OFISA mkuu wa Juventus Giuseppe Marotta amethibitisha kuwa klabu hiyo iko katika mazungumzo na Palermo kea ajili ya kumsajili mshambuliaji Paulo Dybala lakini akaongeza kuwa dili hilo bado in gumu kufanikiwa. Dybala amekuwa katika kiwango bora msimu huu akiwa amefunga mabao 13 katika michezo 30 aliyoichezea Palermo jambo ambalo limemfanya kuzivutia klabu kadhaa zikiwemo Inter Milan, Arsenal na Chelsea. Wakala wa mchezaji huyo tayari amedai kuwa Chelsea wametoa ofa ya euro milioni 41, huku Juventus nao wakitaka kuimarisha safu yao ya ushambuliaji baada ya Carlos tevez kudaiwa kutaka kurejea nyumbani kwao Argentina katika klabu ya Boca Juniors. Marotta amesema wanazungumza na rais wa Palermo Maurizio Zamparini lakini mazungumzo hayo yanaonekana kuwa magumu kutokana na rais huyo kutaka kitita cha euro milioni 50 kea ajili ya kumuachia nyota huyo.
No comments:
Post a Comment