klabu kadhaa zikiwemo Inter Milan, Arsenal na Chelsea. Wakala wa mchezaji huyo tayari amedai kuwa Chelsea wametoa ofa ya euro milioni 41, huku Juventus nao wakitaka kuimarisha safu yao ya ushambuliaji baada ya Carlos tevez kudaiwa kutaka kurejea nyumbani kwao Argentina katika klabu ya Boca Juniors. Marotta amesema wanazungumza na rais wa Palermo Maurizio Zamparini lakini mazungumzo hayo yanaonekana kuwa magumu kutokana na rais huyo kutaka kitita cha euro milioni 50 kea ajili ya kumuachia nyota huyo.

BAYERN NAO WAMNYEMELEA IVANOVIC WA CHELSEA.

KLABU ya Bayern Munich iko tayari kuongeza nguvu zake kea ajili ya kumuiba Branislav Ivanovic kutoka Chelsea katika majira ya kiangazi. Beki huyo wa kimataifa wa Serbia amebakisha mkataba wa mwaka mmoja Stamford Bridge na mabingwa hao wa Bundesliga wameungana na Paris Saint-Germain kufuatilia maendeleo ya mustabali wa mchezaji huyo kea karibu. Ivanovic amepewa ofa ya kuongezwa mkataba wa mwaka mmoja kama sera za timu hiyo zinavyotaka kwa wachezaji waliozidi umri wa miaka 30 lakini bado hajakubali kusaini. Beki huyo amekuwa tegemeo kea Chelsea toka alipojiunga nao kea kitita cha paundi milioni 9.5 akitokea klabu ya Lokomotiv Moscow ya Urusi mwaka 2008.

SKRTEL ASISITIZA KUBAKIA LIVERPOOL.

BEKI wa Liverpool, Martin Skrtel amesema hana mpango wao kuondoka katika timu hiyo wakati wakala wake akitangaza mteja wake huyo kukaribia kukamilisha mazungumzo ya mkataba mpya. Skrtel in mmoja kati ya wachezaji kadhaa wa Liverpool waliokuwa wakihusishwa na tetesi za kuondoka Anfield majira ya kiangazi. Klabu za Wolfsburg na Napoli zote zimeripotiwa kutaka kumsajili mchezaji huyo ambaye alijiunga na Liverpool akitokea Zenit St Petersburg Januari mwaka 2008. Hata hivyo, nyota huyo wa kimataifa wa Slovakia ambaye amebakisha miezi 14 katika mkataba wake wa sasa aliosaini mwaka 2012, amesema hana mpango wa kwenda popote. Wakala wa mchezaji huyo Karol Csonto amesisitiza kuwa ofa pekee iliyopo mezani kea ajili ya mchezaji huyo ni mkataba mpya ambao anatarajia kutia saini mapema iwezekanavyo.

WAKALA WA TOURE ADAI MTEJA HAJALI SANA FEDHA.

WAKALA wa Yaya Toure, Dimitri Seluk anatarajiwa kusimamisha mazungumzo na Manchester City baada ya kudai vilabu kadhaa vimejitokeza kutaka kumsajili kiungo huyo. Taarifa zinadai kuwa Toure amekuwa hana furaha katika klabu hiyo ambayo imeporomoka mpaka nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu baada ya kupoteza mechi nne kati ya saba za mwisho walizocheza. Nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast amekuwa akilaumiwakwa kucheza chini ya kiwango na kuigharimu timu yake jambo ambalo ndio linamfanya kufikiria mustakabali wake. Toure mwenye umri wa miaka 31 amebakisha miaka miwili katika mkataba wake wa sasa ambao unakadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 10 kea mwaka lakini Seluk amerudia madai ya Toure kuwa pesa sio kigezo kinachoweza kugeuza maamuzi yake. Seluk amesema watu wengi wanadhani Toure atabakia kwasababu ya pesa lakini mwenyewe hajali kuhusu hilo.

JUVENTUS SIO WASINDIKIZAJI LIGI YA MABINGWA ULAYA - ALLEGRI.

MENEJA wa klabu ya Juventus, Massimiliano Allegri amesisitiza kikosi chake hakijaingia katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ili kutimiza idadi ya timu. Juventus maarufu kama vibibi vya Turin ilifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuiondosha AS Monaco kwa jumla ya bao 1-0 baada ya kutoka nao sare ya bila kufungana katika mchezo wa jana na kulinda ushindi wao wa bao 1-0 waliopata nyumbani wiki iliyopita. Akihojiwa Allegri amesema hawataogopa timu yeyote watakayopangiwa nayo katika nusu fainali kwani wamepania kwenda mbali zaidi ya hapo walipo. Mbali na Juventus, mabingwa watetezi wa michuano hiyo Real Madrid nao walifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuwabamiza majirani zao Atletico Madrid kwa bao 1-0 ambalo liliwekwa kimiani na mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez katika dakika ya 88. Ratiba ya nusu fainali inatarajiwa kupangwa kesho ambayo itazijumuisha pia timu za Barcelona na Bayern Munich ambazo nazo zilifuzu baada ya kushinda mechi zao za juzi.

SAGNA ADAI HAJUTII KUJIUNGA NA CITY PAMOJA NA KUSUGUA BENCHI.

BEKI wa klabu ya Manchester City, Bacary Sagna amesisitiza hajutii kuhamia Etihad pamoja na kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza toka aondoke Arsenal. Sagna alijiunga na City kwa uhamisho huru baada ya mkataba wake na Arsenal kumalika Juni mwaka jana lakini amefanikiwa kucheza katika mechi 16 pekee toka ajiunge na mabingwa hao wa Ligi Kuu. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 32 ambaye alikuwa chaguo la kwanza katika kikosi cha Arsenal Wenger, amekuwa akinyimwa namba na Pablo Zabaleta lakini mwenyewe amesema angefanya uamuzi kama huo kama angeambiwa arudie. Sagna amesema amesikia kauli nyingi kutoka kea mashabiki wanaodai kuwa angebakia Arsenal lakini mwenyewe anadhani alifanya uamuzi sahihi kuondoka na atafanya hivyo kama akiambiwa arudie.

Tuesday, April 21, 2015

SMALLING AKUBALI KUSAINI MKATABA MPYA NA UNITED.

BEKI wa klabu ya Manchester United, Chris Smalling amekubali kusaini mkataba mpya ambao utambakisha katika timu hiyo mpaka June mwaka 2019. Smalling mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na United akitokea Fulham mwaka 2010 na ameshinda mataji mawili ya Ligi Kuu akiwa Old Trafford. Akihojiwa meneja wa United, Louis van Gaal amesema Smalling ameimarika na amekua kwa kipindi kifupi ambacho amekuwa akiinoa timu hiyo. Van Gaal aliendelea kudai kuwa beki huyo amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo na amefurahi kusaini mkataba mpya.


DE BRUYNE AWAPA WAKATI MGUMU CITY.

KLABU ya Manchester City inakabiliwa na wakati mgumu katika mbio za usajili wa kiungo wa Wolfsburg Kevin De Bruyne, kufuatia Bayern Munich nao kutangaza kumfukuzia nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji. Mkurugenzi wa soka wa City, Txiti Begiristain ameshafanya mazungumzo na wawakilishi wa De Bruyne na amekuwa akimtazama mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea akicheza kwa wiki kadhaa. Lakini De Bruyne ambaye aliwahi kuichezea Chelsea michezo tisa baada ya kusajiliwa kwa paundi milioni saba akitokea Genk Januari mwaka 2012, ameweka wazi nia yake ya kubakia Ujerumani. Wolfsburg wenyewe tayari wameonyesha nia ya kumuongeza mkataba mpya ambao utambakisha hapo mpaka mwaka 2020.

ANCELOTTI ATAMBA MAJERUHI HAYAWEZI KUWAZUIA KUWATOA ATLETICO MADRID.

MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti ana uhakika kikosi kiko imara kukabiliana na mahasimu wao wa jiji Atletico Madrid katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kesho. Kikosi cha Madrid kinakabiliwa na nyota kadhaa majeruhi akiwemo Luka Modric, Gareth Bale na Karim Benzema. Katika mchezo wa kwanza uliochezwa wiki iliyopita timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana. Akihojiwa Ancelotti amesema hana shaka sana kuelekea katika mchezo huo utakaofanyika katika Uwanja wa Santiago Bernabeu pamoja na majeruhi alionao. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa anadhani Isco ataweza kuiziba nafasi ya Modric katika nafasi ya kiungo huku Jese na Chicharito wakitarajiwa kuziba nafasi za Benzema na Bale.

IBRAHIMOVIC KUONGOZA JAHAZI LA PSG.

MSHAMBULIAJI mahiri wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG, Zlatan Ibrahimovic anatarajiwa kurejea katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona leo. Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 33 alikuwa nje akitumikia adhabu wakati PSG walipochapwa mabao 3-1 jijini Parislakini anatarajiwa kurejea katika mchezo wa leo sambamba na kiungo marco Verratti. Kiungo wa Barcelona Andres Iniesta naye yuko fiti pamoja na kutolewa nje katika mchezo wa wiki iliyopita kutokana na majeruhi. Luis Suarez ambaye alifunga mabao mawili murua katika mchezo wa mkondo wa kwanza anatarajiwa kucheza akiwa sambamba na washambuliaji wengine Lionel Messi na Neymar. PSG ambao wanakutana kwa mara ya nne na Barcelona katika michuano hiyo msimu huu itamkosa beki wake mahiri Thiago Silva.

VILLA YASHITAKIWA NA FA KWA VURUGU.

KLABU ya Aston Villa imeshitakiwa na Chama cha Soka cha Uingereza-FA kwa mashabiki kuvamia uwanja mwishoni mwa mchezo wa robo fainali ya michuano ya Kombe la FA ambao walishinda mabao 2-0 dhidi ya West Bromwich. Baadhi ya mashabiki wa wa nyumbani walivamia uwanja wa Villa Park katika dakika za majeruhi na wakati mchezo umemalizika wakati viti vilipokuwa vikirushwa kutoka jukwaa la mashabiki wa West Brom Machi 7 mwaka huu. Katika tukio hilo wachezaji kadhaa wa West Brom walionekana kusukumwa na mashabiki waliokuwa wamevamia uwanjani. Klabu ya Reading nayo imeshitakiwa kwa kosa kama hilo baada ya mashabiki wake nao kuvamia uwanjani baada ya mchezo dhidi ya Bradford. Timu zote mbili zimepewa mpaka Aprili 23 mwaka huu kujibu tuhuma hizo kabla ya kulimwa adhabu.

PROMOTA AWA BUBU KUHUSU TIKETI ZA PAMBANO LA MAYWEATHER NA PAQUIAO.

PROMOTA Bob Arum bado ameshindwa kutoa ufafanuzi wa kwanini hakuna tiketi za jumla kwa ajili ya pambano la ngumi kati ya Floyd Mayweather na Manny Paquiao litakalofanyika jijini Las Vegas Mei 2 mwaka huu. Ukumbi wa MGM Grand una uwezo wa kuingiza watazamaji 16,500 lakini ni tiketi 1,000 pekee zinazotarajiwa kutolewa kwa ajili ya mashabiki wa kawaida wanaotaka kushuhudia pambano hilo. Inaaminika kuwa mkataba na ukumbi huo bado haujasainiwa wakati tiketi pia haziko sokoni kwa ajili ya kumbi nyingine zenye uwezo wa kuandaa pambano hilo. Arum alisitisha mkutano na wanahabari jana kabla ya hajaanza kuulizwa maswali. Bei ya tiketi za pambano hilo tayari imeshatangazwa kuwa kiasi cha kati ya dola 1,500 kwa tiketi za kawaida huku zile maalumu zikiwa dola 7,500.


HAKUNA KITAKACHOWAZUIA URUSI KUANDAA KOMBE LA DUNIA LA KIHISTORIA.

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter amesema hakuna kitakachowazuia Urusi kuandaa michuano ya kihistoria ya Kombe la Dunia mwaka 2018. Kauli hiyo ya Blatter ameitoa wakati alipotembelea moja ya viwanja vinavyotarajiwa kutumika kea ajili ya michuano hiyo uliopo jijini Sochi. Blatter amesema anajivunia kuona Urusi ikijiandaa tayari kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia na hayo yote yanafanyika kwasababu ya rais wan chi hiyo Vladimir Putin. Blatter amesema michuano hiyo itakuwa ya 10 kwake baada ya kufanya kazi kea zaidi ya miaka 40 na shirikisho hilo na anategemea kuwa fainali za kipekee. Rais huyo pia aliwashukuru waziri wa michezo wan chi hiyo Vitaly Mutko na Ofisa Mkuu wa Kamati ya Maandalizi Alexei Sorokin kea ushirikiano wa hali wanaoonyesha kuhakikisha wanafanikisha tukio hilo adhimu.

Monday, April 20, 2015

INIESTA RUKSA KUIVAA PSG KESHO.

KIUNGO wa klabu ya Barcelona Andres Iniesta amepewa ruhusa ya kucheza katika mchezo wa maruadiano war obo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris saint-Germain utakaofanyika kesho. Nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi aliumia mgongoni wakati wa ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliofanyika jijini Paris wiki iliyopita na kumfanya kuukosa mchezo wa Jumamosi iliyopita wa La Liga ambao waliwafunga Valencia mabao 2-0. Katika taarifa yake klabu hiyo ilithibitisha taarifa hizo za Iniesta kuruhusiwa kucheza katika mchezo wa kesho. Taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa sasa itakuwa ni jukumu la meneja Luis Enrique kuamua kumtumia mchezaji huyo au la katika mchezo hu marudiano wakitafuta tiketi ya kutinga nusu fainali.

BALE KUIKOSA ATLETICO MADRID.

KLABU ya Real Madrid inatarajia kumkosa winga wake mahiri Gareth Bale katika mchezo wa maruadiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid kesho kutwa. Bale alipata majeruhi ambayo yalimfanya kutolewa nje katika mchezo wa La Liga ambao Madrid ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Malaga Jumamosi iliyopita na alitegemewa kuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki tatu. Katika taarifa yake klabu hiyo ilithibitisha taarifa za majeruhi ya mchezaji na kwamba ataukosa mchezo huo wa kesho kutwa pamoja na mingine kadhaa wakati akiendelea kupona. Madrid itaingia katika mchezo huo marudiano utakaofanyika katika Uwanja wa Santiago Bernabeu ikitafuta ushindi baada ya kutoka sare ya bila ya kufungana na majirani zao hao katika mchezo wa kwanza.

RIBERY HATIHATI KUIVAA PORTO.

MENEJA wa klabu ya Bayern Munich, Pep Guardiola amesema kuna hatihati ya winga Franck Ribery kupona kwa wakati kwa ajili ya mchezo wa maruadiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Porto. Ribery amekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi mmoja na Guardiola amesema kuna uwezekano mkubwa wa mchezaji huyo kuukosa mchezo wa marudiano utakaofanyika jijini Munich baada ya kuchapwa kwa mabao 3-1 na Porto katika mchezo wa kwanza uliofanyika nchini Ureno wiki iliyopita. Akihojiwa Guardiola amesema hadhani kama Ribery ataweza kucheza na pamoja na kwamba atazungumza na madaktari wao lakini hadhani kama ataweza. Guardiola ana matumaini ya kubadili matokeo katika mchezo huo huku akiendelea kuwa na msusuru ya majeruhi kwa wachezaji wake muhimu akiwemo Arjen Robben, David Alaba, Javi Martinez na Medhi Benatia.

MODRIC AIPA AHUENI MADRID.

KLABU ya Real Madrid imepata taarifa za ahueni baada ya Luka Modric kudai kuwa anaweza kurejea uwanjani kabla ya mwisho wa msimu. Kiungo huyo aliumia goti lake la kushoto katika mchezo wa La Liga dhidi ya Malaga na Shirikisho la Soka la Croatia lilitangaza siku iliyofuata kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 atakaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita. Kwa upande wa klabu yake ya Madrid wao waligoma kutoa muda haswa ambao Modric atachukua kupona na mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Tottenham Hotspurs sasa amefafanua ana matumaini ya kupona kabla ya kumaliza kwa msimu huu. Akihojiwa Modric ambaye amerejea mwezi uliopita baada ya kupona majeruhi ya msuli, amesema kuumia tena ni jambo linalomuumiza haswa katika kipindi muhimu katika msimu lakini ana matumaini ya kurejea uwanjani mapema zaidi kuliko inavyokadiriwa.

MASHABIKI NANE WA SOKA WAUAWA KATIKA SHAMBULIZI LA BUNDUKI BRAZIL.

WATU nane wameuawa katika klabu ya mashabiki wa soka jijini Sao Paulo, Brazil. Katika taarifa yake polisi wanadai kuwa mashabiki wa klabu ya Corinthians walikuwa wakiandaa mabango yao kuelekea katika mechi wakati watu wenye silaha walipowavamia. Wavamizi hao waliwaamuru mashabiki saba kulala chini kabla ya kuwafyatulia risasi na mtu wa nane yeye alipigwa risasi wakati akijaribu kukimbia. Polisi wanadai kuwa kuuawa kwa mashabiki hao wa kundi la Pavilhao Nove kunahusishwa na mambo ya madawa ya kulevya. Taarifa hiyo ya polisi iliendelea kudai kuwa kundi hilo la mashabiki huenda likawa na mahusiano na makundi ya kihalifu na mauaji hayo yanaweza kuwa na kulipiza kisasi na sio masuala ya soka. Vurugu katika soka nchini Brazil zimekuwa zikikua siku hadi siku huku mashabiki wa timu kadhaa kubwa za miji mikubwa wakitumia umaarufu wa vilabu vyao kuendesha shughuli za kihalifu nje ya uwanja.

KANE ANAPASWA KUWANUNULIWA WENZAKE MSOSI - POCHETTINHO.

MENEJA wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino ametania kuwa Harry Kane anapaswa kuwanunuliwa wachezaji wenzake chakula cha usiku baada ya kufikisha mabao 30 msimu huu. Kane mwenye umri wa miaka 21 amekuwa mchezaji wa kwanza wa Spurs kufikisha idadi hiyo ya mabao toka mshambuliaji Gary Lineker alipofanya hivyo katika msimu wa mwaka 1991-1992. Pochettino alimpongeza Kane na kudai kuwa anastahili hatua hiyo na kutania kuwa anapswa kuwanunulia wachezaji wenzake chakula kwasababu wamekuwa wakifanya jitahada kumsaidia kufunga mabao. Akihojiwa mwenyewe Kane amesema kufikia idadi hiyo ya mabao ni jambo zuri na amewashukuru wachezaji wote kwa ushirikiano wanaompa.