Monday, March 31, 2014

SITAHARAKISHA KUPONA GOTI LANGU - FALCAO.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao amedai kuwa pamoja na kwamba anaendelea vyema kupona kutokana na majeruhi ya goti, hatachukua maamuzi yoyote ya hatari kwa ajili ya kucheza michuano ya Kombe la dunia baadae mwaka huu. Falcao mwenye umri wa miaka 28 aliumia vibaya goti lake wakati akiitumikia klabu yake ya Monaco Januari mwaka huu na mshambuliaji huyo amesema hataharakisha kupona kwake. Nyota huyo amesema ni jambo lililo wazi kuwa anatamani kupona haraka ili aweze kuiwakilisha nchi yake katika michuano ya Kombe la Dunia lakini hataki jambo hilo limuathiri

VALDES NJE MIEZI SABA.

KLABU ya Barcelona, imethibitisha kuwa Victor Valdes amefanyiwa upasuaji wa goti wenye mafanikio na anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi saba akijiuguza. Valdes amefanyiwa upasuaji huo leo baada ya kuchanika msuli wa katikati ya goti lake la kulia katika ushindi wa mabao 3-0 waliopata Barcelona dhidi ya Celta Vigo wiki moja iliyopita. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo imedai kuwa golikipa huyo alifanyiwa upasuaji wenye mafanikio chini madaktari bingwa Ulrich Boenisch na Ricard Pruna huko Augsburg. Kutokana na majeraha hayo ya Valdes ambaye yatamuweka nje katika michuano ya Kombe la Dunia kipindi cha kiangazi, kinafanya kikosi cha Barcelona kinachonolewa na Gerardo Martino kubakiwa na Jose Pinto huku wakiingia katika wakati muhimu wa msimu wa 2013-2014.

FAINALI YA KOMBE LA DUNIA 2010 ILIKUWA NGUMU - WEBB.

MWAMUZI Howard Webb wa Uingereza amekiri kuwa kuna maamuzi moja au mawili ambayo anatamani angeamua tofauti katika mchezo wa fainali ya Kombe la dunia mwaka 2010. Katika fainali hiyo ambayo ilishuhudia Hispania iliitandika Uholanzi kwa bao 1-0 baada ya muda wa nyongeza bao ambalo lilifungwa na Andres Iniesta, Webb alitoa kadi za njano 14 katika dakika 120 zilizochezwa. John Heitinga alitolewa nje kwa kadi nyekundu muda mfupi baada ya Hispania kufunga bao la kuongoza huku faulo ya Nigel de Jong kumrukia teke la karate Xabi Alonso ikilalamikiwa ilitakiwa kuwa kadi nyekundu lakini mchezaji huyo hakutolewa kwa kupewa kadi ya njano pekee. Mwamuzi huyo wa Ligi Kuu anatarajiwa kurejea tena katika michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil kipindi cha kiangazi, ameelezea mapungufu machache aliyofanya katika michuano hiyo iliyopita. Webb aliyekuwa mwamuzi katika mchezo huo amesema pamoja na kwamba mchezo ulikuwa mgumu ni maamuzi machache kama angepata nafasi angeyabadili lakini kwa muda ule unatakiwa kufanya uamuzi kutokana na maelezo uliyonayo na nafasi uliyopo.

KANKAVA APONGEZWA KWA KUOKOA MAISHA YA MCHEZAJI MWENZAKE.

KIUNGO wa klabu ya Dnipro, Jaba Kankava amepongezwa kwa kuokoa maisha ya nahodha wa Dynamo Kiev Oleg Gusev katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Ukraine uliochezwa jana. Gusev alimeza ulimi wake baada ya kugongwa na goti kwa bahati mbaya na kipa wa Dnipro Denis Boyko katika dakika ya 22 ya mchezo na Kankava alikimbia haraka eneo hilo na kuhakikisha anampatia huduma ya kwanza Gusev kabla ya madaktari hawajafika. Gusev alizinduka akiwa katika machela kabla ya kupelekwa katika kliniki ya Boris iliyopo Dnipropettrovsk huku daktari mkuu Mikhail Radutskyy akipongeza uwezo wa haraka wa kufikiri wa Kankava kwa kuepusha janga kubwa ambalo lingeweza kutokea. Daktari amesema ingawa Gusev kwasasa anaendelea vyema lakini ujasiri alioonyesha Kankava ndio uliookoa maisha ya nahodha huyo na kama angechelewa kupata huduma hiyo pengine angeweza kupoteza maisha. Katika mchezo huo Dnipro walishinda kwa mabao 2-0 na kukwea mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa ligi wakiwa nyuma ya vinara Shakhtar Donetsk.

FELLAINI AKWEPA ADHABU.

KIUNGO wa klabu ya Manchester United Marouane Fellaini hatapewa adhabu yoyote kutoka Chama cha Soka cha Uingereza-FA juu ya tuhuma za kumtemea mchezaji mwenzake mate. Fellaini alionekana katika picha za video akisimama juu ya beki wa Manchester City Pablo Zabaleta katika mchezo kati ya timu hizo uliochezwa wiki iliyopita na alikuwa katika hatari ya kufungiwa mechi tatu. Hata hivyo hofu hiyo imeondoka baada ya United kuhabalishwa kuwa Mbeligiji huyo ahatapewa adhabu yoyote. Katika taarifa yake FA ambayo ilikuwa imetaka picha zaidi za video kuchunguza tukio hilo, imedai kuwa hana kosa la kujibu kwasababu hakufanya tukio lolote baya kama ilivyodhaniwa.

NAPOLI KUMPA REINA MKATABA WA KUDUMU.

RAIS wa klabu ya Napoli, Aurelio De Laurentiis amethibitisha kuwa wanaangalia uwezekano wa kumbakisha golikipa Pepe Reina zaidi baada ya kumalizika kwa msimu huu. Reina mwenye umri wa miaka 31 yuko Napoli kwa mkopo wa msimu mmoja kutoka klabu ya Liverpool na amekuwa akicheza vyema katika kipindi alichokuwepo katika Uwanja wa San Paolo chini ya kocha Rafa Banitez. Kufuatia ushindi mnono wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Juventus jana ambao umefufua matumani yao ya kuwashika Roma waliopo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Serie A, De Laurentiis amebainisha kuwa wanaweza kumpa mkataba wa kudumu golikipa huyo wa kimataifa wa Hispania. Rais huyo amesema ameshazungumza na Reina, kama watamaliza ligi wakiwa katika nafasi ya pili atawazadia wote lakini pia anataka golikipa huyo abakie.

WANACHAMA TFF KUANDALIWA KATIBA MFANO YA MAREKBISHO.

KAMATI ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF imekutana Machi 30 mwaka huu kujadili utekelezaji wa maagizo ya TFF kwa wanachama wake kurekebisha Katiba zao ili ziendane na Katiba ya TFF pamoja na ile ya FIFA kabla ya Machi 30 mwaka huu. Vyama vya mikoa Lindi na Dar es Salaam na Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake (TWFA) viliomba kuongezewa muda wakati vingine vimeomba Katiba mama kama angalizo lao la mabadiliko hayo. Klabu ya Simba Sports ndiye mwanachama pekee aliyewasilisha mabadiliko ya Katiba. TFF inawapongeza viongozi na wanachama wa klabu hiyo kwa kufanya mkutano wao kwa utulivu. Kamati itatangaza nyongeza ya muda wa kufanya mabadiliko hayo baada ya kuviandalia vyama vya mikoa na vyama shiriki katiba mfano kwa ajili ya kurahisisha shughuli hiyo. Baada ya kupitia uamuzi wa wanachama wa Simba S.C. Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imeamua ifuatavyo: (i) Kwa kuwa pendekezo la wanachama wa Simba kubadili kipengele na 26 kuhusu sifa za mgombea kinapingana na kipengele na 29 (4) cha Katiba ya TFF, hivyo basi Kamati imeagiza kipengele cha Katiba ya Simba kibaki vilevile bila kubadilishwa. (ii) Vipengele vingine vyote vimepitishwa na vitapelekwa kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo kwa ajili ya kusajiliwa. (iii) Mchakato wa uchaguzi wa Klabu ya Simba uendelee kama ulivyopangwa wakizingatia uamuzi huu wa Kamati. TFF inaitakia Klabu ya Simba uchaguzi mwema. Pia Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imeshauri TFF kuwasiliana na FIFA kupata mwongozo kuhusu katazo la watu wenye rekodi ya kifungo kugombea. TFF imepokea ushauri huo na itaufanyia kazi na kama kuna mabadiliko yoyote kiutaratibu yataanzia katika Katiba ya TFF kupitia Mkutano Mkuu.

AL AHLY WAVULIWA UBINGWA LIGI YA MABINGWA AFRIKA.

MABINGWA watetezi Al Ahly ya Misri wameenguliwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika lakini wenzao Zamalek wamefanikiwa kusonga mbele. Al Ahly yenye maskani yake jijini Cairo walipoteza mchezo wao wa mkondo wa pili hatua ya timu 16 bora kwa kufungwa mabao 2-3 dhidi ya Al Ahli Benghazi ya Libya. Kwa ushindi huo Al Ahly ambao waliing’oa Yanga katika michuano hiyo nao wameng’olewa kwa jumla ya 4-2 na kuifanya Al Ahli Benghazi kutinga hatua muhimu ya makundi. Timu zote zilizoshindwa kusonga mbele baada ya mechi zao za mkondo wa pili zinaangukia katika michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo watatakiwa kucheza hatua ya mtoano kabla ya kuingia katika hatua ya makundi katika michuano hiyo. Katika mechi zingine zilizochezwa jana za michuano hiyo Esperance ya Tunisia nao walifanikiwa kusonga mbele kwajumla ya mabao 4-1 baada ya kuifunga Real Bamako ya Mali kwa mabao 3-0. Wengine ni Zamalek ambao nao walisonga mbele kwa jumla ya mabao 5-0 katika mechi walizokutana na Nkana ya Zambia huku Entente Setif nao wakisonga mbele baada ya kiondosha Coton Sport ya Cameroon kwa jumla ya mabao 2-0.


PELLEGRINI AMPASHA CHADOMO MOURINHO.

MENEJA wa klabu ya Manchester City, Manuel Pellegrini amempasha meneja wa Chelsea Jose Mourinho kuwa kocha yoyote mwenye ujuzi huwa hachezi na akili za watu. Kauli hiyo ya Pellegrini imekuja muda mfupi baada ya Mourinho kudai kuwa timu yake haiku katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu pamoja na ukweli kuwa walioongoza ligi hiyo kwa wiki kadhaa. Mourinho alienda mbali zaidi Jumamosi akidai kuwa ni suala lisilowezekana kwa timu yake kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza toka mwaka 2010 kufuatia kipigo cha kushtusha kutoka kwa Crystal Palace. Lakini Pellegrini amesisitiza kuwa mbinu anazotumia Mourinho haziwezi kumsaidia kwasababu hadhani kama kuna meneja yoyote anayetilia maanani mawazo yake. Pellegrini amesema huwa hajishughulishi kumjibu kwasababu hamwelewi anachosema.

DJOKOVIC ASHINDA TAJI LA SONY OPEN KWA KUMTANDIKA NADAL.

NYOTA wa tenisi Novak Djokovic amefanikiwa kushinda taji la michuano ya wazi ya Sony kwa kumtandika Rafael Nadal katika mchezo wa fainali uliofanyika jijini Miami. Djokivic raia wa Serbia mwenye umri wa miaka 26 alishinda mchezo huo kwa 6-3 6-3 ushindi uliompa taji la nne la michuano hiyo akimzidi Peter Sampras na kuwa nyuma ya nguli mwingine Andre Agassi aliyenyakuwa taji la michuano hiyo mara sita. Baada ya kushindwa kufanya vizuri katika msimu wa viwanja vigumu, Nadal mwenye umri wa miaka 27 anategemea kufanya vizuri wakati ziara ikienda Ulaya kwenye viwanja vya udongo ambapo alifanya vyema kwenye viwanja hivyo msimu uliopita. Katika mchezo huo Djokovic hakuwa na mwalimu wake Boris Becker ambaye anauguza majeraha ya paja baada ya kufanyiwa upasuaji.

RODGERS ATAMBA LIVERPOOL KUENDELEA KUJITANUA KILELENI.

MENEJA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers ana uhakika wa timu yake kukabiliana na changamoto za ushindani wa ubingwa baada ya kurejea kileleni mwa msimo wa Ligi Kuu nchini Uingereza. Liverpool jana usiku waliichabanga Tottenham Hotspurs kwa mabao 4-0 na wanaweza kutawadhwa mabingwa wapya wa ligi hiyo kama wakifanikiwa kushinda mechi zao sita zilizobakia. Rodgers amesema bado alama nyingi zinahitajika na pia itafika mahali mahali kila timu itapoteza alama kabla ya kumalikia kwa msimu hivyo hana hofu yoyote kwasababu ana uhakika na wanavyocheza. Mara ya mwisho Liverpool kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ilikuwa ni Desemba 26 mwaka jana na sasa wamerejea tena baada ya ushindi huo mnono dhidi ya timu ngumu ya Spurs. Liverpool wakiwa wamebakiwa na mechi zingine ngumu mbili dhidi ya mahasimu wao katika kinyang’anyiro cha ligi hiyo City na Chelsea, wanategemea kunyakuwa taji hilo kwa mara ya kwanza toka walipofanya hivyo msimu wa 1989-1990.

Sunday, March 30, 2014

VITALY KLITSCHKO AJITOA KINYANG'ANYIRO CHA URAIS UKRAINE.

MWANASIASA maarufu na bondia wa zamani nchini Ukraine, Vitaly Klitschko amejitoa katika kinyang’anyiro cha mbio za urais nchini humo zilizopangwa kufanyika Mei mwaka huu. Bingwa huyo wa dunia wa mwasumbwi ya uzito wa juu amesema badala yake atamuunga mkono mwanasiasa tajiri Petro Poroshenko katika uchaguzi huo. Wote wawili walikuwa sehemu muhimu ya maandamano mtaani ambayo yalipelekea kung’olewa kwa aliyekuwa rais wan chi hiyo Voktor Yanukovych. Kujitoa kwa Klitschko kunamaanisha kuwa mbio za urais sasa zitakuwa kati ya Poroshenko na aliyekuwa Waziri Mkuu Yulia Tymoshenko ambaye aliyotolewa gerezani hivi karibuni baada ya kuangushwa kwa utawala wa Yanukovych.

REUS ATUMA SALAMU SANTIAGO BERNABEU.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ujerumani, Marco Reus amewaonya Real Madrid kuwa klabu yake ya Borussia Dortmund wako tayari kwa ajili ya mchezo war obo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumatano. Dortmund wamejiweka vyema kwa ajili ya safari yao ya kwenda Hispania kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya timu iliyo katika hatari ya kushuka daraja ya Stuttgart huku Reus akifunga mabao matatu-hat trick. Reus anaamini kiwango alichoonyesha katika mchezo huo ni dalili tosha kwamba amerudi baada ya kusumbuliwa na majeruhi Machi mwaka huu. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 amesema mabao aliyofunga ni muhimu kwani yamewaongezea kujiamini zaidi na sasa wako tayari kwa ajili ya Madrid.

KAKA AFURAHIA KUTIMIZA MECHI YA 300 MILAN.

NAHODHA wa klabu ya AC Milan, Kaka amefurahishwa na kiwango alichokionyesha katika ushindi wa mabao 3-0 waliopata dhidi ya Chievo jana akifikisha mechi yake ya 300 akiwa na klabu hiyo. Kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil alifunga mabao katika kila kipindi, baada ya Mario Balotelli kuipa timu hiyo ushindi wa mapema katika Uwanja wa San Siro na kuifanya timu hiyo kupata ushindi wake wa pili mfululizo. Kaka amesema usiku wa jana ulikuwa ni wa kukumbukwa kwake na amefurahishwa na jinsi alivyocheza sambamba na wachezaji wenzake. Pamoja na Kaka kufurahia ushindi huo mapema kabla ya mchezo huo Ofisa Mkuu wa Milan Adriano Galliani alibainisha kuwa nyota huyo anaweza kuondoka katika majira ya kiangazi.

ANCELOTTI AWASHANGAA MASHABIKI WA MADRID KUMZOMEA RONALDO.

MENEJA wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amewaponda mashabiki wa timu hiyo kwa kumzomea Cristiano Ronaldo katika ushindi wa mabao 5-0 waliopata kutoka kwa Rayo Vallecano jana usiku. Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno alifunga bao la kwanza mapema lakini alizomewa na baadhi ya mashabiki katika Uwanja wa Santiago Bernabeu kwa kushindwa kutoa pasi kwa wenzake sehemu zinakuwa ngumu hivyo kufanya mpira kupotea. Ancelotti amesema hajui kwanini mashabiki hao walikuwa wanamzomea Ronaldo kwasababu anadhani timu ilicheza vyema na kupata ushindi waliohitaji. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa ni jambo la kawaida kuzomewa muda mwingine kama hawachezi vyena lakini kwa jinsi hali ilivyokuwa jana hakuona umuhimu wa mashabiki hao kuzomea.

GUARDIOLA AIHOFIA MAN UNITED.

MENEJA wa klabu ya Bayern Munich, Pep Guardiola ameonyesha kutofurahishwa kiwango cha timu yake katika mchezo dhidi ya Hoffenheim jana na kutaka wachezaji wake kubadilika haraka kabla ya mchezo wao wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa UUlaya dhidi ya Manchester United utakaochezwa Jumanne ijayo katika Uwanja wa Old Trafford. Bayern ambao walitawadhwa mabingwa wa Bundesliga wiki iliyopita walionekana kama watashinda mechi yao ya 20 mfululizo katika Bungesliga baada ya kufunga mabao matatu mapema lakini Hoffenheim walijirudi na kuswazisha mabao yote hivyo timu hizo kwenda sare ya mabao 3-3. Akihojiwa Guardiola amesema Hoffenheim wanastahili pongezi kwa kucheza vyema katika mchezo huo na kuhakikisha wamepata alama. Kocha huyo aliendelea kusema jambo la muhimu ni kuyafanyia kazi mapungufu yao haraka kabla ya kukwaana na United wiki ijayo.

KIPIGO DHIDI YA CRYSTAL PALACE KIMETUNYIMA UBINGWA - MOURINHO.

MENEJA wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho anaamini kuwa kipigo walichopata kutoka kwa Crystal Palace kimewaondolea nafasi ya kunyakuwa taji la Ligi Kuu msimu huu.  Bao pekee la kujifunga lililowekwa wavuni na nahodha John terry lilitosha kuihakikishia ushindi wa bao 1-0 Palace katika Uwanja wa Selhurst Park. Ingawa bado wanaendelea kukaa kuongoza ligi kwa tofauti ya alama moja lakini wanaweza kupitwa na iadha Liverpool au Manchester City kama wakishinda mechi zao za mkononi ambazo hawajacheza. Mourinho amesema matokeo hayo yameondoa matumaini yao ya kuendelea kukaa kileleni kwasababu wanategemea zaidi ya wenzao ambao wanawafukuzia kwasasa.

AUMIA VIBAYA BAADA YA KUANGUKA WAKATI WA UJENZI WA UWANJA BRAZIL.

MFANYAKAZI wa ujenzi ameumizwa vibaya nchini Brazil baada ya kuanguka katika Uwanja wa Corinthians ambao utatumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia baadae mwaka huu. Jina la mfanyakazi huyo halikubainishwa wazi lakini kitengo cha zima moto cha jiji la Sao Paulo wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kumkimbiza majeruhi hospitali. Imeripotiwa kuwa mfanyakazi huyo alianguka umbali wa mita nane na sasa yuko katika hali mbaya hospitali. Uwanja wa Corinthians umepangwa kutumika kwa ajili ya mechi sita za Kombe la Dunia ukiwemo mchezo wa ufunguzi kati ya wenyeji Brazil na Croatia sambamba na ule wa Uingereza na Uruguay. Uwanja huo tayari umeshazua majanga kipindi cha karibuni kufuatia wafanyakazi Fabio Luis Pereira mwenye miaka 42 na Ronaldo Oliviera dos Santos mwenye miaka 44 wote kupoteza maisha katika tukio lilitokea Novemba mwaka jana. Pia kumekuwa ni vifo vingine vilivyotokea wakati wa ujenzi katika viwanja vya Amazonia uliopo Manaus na Mane Garrincha uliopo jijini Brasilia.

Friday, March 28, 2014

HENRY KUKUTANA NA WENGER JULAI.

NAHODHA wa timu ya New York Red Bulls ya Marekani, Thierry Henry amekiri kuwa litakuwa jambo la ajabu kwake kucheza dhidi ya klabu yake ya zamani ya Arsenal wakati watakapofanya ziara Julai mwaka huu. Arsenal na Red Bulls walithibitisha jana kuwa watacheza mechi ya kirafiki Julai 26 ikiwa ni sehemu ya ziara ya klabu hiyo nchini humo. Mechi hiyo itakuwa mahsusi kwa Arsenal kujiandaa na msimu wa 2014-2015 wa Ligi Kuu na Henry ambaye amecheza mechi 254 akiwa na timu hiyo kuanzia mwaka 1999 na 2007 anajua kuwa itakuwa fikra tofauti kucheza na timu yake hiyo ya zamani. Henry amesema mara zote anapocheza dhidi ya Arsenal linakuwa jambo la ajabu kwake, alishawahi kufanya hivyo akiwa na Barcelona walipoenda kucheza michuano ya Kombe la Emirates na sasa wanakuja tena akiwa Marekani.


MARTINEZ APANIA KUMWAGA MIHELA KIANGAZI.

MENEJA wa klabu ya Everton Roberto Martinez amekiri kuwa ana nia ya kutumia fedha kusajili kabla ya kuanza kwa msimu mwingine wa Ligi Kuu kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake. Martinez alithibitisha hilo jana kuwa atatumia fedha katika kipindi cha usajili kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2014-2015 baada ya kujiweka katika nafasi nzuri msimu huu toka achukue mikoba ya kuinoa klabu hiyo Juni mwaka jana. Kocha huyo alimuuza Maroune Fellaini, Nikica Jelavic na Victor Anichebe wakati pia alimtoa kwa mkopo John Heitinga hivyo kuikusanyia klabu paundi milioni 40 na kupunguza mzigo wa mshahara. Martinez alibainisha kuwa hakutumia fedha zozote katika kipindi cha Januari hivyo wakati huo ndio utakuwa muafaka kutumia fedha hizo na nyingune atakazopewa ili kuimarisha kikosi hicho.

MILANGO IKO WAZI KWA VALDES KAMA AKIAMUA KUBAKIA - BARTOMEU.

RAIS wa klabu ya Barcelona, Josep Maria Bartomeu amedai kuwa Victor Valdes bado hajaamua kubakia klabuni hapo katika majira ya kiangazi yanayokuja. Mkataba wa sasa wa Valdes unatarajiwa kumalizika Juni na golikipa huyo wa kimataifa wa Hispania ameweka wazi huko nyuma kuwa huu utakuwa msimu wake wa mwisho na Barcelona, huku Monaco na Manchester City zikihusishwa na kunyemelea saini yake. Hata hivyo, Bartomeu amesisitiza hana taarifa ya ofa yoyote ambayo Valdes amefikia na klabu nyingine na kudai kuwa milango bado iko wazi kama akiamua kubakia baada ya kupona majeraha ya goti aliyopata katika mchezo dhidi ya Celta Vigo. Bartomeu amesema tayari wameshamwambia Valdes kuwa klabu iko upande wake na kwasasa mawazo yake yako katika upasuaji atakaofanyiwa lakini anajua kuwa milango iko wazi kwa ajili yake.

IBRAHIMOVIC YUKO KATIKA KIWANGO BORA MSIMU HUU - BLANC.

MENEJA wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG, Laurent Blanc anaamini kuwa Zlatan Ibrahimovic amekuwa katika msimu wake mzuri toka aanze kucheza soka. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Sweden amefunga mabao 40 katika mashindano yote akiwa na klabu yake hiyo na kuiwezesha kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea taji lao. Na kocha huyo ana uhakika nyota huyo wa zamani wa Barcelona na AC Milan anaweza kuendelea kucheza kwa kiwango cha juu mpaka mwishoni mwa msimu huu. Blanc amesema ana mategemeo Ibrahimovic ataendelea kufunga katika mechi muhimu zinazokuja na haoni kama hilo litamshinda. PSG inatarajiwa kusafiri kuifuata Nice Ijumaa katika mchezo wa ligi kabla ya kuikaribisha jijini Paris Chelsea kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza war obo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

RAMSEY KUIKOSA MAN CITY.

KIUNGO mahiri wa klabu ya Arsenal, Aaron Ramsey anatarajiwa kukosa mechi dhidi ya Manchester City mwishoni mwa wiki hii, baada ya kocha Arsene Wenger kuamua kutomharakisha nyota huyo wa kimataifa wa Wales kurejea kutoka katika majeruhi. Ramsey hatacheza mechi yoyote toka Desemba 26 mwaka jana wakati alipoumia kwenye mchezo dhidi ya West ham United ambao Arsenal walishinda kwa mabao 3-1. Wenger amebainisha kuwa wanatakiwa kuwa wavumilivu kwa nyota huyo ambaye amefunga mabao 13 katika mzunguko wa kwanza wa ligi aliocheza. Kocha huyo amesema Ramsey amekuwa akiendelea vizuri na tayari ameshaanza mazoezi na wenzake lakini inabidi kuvulia zaidi kwa wiki kadhaa kabla ya kumruhusu kurejea uwanjani rasmi. Wenger pia atawakosa nyota wake wengine kama Mesut Ozil na Jack Wilshere katika mchezo huo ambao City watasafiri kuifuata timu hiyo Emirates.

KLOPP AKERWA NA UEFA KUFANYA MAAMUZI WENYEWE BILA KUWASHIRIKISHA.

MENEJA wa klabu ya Borussia Dortmund, Jurgen Klopp amehuzunishwa na kitendo cha Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA kutowashirikisha makocha au wachezaji juu ya michuano mipya ya Ligi ya Mataifa. Michuano hiyo ambayo itashuhudia timu za Ulaya zikigawanywa katika makundi manne, imeanzishwa kwa madhumuni ya kuchukua nafasi ya kalenda ya mechi za kirafiki na kuleta ushindani zaidi. Hata hivyo, Klopp anafikiri mechi zitakazochezwa katika michuano hiyo zitahitaji nguvu zaidi za wachezaji. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 46 amesema anafikiri uamuzi huo ungekuwa tofauti kama viongozi waliotoa uamuzi huo wangekuwa pia wanatakiwa kucheza mechi hizo. Klopp amesema ingekuwa vyema zaidi kama UEFA wangewashirikisha makocha na wachezaji kwa ushauri juu ya uamuzi huo.

GIGGS NA NYOTA WENZAKE WA "CLASS OF 92" WAJIPANGA KUNUNUA TIMU.

RYAN Giggs na wachezaji wengine wanne wa zamani wa Manchester United wamekubaliana na mpango wa kununua timu isiyoshiriki ligi yoyote ya Salford City. Giggs akiwa katika msimu wake wa 24 kama mchezaji Old Trafford ameungana na wachezaji wengine wakiwemo ndugu wawili Gary na Phil Neville, Paul Scholes na Nicky Butt. Giggs mwenye umri wa miaka 40 ambaye kwasasa ni kocha mchezaji wa United amesema wanataka kutumia uzoefu na weledi wao katika soka kusaidia vijana wadogo ambao wanachipukia. Nyota hao hivi sasa wanasubiri Chama Cha Soka cha Uingereza-FA kupitisha mpango wao huo wa kuinunua timu hiyo.

WILLIAMS ATINGA FAINALI SONY OPEN.

MWANADADA nyota wa tenisi kutoka Marekani, Serena Williams ameendeleza rekodi yake ya kushinda mechi 15 mfululizo dhidi ya Maria Sharapova wa Urusi na kutinga fainali yake ya tisa ya michuano ya wazi ya Sony inayofanyika huko Miami. Williams anayeshika namba moja katika orodha za ubora duniani alifanikiwa kumgaragaza Sharapova kwa 6-4 6-3. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Williams amesema haikuwa kazi rahisi kwasababu mpinzani wake alikuwa akifanya vyema hivyo ilibidi atumie nguvu ili kufanya vizuri zaidi na kuweza kushinda mchezo huo. Williams ambaye ameshinda mara sita taji la michuano hiyo sasa atakwaana na aidha Dominika Cibulkova wa Slovakia au Li Na wa China.

Thursday, March 27, 2014

BASEL WALIMWA ADHABU NA FAINI KWA VURUGU ZA MASHABIKI.

KLABU ya Basel imethibitisha kuwa hawatarajii kukata rufani kupinga adhabu ya kufungiwa uwanja wao iliyotolewa na Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA kufuatia vurugu za mashabiki zilizozuka katika mchezo dhidi ya Red Bull Salzburg. Kamati ya nidhamu ya UEFAilitangaza jana kuwa mabingwa hao wa soka wa Switzerland wanatakiwa kucheza mechi yao ya mkondo wa kwanza ya robo fainali ya Europa League dhidi ya Valencia bila mashabiki baada ya kukutwa na makosa mawili ya vurugu za mashabiki wake huko Austria. Mwamuzi Manuel Grafe alilazimika kusimamisha mchezo baada ya mashabiki wa Basel waliosafiri kwenda kutizama mechi hiyo kurusha mafataki katika Uwanja wa Red Bull Arena wakikasirishwa na kadi nyekundu aliyopewa Marek Suchy sambamba na bao la Jinatan Soriano. Basel ambao pia wametozwa faini ya euro milioni 107,000 pamoja na kucheza huku milango ikiwa imefungwa, wameamua kutokana rufani juu ya adhabu hiyo na kulaani vikali vitendo hivyo vilivyofanywa na mashabiki wao.

BARCELONA YAMNASA MESSI MWINGINE KUTOKA DINAMO ZAGREB.

KLABU ya Barcelona imethibitisha kumsajili mchezaji nyota chipukizi Alen Halilovic kutoka klabu ya Dinamo Zagreb. Nyota huyo anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji amekuwa akiwindwa na vilabu mbalimbali barani Ulaya ikiwemo Manchester City, lakini ni Barcelona waliofanikiwa baada ya kutuma ujumbe wao nchini Croatia kumaliza dili hilo. Kinda huyo mwenye umri wa miaka 17 ambaye anatokana na matunda ya shule ya vipaji ya Dinamo amesaini mkataba wa miaka mitano kwa ada ya euro milioni 2.2. Akihojiwa Halilovic ambaye anafananishwa na Messi mdogo amesema ni ngumu kupata maneno ya kuzungumza jinsi anavyojisikia lakini anaishukuru sana Dinamo ambao atawapenda siku zote kwa kumfikisha hapo alipo sasa. Pia kinda huyo aliwashukuru makocha katika shule ya Dinamo waliomfundisha mpaka kufikia sambamba na mashabiki ambao mara zote wamekuwa nyuma yake.

NAJISIKIA NYUMBANI NIKICHEZA SAMBAMBA NA PIRLO - TEVEZ.

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Juventus, Carlos Tevez amesema anajisikia kuwa nyumbani akiwa katika kikosi hicho sambamba na kiungo Andrea Pirlo. Tevez ambaye alijiunga na Juventus akitokea klabu ya Manchester City, ameendeleza wimbi lake la upachikaji mabao akiwa amefunga mabao 19 katika mshindano yote mpaka sasa. Nyota huyo amesema anajisikia vyema kuwemo katika kikosi cha Juventus chini ya kocha Antonio Conte pamoja na wachezaji wenzake akiwemo mkongwe Pirlo. Conte amekigeuza kikosi cha Juventus kuwa cha ushindi na siku zote amekuwata nyota wake kufanya vizuri ndani na nje ya uwanja.

VALDES AIAGA BARCELONA KWA MAUMIVU.

GOLIKIPA wa klabu ya Barcelona, Victor Valdes ataikosa michuano ya Kombe la dunia baada ya kuumia vibaya goti lake la kulia katika ushindi wa mabao 3-0 waliopata dhidi ya Celta Vigo jana usiku. Valdes mwenye umri wa miaka 33 ambaye amesema anaondoka Barcelona mwishoni mwa msimu huu, alionekana akilia machozi wakati akitolewa nje katika machela kwenye dakika ya 23 ya mchezo huo. Klabu ya Barcelona ilithibitisha katika mtandao wake kuwa Valdes aliumia msuli wa ndani ya goti ambao utahitaji upasuaji ili kurekebisha. Kwa majeruhi hayo hawezi kupona kwa wakati na kuwepo katika kikosi cha timu taifa ya Hispania kitakachokwenda kutetea taji lake katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil baadae mwaka huu.

Wednesday, March 26, 2014

CHELSEA KUTENGA ZAIDI YA EURO MILIONI 36 KWA AJILI YA DIEGO COSTA.

KLABU ya Chelsea imeanza mikakati ya kumnasa mshambuliaji nyota wa Atletico Madrid, Diego Costa katika kipindi cha usajili majira ya kiangazi. Vinara hao wa Ligi Kuu wako tayari kutoa zaidi ya euro milioni 36 kwa ajili ya mshambuliaji huyo. Tayari wawakilishi wa Chelsea wameshaomba kukutana na kambi ya Costa na mazungumzo zaidi yanatarajiw akufanyika wiki ijayo. Chelsea wamepania kumnasa nyota huyo kabla ya kumalizika kwa msimu wa ligi na kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia ambayo anatarajiwa kuiwakilisha Hispania kutetea taji lao. Costa mwenye umri wa miaka 25 tayari amefunga mabao 31 katika mechi 41 alizocheza msimu huu katika mashindano yote huku akimfuatia Ronaldo mwenye mabao 26 kwa ufungaji wa mabao kwenye La Liga akiwa na mabao 23.


SAGNA AKATAA KUJIUNGA NA INTER.

RAIS wa klabu ya Inter Milan, Erick Thohir amethibitisha kuwa beki wa klabu ya Arsenal Bacary Sagna amekataa ofa ya kujiunga nao. Mkataba wa Sagna unamalizika katika majira ya kiangazi na tayari imebainika kuwa Arsenal wamempa ofa ya mkataba wa miaka miwili ambao utamfanya kulipwa kitita cha paundi 75,000 kwa wiki. Inter walikuwa na mategemeo ya kumshawishi beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa kuikacha klabu hiyo na kwenda nchini Italia lakini Thohir sasa amebainisha mpango hautawezekana kutokana na Sagna kukataa. Thohir aliwaambia waandishi wa habari kuwa Sagna ameamua kubakia Ligi Kuu ya Uingereza lakini bado wataendelea na mpango wao wa kuimarisha safu yao ya ulinzi.

SIJAWAHI KUWAFUNDISHA XAVI NA INIESTA KUCHEZA SOKA - GUARDIOLA.

MENEJA wa klabu ya Bayern Munich, Pep Guardiola amedai kufanya machache kuwageuza nyota wa Barcelona Xavi na Andres Iniesta kuwa wachezaji bora duniani. Viungo hao wa kimataifa wa Hispania wakiwa chini ya Guardiola alipokuwa Camp Nou waliiwezesha timu hiyo kunyakuwa mataji 14 kutoka mwaka 2008 mpaka 2011, yakiwemo mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Xavi na Iniesta pia walikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Hispania kilichonyakuwa mataji ya Ulaya sambamba Kombe la Dunia, na Guardiola amedai kuwa wachezaji wa aina hiyo hawahitaji kocha ili wacheze katika kiwango bora. Guardiola amesema wachezaji wa Barcelona wanajipa msukumo wenyewe, hajawahi kuwafundisha Xavi na Iniesta kucheza soka kazi yake ilikuwa ni kutoa msaada wa kiufundi kwani wamekuwa wakicheza vyema kwa miaka 20.

MASHABIKI WAMGEUKA FERGUSON KWA KUWACHAGULIA BOMU MOYES.

MASHABIKI wa klabu ya Manchester United wamemgeukia kocha wa zamani wa timu hiyo Sir Alex Ferguson baada ya kuona wakipokea kipigo kutoka mahasimu wao Manchester City katika Uwanja wa Old Trafford jana usiku. City ambao waliwasambaratisha majirani zao hao kwa mabao 3-0 yaliyofungwa na Edin Dzeko na Yaya Toure, waliamsha hasira kwa mashabiki hao na kuanza kuonyesha mabango ya kumlaumu Ferguson ambaye ndiye aliyemchagua David Moyes kuchukua nafasi yake. Mbali na kumshambulia Ferguson lakini pia kulikuwa mabango mbalimbali ya kumpinga Moyes kwenye mchezo huo. Hasira za mashabiki hao zimeibuka kutokana na timu hiyo kushindwa kufanya vyema msimu huu hususani katika uwanja wao wa nyumbani.

MAJERUHI NDIO WANAONIKWAMISHA - WENGER.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amebainisha kuwa Aaron Ramsey amebakisha wiki mbili kabla ya kurejea tena uwanjani na kukiri kuwa ni ngumu kupambana huku wachezaji wako nyota wakiwa majeruhi. Kiungo wa kimataifa wa Wales mara mwisho kuvaa jezi ilikuwa ni Desemba 26 mwaka jana ambapo alishindwa kurejea uwanja mara mbili baada ya majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua kumrudia. Sasa Wenger amesema kiungo huyo amebakisha muda kidogo kabla ya kurejea uwanjani wakati Mesut Ozil, Jack Wilshere na Laurent Koscielny pia wakiendelea kujiuguza. Akizungumza baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Swansea City, Wenger amesema ni jambo ngumu kupambana huku nusu ya wachezaji wako tegemeo wakiwa majeruhi.

KEWELL AAMUA KUTUNDIKA DARUGA.

WINGA wa zamani wa klabu ya Leeds United na Liverpool, Harry Kewell ametangaza rasmi kutundika daruga zake baada ya kucheza soka kwa karibu miongo miwili. Nyota huyo wa kimataifa wa Australia mwenye umri wa miaka 35 alirejea nyumbani kwao na kujiunga na klabu ya Melbourne Heart hatua ambayo ilichukuliwa kama kutafuta nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia baadae mwaka huu nchini Brazil. Hata hivyo mkongwe huyo alishindwa kuwa fiti kwa kukosa mechi tisa katika msimu huu kutokana na kuandamwa na majeruhi ya mara kwa mara. Kewell amesema baada ya kufikiria sana na kupata ushauri wa familia na marafiki ameona ni bora akatundika daruga ingawa bado angetamani kuendelea kucheza. Nyota huyo amesema pamoja na akili kumtaka kuendelea kucheza lakini mwili unaonekana kushindwa kumpa ushirikiano ndio maana ameamua kupumzika.

MOYES AKUBALI LAWAMA ZOTE.

MENEJA wa klabu ya Manchester United, David Moyes amekubali kubeba lawama zote kwa kuporomoka kwa klabu hiyo msimu huu baada ya kipigo walichopata kutoka kwa mahasimu wao Manchester City katika Uwanja wa Old Trafford. Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu kwasasa wako nafasi ya saba kwa tofauti ya alama 18 na vinara Chelsea baada ya timu hiyo kufungwa kwa mara ya sita kwenye uwanja wake nyumbani msimu huu. Moyes amesema yeye huwa anachagua kikosi cha kucheza hivyo anakubali lawama zote, huku akidai kuwa alijua utakuwa mwaka mgumu lakini alitegemea wataleta ushindani. Kipigo hicho kinamaanisha kuwa United wamepoteza mechi nyingi zaidi nyumbani kuliko ukijumlisha misimu mitatu iliyopita. Katika mechi tisa dhidi ya timu kubwa za Ligi Kuu wamefanikiwa kushinda mechi moja dhidi ya Arsenal Novemba mwaka huu.

BAYERN WAWEKA REKODI KWA KUBEBA SAHANI YA BUNGESLIGA MAPEMA ZAIDI.

KLABU ya Bayern Munich wametawadhwa kuwa mabingwa wa soka wa Ujerumani kwa mara ya 24 huku wakiweka rekodi ya kunyakuwa taji hilo wakiwa wamebaki na mechi saba. Ubingwa huo umekuja kufuatia ushindi wa mabao 3-1 waliopata ugenini dhidi ya Hertha Berlin mabao ambayo yalifungwa na kiungo Tony Kroos, Mario Gotze na Franck Ribery. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Guardiola amesema amafurahi kuleta taji lingine muhimu katika klabu hiyo na kuishukuru kwa kumpa nafasi kuwafundisha wachezaji mahiri kama hao. Akiwa tayari ameshanyakuwa taji la tatu katika kipindi kifupi likiwepo la UEFA Super Cup na Klabu Bingwa ya Dunia, Guardiola sasa anaweza kuhamishia nguvu zake kuhakikisha wanatetea taji la Ulaya walilopata mwaka jana.

Tuesday, March 25, 2014

BECKHAM KUJENGA BONGE LA UWANJA MIAMI.

NAHODHA wa zamani wa Uingereza, David Beckham amebainisha mpango wake wa kujenga uwanja wenye uwezo kubeba mashabiki 25,000 karibu na ufukwe jijini Miami kwa ajili ya timu yake anayotaka kuanzisha. Beckham mwenye umri wa miaka 38 alistaafu soka Mei mwaka jana na mapema mwaka huu alitangaza mpango wake wa kuanzisha timu itakayoshiriki Ligi Kuu nchini Marekani-MLS kutoka katika jiji hilo. Beckham amesema watu wanapofikiria Miami haraka wanafikiria kuwa karibu na maji ndio maana amemua kuweka uwanjani huo karibu na maji. Uwanja huo wa wazi utakuwa karibu na uwanja wa timu ya mpira wa kikapu ya Miami heat.

MJI WA PORTO ALEGRI HATARINI KUSHINDWA KUANDAA KOMBE LA DUNIA.

MEYA wa mji wa Porto Alegre uliopo kusini mwa Brazil amesema mji wake unaweza kujitoa kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia Juni mwaka huu kama sheria muhimu hazitapitishwa wiki hii. Jose Fortunati aliviambia vyombo vya habari nchini humo kuwa hakuna mpango mwingine wa kutafuta fedha nyingine nyingi zinazohitajika kwa ajili ya kukamilisha maandalizi yake. Michuano ya Kombe la Dunia inatarajiwa kuanza Juni 12 lakini kuna baadhi ya miji bado haijamaliza ujenzi wake. Uwanja wa Beira Rio uliopo Porto Alegre uko katika hatua za mwisho lakini bado unahitaji nyumba za muda mfupi kwa ajili ya vyombo vya habari, wadhamini na mambo mengine ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA.

ARSENAL YAJIPANGA KWA MAISHA BILA WENGER.

KLABU ya Arsenal ikiwa inategemea kocha wake Arsene Wenger kutia saini mkataba mpya lakini tayari wameshaanza kujipanga kuanza maisha bila ya uwepo wa kocha huyo. Wenger ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimi huu tayari ameahidi kuwa ataendelea kuinoa klabu hiyo. Mazungumzo ya mara ya kwanza kuhusiana na mkataba yalikuwa ni kumpa mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya paundi milioni nane kwa mwaka lakini sasa hivi inanekana atapewa mkataba wa miaka miwili pekee. Lakini kipigo cha mabao 6-0 walichopata toka kwa mahasimu wao Chelsea kunaweza kubadili mustakabali wa Wenger huku klabu hiyo ikionyesha kuvutiwa na kocha wa Everton Roberto Martinez na Jurgen Klopp wa Borussia Dortmund kama mbadala wake pindi atakapoamua kuachia ngazi.

ARSENAL YAWASAFISHA NYOTA WAKE KUFUATIA KADI NYEKUNDU YENYE UTATA.

KLABU ya Arsenal imefanikiwa kuhakikisha kuwa hakuna mchezaji yoyote kati ya Kieran Gibbs au Alex Oxlade-Chamberlain aliyeadhibiwa kufuatia kadi nyekundu yenye utata ilitolewa Jumamosi katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Chelsea. Gibbs alitolewa nje na mwamuzi Andre Marriner badala ya Oxlade-Chamberlain ambaye alishika mpira uliopigwa na Eden Hazard. Chama cha Soka cha Uingereza-FA kilibadilisha kadi nyekundu hiyo na kupatia Oxlade-Chamberlain lakini Arsenal walifanikiwa kushawishi jopo lililokuwa likisikiliza shauri hilo wakiwa kuwa mchezaji hazuia bao kufungwa kwasababu mpira ulikuwa ukielekea nje. Mwamuzi huyo naye pia aliepuka adhabu ambapo yeye pamoja na wasaidizi wake wiki watachezesha mchezo mwingine wa Ligi Kuu.

MMILIKI WA RED BULL ATISHIA KUJITOA MASHINDANO YA LANGALANGA.

MMILIKI wa Red Bull, Dietrich Mateschitz amesema kampuni yake inaweza kujitoa katika mashindano ya langalanga kama hatafurahishwa na jinsi mchezo huo unavyoendeshwa. Kauli yake hiyo imekuja kufuatia dereva wake wa Red Bull Daniel Ricciardo kuenguliwa katika mashindano ya Grand Prix ya Australia na sheria mpya zilizowekwa. Tajiri huyo amesema kuna kiwango cha mambo ambayo watayakubali lakini akiona kama masuala ya siasa yanazidi katika mchezo huo hawatakuwa na budi bali kujitoa. Red Bull imekata rufani dhidi Ricciardo kwa kutolewa katika mashindano hayo ya mwanzoni mwa msimu yaliyofanyika jijini Melbourne kwa kutumia mafuta mengi kuliko ilivyostahili katika sheria mpya na rufani hiyo inatarajiwa kusikilizwa April 14 mwaka huu.

TAJIRI WA KIITALIANO AKATALIWA KUINUNUA LEEDS.

BODI ya Ligi nchini Uingereza imemuengua mfanyabiashara wa Italia Massimo Cellino kununua hisa kubwa katika klabu ya Leeds United. Cellino ambaye anamiliki kampuni ya michezo ya Eleonora, alikubali kununua hisa za asilimia 75 za timu hiyo kutoka Gulf Finance House Capital, Februari mwaka huu. Hata hivyo hatua yake hiyo ilitiliwa shaka wiki iliyopita wakati alipokutwa na hatia ya kushindwa kulipa ushuru wa boti yake ya kifahari. Tajiri huyo amesema ataka rufani kuhusiana na suala hilo ili aweze kuisaidia klabu hiyo ambayo ina matatizo ya kifedha hivi sasa.

UJERUMANI YAKATAA MFUMO WA TEKNOLOGIA YA KOMPYUTA KATIKA MSTARI WA GOLI.

Mpira ukiingia pembeni ya nyavu na mwmauzi kukubali kuwa bao katika mchezo kati ya Bayer Leverkusen na Hoffenheim
LIGI ya Ujerumani haitatumia mfumo wa teknologia ya kompyuta katika mstari wa goli kufuatia kura zilizopigwa na timu zinazoshiriki ligi za juu. Katika kura hizo kulikuwa kunahitajika theluthi mbili ya kura kati ya timu zinazoshiriki Bundesliga na zile za Ligi Daraja la Kwanza lakini ni timu tatu pekee kati ya 18 za daraja hilo zilipiga kura ya kukubali mfumo huo. Ligi Kuu nchini Uingereza imeshaanza kutumia mfumo huo msimu huu na utatumika pia katika michuano ya Kombe la Dunia katika kipindi cha majira ya kiangazi nchini Brazil. Rais wa Ligi za Soka nchini Ujerumani Reinhard Rauball amesema suala hilo wameshaliondoa mezani kwasasa kutokana na kura kutofikia. Suala la matumizi ya mfumo huo lilizua mjadala mkubwa Octoba mwaka jana wakati mwamuzi Stefan Kiessling alipowapa bao Bayer Leverkusen katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Hoffenheim ingawa mpira uliingia wavuni kupitia katika tundu lililokuwa pembezoni mwa neti. Hoffenheim walikata rufani mchezo huo urudiwe lakini ikatupiliwa mbali.

RANIERI AMSAMEHE ABIDAL BAADA YA KUOMBA RADHI.

MENEJA wa klabu ya Monaco, Claudio Ranieri amemrejesha Erick Abidal katika kikosi chake baada ya beki huyo kuomba radhi kwa kuondoka katika benchi la wachezaji wa akiba bila kuaga mwishoni mwa wiki iliyopita. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa, aliondoka katika Uwanja wa Louis II kabla ya mchezo wa ligi kati ya Monaco na Lille ikiripotiwa kuwa alifanya hivyo baada ya kugundua hatakuwepo katika kikosi cha kwanza kwenye mchezo huo. Hata hivyo, Ranieri amethibitisha kuwa Abidal atakuwepo katika kikosi chake katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Ufaransa baada ya kuomba kwa kitendo hicho. Ranieri amesema hana tatizo na Abidal tena kwasababu kulifanyika mkutano na makamu wa rais wa klabu hiyo Vadim Vasilyev na ameomba radhi. Abidal mwenyewe aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akiwaomba radhi mashabiki na wachezaji wenzake kwa kitendo chake hicho huku akidai mambo yameshakwisha na kila kitu kiko sawa.

Saturday, March 22, 2014

SUAREZ ATUPIA TATU LIVERPOOL IKISHINDA 6-3.

MAN CITY YAMCHANA FULHAM 5-0, YAYA TOURE ATUPIA TATU PEKE YAKE.

WENGER AKUBALI LAWAMA KUFUATIA KIPIGO CHA MABAO 6-0.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amekubali kubeba lawama zote kufuatia kipigo cha kudhalilisha cha mabao 6-0 ilichopata kutoka kwa mahasimu wao aktika mbio za ubingwa Chelsea. Wenger ambaye alitimiza mechi yake ya 1,000 katika mchezo huo ameeleza kuwa kama siku mbaya katika kazi yake ya ukocha baada ya kikosi chake kujikuta nyuma kwa mabao 3-0 huku wakiwa pungufu baada ya dakika 17. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Wenger amesema hilo ni kosa lake na anakubalia kubeba lawama zote kwa kiwango wachocheza hivyo hadhani kama kuna haja ya kuzungumza sana kutokana na makosa waliyofanya. Wenger amesema jambo la muhimu ni kusahau maumivu ya mechi hiyo na kuhamishia nguvu katika mchezo wa Jumanne dhidi ya Swansea City.

KAMA ULI-MISS HIVI NDIVYO MOURINHO ALIVYOMDHALILISHA WENGER KWA MABAO 6-0.

NAUJUA UDHAIFU WA BAYERN HIVYO MSIWE NA HOFU - MOYES.

MENEJA wa klabu ya Manchester United, David Moyes amesema ameshagundua udhaifu wa mchezo wa Bayern Munich na atajaribu kuutumia ili wakati timu hizo zitakapokutana katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. United wamepangwa na mabingwa hao watetezi katika ratiba iliyopangwa Ijumaa baada ya kuizabua Olympiakos na kutinga hatua hiyo. Bayern kwasasa wako kileleni mwa msimamo wa Bundesliga kwa tofauti ya alama 23 huku wakiwa wamecheza mechi 50 bila kufungwa lakini Moyes bado anaamini United inayoweza kupata matokeo katika mchezo huo. Moyes amesema amejaribu kuchukua vitu vichache kwa ajili ya kuvifanyia kazi ambavyo anaamini ndio udhaifu wa Bayern walionao na ni mategemeo yake vinaweza kusaidia.

MICHUANO YA SONY OPEN YAZIDI KUNOGA.

BINGWA mtetezi Andy Murray amefanikiwa kumfunga Matthew Ebden wa Australia na kutinga mzunguko wa tatu wa michuano ya wazi ya Sony inayofanyika jijini Miami, Marekani. Haikuwa kazi rahisi kwa Murray kutinga hatua hiyo kwani alipoteza seti ya kwanza kabla ya kuzinduka na kufanikiwa kumshinda Abden kwa 3-6 6-0 6-1. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Murray amesema kitendo cha kumkosa kocha wake wa siku nyingi ambaye alimtimua wiki iliyopita, imekuwa ngumu lakini anakiwa kusahau hayo na kuhakikisha anacheza kwa kiango bora zaidi. Murray ambaye alimfunga David Ferrer katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo iliyochezwa mwaka jana, sasa ataungana na Novak Djokovic na bingwa mara mbili wa michuano hiyo Roger Federer katika hatua inayofuata.

MOURINHO ALALAMIKIA FA KUTOMTENDEA HAKI.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amedai kuwa Chama cha Soka cha Uingereza-FA, huwa kinamfanyia visivyo baada ya kushitakiwa kwa tabia zisizo za kiungwana kwa kufukuzwa katika benchi lake la ufundi katika mchezo dhidi ya Aston Villa. Mourinho alitolewa baada ya kuingia uwanjani kuzungumza na mwamuzi Chris Foy akipinga kutolea nje kwa kadi nyekundu kwa Ramires ambapo Chelsea iliambulia kipigo cha bao 1-0 katika Uwanjwa Villa Park. Wakati Mourinho akiwa tayari amebainisha kukata rufani kuhusiana na suala hilo amebainisha pia anavyochanganyikiwa na jinsi FA wanavyomfanyia. Mourinho amesema pamoja na kutendewa ndivyo sivyo lakini bado anaendelea kuwa na imani ya juu kwa waamuzi wa Ligi Kuu.