Monday, January 30, 2012

AFCON 2012: WENYEJI GUINEA YA IKWETA YAMUONGEZA MKATABA KOCHA WAO.

Baada ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika wenyeji wa michuano hiyo Guinea ya Ikweta wameamua kumuongeza mkataba kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Gilson Paulo mkataba wa mwaka mmoja. Kocha huyo kutoka Brazil alichukua kibarua cha kuinoa timu hiyo ikiwa ni wiki chache tu kabla ya mashindano hayo baada ya ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo kujiuzulu wadhifa wake kwa kutokuelewana na uongozi wa soka nchini humo. Paulo mwenye miaka 62 alikuwa amepewa mkataba wa miezi miwili tu kuinoa timu hiyo lakini kutokana na kazi nzuri aliyofanya kuiwezesha timu hiyo kushinda michezo yake miwili ya kwanza na kuingia hatua ya robo fainali wameamua kumuongeza mkataba huo kama zawadi. Taarifa iliyotumwa katika mtandao wa serikali ya nchi hiyo ilithibitisha kweli suala la kumuongeza mkataba wa mwaka mmoja kocha huyo ambaye atakuwa akilipwa kiasi cha dola 15,000 kwa mwezi.

MENSAH KUREJEA UWANJANI KARIBUNI.

NAHODHA wa timu ya taifa ya Ghana John Mensah amesema anaendelea vyema kuvuatia majeruhi ya msuli aliyoyapata katika mchezo wa makundi wa Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi Botswana. Mensah amesema kuwa anajisikia vyema kila siku ambapo daktari wake amesema baada ya kumfanyia uchunguzi jijini Libreville kuwa hayakuwa majeraha makubwa na atarejea uwanjani katika kipindi cha karibuni. Beki huyo tegemeo wa timu hiyo alitolewa nje katika mchezo wa ufunguzi wa kundi D dhidi ya Btswana jijini Franceville lakini alipewa adhabu ya kufungiwa mchezo mmoja hivyo inamaanisha kama akipona sawasawa anaweza kucheza katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi Jumatano. Kurejea kwa Mensah kutampa wakati mgumu kocha wa timu hiyo Goran Stevanovic haswa ikizingatiwa kuwa mabeki wake wote wanne watakuwepo akiwemo Isaac Vorsah ambaye alikuwa akitumikia adhabu ya kufungiwa michezo miwili na John Boye.

MCLEISH ATAKA FA ICHUNGUZE TUKIO LA VAN PERSIE.

MENEJA wa Aston Villa Alex McLeish amelitaka Shirikisho la Soka nchini Uingereza-FA kuchunguza kwa makini tukio la mshambuliaji wa Arsenal Robin va Persie kumpiga kiwiko mchezaji wake Carlos Cuellar wakati timu hizo zilipokutana katika mchezo wa Kombe la FA Jumapili. Kocha huyo anadai kuwa ni bahati kwa mchezaji kukosa kadi nyekundu kwa kumpiga kiwiko beki huyo wa kimataifa kutoka Hispania wakati wakigombania mpira wa juu dakika ya 64 ambapo katika mchezo huo Arsenal ilishinda mabao 3-2. Mwamuzi aliyechezesha mchezo huo hakuchukua hatua yoyote kwenye tukio hilo na MacLeish anahitaji FA kuangalia upya tukio hilo katika mkanda wa video ili kuona kama mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi anahitaji adhabu au la. Kabla ya tukio hilo Van Persie alikuwa ameshafunga mabao mawili kwa njia ya penati na kuisaidia timu yake kutoka nyuma kwa mabao mawili mpaka ushindi na kuiwezesha timu hiyo kuingia mzunguko wa tano wa kombe ambapo sasa itakutana na mshindi kati ya Sunderland au Middlesbrough.

KOCHA SENEGAL AGOMA KUBWAGA MANYANGA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Senegal Amara Traore amekataa kubwaga manyanga kuinoa timu hiyo pamoja na vipigo vitatu walivyopata katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ukiwemo mchezo wa mwisho wa kundi A dhidi ya Libya. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo kocha huyo amesema kuwa hataachia ngazi kuinoa klabu hiyo kwakuwa bado ana nia thabiti ya kuendelea kuifundisha. Senegal iliingia katika michuano hiyo ikiwa ni timu inayopewa nafasi ya kunyakuwa kombe hilo lakini ilijikuta ikipoteza michezo yote mitatu kwa kufungwa mabao 2-1 katika kila mchezo. Naye kocha wa Morocco Eric Gerets alionyesha nia ya kubakia kukinoa kikosi hicho pamoja na timu yake ambayo nayo ilikuwa ikipewa nafasi kutolea mapema katika michuano hiyo.

Friday, January 27, 2012

AFCON 2012: GABON, TUNISIA UWANJANI LEO KUTAFUTA TIKETI ZA ROBO FAINALI.

WENYEJI Gabon na bingwa wa zamani wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Tunisia zinaweza kusonga mbele katika hatua robo fainali ya michuano hiyo kama watashinda michezo yao ya leo ya Kundi C jijini Libreville. Gabon ambao ni wenyeji michuano wakishirikiana na Equatorial Guinea itabidi ishinde mchezo wake dhidi ya Morocco ambao walipoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Tunisia Jumatatu. Morocco kama wakikubali kipigo katika mchezo huo watakuwa wametolewa katika michuano hiyo na hivyo kuwa timu ya pili kigogo kuyaaga mashindano hayo baada ya Senegal. Tunisia ambao waliwahi kushinda michuano hiyo wakati walipoiandaa miaka nane iliyopita watakuwa kibarua kizito cha kuifunga Niger ambao nao walipoteza mchezo wa kwanza kwa wenyeji Gabon.

GYAN HATIHATI KUIVAA MALI.

MSHAMBULIAJI wa Ghana Asamoah Gyan jana alilazimika kusitisha mazoezi kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu yaliyokuwa yakimsumbua. Gyan ambaye kwasasa anacheza soka Uarabuni alikuwa katika hatihati ya kukosa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kutokana na kusumbuliwa na misuli maumivu aliyoyapata mwezi uliopita. Mchezaji huyo alianza vyema pamoja na wenzake wanaounda kikosi cha Ghana lakini kabla muda wa mazoezi kuisha alitoka nje na kukaa benchi huku akifunga kifundo chake cha mguu kwa barafu.
Baadae alichukuliwa na madaktari wa timu hiyo na kusindikizwa katika hoteli waliyofikia ambayo haiku mbali na uwanja huo wa mazoezi kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Naye nahodha wa timu hiyo John Mensah pia hakushiriki mazoezi na kikosi hicho kwa siku ya pili kutokana na maumivu ya misuli yaliyokuwa yakimsumbua lakini daktari wa timu hiyo amesema hayawezi kumuweka nje kwa kipindi kirefu.

RIBERY FITI KUIVAA WOLFSBURG.

VINARA wa Ligi Kuu nchini Ujerumani Bayern Munich wamejipanga kumrejesha winga wake machachari Franck Ribery kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya Wolfsburg pamoja na maumivu ya mgongo yanayomsumbua mchezaji huyo. Ribery alifanya mazoezi pamoja na wenzake jana pamoja na kulalamika kusumbuliwa na maumivu ya mgongo ambapo baadae daktari wa timu hiyo Hans-Wilhelm Mueller alimfanyia uchunguzi. Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa mchezaji huyo toka alipopewa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Cologne kabla ya Christmas mwaka jana. Munich inajipanga kurejea katika kiwango chake baada ya kufungwa mabao 3-1 na Borussia Moenchengladbach Ijumaa iliyopita lakini pamoja na kipigo hicho bado wanaongoza ligi kwa tofauti ya magoli huku wakiwa wamefungana alama sawa na Schalke na Borussia Dortmund.

Ivory Coast v Burkina Faso 2-0 All Goals and Highlights

Sudan vs Angola 2-2 All Goals & Highlights [26/1/2012] - [HD]

Thursday, January 26, 2012

BOLTON YAMNYAKUA BEKI WA NY REDBULL.

KLABU ya Bolton Wanderers imetangaza kumyakuwa beki wa kimataifa wa Marekani Tim Ream anayechezea klabu ya New York Redbull kwa ada ambayo haikuwekwa wazi. Beki huyo wa kati mwenye miaka 24 ambaye alitumia muda wa wiki nzima kufanya mazoezi na klabu hiyo ametia saini mkataba utakaomwezesha kuichezea klabu hiyo kwa muda wa miaka mitatu. Ream ametua klabuni hapo ikiwa ni wiki moja tu toka Bolton imuuze beki wake wa kati wa kimataifa wa Uingereza Gary Cahill kwenda timu ya Chelsea. Kocha wa Bolton Owen Coyle amesema ujio wa mchezaji huyo itakakuwa ni ahueni kubwa baada ya kumpoteza Cahill na ni mategemeo yake atazoea haraka mikikimikiki ya Ligi Kuu nchini Uingereza.

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.

WARUNDI KUICHEZESHA SIMBA KIGALI 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Burundi kuchezesha mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba ya Tanzania na Kiyovu Sport ya Rwanda itakayochezwa jijini Kigali. Waamuzi hao ni Thierry Nkurinziza atakayekuwa katikati wakati wasaidizi wake ni Jean-Claude Birumushahu na Jean-Marie Hakizimana. Mwamuzi wa akiba atakuwa Hudu Munyemana kutoka Rwanda. Kamishna wa mechi hiyo ni Abbas Sendyowa kutoka Uganda. Mechi hiyo namba 13 itachezwa Februari 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Amahoro jijini Kigali, na itaanza saa 9.30 kwa saa za Rwanda. Mechi ya marudiano itachezwa Machi 4 mwaka huu, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.CAF YAMTEUA LIUNDA KUSIMAMIA MECHI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Leslie Liunda wa Tanzania kuwa Kamishna wa mechi namba 3 ya Ligi ya Mabingwa kati ya AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Atletico Olympique ya Burundi itakayochezwa kati ya Februari 17, 18 na 19 mwaka huu jijini Kinshasa. Waamuzi wa mechi hiyo ambao wanatoka Gabon watakuwa Mbourou Roponat, Wilfred Nziengu na David Obamba. Mwamuzi wa akiba kutoka DRC ni Mupemba Nkongolo. Mechi ya marudiano kwa timu hizo itachezwa kati ya Machi 2, 3 na 4 jijini Bujumbura ambapo Kamishna atakuwa Eugene Katamban kutoka Uganda.TAMASHA LA KUVUMBUA VIPAJI (GRASSROOT) DAR
Tamasha la mafunzo ya kuhamasisha watoto kucheza mpira wa miguu na kuvumbua vipaji (Grassroot) kwa shule maalum zilizochaguliwa katika Mkoa wa Dar es Salaam linaendelea Februari 3 mwaka huu. Siku hiyo tamasha hilo litafanyika katika Shule ya Msingi Mtoni Kijichi wilayani Temeke kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 6 mchana. Februari 10 mwaka huu tamasha lingine litafanyika katika Shule ya Msingi Kinyerezi wilayani Ilala. Watoto (wa kike na kiume) wanaotakiwa kushiriki katika matamasha hayo ambayo yataendelea kila wiki katika shule mbalimbali za Dar es Salaam hadi Agosti 24 mwaka huu ni wa kuanzia umri wa miaka 6 hadi 12. Matamasha hayo ni mwendelezo wa uzinduzi wa Grassroot katika tamasha (festival) kubwa lililofanyika Desemba 17 mwaka jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watoto 1,200 baada ya semina iliyoendeshwa na Mkufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

AFCON 2012: KOCHA WA GUINEA AFIWA NA BABA YAKE.

WAKATI akipoteza mchezo dhidi ya Mali kwa bao 1-0 wakati wa mchezo wa kundi D Jumanne kocha wa Guinea Michel Dussuyer alipata pigo lingine katika muda huohuo baada ya kufiwa na baba yake huko kwao Ufaransa. Mwishoni mwa mchezo huo uliokuwa na upinzani mkubwa kocha huyo alipigiwa simu kupewa taarifa kuwa baba yake aliyekuwa na umri wa miaka 82 amefariki dunia. Akihojiwa Dussuyer amesema ulikuwa ni usiku usiokuwa mzuri kwake baada kumpoteza baba yake halafu muda huohuo kupoteza mchezo pia. Tukio kama hilo liliwahi kutokea mwaka 2008 katika michuano kama hiyo baada ya aliyekuwa kocha wa Ivory Coast Ulrich Stielike aliiacha timu hiyo katikati ya mashindano baada ya kufiwa na motto wake kiume huko kwao.

AFCON 2012: MASTAA SENEGAL WAAGA MAPEMA MICHUANO HIYO.

TIMU ya taifa ya Senegal inakuwa timu ya kwanza kuondoshwa katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kukubali kipigo kutoka kwa wenyeji wa michuano hiyo Equatorial Guinea cha mabao 2-1. Senegal ambao waliingia katika michuano hiyo ikiwa ni timu inayopewa nafasi kubwa ya kunyakuwa michuano hiyo ilijikuta katika wakati mgumu baada ya wenyeji kutangulia kufunga bao dakika ya 62 kupitia kwa Iban Randy. Baada ya bao hilo Senegal walikuja juu na kusawazisha katika dakika ya 89 ya mchezo huo kabla ya mshambuliaji wa Equatorial Guinea kupigilia msumari wa mwisho dakika ya 90 na kupeleka kilio kwa timu hiyo. Kwa matokeo hayo wenyeji hao ambao walikuwa wakishangiliwa kwa nguvu na mashabiki wao waliojazana uwanjani watakuwa wametinga hatua ya robo fainali.

BALOTELLI AKUBALI ADHABU YA MECHI NNE.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Italia na Manchester City Mario Balotelli ameanza kuitumikia adhabu yake ya kufungiwa michezo minne baada ya kukubali adhabu hiyo iliyotolewa na Shrikisho la Soka la Uingereza-FA kwa kumpiga kwa makusudi kiungo wa Tottenham Hotspurs Scott Parker katika mchezo wao wa Jumapili iliyopita. Balotelli mwenye umri wa miaka 21 alikosa mchezo wa Jumatano ambao timu yake ilitolewa katika nusu fainali ya pili ya Kombe la Ligi dhidi ya Liverpool na pia atakosa michezo mingine mitatu ya Ligi Kuu nchini humo. Katika tukio alilofanya mchezaji huyo katika mchezo huo mwamuzi Howard Webb aliyechezesha mchezo huo hakumpa kadi ingawa baadae amesema kuwa kama angeona tukio hilo basi anngetoa kadi nyekundu kwa mchezaji huyo.   Michezo mingine ya Ligi Kuu ambayo Balotelli atakosa ni pamoja na mchezo baina ya timu hiyo na Everton, Fulham na Aston Villa.

Wednesday, January 25, 2012

Barcelona Vs Real Madrid 2-2 All Goals & Match Highlights (January 25th,...

Equatorial Guinea 2 - 1 Senegal - AFCON 2012 - All Goals - Equatorial Gu...

AFCON 2012: ZAMBIA YAJIWEKEA MAZINGIRA MAZURI YA KUSONGA MBELE.

MENSAH NJE MECHI MBILI.

John Mensah
NAHODHA wa timu ya Ghana John Mensah hatakuwa sehemu ya kikosi hicho katika michezo miwili iliyobakia katika hatua za makundi kufuatia kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo baina ya timu yake na Botswana. Mensah alipewa kadi hiyo dakika ya 66 baada ya kumwangusha mshambuliaji wa Botswana Jerome Ramatlhakwane wakati akiwa katika harakati za kufunga bao. Kwa mujibu wa sheria za Shrikisho la Soka Afrika-CAF Mensah mwenye miaka 29 atafungiwa mechi mbili kutokana na kadi hiyo hivyo kumfanya akose michezo miwili muhimu inayofuatia katika hatua za makundi. Hiyo ni kadi nyekundu ya pili kwa mchezaji katika michuano hiyo huku nyingine akiwa alipewa kwa kufanya kosa kama hilo katika michuano ya mwaka 2008 dhidi ya Nigeria ambapo Ghana ilifanikiwa kushinda mabao 2-1 na kutinga hatua ya nusu fainali.

KOCHA WA IVORY COAST AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUSAHAU RAHA ZA ULAYA.

Francois Zahoui
KOCHA wa timu ya taifa ya Ivory Coast Francois Zahoui amewatahadharisha wachezaji wake kusahau mazingira ya Ulaya katika vilabu wanavyocheza na kukumbuka kuwa wapo mazingira magumu ya katika michuano Kombe la Mataifa ya Afrika. Kauli hiyo imekuja kufuatia timu hiyo ambayo inapewa nafasi kubwa ya kunyakuwa michuano hiyo kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Sudan katika mchezo wao wa kwanza. Akihojiwa na waandishi wa habari Zahoui amesema wakati unacheza Ulaya kunakuwa na waamuzi ambao wanajua jinsi ya kufanya kazi yao pamoja na viwanja bora kabisa lakini katika mazingira ya Afrika tunacheza kwenye joto huku waamuzi wakifanya lile wanaloweza. Ivory Coast itacheza na Burkina Faso katika mchezo wake unaofuatia wa kundi B kesho huku ikiwa na mategemeo ya kuonyesha cheche zake kutokana na wachezaji nyota wanaocheza vilabu vikubwa Ulaya.

Mali vs Guinea Full Highlights - CAN 2012

Ghana v Botswana 1-0 All Goals and Highlights

WAKALA WA BALOTELLI AMSHUTUMU MWAMUZI.

WAKALA wa mshambuliaji wa Manchester City Mario Balotelli amemshutumu mwamuzi Howard Webb kwa kudanganya kuwa mteja wake huyo alimpiga kichwa Luke Parker wa Tottenham Hotspurs wakati timu hizo zilipokutana Jumapili. Webb ambaye alikuwa mwamuzi katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 hakuchukua hatua yoyote tukio hilo lilipotokea lakini alipohojiwa amesema kuwa kama angeliona hilo tukio basi lazima angempa kadi nyekundu Balotelli. Wakala huyo wa Balotelli anayeitwa Mino Raiola amesema amekasirishwa na kauli ya Webb akidai hakuliona tukio wakati wa mchezo huo wakati anaonekana hakuwa mbali na sehemu tukio lilipotokea wakati wa mchezo huo. Baada ya mchezo huo Shrikisho la Soka Uingereza-FA limetoa adhabu ya kumfungia michezo minne mchezaji huyo huku likimpa siku mbili kukata rufani.

Tuesday, January 24, 2012

YANGA YATAKIWA KUMLIPA NJOROGE SH. MILIONI 17.

John Njoroge
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kupitia kitengo chake cha utatuzi wa migogoro (Dispute Resolution Chamber- DRC) limeagiza klabu ya Yanga kumlipa mchezaji John Njoroge sh. 17,159,800 ikiwa ni fidia kwa kuvunja mkataba wake kinyume cha taratibu. Uamuzi huo wa DRC chini ya Jaji Theo van Seggelen ambaye ni raia wa Uholanzi ulifanywa Desemba 7 mwaka jana jijini Zurich, Uswisi na kutumwa TFF kwa njia ya DHL, Januari 17 mwaka huu. Njoroge ambaye ni raia wa Kenya aliwasilisha kesi yake FIFA kupinga Yanga kuvunja mkataba alioingia wa kuichezea timu yao kinyume na makubaliano. Mchezaji huyo hivi sasa anachezea timu ya Tusker ambayo ni mabingwa wa Kenya. Yanga ina siku nne za kukata rufani kupinga uamuzi huo kuanzia tarehe iliyoupokea kama inataka kufanya hivyo. Klabu hiyo inatakiwa iwe imeshamlipa Njoroge ndani ya siku 30 tangu ilipopokea uamuzi huo. Ikishindwa kulipa ndani ya muda huo, itatozwa riba ya asilimia 5 kwa mwaka ya fedha hizo. Ikiwa Yanga itashindwa kulipa ndani ya muda huo vilevile suala hilo litafikishwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ya FIFA kwa hatua zaidi.

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.

MAREKEBISHO YA RATIBA LIGI KUU YA VODACOM 
Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya marekebisho madogo kwenye ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom kutokana na Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kutumika kwa sherehe za kitaifa za kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Mechi namba 111 kati ya Toto Africans na African Lyon ambayo kwa mujibu wa ratiba ilikuwa ichezwe Februari 5 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza sasa itachezwa Aprili 18 mwaka huu. Mabadiliko hayo yamefanyika baada ya wamiliki wa Uwanja wa CCM Kirumba, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kueleza kuwa watautumia kwa sherehe za kuzaliwa chama chao, hivyo hautakuwa na nafasi kwa Februari 4, 5 na 6 mwaka huu. Uamuzi huo umesababisha pia mabadiliko kwa mechi nyingine mbili. Mechi namba 168 kati ya Villa Squad na African Lyon iliyokuwa ichezwe Aprili 18 mwaka huu Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam, sasa itachezwa Aprili 22 mwaka huu. Pia mechi namba 170 kati ya Azam na Toto Africans iliyokuwa ichezwe Aprili 29 mwaka huu jijini Dar es Salaam sasa imerudishwa nyuma hadi Aprili 26 mwaka huu ambayo ni Sikukuu ya Muungano.VIINGILIO MECHI YA TWIGA STARS, NAMIBIA 
Kiingilio cha chini kwa mechi ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Twiga Stars na Namibia itakayochezwa Jumapili (Januari 29 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 2,000. Kiwango hicho ni kwa washabiki kwa viti vya bluu na kijani. Viti hivyo kwa pamoja vinachukua jumla ya watazamaji 36,693 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua washabiki 60,000. Pia kutakuwa na kiingilio cha watoto wenye umri wa chini ya miaka 10 ambacho ni sh. 1,000. Watoto watakaotumia tiketi hizo wanatakiwa kuingia uwanjani wakiwa na wazazi au walezi wao. Viingilio vingine kwa mechi hiyo ni sh. 3,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 5,000 kwa VIP B na C n ash. 10,000 kwa VIP A. Namibia inatarajia kuwasili nchini Ijumaa (Januari 27 mwaka huu) saa 12.45 jioni kwa ndege ya South Africa Airways.LIGI KUU VODACOM KUWANIA UBINGWA WA BARA
Mzunguko wa 14 wa Ligi Kuu ya Vodacom unamalizika kesho (Januari 25 mwaka huu) kwa mechi mbili zitakazochezwa kwenye viwanja tofauti jijini Dar es Salaam. Simba itakuwa mwenyeji wa Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Viingilio vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP B na C, sh. 15,000 kwa VIP A. Nayo Azam itakuwa mgeni wa African Lyon katika mechi namba 97 itakayochezwa Uwanja wa Chamazi. Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 10,000 kwa Jukwaa Kuu na sh. 3,000 mzunguko.

GYAN FITI KUIVAA BOTSWANA.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ghana Asamoah Gyan leo anatarajiwa kukiongoza kikosi cha nchi hiyo katika mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua. Mshambuliaji huyo amekuwa katika hatihati ya kutocheza michuano hiyo kufuatia kuumia kifundo cha mguu lakini imethibitika kuwa Gyan yuko fiti na atacheza mchezo wao wa ufunguzi katika kundi D dhidi ya Botswana jijini Franceville. Uwanja wa Franceville watakaotumia Ghana pia utatumiwa na timu zingine za kundi hilo kutoka Magharibi mwa Afrika ambao ni mahasimu timu za Mali na Guinea ambazo kila moja zitahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele. Timu zote nne zilizopo katika kundi D ndizo zilikuwa za mwisho kuwasili katika michuano hiyo ambayo imeandaliwa kwa pamoja na Guinea ya Ikweta na Gabon.

RUFANI YA BIN HAMMAM YASIKILIZWA CAS.

RUFANI ya aliyekuwa mgombea wa zamani wa Urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Mohamed bin Hammam ya kulisimamisha Shirikisho la Soka barani Asia-AFC kutochagua rais mwingine imesikilizwa Jumatatu na na Mahakama ya juu ya Michezo-CAS. Bin Hammam mwenyewe hakuhudhuria mahakamani wakati shauri lake hilo likisikilizwa na CAS na wakili wake kutoka Marekani Eugene Gulland alikataa kuzungumza lolote kwa waandishi wa habari. Bin Hammam alikata rufani kuzuia AFC kuchagua rais mwingine wakati yeye akijaribu kubadilisha adhabu aliyopewa na FIFA ya kufungiwa kujishughulisha na shughuli zozote za michezo maisha kutokana na kashfa ya kununua viongozi wa soka wa Caribbean ili wampigie kura. Kwasasa Zhang Jilong kutoka China ndio anakaimu nafasi ya Bin Hammam katika AFC na pia ndiye aliyechukua nafasi ya mjumbe wa FIFA ambayo Bin Hammam alikuwa akiishilia toka mwaka 1996.

BALOTELLI KIKAANGONI TENA.

MSHAMBULIAJI wa Manchester City Mario Balotelli ameshtakiwa kwa vurugu alizofanya wakati wa mchezo baina ya timu yake na Tottenham Hotspurs uliofanyika Jumapili. Balotelli alionekana akimgonga kichwani kiungo wa Tottenham Scott Parker lakini mwamuzi wa mchezo huo Howard Webb hakuchukua hatua yoyote huku Muitaliano huyo akifunga bao la penati dakika za majeruhi na kuipa ushindi timu yake wa mabao 3-2. Balotelli ambaye kwa kosa hilo anaweza kufungiwa michezo minne amepewa mpaka Jumatano jioni awe amekata rufani kuhusiana na tukio hilo. Kama akiamua kukata rufani ataweza kucheza mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la Ligi dhidi ya Liverpool Jumatano lakini asipokata rufani anaweza kupata adhabu kubwa zaidi ya hiyo.

Monday, January 23, 2012

Tunisia v Morocco 2-1 All Goals and Highlights

Gabon vs Niger Goal Stéphane N'Guema 2-0 23.01.2012

AFCON 2012: MICHEZO YA LEO JIONI.

GABON VS NIGER 19:00 (EAT)


MOROCCO VS TUNISIA 22:00 (EAT)

TAARIFA KUTOKA TFF LEO.

WABUNGE KUCHANGIA TWIGA STARS 
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia timu ya Bunge wameomba kucheza mechi maalumu dhidi ya Twiga Stars kabla ya kuwasilisha mchango wao kwa timu hiyo. Benchi la Ufundi la Twiga Stars kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekubali kucheza mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya maonesho tu ambapo baada ya kumalizika ndipo Wabunge watakabidhi kile walichopanga kutoa kwa timu. Mechi hiyo itafanyika Alhamisi (Januari 26 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume uliopo Ofisi za TFF kuanzia saa 10 kamili jioni. Twiga Stars na Namibia zitapambana Jumapili (Januari 29 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikiwa ni mechi ya marudiano kuwania tiketi ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.GHARAMA ZA UWANJA- TWIGA STARS VS NAMIBIA
TFF imeiandikia Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuomba iondoe gharama za kutumia Uwanja wa Taifa ambazo ni fixed kwenye mechi kati ya Twiga Stars na Namibia. Lengo la maombi hayo ni kusaidia kupunguza gharama za kuandaa mechi hiyo ambayo bajeti nzima ni sh . 74,660,000. Hiyo inajumuisha usafiri, posho kwa wachezaji, posho kwa benchi la ufundi, gharama za kambi, dawa na maji ya kunywa wakati wa mazoezi na mechi kwa Twiga Stars. Maeneo mengine ni usafiri wa ndege, usafiri wa ndani (magari mawili), posho na hoteli kwa kamishna na waamuzi. Nyingine ni gharama za timu ya Namibia itakayokuwa na watu 25 ambazo ni usafiri wa ndani (magari matatu), hoteli (malazi na chakula) na maji ya kunywa wakati wa mazoezi na mechi. Gharama ambazo ni fixed kwa matumizi ya Uwanja wa Taifa ni pamoja na usafi na ulinzi, umeme, maandalizi ya sehemu ya kuchezea, malipo kwa kampuni ya Wachina na asilimia kumi ya mapato.

MAKAMU WA RAIS WA GHANA ATEMBELEA KAMBI YA KIKOSI HICHO.

MAKAMU wa Rais wa Ghana John Dramani amewaonya wachezaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo kutobweteka na sifa wanazopewa wakati wanatakapoanza safari yao ya kutafuta taji la tano la michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ambalo hawajalichukua katika kipindi cha miaka 30. Kauli ya Dramani imekuja kufuatia kutembelea kambi ya ya kikosi hicho marufu kama Black Stars nchini Gabon ili kuwaongezea morali katika michuano hiyo. Dramani amesema kuwa anasikia taarifa kutoka sehemu mbalimbali kwamba timu zenye majina makubwa hazijashiriki michuano hiyo hivyo itakuwa rahisi kwa Ghana na timu zingine kunyakuwa taji hilo kwa urahisi. Lakini makamu huyo wa rais aliwakumbusha wachezaji hao kuwa hizo timu kubwa ambazo hazikushiriki zilitolewa na timu ambazo zinashiriki michuano hiyo hivyo sio timu za kubeza kwani na zimeonyesha kwamba zinaweza. Katika msafara wa Dramani aliongozana na Waziri wa Habari Baba Jamal, Mkurugenzi Mkuu katika ofisi yake Roger Ansogwine, Maofisa wa Baraza la Michezo pamoja na waandishi wa habari.

MOURINHO AGOMA KUJIBU MASWALI.

MENEJA wa Real Madrid Jose Mourinho amekataa kujibu maswali kuhusu taarifa zilizovuja kwamba kuna mpasuko katika chumba cha kubadilishia nguo cha klabu hiyo na kusema hakukasirika pale mashabiki wa klabu hiyo walimpomzomea wakati wa mchezo dhidi ya Atletico Bilbao Jumapili ambapo walishinda mabao 4-1. Madrid imepitia katika kipindi kigumu siku za karibuni baada ya kupoteza mchezo katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Mfalme ambapo walifungwa mabao 2-1 na mahasimu wao Barcelona. Katika mchezo huo Pepe alionekana kwa makusudi akimkanyaga mkono Messi huku mwenyewe akipinga na kudai kwamba ilikuwa bahati mbaya lakini magazeti ya Hispania yamekuwa yakimshambulia kwa kuonyesha mchezo usio wa kiungwana. Gazeti mo ja kubwa la nchi hiyo la kila siku la Marca liliripoti Jumapili kuwa Mourinho na beki wake Sergio Ramos hawakuwa katika maelewano mazuri wakati wa mazoezi Ijumaa na kusema kuwa kuna ufa mkubwa kati ya Mourinho na baadhi ya wachezaji wa kimataifa wa Hispania waliopo katika klabu hiyo.

Real Madrid vs Athletic Bilbao 4-1 All Goals & Full highlights 22/1/2012

Saturday, January 21, 2012

AFCON 2012: GHANA YATUA GABON.

TIMU ya taifa ya Ghana ambayo inapigiwa chapuo kunyakuwa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu imetua katika jiji la Libreville Ijumaa jioni tayari kwa michuano hiyo na kupelekwa katika kambi yake iliyopo katika mji wa Fanceville. Ghana inatarajiwa kuanza mchezo wake ufunguzi na timu ya Botswana katika kundi D Jumanne kabla ya kucheza na Mali pamoja na Guinea michezo ambayo itachezwa katika Uwanja wa Franceville. Kocha wa Ghana Goran Stevanovic alimaliza maandalizi yake nchini Afrika Kusini Jumatano ambapo alishuhudia kikosi chake kikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Platinum Stars ya nchini humo. Ghana imeshawahi kutwaa taji Mataifa ya Afrika mara nne lakini haijawahi kutwa taji hilo tena kwa kipindi cha miaka 30 sasa hivyo huu utakuwa ndio wakati muafaka haswa ikizingatiwa kuwa timu vigogo zote zimetolea mapema katika hatua ya kufuzu.

BLATTER ADAI URUSI IKO MBALI KATIKA MAANDALIZI YA KOMBE LA DUNIA KULIKO BRAZIL.

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA amesema nchi ya Urusi tayari imeshajiandaa na Kombe la Dunia litakalofanyika nchini 2018 kuliko Brazil ambao wao wataandaa michuano hiyo 2014. Akiongea na waandishi wa habari nchini humo Blatter amesema Urusi tayari wako mbali katika maandalizi hayo kuliko Brazil ambapo tunapata matatizo mengi kuliko hapa. Blatter aliendelea kusema mpaka mwezi uliopita nchi hiyo iliyopo Amerika Kusini bado ilikuwa na matatizo katika viwanja vyake vya ndege, barabara na usafiri wa umma lakini haiko hivyo kwa Urusi. Urusi walipata nafasi ya kuandaa michuano hiyo mikubwa kwa mara ya kwanza wakati walipoishinda Uingereza pamoja na nchi mbilimbili zilizokuwa nazo zikigombea nafasi hiyo ambazo ni Hispania na Ureno pamoja na Ubelgiji na Uholanzi Desemba 2010 mwaka juzi.

AFCON 2012: TUNISIA, MOROCCO WAHUDHURIA IBADA KATIKA MSIKITI MMOJA NCHINI GABON.

TIMU za taifa za Tunisia na Morocco Ijumaa zilihudhuria ibada kwa pamoja katika msikiti uliopo jijini Libreville kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ambayo inatarajiwa kuanza leo. Timu hizo ambazo zinatarajiwa kucheza Jumatatu walikaribishwa na Imam wa msikiti huo huku akiwaombea kufanya vizuri katika mchezo wao uliopo mbele yao. Kabla ya kukutana katika mchezo wa Jumatatu timu hizo ambazo ni mahasimu zitaendelea kuonana mara kwa mara haswa ikizingatiwa kuwa wote wamewekwa katika hoteli moja ya Laico iliyoko katika mji mkuu wa Gabon. Akihojiwa Nahodha msaidizi wa Tunisia Aymen Mathlouthi amesema mchezo baina yao na Morocco ni muhimu kushinda kwani ndio utakaoleta dira kwa mechi zao zote watakazocheza katika michuano hiyo.

REBELO AWAJIBU FIFA.

Aldo Rebelo
WAZIRI wa Michezo wa Brazil Aldo Rebelo amesema kuwa nchi hiyo inaweza kuandaa michuano ya Kombe la Dunia 2014 bila kugombana na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Kauli ya Rebelo imekuja kufuatia Katibu Mkuu wa FIFA Jerome Valcke kupinga vikali ucheleweshwaji wa muswada wa sheria katika Kombe la Dunia unaofanywa na bunge la nchi hiyo. FIFA pia ilikuwa na wasiwasi kuhusu utaratibu wa sasa wa nchi ambayo imepiga marufuku uuzwaji wa vileo viwanjani na kulalamikia ujenzi unaokwenda taratibu wa baadhi ya viwanja ambapo mpaka sasa wako nyuma ya muda. Rebelo amesema akiiambia luninga moja ya michezo nchini humo kuwa Brazil imejiandaa vya kutosha kuhakikisha inaandaa Kombe la Dunia kwa mafanikio na hakuna haja ya kuzozana na FIFA kwa kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa.

Thursday, January 19, 2012

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.

LIGI KUU YA VODACOM KUANZA JUMAMOSI
Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza keshokutwa (Januari 21 mwaka huu) kwa mechi nne. Moro United itaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Mtibwa Sugar itaoneshana kazi na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani. Nayo Toto Africans itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mlandizi mkoani Pwani na Villa Squad itapambana na Kagera Sugar katika Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam. Januari 22 mwaka huu JKT Ruvu na Polisi Dodoma zitapepetana Uwanja wa Azam Chamazi wakati Januari 22 mwaka huu Dar es Salaam itakuwa na mechi mbili; African Lyon na Azam (Uwanja wa Azam Chamazi) na Simba na Coastal Union (Uwanja wa Taifa). Ratiba kwa ajili ya waamuzi na makamishna kwa mechi 35 za mwanzo tayari imeshatoka. Waamuzi wa kati 16 wameteuliwa kuchezesha mechi hizo huku watatu wakiwa wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA). Makamishna ni 28 huku watathmini wa waamuzi (referees assessors) wakiwa kwenye mechi tano. Watathmini hao ni Charles Mchau, Soud Abdi, Emmanuel Chaula, Army Sentimea na Joseph Mapunda.

HAKI ZA MATANGAZO YA TELEVISHENI
Mpaka sasa hakuna kituo cha televisheni ambacho kimeomba na kushinda tenda ya kuonesha moja kwa moja (live) mechi za Ligi Kuu ya Vodacom. Kwa upande wa vituo vya redio, vyote vimepewa haki ya kutangaza moja kwa moja mechi za ligi hiyo kwa masharti yafuatayo; Kuitambulisha ligi hiyo kwa jina lake (Ligi Kuu ya Vodacom) wakati wa matangazo hayo ya moja kwa moja, na pia kuweka matangazo ya mdhamini (Vodacom) wakati wakitangaza mechi husika. Hata hivyo, vituo vya redio bado vinaruhusiwa kuendelea kutafuta/kutumia matangazo ya wadhamini wao, lakini ambao si washindani wa kibiashara wa Vodacom.

MECHI YA TOTO AFRICANS VS AFRICAN LYON
Mechi kati ya Toto Africans na African Lyon ambayo kwa mujibu wa ratiba ilikuwa ichezwe Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza haitakuwepo, na sasa itapangiwa tarehe nyingine. Juzi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilipokea barua kutoka kwa wamiliki wa Uwanja wa CCM Kirumba ikieleza kuwa Februari 5 mwaka huu uwanja huo utatumika kwa sherehe za kitaifa za kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivyo hautaweza kutumika kwa Februari 4, 5 na 6 mwaka huu.

MWENYEKITI WA ARSENAL ADAI KLABU HIYO HAIWEZI KUYUMBA HATA KAM ITASHINDWA KUSHIRIKI CHAMPIONS LEAGUE.

MWENYEKITI wa klabu Arsenal Peter Hill-Wood amedai kuwa klabu hiyo haitakuwa katika hali mbaya kama itakosa tiketi ya kushiriki michuano ya KJlabu Bingwa ya Ulaya msimu huu. Arsenal inayonolewa na na kocha Arsene Wenger kwasasa inashika nafasi ya tano katika msimamowa Ligi Kuu nchini Uingereza wakiwa na alama nne nyuma ya Chelsea inayoshika nafasi ya nne huku Newcastle wakiwa nafasi ya sita na alama sawa na timu hiyo inayotoka Kaskazini mwa jiji la London. Kata hivyo Hill-Wood akiri kuwa itakuwa vizuri kama timu hiyo itamaliza msimu wa ligi hiyo ikiwa nafasi nne za juu amesema klabu hiyo siku zote huwa inajiandaa na hatima ya kutoshiriki michuano mikubwa ya vilabu barani Ulaya. Alipoulizwa kuhusu matumaini ya klabu hiyo kunyakuwa Kombe la Klabu Bingwa la Ulaya, Hill-Wood amesema bado wanapambana na hakuna la zaidi.

TUKIO LIKIONYESHA PEPE ALIVYOMKANYAGA MESSI KATIKA MCHEZO HUO.

Real Madrid vs F.C Barcelona (18.01.2012) Copa Del Rey.Реал Мадрид-Барсе...

MOURINHO AKUBALI LAWAMA KUFUATIA KIPIGO KINGINE KUTOKA KWA BARCA.

KOCHA wa Real Madrid Jose Mourinho amekubali lawama kufuatia kufungwa kwa kikosi chake mabao 2-1 dhidi ya Barcelona katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Ligi uliofanyika katika Uwanja wa Santiago Bernabeu jana usiku. Bao la mapema lilifungwa na mshambuliaji wake Criastiano Ronaldo lilishindwa kutosheleza kuipa timu hiyo ushindi baada ya bao la kusawazisha la Carles Puyol na ushindi la Eric Abidal kutoka kifua mbele huku wakisubiri mchezo wa marudiano Jumatano ijayo katika Uwanja wa Camp Nou. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Mourinho amesema kuwa anakubali lawama zote haswa kama timu yake imefungwa kwani timu ikishinda inakuwa ni furaha kwa kila mtu na ukifungwa unakuwa peke yako na ana fahamu hilo kwakuwa kuwa yuko katika mchezo wa soka kwa muda mrefu. Mourinho pia amesema beki wake Pepe anafaa kuadhibiwa kama akikutwa na makosa ya kumkanyaga kwa makusudi mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi katika mchezo huo kitendo ambacho mwamuzi hakuona.

KERORO RUKSA BRAZIL 2014.

KATIBU Mkuu wa Shrikisho la Soka Duniani-FIFA Jerome Valcke amesema bia zitauzwa katika viwanja vyote 12 vitakavyotumiwa katika michuano nya Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka 2014. Kauli ya Valcke imekuja kufuatia mvutano wa FIFA na serikali ya nchi hiyo ambayo ilikataza uuzwaji wa vileo katika viwanja vya mpira nchini humo lakini katibu huyo alisisitiza bia lazima zitakuwepo. Upigaji kura kwa ajili kupitisha sheria za Kombe la Dunia ulisimama kufuatia kutofautiana kati ya FIFA na waandaji wa michuano hiyo kuhusu suala la kuuza vileo uwanjani. Akihojiwa kuhusu suala hilo Valcke amesema vileo vimekuwa sehemu ya Kombe la Dunia na hatutahitaji majadiliano kuhusu hilo kwani vileo lazima vitakuwepo katika michuano hiyo. Uuzwaji wa vileo ulipigwa marufuku katika viwanja vyote nchini Brazil mwaka 2003 na imekuwa kama katiba kwa mashabiki ili kuzuia vurugu kwa mashabiki watukutu.

BECKHAM ASAINI MKTABA WA MIAKA MIWILI GALAXY.

Nahodha wa zamani wa Uingereza David Beckham anatarajiwa kurejea katika klabu ya Los Angeles Galaxy ya Marekani kwa mkataba mwingine wa miaka miwili. Katika taarifa yake Beckham amesema kuwa yalikuwa ni mamuzi muhimu kwake kwani klabu nyingi kutoka pembe zote za dunia zilikuwa zikimuhitaji lakini bado anafurahia kucheza soka nchini Marekani na kushinda vikombe akiwa na Galaxy. Beckham alindelea kusema kuwa ameshuhudia kwa mara ya kwanza mchezo wa soka unavyojizolea umaarufu nchini humo na ameamua kujikita zaidi kuukuza zaidi mchezo huo ambapo pia familia yake imeonekana kufurahia maisha nchini humo. Mkataba wa miaka mitano na Galaxy ulimalizika mwaka uliopita na kuna tetesi zilivuma kuwa Beckham ambye aliwahi kuzichezea klabu za Manchester United na Real Madrid alikuwa akitakiwa na klabu ya Paris Saint-German na baadhi ya vilabu vya Uingereza.

Wednesday, January 18, 2012

MARADONA APATA NAFUU.

MCHEZAJI nguli wa zamani wa Argentina Diego Maradona amewahakikishia mashabiki wake kuwa yuko katika hali nzuri baada ya kufanyiwa upasuaji kuondoa mawe katika figo. Maradona ambaye ni kocha wa Al Wasl ya Falme za Kiarabu-UAE alifanyiwa upasuaji Dubai baada ya kupata maumivu ya tumbo lakini aliruhusiwa kutoka hospitalini jumatatu. Muargentina huyo anatarajiwa kurejea katika benchi la ufundi wakati kikosi chake kitakapopambana na timu ya Al Sharjah Jumatatu ambapo baadae wiki hii atakiongoza kikosi hicho mazoezini. Timu ya Al Wasl kwasasa inashika nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu nchini humo wakiwa na alama 12 nyuma ya vinara wa ligi hiyo timu ya Al Ain huku wakiwa wamebakiwa na michezo 11 kabla msimu kumalizika.

TEVEZ KUSAINI PSG.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Argentina Carlos Tevez anatarajiwa kusaini mkataba na timu ya Paris Saint German-PSG baada ya klabu hiyo na klabu ya Manchester City kufikia makubaliano. PSG inataka kumsajili mchezaji huyo ambaye hajacheza katika kikosi cha City toka alivyokataa kupasha misuli moto katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mkataba wa miaka mitatu na nusu ingawa ada ya uhamisho haikutajwa. Mabingwa wa Italia klabu ya AC Milan ilishindwa kumnyakuwa Tevez kufuatia mshambuliaji wake kutoka Brazil Alexandre Pato kukataa kujiunga na klabu ya PSG kwa ada ya euro milioni 28.
Mkurugenzi wa Michezo wa PSG Leonardo amekuwa na mawasiliano ya karibu na mchezaji huyo wa ambaye pia ameshawahi kuzichezea klabu za Lazio, Manchester United na Boca Juniors toka mzozo na klabu yake ya City ulipoanza.

PRINCE BOATENG NJE WIKI NNE.

KIUNGO wa AC Milan Kevin-Prince Boateng atakuwa nje uwanja kwa muda wa wiki nne kufuatia majeraha ya misuli yanayomsumbua. Katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo Jumatatu kiungo huyo aliumia katika mchezo wa Jumapili iliyopita dhidi ya mahasimu wao Inter Milan ambapo Milan walipoteza mchezo huo kwa kufungwa bao 1-0. Taarifa hiyo ilieleza kuwa mchezaji huyo alipata tatizo la msuli wake wa mguu wa kushoto kukamaa na atafanyiwa tathmini tena siku saba zijazo. Tatizo la majeruhi limekuwa likiiandama klabu hiyo na kumkosa Boateng itakuwa pigo kubwa baada ya viungo wengine Gennaro Gattuso na Alberto Aquilani kuwa nje ya dimba katika kipindi hiki.

"IBRAHIMOVIC KUZEEKEA MILAN". WAKALA.

WAKALA wa mshambuliaji wa kimatifa kutoka Sweden Zlatan Ibrahimovic amedai kuwa mteja wake huyo anataka kumalizia soka lake akiwa na klabu ya AC Milan. Wakala huyo aitwaye Mino Raiola alisisiza kuwa hakuna ukweli wowote kuwa mteja wake huyo hana furaha katika klabu hiyo na anawaza kuikacha mwishoni mwa msimu huu. Raiola amesema tatizo kubwa linalomsumbua mteja wake ni kupoteza mchezo baina yao dhidi ya watani wao wa jadi Inter Milan kwa bao 1-0 Jumapili katika Uwanja wa San Siro na si zaidi ya hapo. Raiola alikiri pia Ibrahimovic bado alikuwa akihitaji Carlos Tevez kujiunga na klabu hiyo ingawa suala hilo kwasasa linaonekana halitawezekana baada ya timu hiyo kusimamisha mazungumzo na mshambuliaji huyo wa Manchester City.

Tuesday, January 17, 2012

PIRES AFURAHIA MAISHA YA INDIA.

KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa Robert Pires ameweka wazi msisimko wake kufuatia ufunguzi wa kihistoria wa Ligi Kuu nchini India. Nchi hiyo ambayo imejikita zaidi katika michuano ya kriketi, Pires pamoja na mastaa wengine ambao walipata kutamba Ulaya watakuwa jijini Kolkata ambapo klabu sita zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo. Akihojiwa mchezaji ambaye mkataba wake wa mwaka mmoja na Aston Villa umemalizika amesema kuwa hana kitu cha kufanya Ulaya hivyo haoni sababu ya kutojaribu kitu kipya ambacho hakijulikani na hajawahi kufika huko. Chama cha Soka cha nchi hiyo kwa kushirikiana na kampuni Celebrity Management Group-CMG kwa pamoja wamepania kuitangaza ligi hiyo kwa kuwaleta wacheza nyota kutoka Ulaya kuchezea ligi hiyo.

HATIMAYE RONALDINHO ASAFIRI NA FLAMENGO.

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Flamengo ya Brazil Ronaldinho amesafiri na kikosi hicho Jumatatu kuelekea nchini Bolivia kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Klabu Bingwa ya Amerika Kusini. Ronaldinho amesafiri na timu hiyo pmoja na vitisho alivyotoa vya kutosafiri na kikosi hicho endapo hatalipwa mshahara wake wa miezi mitano ambao hajalipwa na klabu hiyo. Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Barcelona na AC Milan amekuwa sehemu ya wachezaji 16 wanaounda kikosi hicho waliosafiri kwa ya mchezo wa ugenini dhidi ya timu ya Real Potosi. Wakala wa Ronaldinho Roberto Assis ambaye pia ni kaka yake amesema wamefikia makubaliano na klabu hiyo pamoja na kampuni ambayo inalipa sehemu ya mshahara wa mchezo kuwa watalipa fedha hizo zinakadiriwa kufikia kiasi cha euri milioni mbili Jumatano.

WE'RE FINALLY READ-AFCONS CO HOSTS.

WENYEJI wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu nchi za Equatorial Guinea na Gabon wana ukakika licha ya wasiwasi uliokuwepo na baada ya uwekezaji mkubwa waliofanya katika viwanja, barabara na mahoteli sasa wako tayari kwa ajili michuano hiyo mikubwa barani Afrika. Wakati wanakubaliana kuandaa michuano hiyo nchi hizo mbili ambazo zina utajiri mkubwa wa mafuta katika ukanda wa Magharibi mwa Afrika wamepitia katika magumu mengi mpaka kufikia hatua hiyo ya mwishoni. Equatorial Guinea imejenga kiwanja kimoja kipya chenye uwezo wa kuchukua watu 15,000 uwanja ambao umejengwa katika jiji la Malabo wakati uwanja uliopo katika jiji la Bata ambao ndio utakuwa wa ufunguzi wa michuano hiyo Jumamosi una uwezo wa kumeza watu 38,000. Gharama za viwanja vyote viwili zinakadiriwa kufikia kiasi cha euro milioni 75 huku asilimia 85 ya barabara za nchi hiyo zikiwa zimefanyiwa marekebisho na zingine kujengwa upya huku mahoteli katika jiji la Malabo nazo zikiwa zimefanyiwa marekebisho na nyingine zikiwa ni mpya. Wakati Equatorial Guinea ikifanya hayo hali ilikuwa tofauti kwa Gabon ambao wao walichelewa ujenzi kwani tokea mwaka 2006 walipopewa dhamana ya kuandaa michuano hiyo mpaka 2009 hakuna chochote kilichofanyika kwa ajili ya maandalizi hayo. Ilikuwa ni wakati Rais wan chi hiyo Ali Bongo Ondimba alipoingia madarakani kazi rasmi za ujenzi zilipoanza huku kamati ya maandalizi ikiingiwa na utata mkubwa baada ya kubadilisha viongozi wake mara tatu. Mwezi Machi mwaka jana Shirikisho la Soka la Afrika-CAF lilikiri kuwa na wasiwasi kutokana na maandalizi yanavyokwenda taratibu na matokeo yake uwanja wa kihistoria wa Omar Bongo umeshindwa kutumika katika michuano hiyo kwakuwa bado uko katika ukarabati. Michezo ambayo ilitakiwa kufanyika jijini Libreville sasa itachezwa katika Uwanja wa Amitie Agonje ambao ulimalizika Novemba mwaka jana wakati ukarabati wa Uwanja wa Franceville ukiwa ndio kwanza umekamilika.

Monday, January 16, 2012

Barcelona vs Real Betis 4-2 All Goals & full highlights (January 15th, 2...

MARADONA ALAZWA DUBAI.

KLABU ya Al Wasl ya Dubai imetangaza kuwa kocha wake mkuu Diego Maradona amelazwa katika Hospitali moja nchini humo baada ya kugundilika kuwa na mawe katika figo yake. Maradona mwenye umri wa miaka 51 alienda hospitalini hapo mapema Jumapili iliyopita kwa ajili uchunguzi na kwasasa amewekwa katika uangalizi ili baadae aweze`kufanyiwa upasuaji kuondoa mawe hayo. Msemaji wa klabu ya Al Wasl amesema kuwa mchezaji huyo alikuwa akijisikia maumivu kabla ya kupelekwa hospitalini hapo ambapo alitarajiwa kufanyiwa upasuaji Jumapili jioni kabla ya kuruhusiwa leo. Klabu hiyo ilitarajiwa kutoa taarifa zaidi kuhusu afya ya Maradona inavyoendelea baadae leo.

MTANDAOWA TWITTER WAMKATISHA MTU MMOJA KWA KUTOA UJUMBE WA KIBAGUZI.

POLISI nchini Uingereza wamemkamata mtu mmoja kufuatia kutuma ujumbe wa kibaguzi katika mtandao wa kijamii wa Twitter kuwalenga wachezaji wawili wa Rangers. Mtu huyo mwenye umri wa miaka 41 ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja anashikiliwa na polisi baada ya malalamiko kuwa beki wa Rangers Kyle Bartley na mchezaji mwezie wa timu hiyo Maurice Edu kutumiwa ujumbe huo wakibaguzi kwenye Twitter. Bartley ambaye yuko kwa mkopo kwa mabingwa hao wa nchini Scotland akitokea klabu ya Arsenal aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa amesikitishwa sana na kauli ya huyo mtu na anashangaa kwamba mpaka kipindi hiki bado watu wana mambo kama hayo ila anaamini pilisi watafanya kazi yao. Edu naye aliandika katika ukurasa wake kuwa imekuwa ni siku mbaya kwake kuona kwamba watu wanafikiria kuandika ujumbe wa kibaguzi katika mtandao huo badala ya kupinga vitu hivyo katika karne hii.

BARCA YAJIPANGA KUPINGA KADI YA INIESTA.

MENEJA wa Barcelona Pep Guardiola amefafanua kuwa klabu hiyo inajipanga kukata rufani ili kupinga hatua ya mchezaji wake Andres Iniesta kupewa kadi ya njano katika mchezo baina ya timu na Real Betis ambao walishinda kwa mabao 4-2 katika Uwanja wa Camp Nou. Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania alipewa kadi hiyo kwa kujiangusha katika eneo la hatari katika kipindi cha pili cha mchezo huo ingawa hata hivyo ilionekana dhahiri kabisa kwamba beki wa Betis Jefferson Montero alimkwatua. Guardiola akihojiwa baada ya mchezo huo amesema kuwa haikuwa penati kwakuwa mwamuzi hakuona tukio lile vizuri lakini wanatarajia kupinga Iniesta kupewa kadi ya njano. Guardiola pia alikisifia kikosi chake kwa moyo wa kujituma walioonyesha kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu muhimu katika mchezo huo.

GHANA YAFURAHISHWA NA UJIO WA ESSIEN.


SHIRIKISHO la Soka nchini Ghana-GFA limesema limefurahishwa kwa hatua ya kiungo wake Michael Essien kurejea uwanjani baada ya kukaa nje kutokana na majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua. Essien alikuwa nje ya uwanja karibu miezi sita na matokeo yake amekosa fainali zingine za Kombe la Mataifa ya Afrika inayotarajiwa kuanza Januari 21 mwaka huu huko Gabon na Equatorial Guinea. Rais wa GFA Kwesi Nyantakyi amesema katika taarifa yake kuwa kurudi kwa mchezaji huyo ni jambo kubwa kwa kwa klabu yake ya Chelsea pamoja na nchi yake. Nyantakyi aliendelea kusema kuwa pamoja na kwamba mchezaji huyo atakosa michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika lakini wanamuombea kupona huko kumpe changamoto mpya ili hapo baadae aweze kurejea kulitumikia taifa lake.

Sunday, January 15, 2012

YANGA YAIFUNGA SOFAPAKA.

Mabingwa wa Tanzania Bara na Afrika Mashariki na Kati, Yanga wameendeleza ushindi katika michezo ya kirafiki, baada ya kuwafunga Sofapaka ya Kenya jana katika uwanja wa Taifa. Katika mchezo wa leo uliochezwa katika uwanja wa Taifa, Yanga wamewachapa Sofapaka toka Kenya goli 2-1 katika mchezo wa  kujipima ubavu, ambapo Yanga waliutumia mchezo kwa ajili ya maandalizi wa ligi kuu ya Vodacom na michuano ya klabu bingwa Afrika. Yanga walianza kuandika goli la kwanza kupitia kwa mchezaji bora wa Uganda kwa mwaka 2011, Hamis Kiiza katika dakika ya 29 kabla ya kurejea tena nyavuni katika dakika ya 60. Goli la Sofapaka lilifungwa na Thomas Wanyama katika dakika ya 88. Leo katika uwanja wa Taifa Mnyama Simba atacheza na mabingwa wa Kenya Tusker saa kumi jioni.

CECAFA KAGAME CUP YAREJEA TENA DAR ES SALAAM.

UDHAMINI mnono unaopatikana Tanzania umelifanya Baraza la vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kuamua kurudisha Kombe la Kagame jijini Dar es Salaam tena mwaka huu. Michuano hiyo ya Kagame iliyofanyika mwaka jana na kushuhudia Yanga ikitwaa ubingwa baada ya kuifunga Simba katika fainali huku umeme ukikatika Uwanja wa Taifa, mwaka huu yalipangwa kufanyika Rwanda. Akizungumza na gazeti la The New Times la Rwanda, Katibu mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye, alisema wameamua kurudisha mashindano hayo Tanzania kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana mwaka jana. Pamoja na mafanikio ya mashindano hayo, Cecafa pia kuna jambo moja la muhimu la kupatikana kwa wadhamini Tanzania ambao wameshapata siku moja iliyopita. Taarifa hiyo inalifanya jiji la Dar es Salaam kuwa mwenyeji kwa mara ya pili mfululizo kwa Kombe la Kagame kama ilivyokuwa kwa Kombe la Chalenji lililofanyika mwaka jana na kushudia Uganda 'Cranes' wakitwaa ubingwa huo kwa kuichapa Rwanda. Zanzibar na Sudan pia walikuwa wakipewa nafasi ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa kwa klabu Afrika Mashariki na Kati, lakini tatizo la fedha limewakosesha nafasi hiyo. Fainali ya mwaka jana ya Kombe la Kagame, ilizikutanisha timu zote za Tanzania, Simba na Yanga na kushuhudia kocha Sam Timbe akipata taji lake la nne la Kombe la Kagame baada ya kufanya hivyo akiwa na SC Villa (2005), Polisi (2006), Atraco (2009) na Yanga (2011).

Mallorca vs Real Madrid 1-2 - All Goals & Highlights 14.01.2012

CANNAVARO ATIMKIA INDIA.

NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa la Italia iliyonyakuwa Kombe la Dunia mwaka 2006 Fabio Cannavaro ameamua kuvaa tena daruga baada ya kustaafu na kuelekea nchini India. Cannavaro ambae aliisaidia timu yake Iitalia kunyakuwa kombe hilo akiwa kama beki atakuwa sehemu ya michuano itayoshirikisha timu sita huko nchini India mashindano ambayo yameandaliwa na Chama cha Soka cha nchi hiyo wakishirikiana na kampuni ya CMG. Beki huyo atakuwa na majina mengine maarufu katika ulimwengu wa soka wakiwemo Robbie Fowler na John Barnes wa Uingereza, Mfaransa Robert Pires, Hernan Crespo na Juan Pablo Sorin wa Argentina, Fernando Morientes wa Hispania na Jay Jay Okocha wa Nigeria ni mojawapo ya sura mpya zitakazoonekana katika Ligi Kuu nchini India. Katika mtandao wa kijamii wa Twitter Cannavaro amesema kuwa ameamua kurejea uwanjani tena akiwa na klabu ya West Bengal ya nchini India lakini hakueleza ni kwa kipindi gani ataichezea klabu hiyo.

BERLUSCONI AMKUMBATIA MKWEWE PATO.

MMILIKI wa klabu ya AC Milan Silvio Berlusconi amesema ameamua kumbakisha mshambuliaji wa klabu hiyo Alexandre Pato kuliko kumuuza katika klabu ya Paris Saint-German ya Ufaransa kwa ada iliyoripotiwa kuwa kiasi cha euro milioni 35. Pato alitoa taarifa rasmi Alhamisi iliyopita kuhusu mustakabali wake wa baadae na mabingwa hao wa Serie A uamuzi huo unaonekana utasimamisha mbio za klabu hiyo za kumnyakuwa mshambuliaji wa Manchester City Carlos tevez. Katika taarifa aliyoitoa Berluscon Jumamosi amesema kuwa makubaliano ya kumuuza Pato hayakumridhisha kiufundi wala kiuchumi na anaamini maamuzi aliyochukua ni sahihi kwa klabu hiyo. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil alijunga na klabu hiyo mwaka 2007 na sasa anatoka binti wa Berlusconi aitwaye Barbara.

WENGER ADAI DIRISHA DOGO LA USAJILI LINAWAPA WACHEZAJI KIBURI.

MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger anaamini kuwa usajili katika kipindi cha dirisha dogo unatakiwa ufutwe kwa kuwa unawapa nguvu wachezaji ambao wanakuwa hawana furaha katika timu zao. Wenger aliuambia mtandao wa klabu hiyo kuwa kwa mawazo yake dirisha dogo la usajili liondelewe na badala yake liachwe wazi kwa mwaka wote au kulifunga kwa mwaka mzima. Meneja huyo aliongeza kuwa kila mtu anakaa roho juu inapofika kipindi cha Novemba mpaka Januari halafu na wachezaji nao wanapata mawazo tofauti kwamba kama wasipocheza basi wanaweza kuondoka ikifika Januari hiyo inawapunguzia kujituma. Wenger amesema ukiwa kama mchezaji hata kama hujapangwa kucheza lakini unatakiwa kujituma kwa klabu husika katika maisha yako yote na kupigania nafasi yako katika kikosi cha kwanza.

Saturday, January 14, 2012

AVB AFURAHISHWA NA UJIO WA ESSIEN.

KIUNGO wa timu ya Chelsea jana alicheza mchezo wake wa kwanza wakati timu yake iliposhinda mchezo dhidi ya Sunderland kwa bao 1-0 katika Uwanja wa Stamford Bridge baada ya siku 273 za kuuguza majeraha. Meneja wa Chelsea Andre Villas-Boas amesema wakati akihojiwa na waandishi wa habari kabla ya mchezo huo kuwa anawapongeza madaktari waliokuwa wakimuuguza mchezaji huyo kwani kurejea kwake uwanjani mwezi mmoja kabla ni jambo la kushangaza. Kiungo huyo wa Kimataifa wa Ghana aliingia katika dakika ya 73 akichukua nafasi ya Frank Lampard na kwa muda mfupi alioingia alibadilisha mchezo juhudi ambazo zilizaa matunda dakika chache baadae. Essien mwenye umri wa miaka 29 aliumia mwanzoni mwa msimu wa ligi majeraha ambayo yamemuweka nje ya dimba kwa muda miezi sita na hatakuwa sehemu ya kikosi cha Ghana kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya makubaliano kwamba lazima apone kabisa ili atumike katika majukumu ya kimataifa.