Thursday, March 27, 2014

VALDES AIAGA BARCELONA KWA MAUMIVU.

GOLIKIPA wa klabu ya Barcelona, Victor Valdes ataikosa michuano ya Kombe la dunia baada ya kuumia vibaya goti lake la kulia katika ushindi wa mabao 3-0 waliopata dhidi ya Celta Vigo jana usiku. Valdes mwenye umri wa miaka 33 ambaye amesema anaondoka Barcelona mwishoni mwa msimu huu, alionekana akilia machozi wakati akitolewa nje katika machela kwenye dakika ya 23 ya mchezo huo. Klabu ya Barcelona ilithibitisha katika mtandao wake kuwa Valdes aliumia msuli wa ndani ya goti ambao utahitaji upasuaji ili kurekebisha. Kwa majeruhi hayo hawezi kupona kwa wakati na kuwepo katika kikosi cha timu taifa ya Hispania kitakachokwenda kutetea taji lake katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil baadae mwaka huu.

No comments:

Post a Comment