Friday, January 22, 2016

BENZEMA AZIDI KUUNGWA MKONO.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ufaransa Karim Benzema amezidi kuungwa mkono kufuatia kuenguliwa kwake katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kitakachoshiriki michuano ya Euro 2016. Benzema anakabiliwa na kesi ya jinai akituhumiwa kutaka pesa kwa usaliti kutoka kwa mchezaji mwenzake wa Ufaransa Mathieu Valbuena hatua ambayo imepelekea kusimamishwa na Shirikisho la Soka la nchi hiyo toka Desemba mwaka jana. Baada ya Zinedine Zidane kueleza kumuunga mkono Benzema katika sakata hilo, mshambuliaji wa zamani wan chi hiyo David Trezeguet naye amejitokeza na kueleza hisia zake kwa nyota huyo. Trezeguet amesema anadhani Benzema anapaswa kuwepo katika michuano ya Euro 2016, hivyo suala lake linapaswa kushughulikiwa haraka na kupatiwa ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment