Sunday, January 15, 2012

YANGA YAIFUNGA SOFAPAKA.

Mabingwa wa Tanzania Bara na Afrika Mashariki na Kati, Yanga wameendeleza ushindi katika michezo ya kirafiki, baada ya kuwafunga Sofapaka ya Kenya jana katika uwanja wa Taifa. Katika mchezo wa leo uliochezwa katika uwanja wa Taifa, Yanga wamewachapa Sofapaka toka Kenya goli 2-1 katika mchezo wa  kujipima ubavu, ambapo Yanga waliutumia mchezo kwa ajili ya maandalizi wa ligi kuu ya Vodacom na michuano ya klabu bingwa Afrika. Yanga walianza kuandika goli la kwanza kupitia kwa mchezaji bora wa Uganda kwa mwaka 2011, Hamis Kiiza katika dakika ya 29 kabla ya kurejea tena nyavuni katika dakika ya 60. Goli la Sofapaka lilifungwa na Thomas Wanyama katika dakika ya 88. Leo katika uwanja wa Taifa Mnyama Simba atacheza na mabingwa wa Kenya Tusker saa kumi jioni.

No comments:

Post a Comment