Wednesday, March 26, 2014

CHELSEA KUTENGA ZAIDI YA EURO MILIONI 36 KWA AJILI YA DIEGO COSTA.

KLABU ya Chelsea imeanza mikakati ya kumnasa mshambuliaji nyota wa Atletico Madrid, Diego Costa katika kipindi cha usajili majira ya kiangazi. Vinara hao wa Ligi Kuu wako tayari kutoa zaidi ya euro milioni 36 kwa ajili ya mshambuliaji huyo. Tayari wawakilishi wa Chelsea wameshaomba kukutana na kambi ya Costa na mazungumzo zaidi yanatarajiw akufanyika wiki ijayo. Chelsea wamepania kumnasa nyota huyo kabla ya kumalizika kwa msimu wa ligi na kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia ambayo anatarajiwa kuiwakilisha Hispania kutetea taji lao. Costa mwenye umri wa miaka 25 tayari amefunga mabao 31 katika mechi 41 alizocheza msimu huu katika mashindano yote huku akimfuatia Ronaldo mwenye mabao 26 kwa ufungaji wa mabao kwenye La Liga akiwa na mabao 23.


No comments:

Post a Comment