Sunday, September 30, 2012

URUSI YATANGAZA MIJI ITAKAYOTUMIKA KOMBE LA DUNIA.

NCHI ya Urusi imetangaza miji 11 ambayo itakuwa wenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia 2018 ikiwa ni mradi wa kwanza mkubwa kufanywa na nchi toka kuanguka kwa iliyokuwa USSR. Michuano hiyo mikubwa kabisa duniani itachezwa katika miji ya Moscow, Saint Petersburg, Sochi mji ambao pia uwakuwa mwenyeji wa michuano ya Olimpiki ya kipindi cha baridi 2014, Kazan, Yekaterinburg, Kaliningrad, Nizhny Novgorod, Samara, Rostov-on-Don, Saransk na Volgograd. Katika sherehe hizo zilizokuwa zikionyeshwa moja kwa moja katika luninga, huku zikiongozwa na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter na Waziri wa Michezo wa nchi hiyo Vitaly Mutkoongozwa miji miwili ya Yaroslavl na Krasnodar iliondolewa katika orodha iliyokuwa na miji 13. Tofauti na michuano ya Olimpiki ya kipindi cha baridi, Kombe la Dunia litaihitaji serikali kutumia mabilioni ya dola kwa ajili kuendeleza viwanja, utalii na miundo mbinu ya usafiri kwa nchi nzima. Urusi ilipewa nafasi ya kuandaa Kombe la Dunia 2018 katika uchaguzi uliogubikwa na utata Desemba mwaka 2010 ambapo ulishuhudia nchi ya Qatar nayo ikipewa nafasi ya kuandaa michuano 2022 kwa kuishinda Uingereza ambayo nayo ilikuwa inataka nafasi hiyo.

RONALDO ATAMANI KUWA MCHEZAJI ANAYELIPWA ZAIDI DUNIANI.

TAMAA ya mshambuliaji nyota wa klabu ya Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani kunaongeza kukua kwa mgawanyiko ndani ya klabu hiyo kitendo ambacho kinavistua vilabu vingine tajiri barani Ulaya. Mmiliki wa klabu ya Chelsea pamoja na tajiri wa kiarabu anayemiliki Manchester City na klabu ya Paris saint-Germain ya Ufaransa ndio wanaoongoza katika orodha ya timu ambazo zinawinda saini ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 27. Mshahara wa Ronaldo wa Euro milioni 7.98 ambao ni nusu na mshahara anaopata Samuel Eto’o katika klabu ya Anzi ya Urusi unamfanya nyota huyo kuwa wa 10 miongoni mwa orodha ya wachezaji wanaolipwa zaidi duniani. Nyota alikuwa akihitaji nyongeza ya asilimia 50 katika mshahara wake lakini suala hilo litakuwa gumu katika klabu hiyo kutokana na hali mtikisiko wa kiuchumi ulioikumba nchi hiyo katika kipindi cha hivi karibuni. Mapema mwezi huu Ronaldo alihojiwa na kudai kuwa suala la kitaaluma ndilo linalomsababisha akose furaha na klabu hiyo inajua hilo kauli ambayo ilizua mijadala katika vyombo mbalimbali vya habari duniani juu ya mstakabali wa mbeleni wa nyota huyo.

NILIPANGA KUMPUMZISHA TERRY - DI MATTEO.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Roberto di Matteo amekiri kuwa alitaka kumuondoa John Terry katika kikosi chake ambacho kiliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Arsenal katika Uwanja wa Emirates jana. Terry alijumuishwa katika kikosi hicho ikiwa ni siku mbili toka alipofungiwa mechi nne na kutozwa faini ya paundi 220,000 na Chama cha Soka nchini Uingereza-FA baada ya kukutwa na hatia ya kumfanyia ubaguzi wa rangi beki wa Queens Park Rangers, Anton Ferdinand. Adhabu imekuja kufuatia tukio baina ya timu hizo ambazo ni mahasimu wa Magharibi mwa jiji la London Octoba mwaka jana ingawa hatahivyo adhabu itaanza pale ambapo muda wa kukata rufani utakapokwisha. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Di Matteo ambaye ni kiungo wa zamani wa kimataifa wa Italia na Chelsea amesema kuwa alifikiri kumuacha nahodha wake huyo katika mchezo huo lakini uamuzi wa kumjumuisha ulikuwa mzuri kutoka kiwango bora alichoonyesha.

MWAMUZI ALITUPUNJA MUDA WA NYONGEZA - FERGUSON.

MENEJA wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema kuwa muda wa dakika nne za nyongeza alizotoa mwamuzi wakati timu yake ikifungwa Tottenham Hotspurs hazikuwa sahihi. Clint Dempsey ndiye aliyefunga bao la ushindi na kuifanya Spurs kutoka na ushindi wa mabao 3-2 katika Uwanja wa Old Traford kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 23. Ferguson amesema kuwa dakika nne za nyongeza zilizotolewa na mwamuzi zilikuwa chache kutokana na Spurs kupoteza dakika nyingi katika mchezo huo. Kocha huyo aliendelea kusema kuwa ni kitu kinachokatisha tamaa kwasababu walikuwa na rekodi nzuri lakini anadhani mwamuzi alichangia kuwafanya wapoteze mchezo huo baada ya kuongeza muda mchache kulinganisha na ule ambao wapinzani walikuwa wakipoteza katika dakika 90. Hicho kinakuwa kipigo cha pili kwa United katika michezo sita ya Ligi Kuu nchini Uingereza waliyocheza msimu huu ambapo sasa wanashika nafasi ya tatu nyuma ya vinara wa ligi hiyo Chelsea na Everton.

Saturday, September 29, 2012

Sevilla vs Barcelona 2 - 3 Full Highlights & All Goals

Manchester United Vs Tottenham 2-3 All Highlights And Goals 9-29-2012 HD

Parma vs Milan 1-1 Highlights Ampia Sintesi 29-09-2012

AS Roma vs Juventus Score 1- 4 Highlights & Goals 21st March 2009

Dortmund v B. Moenchengladbach 5-0 29th September 2012

Freestyle football competition - Red Bull Street Style 2012 Switzerland

The Best Street Football Skills Ever 2011!

Top 7 Athletes NOT to Sleep With ... besides Tiger Woods!

17 Craziest Field Crashers!!!

football skills - Zidane, Ronaldo and Ronaldinho

Friday, September 28, 2012

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.

TFF YATOA ITC KWA WACHEZAJI WANNE
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wanne waliokuwa wakichezea timu mbalimbali nchini. Wachezaji hao ni Tony Ndolo aliyejiunga na KCC ya Uganda kutoka Toto Africans, Felix Amech Stanley aliyekwenda Bahla ya Oman kutoka Coastal Union, Ernest Boakye kutoka Yanga aliyejiunga na Tripoli Athletics Club ya Lebanon na Derrick Walulya aliyerejea URA ya Uganda kutoka Simba.

15 WACHUKUA FOMU UCHAGUZI TWFA
Wanamichezo 15 wamechukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao. Waliochukua fomu za kuwania uenyekiti ni Lina Kessy, Isabellah Kapera na Joan Minja. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imeombwa na Roseleen Kisiwa pekee wakati Katibu Mkuu ni Amina Karuma na Cecilia Makafu. Macky Mhango pia ni mwombaji pekee aliyeomba nafasi ya Katibu Msaidizi. Waombaji watatu wa nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni Furaha Francis, Juliet Mndeme na Zena Chande. Nafasi ya Mhazini nayo ina mwombaji mmoja tu ambaye ni Rose Msamila. Sophia Charles, Rahim Maguza, Telephonia Temba na Jasmin Badar Soud wao wanaomba nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya chama hicho kwenye uchaguzi huo ambao utaendeshwa na Kamati ya Uchaguzi ya TWFA chini ya Ombeni Zavalla.

MKUTANO VODACOM, KLABU ZA LIGI KUU
Klabu za Ligi Kuu na mdhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom zimekutana jana (Septemba 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo yalilenga kipengele ya upekee (exclusivity) kilichopo kwenye mkataba wa udhamini ambacho kitaendelea kuwepo. Klabu zilikuwa zimeomba kwa mdhamini kuangalia uwezekano wa kukiondoa. Pande hizo zimekubaliana kuunda kamati ya pamoja kwa ajili ya kuitafutia kila klabu mdhamini binafsi kwa lengo la kuhakikisha zinashiriki kikamilifu katika ligi hiyo. Klabu zote zimeshapata vifaa kutoka kwa Vodacom ukiondoa African Lyon ambayo ilitarajia kuchukua vifaa hivyo leo kutoka kwa mdhamini wa ligi hiyo.

MCHAKATO WA UCHAGUZI WA VIONGOZI TAFCA
Mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) unaanza rasmi Septemba 30 mwaka huu kwa uchukuaji fomu kwa wagombea. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA, Ramadhan Mambosasa, fomu kwa waombaji uongozi zitaanza kutolewa Septemba 30 mwaka huu, na mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu hizo ni Oktoba 4 mwaka huu. Fomu hizo zinapatikana ofisi za TAFCA zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 alasiri. Ada ya fomu kwa waombaji wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu Msaidizi ni sh. 200,000. Nafasi zilizobaki za Mhazini, mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wajumbe wa Kamati ya Utendaji, ada ya fomu ni sh. 100,000. Uchaguzi wa TAFCA umepangwa kufanyika Novemba 10 mwaka huu.

CHELSEA USO KWA USO NA ARSENAL.

KLABU ya Chelsea inatarajia kuendelea kujikita kileleni mwa Ligi Kuu nchini Uingereza kwa kushinda mchezo wao wa kesho dhidi ya mahasimu wao wa jiji la London Arsenal katika mchezo wao wa kwanza toka nahodha wao John Terry afungiwe kutokana na ubaguzi wa rangi. Terry amefungiwa mechi nne na Chama cha Soka cha Uingereza-FA jana baada ya kukutwa na hatia ya kumfanyia vitendo vya ubaguzi wa rangi beki wa timu ya Queens Park Rangers-QPR Anton Ferdinand na pia kutozwa faini ya paundi 220,000. Terry amepewa siku14 toka atapopokei barua ya uamuzi uliofikiwa na FA kukata rufani kama hakuridhishwa na hukumu hiyo aliyopewa kufuatia tukio hilo ambalo lilitokea wakati wa mchezo wa baina ya Chelsea na QPR uliochezwa katika Uwanja wa Loftus Road Octoba 23 mwaka jana. Adhabu hiyo haitaanza kufanya kazi mpaka muda wa kukata rufani utakapokwisha hiyo inamaanisha kuwa beki huyo atakuwepo katika mchezo wa kesho dhidi ya Arsenal ambao utachezwa katika Uwanja wa Emirates.

XAVI AWABEZA MAHASIMU WAO MADRID.

KIUNGO nyota wa klabu ya Barcelona Xavi Hernandez anafikiri kuwa kuongoza kwao kwa alama nane zaidi ya Real Madrid kunawapa wakati mgumu mahasimu wao hao katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga. Barcelona ambao kiwango chao kimekuwa kinapanda na kushuka msimu huu kutokana na mabeki wake tegemeo kuwa kupata majeruhi ya mara kwa mara watasafiri kuifuata Sevilla kesho ili kutafuta ushindi wake sita ukilingasha na Madrid ambao wameshinda wameshinda mechi mbili pekee msimu huu. Xavi amesema kuwa unapokuwa mbele kwa alama unakuwa unacheza kwa kutulia zaidi kuliko nafasi waliyonayo mahaimu wao Madrid ambao hivi sasa inabidi washinde kila mchezo ili kupunguza pengo. Tatizo kubwa la Barcelona msimu huu limekuwa ni kwa mabeki wake ambapo Gerard Pique Carles Puyol na Adriano wote ni majeruhi lakini kiungo wa zamani wa Arsenal aliyesajiliwa msimu huu Alex Song ameonekana kumudu vyema nafasi ya beki wa kati katika michezo ya hivi karibuni.

KOMBE LA DUNIA 2014 BRAZIL KUCHEZWA MCHANA.

BAADHI ya timu zitakazoshiriki michuano ya Kombe la Dunia 2014 zinatarajiwa kucheza mechi za mchana katika baadhi ya viwanja nchini Brazil baada ya kutolewa ratiba ya muda zitakapochezwa mechi za michuano hiyo. Mechi nyingi kati ya 64 zinatarajiwa kuchezwa mchana kitu ambacho hakitakuwa na tatizo kwa miji iliyopo upande wa Kusini mwa nchi hiyo ambapo kuna baridi lakini inaweza kuwa tatizo kwa wachezaji kucheza katika katika joto kali kwa timu ambazo zitapangwa katika miji iliyopo upande wa Kaskasini na Kaskazini-Mashariki. Jografia ya nchi hiyo inaonyesha kuwa kipindi cha mwezi June na Julai ni kipindi cha baridi kwa miji iliyopo upande wa Kusini mwa nchi hiyo lakini hali huwa ya kitropiki yaani joto katika sehemu za Kaskazini. Sehemu kubwa ya nchi ya Brazil imepishana masaa matatu na bara la Ulaya kitu ambacho kitakuwa kizuri kwa watazamaji wa televisheni wa bara hilo ambao watakuwa wakiona michuano hiyo jioni. Lakini muda huo utakuwa mzigo mkubwa kwa watazamaji wa bara la Asia itabidi wasubiri mpaka usiku wa manane ili waweze kushuhudia michuano hiyo.

HAMILTON AHAMIA MERCEDES.

Dereva nyota wa mbio za magari yaendayo kasi ya Langalanga, Lewis Hamilton anatarajiwa kuihama timu ya McLaren baada ya kusaini mkataba na timu ya Mercedes kwa ajili ya msimu ujao. Uhamisho huo utamlazimu dereva nyota kutoka Ujerumani Michael Schumacher kuondoka katika timu ya Mercedes lakini bado haijakuwa wazi kama nguli huyo atastaafu au atatafuta timu nyingine kwa ajili ya msimu ujao. Dereva kutoka timu ya Sauber, Sergio Perez ndio amesajiliwa na MacLaren ili kuziba pengo la Hamilton. Uamuzi huo wa Hamilton utakuwa ni pigo kubwa kwa MacLaren ambapo sasa itabidi waendelee bila ya kuwepo kwa dereva wao huyo ambaye wamekuwa nae toka akiwa na umri wa miaka 13.

Thursday, September 27, 2012

WENGER AMSIHI WALCOTT KUWA NA SUBIRA.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amempongeza mshambuliaji wake nyota Theo Walcott kwa kiwango alichokionyesha jana lakini amemwambia kuwa inabidi awe mvumilivu kuhusu ombi lake la kubadilishwa na kuwa mshambuliaji wa kati. Walcott mwenye umri wa miaka 23 alifunga mabao mawili katika ushindi wa mabao sita iliyopata timu hiyo katika mzunguko wa tatu wa michuano ya Kombe la Capital One. Wenger alimsifu mchezaji kwa uwezo wake mkubwa wa kumalizia pindi awapo mbele goli lakini kwasasa amemuomba awe mvumilivu kwakuwa kuna mchuano mkubwa wa kugombea namba ya sehemu hiyo na timu inafanya vizuri. Meneja huyo ambaye kwasasa amuwa akipenda kumtumia mshambuliaji nyota wa kimataifa kutoka Ivory Coast, Gervinho amesema kuwa muda wa Walcott kutumika katika nafasi hiyo utawadia.

MECHI ZA CAPITAL ONE CUP MZUNGUKO WA NNE.

KLABU ya Chelsea inatarajiwa kupambana na Manchester United katika mzunguko wa nne wa michuano ya Kombe la Ligi baada ya kushinda michezo yao dhidi ya Wolves na Newcastle katika mzunguko wa tatu. Mabingwa watetezi Liverpool ambao walifanikiwa kuifunga West Bromwich wataikaribisha Swansea katika Uwanja wa Anifield mchezo ambao utashuhudia meneja wa timu hiyo Brendan Rodgers akipambana na klabu yake ya zamani. Leeds United ambao walipata ushindi wa kushangaza wa mabao 2-1 dhidi ya Everton Jumanne watakuwa wageni wa Southampton katika Uwanja wa Elland Road, wakati Aston Villa baada ya kuwaondosha mabingwa wa ligi kuu Manchester City wenyewe wataifuata timu ya Swidon katika mzunguko wa nne. Arsenal ambao walitinga fainali ya michuano hiyo mwaka 2011 wataifuata Reading wakati meneja wa Tottenham Hotspurs Andre Villas-Boas atakipeleka kikosi chake kupambana na Norwich. Katika michezo mingine ya mzunguko wanne ya michuano hiyo Wigan itacheza na Bradford wakati Sunderland itaikaribisha Middlesbrough.

MATOKEO YA CAPITAL ONE CUP.

TIMU ya Manchester United imefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Ligi baada ya kufanikiwa kuifunga Newcastle United kwa mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Old Traford jana. Mbali na United mabingwa watetezi wa michuano hiyo Liverpool nao pia walifanikiwa kusonga baada ya kuifunga West Bromwich kwa mabao 2-1 mabao ambayo yalifungwa na mshambuliaji mpya aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka Real Madrid ya Hispania, Nuri Sahin. Katika michezo mingine ilishuhudia Tottenham Hotspurs ikiifunga Carlisle kwa mabao 3-0 huku mahasimu wao kutoka Kaskazini mwa jiji la London Arsenal wao wakifanya mauaji kwa kuibugiza Coventry City kwa mabao 6-1. Katika mchezo wa jana United walifanya mabadiliko ya wachezaji 11 ambao walicheza katika mchezo dhidi ya Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu Jumapili iliyopita huku mshambuliaji wake nyota Wayne Rooney akirejea baada ya kuumia goti wiki nne zilizopita pamoja na kiungo Darren Fletcher naye akirejea baada ya kuwa nje ya uwanja kwa miezi 10.

Wednesday, September 26, 2012

VODACOM YAZUNGUMZIA KIPENGELE CHA UPEKEE(EXCLUSIVITY)KATIKA MKATABA WA UDHAMINI WA LIGI KUU BARA.

Dar es salaam 25th September 25, 2012, Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imesema suala la kuwepo kwa kipengele cha Upekee “EXCLUSIVITY” katika mkataba wa udhamini wa ligi kuu soka Tanzania bara kati ya kampuni hiyo na shirikisho la soka nchini - TFF ni la muhimu katika kuepuka migongano ya kimasilahi ya kibiashara miongoni mwa wadhamini.

Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa kampuni ya Vodacom Tanzania Bw Kelvin Twissa amesema kampuni ya Vodacom inajali na kuthamini maendeleo ya vilabu nchini na kwamba itaendelea kufanya hivyo kwa kutoa fursa zaidi zinazolenga kukuza kiwango cha uwekezaji katika soka kwa masilahi ya vilabu na taifa kwa ujumla.

Twissa amesema katika kutambua umuhimu wa kupanua wigo wa uwekezazi katika ligi kuu ya Vodacom na maendeleo ya vilabu kwa ujumla, kampuni ya Vodacom Tanzania ilikubali kwa moyo mkunjufu kuruhusu vilabu kutafuta wadhamini wengine ambao siyo makampuni yanayofanya baishara sawa na Vodacom.

Twissa alikuwa akizungumza katika kikao cha pamoja kilichowakutanisha Shirikisho la Soka Tanzania – TFF, Kamati ya Ligi Kuu na Mdhamini Mkuu kampuni ya Vodacom Tanzania kilichoketi jana jijini Dar es salaam.

“Tunatambua na kuheshimu utayari wa makampuni mengine ambayo yapo tayari kushirikiana na sisi katika kudhamini Ligi kuu ya Vodacom nasi tupo tayari kushirikiana nao na hivyo kuleta maendeleo ya mpira wa miguu nchini”Alisema Twissa

“Vodacom Tanzania inajivunia kuwa wadhamini wakuu wa ligi hii,tumeamua kuboresha udhamini wetu kwa sababu tunatambua umuhimu wa michezo kwa Taifa letu, sasa michezo si kwa ajili ya burudani tu bali imekuwa chanzo cha ajira na kuboresha maisha ya wanaojihusisha nayo,” Aliongeza Twissa.

“Tunaviomba vilabu vinavyoshiriki ligi kuu, vyombo vya habari na umma kwa ujumla kutambua kuwa azma ya Vodacom ni kuona mpira wa miguu unasonga mbele zaidi na ndio maana tumekuwa katika udhamni huu kwa zaidi ya miaka saba tukipitia vipindi tofauti lakini hatukuwahi kukata tamaa. Hivyo si vyema wakati huu soka yetu inapokua tukaruhusu hali inayoweza kusababisha changamoto katika uwekezaji wa soka.” Aliongeza Twisa

Twissa amesema kampuni ya Vodacom itaendelea kushirikiana na TFF, Kamati ya Ligi na wadau wengine wote wa mpira wa miguu nchini katika kukuza uwekezaji kwa kusaidia vilabu kupata wadhamini watakaosaidia maendeleo ya vilabu hivyo.

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.

KAMATI YA UCHAGUZI TFF YATUPA RUFANI YA WARUFANI IRFA
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana jana (Septemba 25 mwaka huu) kusikiliza rufani iliyowasilishwa mbele yake na warufani Mussa H. Mahundi, Abou O. Sillia na Alex Mgongolwa dhidi ya Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Iringa (IRFA) iliyoomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa IRFA uliofanyika Septemba 8 mwaka huu Mufindi, Iringa, na kuomba uchaguzi huo ufanyike upya kwa kuendeshwa na kusimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Deogratias Lyatto, baada ya kupitia maelezo ya warufani na warufaniwa, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imejiridhisha kuwa rufani iliyowasilishwa mbele yake na Mahundi, Sillia na Mgongolwa ilikosa sifa ya kuwa rufani kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, Ibara ya 8(2), Ibara ya 21(3) na 24(2). Kwa kutozingatia matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imetupa rufani hiyo.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya IRFA kuchukua hatua dhidi ya Abuu Changawa kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, Ibara ya 28(6) kwa kuingilia mchakato wa uchaguzi wa IRFA siku ya uchaguzi.

SHUKRANI KWA WADAU SERENGETI BOYS

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawashukuru wadau waliofanikisha kwa njia mbalimbali ziara ya timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) iliyofanyika hivi karibuni katika mikoa ya Mbeya na Njombe. Wadau hao ni Chama cha Mpira wa Miguu Mbeya Mjini (MUFA) chini ya Mwenyekiti wake Suleiman Haroub, Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Njombe (NJOREFA), Stanley Lugenge, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA) na Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Njombe (NDFA).
Wengine ni Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Makambako (MDFA), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA), na klabu za Mbozi United, Kyela United, Tanzania Prisons na Mbeya City. Serengeti Boys inaendelea na kambi yake jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya kwanza ya mchujo ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 dhidi ya Misri itakayochezwa Oktoba 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

KAMSHINA MMOJA AONDOLEWA KWENYE LIGI

Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana jana (Septemba 25 mwaka huu) kupitia ripoti za mechi 21 za Ligi Kuu ya Vodacom ambazo zimeshachezwa mpaka sasa, na kuzifanyia uamuzi wa kikanuni ikiwemo kumuondoa Kamishna mmoja. George Komba aliyekuwa Kamishna kwenye mechi namba 20 kati ya Simba na Ruvu Shooting ameondolewa kwenye orodha ya makamishna wa ligi kutokana na upungufu uliojitokeza katika ripoti yake.
Klabu ambazo zimeandikwa barua za onyo ni African Lyon kwa kwenda uwanjani na jezi tofauti na zile ilizoonesha kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (pre match meeting), Mtibwa Sugar kwa kuchelewa kuwasilisha leseni za wachezaji wake wakati wa mechi na Ruvu Shooting kwa ushangiliaji uliopita kiasi kwenye mechi yao dhidi ya Simba. Kamati pia imethibitisha kadi nyekundu ya Emmanuel Okwi kwa kumpiga kiwiko Kessy Mapande wa JKT Ruvu, hivyo kwa mujibu wa Kanuni ya 25(1)() anakosa mechi tatu na kulipa faini ya sh. 500,000. Mchezaji huyo atakosa mechi namba 20, 27 na 80. Kwa upande wa waamuzi, Ronald Swai ameandikiwa barua ya onyo kutokana na upungufu alioonesha kwenye mechi kati ya Simba na Ruvu Shooting iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Wamiliki wa viwanja vya Mkwakwani, Tanga na Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya wameandikiwa barua ya kuvifanyia marekebisho viwanja vyao katika maeneo mbalimbali yenye upungufu ikiwemo uzio wa kutenganisha wachezaji na washabiki. Mchezaji Faustin Lukoo wa Polisi Moro ambaye kwa mujibu wa ripoti ya mwamuzi aliyemtoa nje kwa kadi nyekundu alimtukana mchezaji mwenzake kwenye mechi dhidi ya African Lyon na Katibu wa Oljoro JKT aliyemwaga maji kwenye chumba cha timu ya Polisi Moro, masuala yao ni ya kinidhamu, hivyo yamepelekwa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi kwa ajili ya hatua zaidi. Kwa klabu ambazo timu zao mpaka sasa zinacheza mechi bila kuwa na logo ya mdhamini, suala hilo limepelekwa kwa wadhamini Vodacom kwa vile wenyewe ndiyo wanaogawa vifaa hivyo.

MUSONYE AMPONDA KOCHA WA HARAMBEE STARS.

KATIBU Mkuu wa Baraza la Michezo kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati-CECAFA, Nicholas Musonye amemjia juu kocha wa timu ya taifa ya Kenya-Harambee Stars Henry Michel kwa kauli yake kuhusiana na michuano ya Kombe la Challenge. Musonye amejia juu Michel kufuatia kauli yake aliyotoa kuwa anaipa umuhimu wa kwanza mechi za kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani-CHAN tofauti na michuano hiyo ya CECAFA. Akihojiwa kuhusiana na kauli aliyotoa Michel, Musonye amesema kuwa hakuna chochote cha maana kocha huyo alichofanya katika kuendeleza soka la Afrika na kama yeye ndiye angetakiwa kumwajiri asingefanya hivyo. Musonye aliendelea kusema kuwa kocha huyo angetimiza wajibu wake katika timu hiyo na sio kujiingiza katika siasa ambazo zimetawala kwenye Shirikisho la Soka nchini Kenya-FKF. Mara ya mwisho Kenya kunyakuwa Kombe la CECAFA ilikuwa mwaka 2002 ambapo Dennis Oliech alifunga bao la ushindi kwa timu hiyo dhidi ya Tanzania-Taifa Stars katika fainali ambayo walishinda mabao 3-2.

SCOLARI APEWA SHAVU BRAZIL.

LUIZ Felipe Scolari ambaye aliiwezesha Brazil kunyakuwa taji lake la tano la Kombe la Dunia mwaka 2002 akiwa kocha wa timu hiyo amesema kuwa anatarajia kuanza tena kazi ukocha mwaka 2013. Kocha huyo anayejulikana kwa misimamo isiyopinda amesema kuwa anatarajiwa kupata kibarua mwakani lakini hajaweka wazi kama itakuwa akinoa timu za taifa au klabu ingawa huko nyuma amesema kuwa anatamani awe kocha wa timu yoyote ya taifa katika Kombe la Dunia mwaka 2014 litakalofanyika Brazil. Scolari ambaye mbali na kuipa Brazil Kombe la Dunia mwaka 2002 pia ameiwezesha klabu ya Palmeiras ya nchi hiyo kunyakuwa ubingwa taifa mara nane klabu ya kubwaga manyanga wiki mbili zilizopita kwasababu ya kushindwa kuitoa timu hiyo katika mstari wa kushuka daraja. Kauli hiyo ya Scolari aliitoa jana wakati Waziri wa Michezo wa Brazil akimtangaza kocha huyo kufanya kazi mshauri ambaye atakuwa akiwahubiria vijana uzoefu wake katika mchezo wa soka na kutangaza Kombe la Dunia.

CHELSEA YAMTENGEA FALCAO KITITA CHA PAUNDI MILIONI 45.

KLABU ya Chelsea imepanga kutenga kitita cha paundi milioni 45 ili kumnasa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Colombia Radamel Falcao. Mazungumzo ya kwanza juu ya uhamisho wa mchezaji huyo kutoka Atletico Madrid katika kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari mwakani tayari yameshaanza na mmiliki wa Chelsea Roman Abramovic tayari amemtengea pesa mchezaji huyo ambaye aliisambaratisha timu hiyo katika michuano ya Super Cup. Chelsea ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wanaamini kuwa itakuwa ngumu kwao kutetea taji hilo kama watakuwa wakimtegemea mshambuliaji mmoja ambaye ni Fernando Torres. Falcao mwenye umri wa miaka 26 tayari amefunga mabao 115 katika kipindi cha miaka mitatu ambacho amecheza soka Ulaya yakiwemo mabao matatu aliyoifunga Chelsea katika fainali ya Super Cup iliyofanyika jijini Monaco.

BOND AFARIKI DUNIA.

MENEJA wa zamani wa klabu za Norwich na Manchester City za Uingereza, John Bond amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79. Katika kipindi cha miaka mitatu ambayo alikuwa akiinoa City, Bond aliiwezesha klabu hiyo kutinga fainali ya Kombe la FA mwaka 1981 lakini alipoteza mchezo wa fainali kwa Tottenham Hotspurs. Mbali na kuifikisha City katika fainali ya FA, Bond pia aliiwezesha Norwich kutinga fainali ya ya Kombe la Ligi mwaka 1975 ambapo walipoteza mchezo huo kwa klabu ya Aston Villa kwa kufungwa bao 1-0. Mbali na kuzinoa klabu hizo Bond aliwahi kucheza katika klabu ya West Ham kwa kipindi cha miaka 16 akiwa amecheza michezo 144 na kuisaidia timu hiyo kushinda Kombe la FA mwaka 1964.

Tuesday, September 25, 2012

TAARIFA KUTOKA TFF LEO.

LIGI KUU VODACOM KUENDELEA KESHO
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Septemba 26 mwaka huu) kwa mechi mbili zitakazochezwa katika miji ya Tanga na Morogoro. Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Polisi Morogoro na Toto Africans ya Mwanza. Polisi Morogoro ambayo imepanda daraja msimu huu imeshacheza mechi tatu na kufanikiwa kupata pointi moja tu baada ya kutoka suluhu na Mtibwa Sugar katika mechi ya kwanza. Nayo Toto Africans ambayo katika mechi iliyopita ugenini ililazimisha suluhu dhidi ya Coastal Union, yenyewe ina pointi tatu baada ya kutoka sare katika mechi zote tatu ilizocheza chini ya kocha John Tegete. Mechi nyingine ya ligi hiyo itakuwa kati ya Coastal Union ambayo itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Kagera Sugar inayofundishwa na Abdallah Kibaden, wikiendi iliyopita iliondoka na pointi zote tatu kwenye uwanja huo baada ya kuifunga Mgambo Shooting bao 1-0. Ligi hiyo itaingia kwenye Super Weekend kuanzia Ijumaa (Septemba 28 mwaka huu) kwa mechi kati ya Azam na JKT Ruvu itakayochezwa Uwanja wa Taifa itaoneshwa moja kwa moja (live) na kituo cha SuperSport kuanzia saa 1 kamili usiku.

YANGA HATARINI KUSHUSHWA DARAJA - TFF.

Tumepokea barua kutoka Kitengo cha Sheria cha Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpirawa Miguu (FIFA) likitutaka tuitaarifu Yanga kuhusu mashtaka yaliyowasilishwa na kocha wazamani wa klabu ya Yanga, Kostadin Papic. Katika malalamiko yake, Papic anadai kuwa hajalipwa malimbikizo ya mshahara wake yanayofikia kiasi cha Dola 12,300 za Kimarekani. Katika barua yake, kocha huyo anadai kuwa alikuwa akiwasiliana na maofisa na viongozi waYanga, lakini hakupata ushirikiano na hivyo kuamua kwenda FIFA. TFF ilifanya juhudi za kuwasiliana na Yanga kuhusu malalamiko hayo ili kujaribu kumzuia kocha huyo asishtaki FIFA, lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda.
Kama chombo kinachosimamia uendeshaji wa mpira wa miguu nchini, TFF imesikitishwa na habari hizo na inaiomba klabu ya Yanga kufanya kila jitihada kuhakikisha kuwa inawasilishataarifa zote muhimu na nyaraka zinazohusiana na stahiki za kocha huyo ili kama ilishamalizana naye, sifa ya klabu ya Yanga isafishwe. Tayari barua imeshaandikwa kwa klabu ya Yanga kuitaka itekeleze utashi huo mapemz iwezekanavyo. Tukio hilo, si tu linachafua sifa ya klabu ya Yanga, bali soka ya Tanzania kwa ujumla kutokana na ukweli kwamba ikishadhihirika kuwa kuna tatizo la malipo ya makocha nchini, ni dhahiri kuwa itakuwa ni vigumu kwa klabu zetu na hata timu za taifa kupata makocha wazuri kutoka nje kwa kuwa watakuwa wamejengeka hofu ya kufanya kazi nchini. Hili ni tukio la pili kwa Yanga baada ya mchezaji wake mwingine, John Njoroge kuishtaki klabu hiyo FIFA na kushinda kesi yake iliyoamuliwa mwezi Januari na Kitengo cha Usuluhishi wa Migogoro cha FIFA (DRC). Ushindi wa Njoroge unamaanisha kuwa iwapo Yanga itashindwa kutekeleza kumlipa mchezaji huyo kasi cha Sh milioni 17, inaweza kujikuta katika adhabu ambayo itatulazimisha tuishushe daraja; kuinyang’anya pointi kwa kiwango kitakachotajwa na FIFA; kuipiga faini au adhabu zote kwenda kwa pamoja. Tunaiomba Yanga itekeleze hukumu hiyo kwa wakati uliotajwa kwenye barua ya FIFA ili kuepuka hatua hizo. Suala la Njoroge ni moja kati ya matukio mengi yanayohusu ukiukwaji wa taratibu za kuvunja mikataba yanayofanywa na klabu zetu. Kuna malalamiko ya wachezaji wengi dhidi ya klabu zao za zamani kuhusu kutolipwa stahiki zao. Hivyo TFF inatoa wito kwa klabu kujiepusha na vitendo hivyo kwa kuwa vinawanyima haki wachezaji, lakini pia vinachafua sifa ya nchi iwapo wachezaji wanachukua hatua za kwenda kwenye vyombo vya juu. Tumekuwa tukisoma kwenye vyombo vya habari kuhusu kutimuliwa kwa sekretarieti nzima ya Yanga kutokana na kuonekana kuwa ina udhaifu. Taarifa hizo hazijaifikia rasmi TFF. Kiutaratibu, Yanga inatakiwa iwsasilishe majina ya maofisa watakaofanya kazi na TFF kwa sasa na itakapoajiri sekretarieti ya kudumu, basi itume barua nyingine ya kuwatambulisha watendaji wake. Kama itakuwa imeitimua sekretarieti nzima, basi TFF inapokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa. Si nia ya TFF kutetea watendaji wazembe, lakini klabu hazina budi kufuatilia kwa karibu utendaji wa sekretarieti zao ili isije ikafikia wakati sekretarieti nzima inaondolewa kwa makosa ambayo yangeweza kusahihishwa kama kungekuwa na ufuatiliaji wa karibu. TFF imekuwa ikitoa mafunzo kwa watendaji wa klabu ili waweze kufanya kazi zao vizuri na kwa mintaarafu ya mpira wa miguu na hivyo kuondolewa kwa timu nzima kama hiyo kunamaanisha kuwa ni upotevu wa rasilimali ambayo imetumika kuwapa elimu ya kutenda kazi zao vizuri. TFF ilishafanya kozi ya Event Management kwa ajili ya watendaji wa klabu; semina ya kuangalia upya maazimio ya Bagamoyo kwa watendaji na viongozi na pia kozi ya utawala hivyo haipendi juhudi hizi zipotee kirahisi.

ILIKUWA NIJIUNGE NA TOTTENHAM - HAZARD.

NYOTA wa klabu ya Chelsea Eden Hazard ameweka wazi kuwa alikuwa ajiunge na klabu ya Tottenham Hotspurs lakini alibadilisha mawazo baada ya klabu hiyo kushindwa kufuzu michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya. Hazard pia alikataa nafasi ya kujiunga na klabu za Manchester United na Manchester City kabla ya kukubali kujiunga na Chelsea akitokea Lille kwa ada ya paundi milioni 32. Akizungumza kwa mara ya kwanza kuhusiana na sakata la uhamisho wake ambao ulizua mjadala katika kipindi hicho Hazard amesema kuwa aliyekuwa meneja wa Tottenham Harry Redknapp alimfuata kumsajili ili akazibe pengo la Luka Modric. Nyota huyo anasema kuwa katika kipindi hicho ambapo Spurs ilikuwa katika nafasi ya tatu alishawishika kujiunga na klabu hiyo lakini ilipokosa nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa alibadilisha mawazo na kuangalia ofa za klabu nyingine.

WALCOTT ATAMANI KUVAA VIATU VYA HENRY.

MSHAMBULIAJI nyota wa pembeni wa klabu ya Arsenal, Theo Walcott amesema kuwa nataka kubakia klabuni hapo na kuwa nguli wa klabu hiyo kama ilivyokuwa kwa mshambuliaji nyota wa klabu hiyo yenye maskani yake Kaskazini mwa jiji la London Thierry Henry. Nyota huyo alikanusha tuhuma kuwa kuchelewa kwake kusaini mkataba mpya kunahusiana na suala la fedha lakini alikubali kuwa suala ya kusaini mkataba mwingine litachukua muda. Meneja wa klabu ya Arsenal alionya wiki iliyopita kuwa wanaweza kulazimika kumuuza mchezaji huyo kitu ambapo kilikaribia kutokea msimu uliopita kama hawatafikia makubaliano pindi dirisha la usajili likifunguliwa tena. Walcott amekuwa akitaka kuhakikishiwa kupata namba muda wote katika kikosi cha Wenger na apangwe kama mshambuliaji wa kati. Wenger alimuondoa Henry ambaye alikuwa anacheza kama winga na kuja kuwa mshambuliaji anayeongoza kwa mabao katika historia ya klabu hiyo na Walcott ambaye ndiye amerithi jezi namba 14 aliyokuwa akivaa nguli naye aje kufikia mafanikio yake.

Rayo Vallecano vs Real Madrid [0-2] All Goals & Highlights HD

Monday, September 24, 2012

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.

PONGEZI KWA UONGOZI MPYA KRFA, MARFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa vyama vya mpira wa miguu mikoa ya Kilimanjaro (KRFA) na Manyara (MARFA) katika uchaguzi uliofanyika juzi (Septemba 22 mwaka huu). Ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza vyama hivyo unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa KRFA na ule wa MARFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo katika mikoa hiyo. TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa kamati za utendaji za MARFA na KRFA zinazoongozwa na Elley Mbise na Goodluck Moshi, kwani viongozi hao wapya wana changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha wanaendesha shughuli za mpira wa miguu kwa kuzingatia katiba zao na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yao. Pia tunatoa pongezi kwa kamati za uchaguzi za IRFA na MARFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF. 
Viongozi waliochaguliwa kuongoza MARFA ni Elley Mbise (Mwenyekiti), Wilson Ihucha (Makamu Mwenyekiti), Apollinary Kayungi (Katibu), Peter Abong’o (Mhazini), Khalid Mwinyi (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Phortinatus Kalewa (Mwakilishi wa Klabu TFF) na Peter Yaghambe (Mjumbe). Kwa upande wa KRFA waliochanguliwa ni Goodluck Moshi (Mwenyekiti), Mohamed Musa (Katibu), Kenneth Mwenda (Mwakilishi wa Klabu TFF), Kusiaga Kiyata (Mhazini) na Denis Msemo (Mjumbe). Nafasi zilizowazi baada ya kukosa wagombea wenye sifa kwenye vyama hivyo zitajazwa baadaye.

WASHABIKI 65,458 WAZISHUHUDIA SIMBA, YANGA WIKIENDI
Mechi za Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara za Simba na Yanga zilizochezwa wikiendi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zimeshuhudiwa na washabiki 65,458. Yanga ambayo iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya JKT Ruvu, Jumamosi (Septemba 22 mwaka huu) mechi yao ilishuhudiwa na washabiki 15,770 wakati ile ya Simba na Ruvu Shooting iliyochezwa jana (Septemba 23 mwaka huu) ilikuwa na washabiki 9,688. Simba ilishinda mabao 2-1. Wakati mechi ya Yanga iliingiza sh. 88,251,000 ile ya Simba dhidi ya Ruvu Shooting Stars mapato yalikuwa sh. 55,454,000. Mechi ya Yanga kila timu ilipata sh. 19,846,194.92 huku ile ya Simba kila timu ilipata sh.11,350,774.58.

MECHI YA AZAM, MTIBWA SUGAR ZAINGIA MIL 2.5/-
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Mtibwa Sugar iliyochezwa juzi (Septemba 22 mwaka huu) Uwanja wa Chamazi imeingiza sh. 2,509,000 ambapo kila timu imepata mgawo wa sh. 301,661. Washabiki 827 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyomalizika kwa Azam kuibuka na ushindi wa bao 1-0. Nayo mechi ya ligi hiyo kati ya African Lyon na Tanzania Prisons iliyochezwa jana (Septemba 23 mwaka huu) kwenye uwanja huo imeingiza sh. 245,000 huku kila timu ikipata sh. 32,286. Prisons ilishinda mechi hiyo kwa mabao 2-1.

KLITSCHKO ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA SANDERS.

BONDIA nyota wa uzito wa juu Vitali Klitschko ametuma salamu zake za rambirambi kwa Corrie Sanders akimuelezea bondia huyo wa zamani wa uzito wa juu raia wa Afrika Kusini kama mpinzani mgumu zaidi kati ya wote aliopambana nao. Klitschko mwenye umri wa miaka 41 ambaye ni bingwa wa dunia wa uzito wa juu wa WBC alimuelezea Sanders kama bondia mwenye kasi na uwezo mkubwa wa kushambulia na kukwepa masumbwi kipindi alichokuwa ulingoni. Sanders mwenye umri wa miaka 46 ambaye alifariki dunia Jumapili baada ya kupigwa risasi na majambazi waliovamia mgahawa aliokuwepo, alimpiga mdogo wake Vitali anayeitwa Wladimir katika pambano lililofanyika jijini Hanover, Ujerumani mwaka 2003. Alimsimamisha bondia huyo raia Ukraine ambaye kwasasa anashikilia mikanda ya ubingwa wa WBA, IBF, WBO na IBO katika raundi ya pili na kunyakuwa taji la WBO kipindi hicho. Sanders alipigana na Vitali katika pambano lililofanyika jijini Los Angeles, Marekani mwaka mmoja baadae kugombea mkanda wa WBC lakini alishindwa kuendeleza ubabe kwa ndugu hao na kudundwa katika raundi ya nane ya mchezo huo.

SENEGAL YAPANGA KUMFUNGULIA DIOUF.

NAFASI ya mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal El-Hadji Diouf kuitumikia timu yake ya taifa inaonekana bado ipo tofauti na ilivyokuwa mwaka uliopita.
Mshambuliaji huyo anayecheza katika klabu ya Leeds United ambaye alifungiwa miaka mitano kujishughulisha na shughuli zozote za kimichezi nchini kwake anaweza kupumua baada ya Shirikisho la Soka la nchi hiyo-FSF kusema kuwa litaangalia upya adhabu hiyo. Akiohijiwa kuhusiana na suala hilo Makamu wa Rais wa FSF Louis Lamonte alithibisha kuwa ni kweli wamekuwa katika vikao vya kujadili juu ya kupunguza adhabu hiyo ya Diouf katika vikao vyake ambavyo imekaa hivi karibuni. Lamonte amesema kuwa Diouf ameifanyia mengi mazuri nchi yake katika soka ambayo vijana wa nchi nzima wangependa kufikia mafanikio hayo nduio maana wameona ni vyema kuweka suala hilo mezani na kuliangalia upya. Lamonte pia amesema Diouf ni mmoja ya wachezaji wachache ambao walihudhuria katika mechi ambazo timu ya taifa ya nchi hiyo ilicheza jijini Coventry katika michuano ya Olimpiki huku akijitegemea mwenyewe kwa usafiri.

VETTEL ANUSANUSA TAJI LA DUNIA LA LANGALANGA.

Dereva nyota wa mashindano ya langalanga Sebastian Vettel ameonyesha kurejesha makali yake na kurejesha matumaini ya kunyakuwa taji la michuano hiyo kwa mwaka huu baada ya kushinda michuano ya Grand Prix ya Singapore. Ushindi huo unamsogeza karibu na kiongozi wa mbio hizo Fernando Alonso ambaye ana alama 29 zaidi ya Vettel huku yakiwa yamebakia mashindano sita pekee kwa msimu huu. Wadau wengi wa mbio hizo wamesema Vettel ambaye yuko katika timu ya Red Bull ana nafasi kubwa ya kunyakuwa taji lake la tatu la Dunia msimu huu baada ya dereva wa MacLaren Lewis Hamilton kushindwa kutamba katika mbio za Singapore baada ya gari lake kuharibika. Vettel ambaye pia atashiriki mbio za Grand Prix za Japan wiki ijayo amesema ameridhika na nafasi aliyopo hivi sasa baada ya kushinda mashindano ya Singapore na ni matarajio yake ataendelea kufanya vizuri huko mbele ingawa amedai bado ana upinzani mkubwa. Msimamo wa madereva hao katika orodha na alama walizonazo ni Alonso alama 194, Vettel alama 169, Kimi Raikkonen alama 149, Hamilton alama 142 na Mark Webber mwenye alama 132.

HORNE ASHTUSHWA NA TAARIFA ZA TERRY.

Katibu Mkuu wa chama cha soka cha Uingereza- FA- Alex Horne ameelezea kustushwa kwake na maamuzi ya JOHN TERRY ya kustaafu kucheza soka la kimataifa. Terry mwenye umri wa miaka 31 hapo jana alitoa taarifa ya kuachana na soka la kimataifa saa 24 kabla ya FA kusikiliza kesi ya tuhuma za kibaguzi inayomkabili dhidi ya mchezaji wa Queens Park Rangers Anton Ferdnand ambapo amedai chama hicho kimefanya nafasi yake katika timu ya taifa kuwa ngumu. Nahodha huyo wa Chelsea ambaye amewahi kunyang’anywa unahodha wa Uingereza na FA mara mbili amesema kitendo cha chama hicho kuendelea na uchunguzi wa mashtaka dhidi yake wakati Mahakama ikiwa tayari imefanya uamuzi na kumkuta hana hatia inamnyima nafasi ya kutimiza wajibu wake katika timu ya Taifa. Lakini Horne akizungumzia kuhusu kesi hiyo inayotarajia kusilikizwa hii leo katika Uwanja wa Wembley amesema hadhani kama FA imemnyima Terry nafasi katika timu ya taifa na kesi hiyo haihusiani na masuala ya kimataifa ya mlinzi huyo. Kama FA itamkuta Terry na hatia ya kumtolea maneno ya kibaguzi mchezaji huyo Octoba 23 mwaka huu huenda akafungiwa kucheza michezo ya ndani kwa muda mrefu.

Sunday, September 23, 2012

ABU TRIKA HAUZWI - AL AHLY.

KLABU kongwe ya soka nchini Misri Al Ahly imetangaza kuwa mshambuliaji wake nyota Mohammed Abu Trika hauzwi na kupinga madai kuwa amepanga kuihama timu hiyo. Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Haji Khashaba amesema kuwa Trika hajapewa mkataba wowote wa kumfanya kuondoka klabuni hapo. Kauli hiyo imekuja kufuatia tetesi katika magazeti nchini humo kuwa klabu ya Al Nasr ilikuwa katika harakati za kutaka kumnasa nyota huyo katika kipindi cha usajili cha dirisha dogo Januari mwakani. Lakini Khashba alikanusha taarifa hizo na kusema kuwa hawajazungumza lolote na Al Nasr kuhusiana na suala la uhamisho la mchezaji huyo na hawana mpango wa kumuuza kwa bado wanamuhitaji. Trika anatarajiwa kucheza katika mchezo wa kirafiki kati ya Ahly na Sunshine Stars pamoja na maamuzi ya bodi ya klabu hiyo kumfungia miezi miwili baada ya kukataa kucheza katika mchezo wa Super Cup ingawa baadae aliomba radhi kutokana na tukio hilo.

HENRY KUUKARABATI UWANJA WA ANFIELD.

MMILIKI wa klabu ya Liverpool kutoka Marekani John Henry anatarajiwa kumaliza utata wa miaka 10 kwa kujitolea kuendeleza Uwanja wa Anfield ufikie uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000 vikiwemo viti vya ziada 7,000.
Hatahivyo kumekuwepo na taarifa kuwa mpaka sasa hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa kati ya suala la kuufanyia ukarabati uwanja huo au kujenga mwingine mpya katika eneo lingine tofauti na hapo Anfield. Kazi hiyo ya kupanua uwanja huo inatarajiwa kutumia kiasi cha paundi milioni 150 ikiwa ni tofauti kubwa na kujenga uwanja mpya ambao utaigharimu timu hiyo paundi milioni 400 ingawa mpaka sasa paundi milioni 50 tayari zimeshatumika katika miradi na michoro ya uwanja mpya. Halmashauri ya jiji la Liverpool imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na klabu hiyo kuhusiana na suala la uwanja kwa miaka kadhaa ambapo wamekuwa wakitoa nafasi kubwa kujengwe uwanja mpya ambao watautumia pamoja na majirani zao klabu ya Everton. Kwasasa uwanja wa Anfield una uwezo wa kupokea mashabiki 45,000 pekee wakizidiwa na klabu kama Manchester United ambayo uwanja wake wa Old Traford una uwezo wa kubeba mashabiki 76,000 wakati Arsenal uwanja wao wa Emirates una uwezo wa kubeba mashabiki 60,000.

HAKUNA WA KUZIBA PENGO LA XAVI BARCELONA - FABREGAS.

KIUNGO nyota wa klabu ya Barcelona, Cesc Fabregas amemmwagia sifa mkongwe wa klabu hiyo Xavi Hernandez kwamba amekuwa nguzo muhimu katika kipindi chote ambacho amecheza hapo. Kauli ya Fabregas imekuja kufuatia Barcelona kuhangaika kuipita ngome ya Granada katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania jana usiku kabla ya kiungo huyo mwenye miaka 32 kufanikiwa kufunga bao katika dakika za lala salama na kuipa ushindi wa mabao 2-0. Fabregas ambaye alirejea katika klabu yake hiyo baada ya kuondoka kwenda Arsenal mwaka 2006 anaamini kuwa pengo la Xavi litakuwa gumu kuzibika wakati wake wa kustaafu utapofika. Barcelona imeendeleza rekodi yake nzuri ya kushinda michezo yake yote mitano ya ligi waliyocheza msimu huu na kuwaacha mbali mahasimu wao ambao ndio mabingwa watetezi wa ligi hiyo Real Madrid baada ya kuanza msimu wao vibaya kwa kupoteza baadhi ya michezo.

NTAJIHAMI DHIDI YA MALDONADO - HAMILTON.

DEREVA wa magari yaendayo kasi maarufu kama langalanga kutoka timu ya McLaren, Lewis Hamilton amesema atajitahidi kuwa mwangalifu zaidi katika mashindano ya Singapore Grand Prix ili kuhakikisha hapati ajali. Hamilton anatarajiwa kuanza mbio hizo akiwa sambasamba na Pastor Maldonado wa timu ya Williams ambaye waligongana miezi 18 iliyopita. Akihojiwa Hamilton amesema kuwa katika mbio hizo atajaribu kuwa mwangalifu na kukaa mbali na mpinzani wake huyo na anatarajia na yeye atafanya hivyo. Hamilton na Maldonado waligongana katika mashindano ya Grand Prix ya Ulaya na kupelekea gari la Hamilton kushindwa kuendelea na mashindano hayo huku naye Maldonado akikosa nafasi ya kumaliza katika nafasi za juu.

BARCELONA YAENDELEZA UBABE HISPANIA.

KLABU ya Barcelona imeendeleza wimbi lake la ushindi katika Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga baada ya kufanikiwa kuifunga Granada kwa mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Camp Nou jana usiku.
Timu hiyo ilibidi ifanye kazi ya ziada baada ya Granada kutaka kugawana alama lakini bao la mchezaji Xavi Hernandez alilofunga dakika tatu kabla ya mpira kumalizika liliihakikishia ushindi wa alama zote tatu timu hiyo. Mara baada ya bao hilo Granada walionekana kushindwa kumudu vishindo vya Barcelona waliokuwa wakishambulia kwa kasi lango la wapinzani wao ambapo kabla ya kipenga cha mwisho beki wa timu hiyo alijifunga mwenyewe akiwa katika harakati za kuokoa shuti la chini kwa chini lililopigwa na mshambuliaji nyota wa timu hiyo Lionel Messi. Ushindi huo umeipaisha Barcelona ambao wanaongoza ligi hiyo wakiwa na alama 15 katika michezo mitano waliyocheza wakiongeza pengo la tofauti ya alama 11 na mahasimu wao Real Madrid ambao watacheza na Rayo Vallecano baadae leo wakisaka ushindi wa kwanza ugenini.

Friday, September 21, 2012

FIFA YAIONYA JAMAICA JUU YA SUALA LA KUVAMIA UWANJA MASHABIKI WAKE.

JAMAICA imeonywa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA juu ya suala la kuvamia uwanja kufuatia ushindi wa kushangaza wa mabao 2-1 wa timu hiyo dhidi ya Marekani katika mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia uliochezwa mwezi huu. Mamia ya mashabiki wenye furaha wa nchi hiyo walikimbia kuvamia uwanja mara baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa na kwenda kuwapongeza wachezaji wa timu hiyo baada ya kupata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Marekani. Katika taarifa yake ambayo imetimwa kwa Shirikisho la Soka la Jamaica-JFF, FIFA imesema kuwa hilo litakuwani onyo la mwisho kwa nchi hiyo kuzuia tukio kama hilo kutotokea tena. Rais wa JFF, Horace Burrell ameahidi kuwa watakuwa makini kuimalisha ulinzi katika michezo itakayokuja ili kuzuia matukio kama hayo kutokea tena. Guatemala, United States na Jamaica wote wana alama saba kutokana na michezo minne waliyocheza katika kundi A amapo Jamaica inakabiliwa na mchezo mwingine dhidi ya Antigua unaotarajiwa kuchezwa Octoba 16 mwaka huu.

DROGBA AFURAHIA MAISHA YA CHINA.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ivory Coast Didier Drogba amesisitiza kuwa ana furaha kuwepo nchini China na amepanga kuitumikia miaka miwli na nusu ya mkataba wake katika klabu ya Shanghai Shenhua. Drogba mwenye umri wa miaka 34 aliondoka katika klabu ya Chelsea majira yakiangazi na kujiunga na Shanghai. Kumekuwa na taarifa kuwa matatizo ya kifedha yanayoikabili klabu hiyo yanaweza kumkimbiza mchezaji huyo kurejea katika klabu za Ligi Kuu nchini Uingereza. Drogba ambaye ameshafunga mabao matano katika michezo saba aliyocheza katika timu hiyo amedai kuwa anafurahia kuwepo nchini humo ingawa akakiri kuwa anaipenda ligi ya Uingereza kwakuwa ndio ligi bora duniani lakini hajutii uamuzi wake wa kuondoka. Drogba alifunga mabao 157 katika kipindi cha miaka nane ambayo ameitumikia Chelsea na alikuw nguzo muhimu kuiwezesha klabu kunyakuwa taji lake la kwanza la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.

MEXICO KUGOMBANIA NAFASI YA KUANDAA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2026.

Justino Compean.
OFISA mkuuu wa Shirikisho la Soka nchini Mexico, Justino Compean amesema kuwa nchi hiyo itaomba nafasi ya kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2026. Mexico imewahi kuandaa michuano hiyo mwaka 1970 na 1986 na kama wakifanikiwa kupata nafasi ya kuandaa michuano hiyo mwaka 2026 itakuwa nchi ya kwanza kuandaa michuano hiyo mikubwa kabisa duniani mara tatu. Compean amesema kuwa Mexico ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa wakati walipokuwa wenyeji wa michuano iliyopita hivyo wanahitaji tena kuandaa Kombe la Dunia lakini wanatarajia upinzani mkubwa kutoka Marekani. Brazil ambao ndio watakuwa wenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 watakuwa wakiandaa michuano hiyo kwa mara ya pili huku Urusi wenyewe watakuwa wenyeji wa michuano hiyo mwaka 2018 na Qatar wataandaa michuano ya mwaka 2022. Nchi nyingine ambazo zimewahi kuandaa michuano hiyo mara mbili ni pamoja na Italia mwaka 1934 na 1990, Ufaransa mwaka 1938 na 1998 pamoja na Ujerumani mwaka 1974 kipindi hicho ikiitwa Ujerumani Magharibi na 2006.

Thursday, September 20, 2012

TAARIFA KUTOKA TFF.

KLABU LIGI KUU, WADHAMINI VODACOM KUTETA
Klabu za Ligi Kuu ya Vodacom zimekubaliana kukutana na mdhamini (kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom) kuzungumzia kipengele cha mkataba wa ligi hiyo kinachozuia kampuni nyingine za mawasiliano kudhamini timu zinazocheza Ligi Kuu. Maazimio hayo yalifikiwa jana (Septemba 18 mwaka huu) katika kikao kati ya klabu hizo na Kamati ya Ligi kilichofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wallace Karia.
Wengine waliohudhuria kikao hicho ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura. Maazimio mengine ya kikao hicho ni TFF kuiandikia barua African Lyon ambayo itaipeleka kwa mdhamini wake (Zantel) ikielezea hatua hiyo ili kusimamisha udhamini huo wakati ikisubiri matokeo ya mazungumzo kati ya klabu hizo na mdhamini wa Ligi Kuu juu ya kipengele cha kuzuia washindani wa Vodacom. Katika mkutano huo, watendaji wawili wa Kamati ya Ligi ambayo iko katika kipindi cha mpito kuelekea kuundwa kwa Bodi ya Ligi walitambulishwa kwa klabu hizo. Watendaji hao ni Silas Mwakibinga ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) na Joel Balisidya ambaye ni Ofisa wa Ligi (LO).

SHAKIRA, PIQUE WATEGEMEA MTOTO.

MWANAMUZIKI nyota kutoka Colombia, Shakira amesema kuwa anategemea kupata mtoto wa kwanza na mpenzi wake ambaye ni mcheza soka wa kimataifa wa Hispania, Gerard Pique. Shakira mwenye umri wa miaka 35 aliandika katika mtandao wake kuwa yeye pamoja na Pique wako katika kilele cha furaha wakisubiria kuzaliwa kwa mtoto wao wa kwanza na hilo ndio jambo pekee ambalo wanalitilia mkazo kwasasa. Mapema wiki hii mwanamuziki huyo pamoja na nyota mwingine wa R&B Usher Raymond walithibitishwa kuziba nafasi za Christina Aguilera na Cee Lo Green katika msimu wa nne wa mashindano ya kuimba yanayoandaliwa na NBC yanaoitwa The Voice. Shakira alianza kujulikana kimataifa katika muziki wa pop baada ya kuipua wimbo wake uliotamba mwaka 2006 unaoitwa Hips Don’t Lie na alikutana na Pique mwenye umri wa miaka 25 katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini.

MAOFISA WA SOKA CAMEROON KUMWANGUKIA ETO'O.

MAOFISA wa soka nchini Cameroon wamegawanyika juu ya ujumbe ambao utasafiri kuelekea nchini Urusi kujaribu kuongea na mshambuliaji nyota na nahodha wa zamani wan chi hiyo Samuel Eto’o kujaribu kubadilisha uamuzi wake wa kuachana na soka la kimataifa. Kufuatia kuteuliwa kwake kuziba nafasi ya aliyekuwa kocha wan chi hiyo Denisi Lavagne, Jean Paul Akono ameweka suala ya kumrejesha mchezaji huyo kama jukumu lake la kwanza kabla timu hiyo haijakabiliwa na mchezo wa pili wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Cape Verde Octoba 13 mwaka huu. Kumekuwa na msuguano wa chini kwa chini kwakuwa baadhi ya maofisa wa wizara ya michezo ya nchi pamoja na wale wa soka wamekuwa wakipinga suala hilo la kwenda kumwangukia mchezaji huyo ili arejee kuitumikia Cameroon. Cameroon iko katika hatari ya kushindwa kufuzu michuano hiyo baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Cape Verde katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Praia lakini kabla ya hapo Eto’o alijitoa katika timu hiyo kwa kile alichodai uongozi mbovu wa soka nchini humo.