Sunday, January 31, 2016

CHELSEA KUIVAA MAN CITY KATIKA ROUND YA TANO YA FA.

KLABU ya Chelsea imepangwa kucheza na Manchester City katika ratiba ya mzunguko wa tano ya michuano ya Kombe la FA iliyotolewa jana.Klabu ya League One ya Shrewsbury Town, timu pekee ya daraja la chini iliyobaki wenye wanatarajiwa kuwa wenyeji wa Manchester United huko New Meadow.Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Arsenal wao wataivaa Hull City ikiwa ni maruadio ya fainali ya mwaka 2014, wakati Crystal Palace wao watakuwa wageni wa Tottenham Hotspurs na Bournemouth wakiwa wenyeji wa Everton mechi mbili ambazo zitakutanisha timu zote za Ligi Kuu.Mechi zingine zitawakutanisha Watford dhidi ya Leeds United, Reading wakisubiri mshindi kati ya West Bromwich Albion na Peterborough wakati Blackburn Rovers nao wakisubiri mshindi katika mechi kati ya Liverpool na West Ham United.Mechi hizo za mzunguko wa tano zinatarajiwa kuchezwa wikiendi ya Februari 19 hadi 22 mwaka huu.

TERRY KUONDOKA CHELSEA MWISHONI MWA MSIMU.

NAHODHA wa Chelsea John Terry amenyimwa ofa ya mkataba mpya na anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.Beki huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 35, ambaye amejiunga na klabu hiyo akiwa na umri wa miaka 14, ameshinda mataji manne ya Ligi Kuu, matano ya Kombe la FA na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Chelsea.Akihojiwa Terry amesema angependa kuendelea kubakia lakini inavyoonekana klabu hiyo ina mipango tofauti.Terry pia amesema bado ataendelea kucheza soka lakini sio kwa klabu yeyote ya Uingereza.

TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.

KLABU ya Chelsea inaripotiwa kumuwania mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann ili aweze kuwa mbadala wa Eden Hazard kama ataondoka majira ya kiangazi.
Chanzo: Daily Mail

KLABU ya Manchester United inatarajia kuwawania nyota wa Tottenham Hotspurs Harry Kane na Dele Alli ambao wamekuwa katika kiwango bora msimu huu.
Chanzo: Express

BEKI wa Paris Saint-Germain Marquinhos anadaiwa kuwindwa na klabu ya Real Madrid ambao wanataka kuimarisha safu yao ya ulinzi kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili na kuanza kutumikia adhabu yao ya kutosajili.
Chanzo: Macca

KLABU ya Newcastle United inaripotiwa kutaka kuimarisha safu yao ya ushambuliaji na wanajipanga kuwafukuzia Seydou Doumbia wa AS Roma na Befetimbi Gomis wa Swansea City.
Chanzo: Le 10 Sport

MSHAMBULIAJI wa Chelsea Lioc Remy anatarajiwa kwenda kwa mkopo Leicester City ambapo inadaiwa kubakia nyaraka chake kabla ya kukamilisha uhamisho huo.
Chanzo: La 10 Sport

KLABU ya Sunderland kwa mara nyingine inataka kumuwania winga Swansea City Andre Ayew majira ya kiangazi baada ya kushindwa kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 kipindi hiki cha Januari.
Chanzo: Daily Mail

Friday, January 29, 2016

HIDDINK ATHIBITISHA UJIO WA PATO NA MIAZGA.

MENEJA wa Chelsea Guus Hiddink amethibitisha kuwa wanajipanga kumsajili beki wa klabu ya New York Red Bulls, Matt Miazga kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili la Januari. Nyota huyo wa kimataifa wa Marekani alikuwa anapenda kuhamia Ulaya na sasa ataelekea Stamford Bridge pamoja na Red Bulls kuwa wagumu kumuuza chipukizi huyo mwenye miaka 20. Akihojiwa Hiddink amesema Miazgo ni mchezaji mzuri anayechipukia na pamoja kwamba hawatamuharakisha lakini ana imani atafanikiwa kupata namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza siku zijazo. Miazga anatarajiwa kujiunga na Chelsea sambamba na Alexandre Pato ambaye Hiddink ameshathibitisha kuwa usajili wake wa mkopo kutoka Corinthians umekamilika.

TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.

KLABU ya Chelsea inaripotiwa kumpa kipaumbele katika mipango yao kocha wa timu ya taifa ya Italia Antonio Conte, wakati wakitafuta mbadala wa muda mrefu wa Jose Mourinho wakati meneja wa muda wa Guus Hiddink atakapomaliza muda wake.
Chanzo: Daily Maily

KLABU ya Newcastle United imeanza mazungumzo ya kutaka kumsajili kwa mkopo beki wa kuhsoto wa Valencia Lucas Orban.
Chanzo: Daily Mail

KLABU ya Leicester City inaripotiwa kukataa ofa ya euro milioni 40 kutoka Chelsea kwa ajili ya kumuachia Jamie Vardy. Ofa hiyo kutoka Chelsea inaripotiwa kumjumuisha Loic Remy.
Chanzo: Fichajes.net

KLABU ya AC Milan imekataa ofa ya Leicester City ya paundi milioni 12.2 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa M’Baye Niang.
Chanzo: Sky Sport Italia

KLABU ya West Ham United inaripotiwa kuwa tayari kutumia fedha nyingi katika usajili wa kiangazi wakati wakijiandaa kuhamia katika uwanja wao mpya mwenye uwezo wa kubeba mashabiki 60,000 ambapo nyota wa Southampton Sadio Mane akitajwa kuwepo katika orodha ya wachezaji watakaowahitaji.
Chanzo: Brentwood Gazette

KLABU ya Liverpool imeamua kumuweka Javier Hernandez katika mipango yake wakati wakijaribu kuimarisha safu yao ya ushambuliaji ambapo inadaiwa kuwa wanaweza kulipa mpaka paundi milioni 20 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Bayer Leverkusen.
Chanzo: The Times

KLABU ya Manchester United imeingia katika vita na Leicester City ya kumsajili mshambuliaji wa CSKA Moscow Ahmed Musa ambaye anaweza kuwagharimu kitita cha paundi milioni 19.
Chanzo: Daily Express

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger anaripotiw akutaka kuimarisha safu yake ya ushambuliaji majira ya kiangazi na moja ya wachezaji anaowahitaji ni mshambuliaji wa Hull City Abel Hernandez.
Chanzo: Tuttomercatoweb.com

KLABU ya Chelsea inadaiwa kupania kuimarisha safu yake ya ulinzi katika kipindi hiki cha usajili na tayari wameanza kumfukuzia beki wa kati wa Atletico Madrid Jose Gimenez baada ya kushindwa kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay majira ya kiangazi mwaka jana.
Chanzo: Evening Standard

VIDIC AAMUA KUTUNDIKA DARUGA ZAKE.

NAHODHA wa zamani Manchester United, Nemanja Vidic ametangaza kustaafu rasmi soka baada ya kuachwa na klabu ya Inter Milan. Beki huyo wa kati raia wa Serbia, ambaye alianza soka lake katika klabu ya Red Stars Belgrade kabla ya kutua Old Trafford ambako alidumu kwa miaka nane na kufanikiwa kunyakuwa mataji matatu ya Ligi Kuu, matatu ya Kombe la Ligi na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa chini ya Sir Alex Ferguson. Vidic alitimkia Inter mwaka 2014 ambako alifanikiwa kucheza mechi 28, hata hivyo toka msimu huu umeanza hajafanikiwa kucheza kutokana na matatizo ya ngiri na maumivu ya mgongo yaliyomsumbua. Katika taarifa yake, Vidic amesema anadhani wakati wake wa kutundika daruga zake umefika kwani majeruhi yanaonekana kukwamisha ndoto zake za kuendelea kucheza. Vidic aliwashukuru wachezaji, viongozi, makocha na wafanyakazi wote ambao wamekuwa pamoja naye katika kipindi chote na klabu zote alizopitia.

DEMBELE AONGEZA MKATABA SPURS.

MCHEZAJI nyota wa Tottenham Hotspurs, Mousa Dembele ameongeza mkataba wa kuitumikia klabu hiyo na kufuata nyayo za Dele Alli. Toka ametua White Hart Lane Agosti mwaka 2012, Dembele amefanikiwa kuichezea klabu hiyo mechi 143 katika mashindano yote, 20 kati ya hizo ikiwa ni msimu huu. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu na Spurs ambao utamuweka hapo mpaka mwaka 2019. Akizungumza na mtandao wa klabu hiyo, Dembele alieleza furaha yake kwa kusaini mkataba mpya na kuahidi kufanya kila awezalo kuisaidia timu hiyo kushinda mtaji.

GARY NEVILLE USO KWA USO NA BARCELONA KOMBE LA MFALME.

KLABU ya Valencia ambayo inanolewa na Muingereza Gary Neville jana ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mfalme baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Las Palmas. Valencia walitinga hatua hiyo kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wao wa mkondo wa kwanza. Valencia sasa watavaana na mabingwa watetezi wa michuano hiyo Barcelona katika mechi za mikondo miwili zitakazochezwa Februari 3 na 10. Nusu fainali nyingine ya michuano hiyo itaikutanisha Sevilla dhidi ya Celta Vigo. Mara ya mwisho Valencia kukutana na Barcelona ilikuwa Desemba mwaka jana ambapo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, ikiwa ni siku tatu toka Neville ateuliwe kuwa kocha wa timu hiyo.

DE BRUYNE NJE WIKI SITA.

KIUNGO mahiri wa Manchester City, Kevin De Bruyne anatarajiwa kukaa nje uwanja kwa kipindi cha wiki sita baada ya kupata majeruhi ya goti juzi. De Bruyne aliumia goti katika mchezo wa Kombe la Ligi ambao City walishinda kwa mabao 3-1 dhidi ya Everton na kutinga fainali ya michuano hiyo. Wakala wa mchezaji huyo, Patrick de Koster amesema amezungumza na mteja wake huyo na kumuahidi kuwa atarejea akiwa na nguvu zaidi. De Bruyne anatarajiwa kukosa mechi muhimu za timu yake ukiwemo ule wa fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Liverpool utakaochezwa Februari 28 pamoja na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Dynamo Kiev.

Thursday, January 28, 2016

TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.

MSHAMBULIAJI nyota wa Bayern Munich, Roberto Lewandowski anadaiwa kuwa tayari kuondoka katika klabu hiyo majira ya kiangazi. Arsenal, Manchester United na Manchester City zote zimekuwa zikifuatilia nyendo za nyota huyo wa kimataifa wa Poland kwa karibu.
Chanzo: The Telegraph

KIUNGO wa West Ham United, Reece Oxford anatarajiwa kujiunga na Charlton Athletic kwa mkopo wa mpaka mwishoni mwa msimu baada ya kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.
Chanzo: Various

KLABU ya Swansea City imetoa ofa ya paundi milioni saba kwa ajili ya mshambuliaji wa Crystal Palace Dwight Gayle ikiwa ni sehemu ya mikakati yao ya kuimarisha safu ya ushambuliaji.
Chanzo: The Guardian

PAMOJA na Alexandre Pato kukaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda Chelsea, AC Milan wanadaiwa bado kuwa na nia ya kumrejesha mchezaji wao huyo wa zamani katika kipindi cha majira ya kiangazi. Milan wanataka kwanza kuona kiwango chake pindi atakapokuwa Stamford Bridge.
Chanzo: La Stampa

KLABU ya Watford inaripotiwa kukaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Fiorentina Mario Suarez.
Chanzo: Marca

DE BRUYNE AWALAZA MACHO CITY.

MENEJA wa Manchester City, Manuel Pellegrini anafikiri Kevin de Bruyne ataweza kucheza tena msimu huu baada ya kiungo huyo kuumia goti lake la kulia katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe Ligi dhidi ya Everton jana. Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24 ambaye alivunja rekodi ya klabu kwa kusajiliwa kwa kitita cha paundi milioni 55, alipata majeruhi hayo katika dakika za majeruhi za mchezo huo walioshinda mabao 3-1. Akihojiwa Pellegrini amesema ana imani kabisa kuwa nyota huyo hawezi kukaa nje ya uwanjani kwa msimu wote uliobakia. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa kwasasa wanasubiria vipimo lakini madaktari wamemuhakikishia halitakuwa tatizo kubwa.

BARCELONA WAPUUZA TETESI ZA NEYMAR KWENDA MADRID.

MAKAMU wa rais wa Barcelona, Jordi Mestre haofii kumpoteza Neymar kwenda Real Madrid, kufuatia tetesi zilizozagaa zinazomhusisha mshambuliaji huyo kuhamia Santiago Bernabeu. Madrid wanadaiwa kuona kama Neymar mwenye umri wa miaka 23 kuwa mbadala wa Cristiano Ronaldo na taarifa zinadai kuwa tayari walishakutana naye katika sherehe za tuzo ya Ballon d’Or zilizofanyika jijini Zurich mapema mwezi huu. Neymar wenyewe tayari alishakanusha tarifa hizo za kukutana na wawakilishi wa Madrid lakini tetesi kuhusu mustakabali wake bado zimeendelea kuvuma kila pembe. Akihojiwa Mestre amesema haoni sababu yeyote ya Neymar kuondoka Barcelona kwani amekuwa akifurahia maisha ya hapo.

BARCELONA YAANZA KUMTOLEA MACHO DYBALA.

KLABU ya Barcelona wanatarajia kumpa kipaumbele mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala, katika usajili wao wa majira ya kiangazi. Mabingwa hao wa Hispania na Ulaya walikuwa wamemlenga Nolito wa Celta Vigo katika kipindi hiki cha usajili lakini sasa wamejitoa baada ya bodi ya klabu hiyo kujiridhisha kuwa usajili wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 hautakuwa na tija. Barcelona sasa wanadaiwa kuwa tayari wameanza mazungumzo ya mwanzo na Juventus wakati wakiendelea kumfuatilia kwa karibu Dybala ambaye amefunga mabao 12 na kusaidia mengine saba katika mechi 20 za Serie A alizocheza msimu huu. Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona, Robert Fernandez anaamini nyota huyo wa kimataifa wa Argentina atakuwa chaguo sahihi kwa klabu hiyo.

YABAINIKA MADRID WALIMFUKUZIA MESSI MARA TATU.

KLABU ya Real Madrid ineripotiwa kutaka kumsajili Lionel Messi zaidi ya mara tatu toka mwaka 2011. Taarifa zinadai kuwa Madrid ndio timu iliyowahi kumfuata nyota huyo wa kimataifa wa Argentina mara tatu tofauti lakini mara zote hizo walikataliwa kwani Messi hakuwa na mpango wa kuondoka Barcelona. Mara ya kwanza Madrid kumfuata Messi ilikuwa mwaka 2011 kufuatia klabu hiyo kuhofia Manchester City wanaweza kumshawishi Cristiano Ronaldo kujiunga nao. Majira ya kiangazi mwaka 2013, Madrid kwa mara nyingine tena walihofu Ronaldo anaweza kuondoka na mmoja wa maofisa wake alikwenda kukutana na wawakilishi wa Messi ili kuona uwezekano wa kumsajili. Mara ya mwisho Madrid kutaka kumuwania Messi ilikuwa mwaka mmoja uliopita lakini kama ilivyokuwa huko nyuma, mara hii pia walikataliwa.

ADEBAYOR AANZA JEURI.

MSHAMBULIAJI mpya wa Crystal Palace, Emmanuel Adebayor amekiri kuwa ataifuatilia klabu hiyo zaidi katika Google baada ya kusajiliwa rasmi jana. Nyota huyo wa kimataifa wa Togo alitambulishwa katika klabu hiyo baada ya kusaini mkataba wa kuitumikia mpaka mwishoni mwa msimu huu. Lakini mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal na Real Madrid ambaye ameondoka Tottenham Hotspurs Septemba mwaka jana, amekiri kuwa hafahamu mengi sana kuhusiana na klabu hiyo. Akihojiwa Adebayor amesema ataingia katika mtandao wa Google ili kufahamu zaidi kuhusu timu hiyo na chochote watakachotaka atawatimizia.

BARCELONA, CELTA VIGO ZATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MFALME.



MABINGWA watetezi wa Kombe la Mfalme, Barcelona wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuichapa Athletic Bilbao jana. Barcelona waliwachapa Bilbao mabao 3-1 ambayo yalifungwa na Luis Suarez, Gerrard Pique na Neymar na kuwafanya kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-2 katika mechi za mikondo miwili walizokutana. Celta de Vigo nao walitinga hatua hiyo baada ya kuwaondosha vijana wa Diego Simeone, Atletico Madrid kwa kuwafunga mabao 3-2 timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana katika mchezo wao wa mkondo wa kwanza. Robo fainali nyingine inatarajiwa kuchezwa baadae leo ambapo Las Palmas watashuka dimbani kukwaana na Valencia huku Mirandes wao wakikabiliana na Sevilla.

Wednesday, January 27, 2016

TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.

KLABU ya Watford inaripotiwa kuwa katika mazungumzo na Liverpool kuhusu uhamisho wa Jerome Sinclair. Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 19 mkataba wake unamalizika majira ya kiangazi na Liverpool wanataka paundi milioni tatu kama watamuuza kipidi hiki cha Januari.
Chanzo: Daily Mail

MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amekutana na wakala wa Granit Xhaka kuzungumzia uwezekano wa kumsajili kiungo huyo wa klabu ya Borussia Monchengladbach.
Chanzo: Sport Bild

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic amekuwa mchezaji anayelipwa zaidi Ufaransa toka mshahara wake uongezeke Januari hii mpaka kufikia kiasi cha euro milioni 1.5 kwa mwezi ukijumlisha na bakshishi.
Chanzo: Le Parisien

KLABU ya Leicester City imeweka dau la paundi ilioni 7.8 kwa ajili ya mshambuliaji wa Chelsea Loic Remy. Newcastle United na Swansea City nazo zinammezea mate nyota huyo.
Chanzo: L’Equipe

KLABU za Wolfsburg, Schalke na Bayer Leverkusen zinapigana vikumbo kumuwania winga wa Fenerbahce Caner Erkin mwenye umri wa miaka 27.
Chanzo: Fanatik

MENEJA wa Atletico Madrid, Diego Simeone anadaiwa kumwambia Fernando Torres kuwa hana mpango wa kumsajili moja kwa moja.

Chanzo: AS

MENEJA wa Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino anatajwa kuwepo katika orodha ya miongoni mwa makocha wanaowindwa na Chelsea kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Guus Hiddink mwishoni mwa msimu huu. Wengine katika orodha hiyo ni pamoja na Diego Simeone, Didier Deschamps na Jorge Sampaoli.
Chanzo: The Times

KLABU ya Chelsea inaripotiwa kumuweka Robin van Persie katika rada zake kama dili la kumnasa Alexandre Pato litashindikana.
Chanzo: Daily Express

RAMIRES AKAMILISHA USAJILI WAKE KWENDA JIANGSU YA CHINA.

KIUNGO wa Chelsea amejiunga rasmi na klabu ya Jiangsu Suning ya China kwa mkataba unaokadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 25. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 28, alisajiliwa Chelsea akitokea Benfica kwa kitita cha paundi milioni 17 mwaka 2010. Jiangsu walimaliza katika nafasi ya tisa katika msimamo wa Ligi Kuu ya China mwaka jana na wanafundishwa na beki wa zamani wa Chelsea Dan Petrescu. Ramires aliisaidia Chelsea kunyakuwa taji la moja la Ligi Kuu, Kombe la FA, Kombe la Ligi, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League.


KIMEELEWEKA, PATO KWENDA CHELSEA.

DEREVA mahiri wa mashindano ya langalanga, Felipe Massa ametuma ujumbe wa kumkaribisha mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Brazil, Alexandre Pato katika klabu ya Chelsea. Massa ambaye ana urafiki wa karibu na Pato alituma picha akiwa pamoja na mpenzi wa mwanasoka huyo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kumtakia kile la heri rafikiye huyo katika maisha yake mapya Uingereza. Ujumbe huo sasa unathibitisha tetesi zilizozagaa kuwa mshambuliaji anakaribia kukamilisha usajili wake wa mkopo kutoka Corinthians kuwa za kweli. Katika ujumbe wake Massa amesema ana uhakika Pato ataisaidia sana Chelsea hivyo akaipongeza klabu hiyo kwa kupata jembe.

SHAKHTAR DONETSK WANATAKA EURO MILIONI 50 KWA TEIXEIRA.

MENEJA wa Shakhtar Donetsk, Mircea Lucescu anaamini Alex Teixeira anayewindwa na Liverpool ana thamani ya paundi milioni 38. Taarifa zilizosambaa zinadai kuwa Liverpool wanapambana kufikia kiwango ambacho kinatakiwa na Donetsk kwa ajili ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26. Ofa ya kwanza ya paundi milioni 24 inadaiwa kukataliwa na sasa wanajipanga kutoa nyingine ya pili. Akihojiwa Lucescu amesema Teixeira ni mchezaji bora ambaye anaimarika kila siku hivyo ana uhakika anaweza kufikia kiwango cha Angel Di Maria katika kipindi kifupi kijacho.

RUMMENIGGE AWAONYA DFB KUHUSU BOATENG.



OFISA mkuu wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge amekionya Chama cha Soka cha Ujerumani-DFB kutoingilia mipango ya kurejea uwanjani ya Jerome Boaten. Boateng alipata majeruhi mabaya ya nyonga Ijumaa iliyopita katika mchezo wa Bundesliga dhidi ya Hamburg na taarifa zilizozagaa ni kuwa atakaa nje ya uwanja kwa miezi zaidi ya minne. Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low ambaye anatarajiwa kutangaza kikosi cha nchi hiyo Mei 31 kwa ajili ya michuano ya Euro 2016, amesema ataacha milango wazi kwa kipindi kirefu kwa ajili ya beki huyo na anamatumaini ataweza kupona kwa wakati. Hata hivyo, Rummenigge akihojiwa na wanahabari aliwaonya DFB kutoingilia suala la Boateng kwani bila hivyo watapambana nao. Rummenigge amesema Boateng ni mwajiriwa wao hivyo masuala yeyote kuhusiana na afya yake klabu ndio inapaswa kuzungumza na sio vinginevyo.

GERVINHO ATIMKIA CHINA.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya AS Roma, Gervinho amehamia katika Ligi Kuu ya China akijiunga na klabu ya Hebei China Fortune FC. Nyota huyo ambaye mara mbili amewahi kuteuliwa kuwa mchezaji bora wa Ivory Coast alitoka Arsenal kwenda Roma mwaka 2013 baada ya kucheza kwa misimu miwili Uingereza. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 amefunga mabao 17 katika mechi 71 za Serie A alizoichezea Roma yakiwemo mabao sita katika mechi 14 msimu huu. Roma tayari ameanza mazungumzo ya kumchukua Stephan El Shaarawy ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Monaco akitokea AC Milan ili aweze kuziba pengo la Gervinho.

PALACE WAMCHUKUA ADEBAYOR.

HATIMAYE klabu ya Crystal Palace imemsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Togo Emmanuel Adebayor kwa uhamisho huru mpaka mwishoni mwa msimu huu. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31, alikuwa yuko huru baada ya kuachwa na Tottenham Hotspurs Septemba mwaka jana, akiwa amefunga mabao 94 katika Ligi Kuu akiwa na Spurs, Arsenal na Manchester City. Wiki mbili zilizopita meneja wa Palace Alan Pardew alithibitisha nia yake ya kumuwania mshambuliaji huyo. Mara ya mwisho kuichezea Spurs ilikuwa ni Mei 3 mwaka jana, ambapo alicheza kwa dakika sita wakati Spurs walipochapwa bao 1-0 na City. Palace kwasasa wanashikilia nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi 23.

Sunday, January 24, 2016

TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.

WAKATI wakiwa katika mipango ya kuhakikisha wanabaki kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu, Leicester City wanaripotiwa kufanya mawasiliano na klabu ya Sampdoria kwa ajili ya kutaka kumsajili mshambuliaji wao Eder.
Chanzo: Sky Sport Italia

KLABU ya Tottenham Hotspurs imemzuia Kevin Wimmer kuondoka katika timu hiyo pamoja na kuwania kwa kiasi kikubwa na klabu ya Schalke ya Ujerumani.
Chanzo: Sky Sports

KLABU ya Real Madrid inajipanga kutenga kitita cha paundi milioni 75 kwa ajili ya kumuwania mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski.
Chanzo: The Sun

KLABU ya Arsenal inaripotiwa kumfuatilia kwa karibu kumnasa kipa Arrizabalaga wa Athletic Bilbao, ambaye wanataka aje kuwa mbadala wa muda mrefu wa Petr Cech.
Chanzo: Don Balon

KLABU za Malaga, Levante na Rayo Vallecano zote zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili kwa mkopo Christian Atsu, huku chipukizi huyo wa Chelsea akikaribia kusitishiwa mkopo wake katika klabu ya Bournemouth baada ya kushindwa kucheza mechi yeyote ya Ligi Kuu.
Chanzo: Sky Sport

NAHODHA wa zamani wa kimataifa wa Ivory Coast, Didier Drogba anatarajiwa kujiunga na klabu yake ya Montreal kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya kufuatia wiki kadhaa za tetesi kuwa anaweza kupewa kibarua katika benchi la ufundi la Guus Hiddink katika klabu ya Chelsea.
Chanzo: TSN

Saturday, January 23, 2016

TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.

KOCHA Carlo Ancelotti anamtaka Karim Benzema kujiunga na Bayern Munich majira ya kiangazi kama Roberto Lewandowski ataondoka Allianz arena.
Chanzo: OK Dario

MSIMU wa kusuasua alionao Cristiano Ronaldo katika klabu ya Real Madrid umepunguza kasi kwa klabu za Manchester United na Paris saint-Germain kumuwania.United wao wameamua kuhamishia nguvu zao kwa Neymar huku PSG wakitarajiwa kumfukuzia Robert Lewandowski.
Chanzo: Fichajes.net

KLABU za Manchester United na Manchester City zinaripotiwa kupigana vikumbo kumuwania nyota wa Barcelona Neymar kufuatia tetesi za mshambuliaji huyo kutaka kuondoka Camp Nou.
Chanzo: Gazzetta World

KIUNGO wa Chelsea Ramirez anatarajiwa kuondoka kabla ya kufungwa dirisha dogo la usajili kipindi hiki cha Januari huku klabu hiyo ikitarajia kuachia fungu litakalotumika kwa usajili majira ya kiangazi.
Chanzo: Daily Mail

KLABU ya Manchester United imefanya mazungumzo zaidi na Benfica kuhusu nia yao ya kumsajili kiungo chipukizi Renato Sanchez mwenye umri wa miaka 18.
Chanzo: Daily Mail

KLABU ya Liverpool inaripotiwa kuanza mazungumzo na Lorient kwa ajili ya kuwania kumsajili beki wa kushoto Raphael Guerreiro majira ya kiangazi.
Chanzo: calcionews24.com

KLABU ya Borussia Dortmund inataka kumsajili wiga wa Chelsea Bertrand Traore kwa mkopo wa mkpa mwishoni mwa msimu.
Chanzo: Bild

MENEJA wa Bayern Munich Pep Guardiola anatarajiwa kutotangaza uhamisho wake kwenda Manchester City kabla ya kumalizika kwa msimu kwa hofu ya mgongano wa kimslahi kama City watapangwa na Bayern katika ratiba ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Chanzo: The Sun

Friday, January 22, 2016

MAN UNITED YAKANUSHA KUKUTANA NA GUARDIOLA.

KLABU ya Manchester United imekanusha kuwa wamekutana na meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola kuhusu uwezekano way eye kuchukua nafasi ya Louis van Gaal. Mtandao wa France Football umedai kuwa mkutano huo ulifanyika wiki iliyopita jijini Paris lakini United wamesisitiza habari hiyo haina ukweli wowote. Guardiola mwenye umri wa miaka 45 anatarajiwa kuondoka Bayern majira ya kiangazi na amesema tayari ameshapata ofa kadhaa kutoka katika klabu za Uingereza. Klabu ya Manchester City ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kumnyakuwa kocha huyo lakini Chelsea na United pia zimekuwa zikihusishwa na tetesi za kumtaka. Bayern walikuwa wameweka kambi yao ya mazoezi huko Doha, Qatar wakati Bundesliga ikiwa katika mapumziko ya majira ya baridi na ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo ambapo timu hiyo itakwaana na Hamburg.

MULLER AIZODOA MAN UNITED.

MSHAMBULIAJI wa Bayern Munich, Thomas Muller ameripotiwa kukataa uhamisho wa majira ya kiangazi kwenda Manchester United. Mara kadhaa United wanadaiwa kumfuata nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwaka jana ka ajili ya kumsajili lakini wamekuwa wakikataliwa. Lakini kukataliwa huko na mkataba mpya aliopewa Muller Allianz Arena havikuwakatisha tama ya kuendelea kumfukuzia nyota huyo. Hata hivyo, Muller mwenye umri wa miaka 26 amewakatalia tena United waliotaka kumsajili kiangazi, akidai anataka kuendelea kubakia Ujerumani.

SWANSEA YAMRUDISHA TABANOU UFARANSA.

KLABU ya Swansea City imemruhusu Franck Tabanou kujiunga tena na klabu yake ya zamani ya Saint-Etienne kwa mkopo wa mpaka mwishoni mwa msimu huu ikiwa ni miezi saba imepita toka wamsajili beki huyo. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa ameshindwa kupata nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Swansea bada ya kucheza mechi tatu pekee. Tabanou aliisaidia Saint-Etienne kufuzu michuno ya Europa League msimu uliopita lakini ameshindwa kabisa kung’aa katika Ligi Kuu. Akihojiwa Tabanou amesema alikwenda Swansea ili kuimarika zaidi lakini jambo la kushangaza wamekuwa wakimnyima nafasi ya kucheza ndio maana ameamua kurejea katika klabu yake ya zamani.

KLABU NNE ZINAMFUKUZIA PATO - WAKALA.

WAKALA wa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Brazil, Alexandre Pato amedai kuwa klabu nne ziko katika mbio za kumuwania mteja wake huyo zikiwemo Chelsea na Liverpool. Taarifa zilizozagaa nchini Brazil zimedai kuwa Chelsea tayari wameshafikia makubaliano ya awali juu ya kumchukua Pato katika kipindi hiki cha Januari, ingwa wakala wake Gilmar Veloz amesisitiza hakuna ofa yeyote iliyopelekwa Corinthians. Akihojiwa Veloz amesema amekuw akisikia tetesi nyingi kuhusu mteja wake lakini ukweli ni kuwa hakuna ofa yeyote iliyoopelekwa katika klabu yake. Veloz aliendelea aliendelea kudai kuwa kuna klabu nne za Ulaya zinazomfukuzia Pato nazo ni Chelsea, Liverpool, Sporting Lisbon na Benfica.

BENZEMA AZIDI KUUNGWA MKONO.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ufaransa Karim Benzema amezidi kuungwa mkono kufuatia kuenguliwa kwake katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kitakachoshiriki michuano ya Euro 2016. Benzema anakabiliwa na kesi ya jinai akituhumiwa kutaka pesa kwa usaliti kutoka kwa mchezaji mwenzake wa Ufaransa Mathieu Valbuena hatua ambayo imepelekea kusimamishwa na Shirikisho la Soka la nchi hiyo toka Desemba mwaka jana. Baada ya Zinedine Zidane kueleza kumuunga mkono Benzema katika sakata hilo, mshambuliaji wa zamani wan chi hiyo David Trezeguet naye amejitokeza na kueleza hisia zake kwa nyota huyo. Trezeguet amesema anadhani Benzema anapaswa kuwepo katika michuano ya Euro 2016, hivyo suala lake linapaswa kushughulikiwa haraka na kupatiwa ufumbuzi.

MASCHERANO AKWEPA JELA.

BEKI wa Barcelona Javier Mascherano ametoa taarifa inayodai kuwa amefikia makubaliano na mamlaka za Hispania kuhusu kesi yake ya kukwepa kodi. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina alisimama mahakamani ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya kukwepa adhabu ya kwenda jela, wakati akisomewa mashitaka mawili ya kukwepa kodi. Hatua hiyo imefikia kufuatia Mascherano kushindwa kuweka wazi mapato aliyopata mwaka 2011 na 2012 ambayo yanakadiriwa kufikia euro milioni 1.5. Taarifa zilizozagaa mapema jana nchini Hispania zilidai kuwa Mascherano alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na kutozwa faini lakini mwenyewe alikanusha tetesi hizo na kudai kuwa wameshafikia makubaliano na wahusika.

KLOPP BADO AMNG'ANG'ANIA STURRIDGE.

MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amepuuza tetesi zinazomhusisha Daniel Sturridge kuondoka Anfield na kudai atamsubiri mshambuliaji huyo mpaka atakapokuwa fiti. Sturridge amecheza mechi tano pekee za Ligi Kuu msimu huu kutokana na kuandamwa na majeruhi. Hatua hiyo ilipelekea nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza kusuhusishwa na tetesi za kuhamia West Ham United wiki hii lakini Klopp amesisitiza kuwa ataendelea kuwa subira kwa mchezaji huyo kadri awezavyo. Klopp amesema ataendelea kumsubiri nyota huyo mpaka atakapopona na wataendelea kumpa msaada wowote atakaohitaji katika kipindi hiki.

Thursday, January 21, 2016

TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Brazil, Neymar na baba yake wameripotiwa kukutana na wawakilishi wa Real Madrid katika sherehe za utoaji tuzo za Ballon d’Or kujadili uhamisho baada ya mazungumzo ya mkataba mpya na Barcelona kusimama.
Chanzo: Onda Cero

WAKATI ikiripotiwa kuwa Chelsea wanakaribia kumsajili nyota wa kimataifa wa Brazil Alexandre Pato, hatua hiyo inaweza kushindikana baada ya Sporting Lisbon nao kutajwa kumuwania mchezaji huyo huku tayari wakiwa wameanza mazungumzo.
Chanzo: A Bola

KLABU ya Fulham itakuwa tayari kumuuza mshambuliaji wake Moussa Dembele kwa paundi milioni sita kwenda Tottenham Hoptspurs kipindi hiki cha Januari lakini watamuhitaji tena kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu.
Chanzo: Evening Standard

KIUNGO wa zamani za Bolton Wanderers, Newcastle United na West Ham United, Kevin Nolan anatarajiwa kutangazwa kama kocha-mchezaji wa klabu ya Leyton Orient ya Ufaransa kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.
Chanzo: Sky Sports

KLABU ya Tottenham Hotspurs nao imeingia katika kinyang’anyiro cha kumuwania Alvaro Morata ili aweze kuja kuwa mbadala wa Harry Kane lakini wanakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Real Madrid, Arsenal na Manchester United ambazo nazo zimeonyesha nia ya kumtaka.
Chanzo: The London Evening Standard

NYOTA wa Chelsea Papy Djolobodji amefanyiwa vipimo vya afya kwa ajili ya uhamisho wake w mkopo kwenda Werder Bremen.
Chanzo: Daily Express


LIVERPOOL YAJITOSA KWA TEIXEIRA.

KLABU ya Liverpool imejitosa rasmi katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Shakhtar Donetsk Alex Teixeira. Taarifa zinadai kuwa meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amepanga kumfanya nyota huyo wa kimataifa wa Brazil kuwa usajili wake kwanza toka akabidhiwe mikoba Anfield. Liverpool inadaiwa kuwa tayari kutoka kitita cha paundi milioni 24.5 kwa ajili ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 26. Hata hivyo, klabu hiyo ya Ukraine inamthaminisha Teixeira ambaye pia anahusishwa na tetesi za kuwindwa na Chelsea, kufikia paundi milioni 39. Klopp anataka kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kufuatia kuumia kwa Danny Ings, Divock Origin a Daniel Sturridge.

OZIL, SANCHEZ FITI KUIVAA CHELSEA.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amedai kuwa nyota wake Alexis sanchez na Mesut ozil wako fiti tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Chelsea Jumapili hii. Vinara hao wa Ligi Kuu wamekuwa bila ya Sanchez ambaye amefunga mabao sita msimu huu, toka Novemba mwaka jana baada ya kupata majeruhi ya msuli wa paja. Kwa upande wa Ozil yeye alikosa mchezo wa ligi uliopita dhidi ya Stoke City uliomalizka kwa sare ya bila kufungana, baada ya kusumbuliwa na majeruhi ya kidole gumba. Akihojiwa Wenger amesema ana habari njema kwani Sanchez na Ozil watakuwepo katika mchezo huo muhimu. Wenger aliendelea kudai kuwa kiungo Francis Coquelin amerejea katika mazoezi kamili toka aumie katika mchezo dhidi ya West Bromwich Albion Novemba mwaka jana wakati Danny Welbeck ambaye hajacheza msimu huu naye akitarajiwa kuanza mazoezi wiki ijayo.

RANIERI AJIVUNIA REKODI PAMOJA NA KUTOLEWA NA FA.


MENEJA wa Leicester City, Claudio Ranieri amedai kuridhishwa na rekodi nzuri waliyonayo dhidi ya Tottenham Hotspurs msimu huu baada ya kuondolewa katika michuano ya Kombe la FA jana usiku. Leicester walishindwa kutamba mbele ya Spurs na kujikuta wakichapwa mabao 2-0 na kuondolewa katika mzunguko wa tatu wa michuano hiyo. Akihojiwa Ranieri amesema ni miaka 10 Spurs wamekuwa wakijenga timu yao ili kufikia nafasi ya kushiriki michuano ya Europa League na Ligi ya Mabingwa. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa hali ni tofauti kwa upande wao kwani ndio kwanza wameanza safari yao na tayari wanashindana nao. Ranieri amesema ni hatua nzuri kwani katika mechi nne walizokutana na Spurs wameshinda moja, kupoteza moja na kutoa sare mbili.

REAL MADRID NDIO KLABU TAJIRI ZAIDI DUNIANI, MAN UNITED YAPOROMOKA.

KLABU ya Real Madrid imetajwa kuwa klabu tajiri zaidi duniani kwa msimu wa 11 mfululizo, wakati Manchester United imeporomoka kutoka nafasi ya pili walipokuwepo mpaka nafasi ya tatu na Barcelona kuchukua nafasi ya pili. Klabu ya Paris Saint-Germain-PSG wao wamekwea kwa nafasi moja mpaka nafasi ya nne wakichukua nafasi ya Bayern Munich walioshuka mpaka nafasi ya tano. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na The Deloitte Money League 2016, imedai kuwa klabu zote tano kwa pamoja zimetengeneza kiasi cha paundi bilioni tano katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Madrid wao wanaongoza kwa kutengeneza kiasi cha paundi milioni 439 wakifiatiwa na mahasimu wao Barcelona waliotengeneza paundi milioni 426 huku Manchester United wakiwepo nafasi ya tatu kwa kutengeneza kiasi cha paundi milioni 392.

VIDIC ATAMANI KUREJEA UINGEREZA.

BEKI wa zamani wa Manchester United, Nemanja Vidic anaripotiwa kutamani kurejea Ligi Kuu na tayari ameshapewa ofa ya kujiunga na Aston Villa. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 35 aliondoka Inter Milan mapema wiki hii baada ya mkataba kusitishwa kwa maelewano. Villa ambao wamepania kuimarisha safu yao ya ulinzi kipindi hiki cha usajili wa Januari, wana hofu ya kuwakosa nyota wa Bordeaux Lamine Sane na Joleon Lescott ambaye anafikiria kwenda China na Marekani. Vidic pia amehusishwa na tetesi za kutakiwa katika klabu za Marekani lakini mwenyewe anapendelea zaidi kurudi Uingereza na Villa wanaangalia uwezo wake kwanza kabla ya kumchukua.

WEST BROM YATAKA PAUNDI MILIONI 30 KWA BERAHINO.

KLABU ya West Bromwich Albion inadaiwa kutaka kiasi cha paundi milioni 30 kwa klabu itakayotaka kumnunua Saido Berahino. Taarifa zinadai kuwa West Brom tayari wamekataa ofa kutoka Chelsea, Tottenham Hotspurs na Newcastle United kwa ajili ya mshambuliaji huyo. Chelsea wanadaiwa kukataliwa kufuatia kutoa ofa ya paundi milioni 18 kwa ajili ya nyota huyo ambaye amekuwa katika kiwango bora msimu huu. Nyota huyo anadaiwa kupendelea zaidi kuhamia jijini London lakini Chelsea au Spurs zitalazimika kulipa paundi milioni 30 kama watahitaji huduma yake.

Wednesday, January 20, 2016

TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.

MENEJA wa Manchester United, Louis van Gaal yuko tayari kuondoka katika timu hiyo majira ya kiangazi ikiwa ni mwa mmoja kabla ya kumalizika kwa mkataba wake wa miaka mitatu, sababu kubwa ikiwa ni shinikizo na shutuma anazopambana nazo.
Chanzo: Daily Mirror

KLABU ya West Ham United, inajipanga kumuwania mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge. West Ham imefikia hatua hiyo kufuatia meneja wa Liverpool Jurgen Klopp kutishwa na majeruhi ya Sturridge hivyo kuwa tayari kupokea kitita cha paundi milioni 18.
Chanzo: Brentwood Gazette

MENEJA wa Watford Quique Sanchez Flores ameamua kuacha kumuwania Emmanuel Adebayor na kuifanya Crystal Palace kuwa na nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji huyo ambaye yuko huru kwasasa baada ya kuachwa na Tottenham Hotspurs.
Chanzo: Evening Standard

MENEJA wa Liverpool Jurgen Klopp ameripotiwa kusisitiza kusajiliwa kwa marc-Andre Ter Stegen ili kuleta ushindani kwa Simon Mignolet ambapo klabu hiyo inedaiwa kutoa ofa ya paundi milioni 10.8 lakini Barcelona wao wanataka paundi milioni 23 kwa kipa huyo.
Chanzo: Don Balon

KLABU ya Tottenham Hotspurs inajiandaa kumuwania kiungo wa Coventry James Maddison na kama wakifanikiwa watamuacha kwa mkopo katika klabu hiyo ya daraja la kwanza mpaka mwishoni mwa msimu huu.
Chanzo: The Independent

KLABU ya Liverpool ilikaribia kumsajili Dele Alli kutoka timu ya MK Dons kiangazi mwaka jana lakini walichemka kwa kumpa ofa ya mshahara wa paundi 4,000 kwa wiki nyota huyo ambaye kwasasa anang’aa katika klabu ya Tottenham Hotspurs.
Chanzo: Daily Mail

WAKALA wa Ezequiel Lavezzi, Alessandro Moggi ametua jijini London leo kufanya mazungumzo na Chelsea, lakini haijajulikana kama wanazungumza kuhusu uhamisho wa mshambuliaji kwenda PSG kipindi hiki cha Januari au kiangazi.
Chanzo: Sky Sport Italia

KLABU ya Chelsea inadaiwa kutaka kusajili wachezaji watatu ambao ni Alexandre Pato, Aymen Abdennour na Alex Teixeira kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili majira ya kiangazi huku wakiwaruhusu Papy Djilobodji na Charly Musonda kuondoka kwa mkopo.
Chanzo: Daily Mail

KLABU ya Liverpool inaripotiwa kuwepo katika mazungumzo na Juventus kwa ajili ya kumsajili Alvaro Morata kwa kitita cha euro milioni 58.1, wakati Arsenal na Manchester United nazo pia zikimmezea mate nyota huyo.
Chanzo: Gazzetta dello Sport

POLISI MATATANI KWA KUWEKA PASSPORT YA MESSI KATIKA MITANDAO YA KIJAMII HUKO DUBAI.

POLISI mmoja wa Dubai anakabiliwa na kifungo cha miezi sita jela na faini ya euro 124,000 kwa kutuma picha za video za pasi ya kusafiria ya mshambuliaji nyota wa Barcelona Lionel Messi, katika mitandao ya kijamii. Polisi huyo wa Uwanja wa Ndege aliyejulikana kwa jina la J.J anatuhumiwa na waendesha mashitaka kwa kuingilia mfumo wa mawasiliano na alikiri kosa la kuvunja Sheria ya Mtandao lakini aliomba kusamehewa. Messi alitua Dubai mwishoni mwa Desemba kuhudhuria sherehe za tuzo ya Globe Soccer ambao alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka na polisi huyo aliomba kama anaweza kupiga picha na nyota huyo lakini ilishindikana kwasababu alikuwa amechoka. Polisi huyo mwenye umri wa miaka 26, baadae aliingia katika chumba cha mawasiliano na kuirekodi video wakati Messi akionyesha pasi yake ya kusafiria kwa wana usalama kabla ya kuituma katika mtandao wa Snapchat.

MAN UNITED YAAMBIWA KUTOA PAUNDI MILIONI 65 KAMA WANAMTAKA LUKAKU.

KLABU ya Manchester United italazimika kulipa kitita cha paundi milioni 65 kama watahitaji kumsajili mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku ambaye yuko katika kiwango bora msimu huu. Lukaku ambaye alisajiliwa Everton akitokea Liverpool kwa kitita cha paundi milioni 28, amefunga mabao 19 katika mshindano yote msimu huu hivyo kuzivutia klabu kubwa zikiwemo Real Madrid, Paris Saint-Germain, Chelsea na Manchester City. Lakini United ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kumsajili kutokana na nia yao ya kuimarisha safu yao ya ushambuliaji ambayo imeonekana kuwa butu msimu huu. United imekuwa ikimfuatilia Lukaku kwa karibu msimu huu lakini Everton wamepania kuendelea kubakia na nyota huyo.

ASHLEY COLE KUTIMKIA MAREKANI.

BEKI wa zamani wa kimataifa wa Uingereza, Ashley Cole amekubali kuhamia klabu ya Los Angeles Galaxy inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani-MLS baada ya kuondoka AS Roma. Cole mwenye umri wa miaka 35, yuko huru kujiunga na mchezaji mwenzake wa zamani wa Uingereza Steven Gerrard baada ya mkataba wake na Roma kuvunjwa kwa maelewano. Beki huyo wa zamani wa klabu za Arsenal na Chelsea alijiunga na klabu hiyo ya Serie A Julai mwaka 2014 na kufanikiwa kucheza mechi 16. Akiwa ameichezea Uingereza mechi 101, Cole amefanikiwa kunyakuwa mataji matatu ya Ligi Kuu, saba ya Kombe la FA, moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya na moja la Europa League.

IRAQ YATANGAZA KUMUUNGA MKONO PRINCE ALI KATIKA UCHAGUZI WA FIFA.

CHAMA cha Soka cha Iraq-IFA kimetangaza kumuunga mkono Prince Ali Bin Al Hussein wa Jordan katika kinyang’anyiro cha urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA mwezi ujao. Prince Ali anatarajiwa kupambana na rais wa Shirikisho la Soka la Asia-AFC, Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa, kaimu katibu mkuu wa zamani wa FIFA, Jerome Champagne, mwanasiasa na mfanyabiashara wa Afrika Kusini Tokyo Sexwale na katibu mkuu wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Gianni Infantino, katika uchaguzi huo wa Februari 26. Rais wa IFA Abdul Khaliq Masood amesema katika taarifa yake iliyotumwa FIFA kuwa wameamua kura ya nchi hiyo itakwenda kwa Prince Ali kwasababu ya mchango wake mkubwa katika maendeleo y soka ya eneo hilo. Hii ni mara ya pili kwa Prince Ali kugombea nafasi hiyo bada ya kushindwa na rais anayeondoka Sepp Blatter katika uchuguzi uliofanyika Mei mwaka jana.

DE GEA HANA MPANGO TENA WA KWENDA MADRID.

GOLIKIPA wa Manchester United David De Gea anaripotiwa kutaka kuendelea kubakia Old Trafford hata kama Real Madrid watarejea kumuwinda tena mwezi huu. Madrid wanatarajiwa kukata rufani adhabu ya kufungiwa kusajili waliyopewa wiki iliyopita lakini kama ikishindikana hawataweza kusajili mchezaji yeyote mpaka kiangazi mwaka 2017. Hata hivyo, bado wana uwezo wa kusajili katika kipindi hiki cha usajili wa Januari na kuna uwezekano wakaanza tena kumfukuzia De Gea. Usajili wa kipa huyo ulishindikana kidogo majira ya kiangazi mwaka jana kutokana na karatasi muhimu kutowasili kwa wakati. De Gea ambaye amesaini mkataba mpya wa miaka minne na United anadaiwa kuwa kwasasa hatoweza kukubali tena kuondoka Old Trafford.

PLATINI KUENDELEA KULAMBA MSHAHARA WA UEFA PAMOJA NA KUFUNGIWA.

SHIRIKISHO la Soka la Ulaya-UEFA limedai kuwa bado wanaendelea kumlipa mshahara rais wake aliyefungiwa Michel Platini mpaka itakapoamuliwa vinginevyo. Taarifa hiyo ya UEFA imekuja baada ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA nalo kudai rais aliyefungiwa Sepp Blatter ataendelea kulipwa stahiki zake mpaka atakapochaguliwa rais mpya katika uchaguzi wa Februari 26. Platini na Blatter wote walisimamishwa kwa siku 90 na kamati ya maadili ya FIFA Octoba 8 mwaka jana na baadae kufungiwa kujishughulisha na masuala ya michezo kwa miaka nane mwezi uliopita. Adhabu ya wawili hao imekuja kufuatia malipo ya dola milioni mbili aliyopewa Platini kutoka kwa Blatter mwaka 2011 kufuatia kazi za soka zilizofanyika miaka nane iliyopita. Msemaji wa UEFA alithjibitisha Platini kuendelea kulipwa stahiki zake na ataendelea kulipwa mpaka utakavyoamuliwa vinginevyo.

SINA MPANGO WA KUONDOKA MAN CITY - BONY.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ivory Coast, Wilfried Bony amedai kuwa hakuna ukweli wowote juu ya tetesi za yeye kutaka kuondoka Manchester City. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27, alihoji sababu za uamuzi wa meneja wake Manuel Pellegrini kumuacha katika kikosi chake Desemba mwaka jana na toka wakati huyo amekuwa akihusishwa na tetesi za kutaka kurejea Swansea City. Hata hivyo akihopjiwa Bony amekanusha taarifa hizo na kudai kuwa anafurahia kuwepo City kwani ni moja ya klabu kubwa nchini Uingereza. Bony alijiunga na City kwa kitita cha paundi milioni 28 na kupewa mkataba wa miaka minne na nusu Januari mwaka jana. Nyota huyo amefunga mabao nane katika mechi 23 alizocheza msimu huu lakini amekuwa akitumika kama mchezaji wa akiba toka mshambuliaji kiongozi Sergio Aguero aliporejea kutoka katika majeruhi Desemba.

INFANTINO AANZA KAMPENI ZA URAIS FIFA.

KATIBU mkuu wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Gianni Infantino amesema Shirikisho la Soka Duniani-FIFA linapaswa kuandaa michuano ya Kombe la Dunia katika bara badala nchi moja au mbili. Kauli hiyo ya Infatino imekuja wakati akianza kampeni zake katika kinyang’anyiro cha urais wa FIFA ambao uchaguzi wake unatarajiwa kufanyika mwezi ujao. Infatino ameahidi michuano mikubwa ya Kombe la Dunia, mageuzi kufuatia kashfa iliyolikumba shirikisho hilo na fedha zaidi kwa nchi wanachama, kama akichaguliwa kuiongoza FIFA katika uchaguzi wa Februari 26 mwaka huu. Infatino ambaye amekuwa akifanya kazi chini rais wa UEFA aliyesimamishwa Michel Platini kwa miaka saba iliyopita amesema Kombe la Dunia kuongezwa na kufikia nchi 40 badala ya 32 za hivi sasa. Mgombea huyo amesema FIFA inapaswa kuangalia uwezekano wa kutanua michuano ya Kombe la Dunia badala ya kufanyika katika nchi moja au mbili iweze kufanyika katika bara zima husika ili kutoa nafasi kwa nchi nyingi zaidi kupata heshima na kunufaika kwa kuwa wenyeji.

Monday, January 18, 2016

TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.

KLABU ya Manchester United imeripotiwa kuwa wanaweza kumsajili mtoto wa nguli wa zamani wa klabu hiyo Peter Schmeichel aitwaye Kasper kama David De Gea atatimkia Real Madrid majira ya kiangazi.
Chanzo: The Sun

KUFUATIA kuanza msimu kwa kusuasua, Chelsea inaweza kuwakosa nyota wake kadhaa majira ya kiangazi wakiwemo Eden Hazard, Diego Costa, Oscar na Thibaut Courtois.
Chanzo: The Sun

KUFUATIA tetesi za Neymar kufikiria kuondoka Camp Nou baada ya kutumbukizwa katika sakata la usajili wake wakati akitokea Santos, klabu ya Barcelona inajaribu kutafuta mbadala wake kama akiondoka na kuna uwezekano wa kuanza kumuwania Eden Hazard wa Chelsea.
Chanzo: Buzz Sport

KLABU ya Swansea City ina matumaini ya kukamilisha usajili wa Scott Sinclair na mshambuliaji wa AS Roma Seydou Doumbia katika kipindi hiki cha Januari.
Chanzo: The Daily Mail

KLABU ya Newcastle United imeruhusiwa na mmiliki wake Mike Ashley kutumia kiasi cha paundi milioni 100 kipindi hiki cha usajili wa Januari ambapo wamepanga kumuwania Saido Berahino kabla ya kumfukuzia Andros Townsend kutoka Tottenham Hotspurs.
Chanzo: The Daily Mail

KLABU ya Arsenal inajipanga kumuwania mshambuliaji wa Juventus Alvaro Morata katika kipindi ambacho Real Madrid watakuwa wakitumikia adhabu yao ya kufungiwa kusajili, kufuatia tetesi za klabu hiyo kutaka kumrejesha nyota huyo Santiago Bernabeu.
Chanzo: The Sun

RONALDO AKIRI KUWA NA MAHUSIANO MAZURI NA MESSI.

MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesisitiza kuwa sasa wana mahusiano mazuri na Lionel Messi na kutania kuwa bado anasubiri malipo yake kwa kutoa huduma ya ukalimani wakati tuzo za Ballon d’ Or. Wawili hao wamekuwa mahasimu wakubwa katika tuzo hizo kwani katika kipindi cha miaka nane iliyopita ni wao ndio wamezitawala. Lakini akihojiwa mara baada ya Madrid kushinda mabao 5-1 dhidi ya Sporting Gijon, nyota huyo wa kimataifa wa Ureno amesisitiza kuwa kwasasa wana mahusiano mazuri na nyota huyo wa Barcelona. Ronaldo amesema wamekuwa karibu zaidi na wamekuwa wakifurahia uhusiano wao mzuri kulinganisha na miaka ya nyuma. Messi na Ronaldo walipanda jukwaani pamoja ambamba na Neymar katika sherehe za tuzo ya Ballon d’Or jijini Zurich na nyota huyo wa zamani wa Manchester United mebainisha kuwa ilibidi awaokoe nyota hao wa Barcelona. Ronaldo amesema wakati wakiwa juu ya jukwaa sio Neymar wala Messi ambaye anaweza kuzungumza kiingereza hivyo alibidi awe mkalimani wao na kutani kuwa alizungumza nao baadae na kuwaomba wamlipe.

UNITED YAMUWANIA SANCHEZ.

KLABU ya Manchester United, imeripotiwa kumuwania chipukizi wa Benfica, Renato Sanchez. Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 18, amekuwa akionyesha kiwango cha juu toka alipoibuka katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo na sasa amekuwa akifuatiliwa na vilabu kadhaa barani Ulaya vikiwemo Newcastle United, Swansea City na Aston Villa. Taarifa zaidi zinadai kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Ureno ambaye ana mkataba unaomalizika mwaka 2020 ana thamani ya paundi milioni 58.8 kwa klabu itakayomuhitaji. Pamoja na hayo United inatajwa kumuwania ingawa haikuwekwa wazi kama watamuhitaji kipindi cha Januari au Kiangazi.