Thursday, May 31, 2012

STARS YAONDOKA BILA BOBAN NA CHOLLO.

Wachezaji wa Kilimanjaro Taifa Stars wameondoka Dsm alfajiri ya leo tayari kwa mchezo wao dhidi ya Ivory Coast utakoachezwa jumamosi huko ABIJAN
Kocha mkuu wa timu hiyo KIM PAULSEN amewataja wachezaji hao wawili zaidi kuwa ni HARUNA MOSH BOBAN na Saidi nassoro chollo ambao ni majeruhi wapya. Wachezaji ambao walikuwa ni majeruhi wakiwa kambini ni NURDIN BAKAR na THOMAS ULIMWENGU. Wakiwa katika uwanja wa Jomo Kenyatta , wachezaji wa TAIFA STARS ilibidi wakae kwa muda wa saa tano kusubiri ndege inayokwenda Ivory coast baada ya ile ya mwanzo muda wake kubadilihwa. Kutokana na kuchelewa huko huenda kikosi cha TAIFA STARS kilichtarajia kuingia IVORY COAST saa nane mchana kwa saa za Afrika mashariki sasa itaingia kati ya Saa mbili au tatu kwa saa za afrika mashariki.

ABIDAL ANAWEZA KUREJEA UWANJANI - DAKTARI.

DAKTARI aliyemfanyia upasuaji beki wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Barcelona, Eric Abidal amesema kuwa mchezaji huyo anaweza kurejea tena uwanjani baada ya kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza ini. Abidal mwenye umri wa miaka 32 alifanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe uliokuwa umeota katika ini lake mwaka uliopita lakini baada ya kurejea tena uwanjani tena alilazimika kufanyiwa upasuaji mwingine wa kupandikiza sehemu ya ini lingine ambalo mpwa wake alijitolea April 10 mwaka huu. Daktari huyo aitwae Juan Carlos Garcia-Valdecasas amesema kuwa ni juu ya mchezaji mwenyewe kuamua kuendelea kucheza au kupumzika kabisa yeye hawezi kumzuia, kwani akiendelea vizuri kama hivi sasa haoni sababu ya mchezaji huyo kushindwa kucheza. Valdecasas aliendelea kusema kuwa ini ni kiungo ambacho huwa kinakuwa katika kipindi cha miezi mitatu hivyo Abidal atakuwa akipona taratibu katika kipindi cha miezi sita au mwaka mmoja na baada ya hapo anaweza kuendelea na maisha yake ya kawaida. Wachezaji wa Barcelona walivaa jezi anayotumia mchezaji huyo wakati wakisheherekea ushindi wa Kombe la Mfalme waliloshinda baada ya kuifunga Athletico Bilbao Ijumaa iliyopita.

BALOTELLI NDANI YA SUTI.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Italia Mario Balotelli ameonyesha kwamba anaweza kuvaa mavazi ya heshima akiamua kutokana na kuzoeleka na mavazi ya vijana katika maeneo mengi ambayo amekuwa akitembea anapokuwa nje ya uwanja. Tukio hilo lilitokea wakati mchezaji huyo pamoja na kikosi kizima cha timu ya taifa ya nchi hiyo walipopiga picha ya pamoja kwa ajili ya michuano ya Ulaya 2012 wakiwa wamevalia suti nyeusi kitendo ambacho hakijazoeleka kwa mchezaji huyo mwenye vituko vingi ndani na nje ya uwanja. 
Kocha wa kikosi hicho Cesare prandelli alimuacha mshambuliaji huyo ambaye anacheza klabu ya Manchester City katika kikosi hicho kutokana na matukio yake ya kushindwa kudhibiti hasira zake lakini Balotelli aliomba radhi na kocha huyo kumjumuisha katika kikosi chake tena. Mapema wiki hii Balotelli alinukuliwa na vyombo vya habari akionya suala la ubaguzi wa rangi katika michuano ya Ulaya ambayo itafanyika nchini Poland na Ukraine kwamba shabiki yeyote atakayemfanyia hivyo basi hatasita kumuua na yeye kwenda jela. Italia imepangwa katika kundi C kwenye michuano hiyo pamoja na timu za Hispania, Croatia na Jamhuri ya Ireland.

LIVERPOOL YAPATA MBADALA WA DALGLISH.

Brendan Rodgers akiwa na mwanae.
KLABU ya Liverpool ya Uingereza imefanikiwa kupata meneja mpya Brendan Rodgers ambaye amekubali kusaini mkataba wa miaka mitatu kwa ajili ya kukinoa kikosi cha timu hiyo. Rodgers alitangazwa ramsi kuwa mbadala wa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Kenny Dalglish ikiwa umepita muda wa saa 24 baada ya kocha huyo kumpa taarifa mwenyekiti wa klabu ya Swansea, Huw Jenkins kuhusu nia yake ya kuondoka katika klabu hiyo. Kazi ya kwanza atakayokutana nayo Rodgers katika klabu hiyo ni kujaribu kumsajili kiungo wa kimataifa wa Iceland, Gylfi Sigurdsson kutoka klabu ya Hoffenheim ya Ujerumani kwa ada ya euro milioni 6.8 baada ya kushindwa kufikia makubaliano na klabu ya Swansea. Rodgers aliongea na maofisa wa Liverpool jana akiwemo mwenyekiti wa klabu hiyo Tom Warner baada ya Swansea kuikubalia klabu hiyo kufanya mazungumzo na kocha huyo ambaye ni raia wa Ireland ya Kaskazini. Katika taarifa yake Jenkins amethibitisha kufanya mazungumzo na Rodgers kuhusu nia yake hiyo na kwasasa wako katika mazungumzo na klabu ya Liverpool kuhusiana na suala hilo ambalo anategemea litaweza kumalizika katika kipindi cha saa 24 zijazo.

Wednesday, May 30, 2012

TAARIFA KUTOKA TFF LEO.

TAIFA STARS KWENDA ABDIJAN KESHO ALFAJIRI
Kikosi cha wachezaji 23 na viongozi tisa kinatarajia kuondoka kesho (Mei 31 mwaka huu) saa 11.10 alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kwenda Abidjan, Ivory Coast kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia itakayochezwa Juni 2 mwaka huu. Wachezaji wanaoondoka ni nahodha Juma Kaseja, nahodha msaidizi Aggrey Morris, Mwadini Ally, Deogratius Munishi, Nassor Masoud Cholo, Amir Maftah, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Waziri Salum, Shomari Kapombe na Juma Nyoso. Wengine ni Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar, Shabani Nditi, Edward Christopher, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Mbwana Samata, Ramadhan Singano, Simon Msuva, Haruna Moshi na John Bocco. Wachezaji waliobaki kutokana na kuwa majeruhi ni mshambuliaji Thomas Ulimwengu anayecheza timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kiungo wa Yanga, Nurdin Bakari. Viongozi wanaofuatana na timu hiyo ni Kocha Mkuu Kim Poulsen, Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Mukebezi (Meneja wa timu), Juma Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Physiotherapist) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa). Msafara huo unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Crescentius Magori wakati naibu kiongozi wa msafara ni Makamu wa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) Haji Ameir Haji. Timu hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeagwa leo (Mei 30 mwaka huu) na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala ambaye aliwataka wachezaji hao kwenda kuiwakilisha vizuri Tanzania kwenye mechi hiyo. Hafla hiyo ya kukabidhi Bendera ya Taifa pia ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi, Rais wa TFF, Leodegar Tenga na Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe. Mechi itachezwa kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abijan kuanzia saa 11 kamili kwa saa za Ivory Coast. Mwamuzi atakuwa Slim Jedidi wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Bechir Hassani, wote kutoka Tunisia. Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Sherif Hassan kutoka Misri. Mwamuzi wa akiba ni Youssef Essrayri pia kutoka Tunisia. Mtathmini wa waamuzi ni Rachid Medjiba kutoka Algeria wakati Kamishna wa pambano hilo atakuwa Saleh Issa Mahamat kutoka Chad. Stars itarajea nyumbani Juni 5 mwaka huu saa 1.40 na kuingia moja kwa moja kambini kujiandaa kwa mechi dhidi ya Gambia itakayofanyika Juni 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

KIKOSI CHA UJERUMANI KUTEMBELEA KAMBI YA NAZI NCHINI POLAND.

KIKOSI cha timu ya taifa ya Ujerumani pamoja na kocha wao Joachim Loew na nahodha Philipp Lahm wanatarajiwa kutembelea kambi kubwa ya watu wa Nazi waliofariki kipindi cha vita kuu ya pili ya dunia iliyopo katika mji wa Auschwitz nchini Poland kabla ya kuanza kwa michuano ya Ulaya. Zaidi ya watu milioni 1.5 wengi wao wakiwa wayahudi walikufa katika kambi hiyo katika kipindi cha kati ya mwaka 1940 na 1945, wengine kwa kuwekewa hewa ya sumu katika vyumba maalumu, baridi kali, njaa, magonjwa na wengine kutumikishwa kazi ngumu. Mbali na rais wa Shirikisho la Soka Ujerumani-DFB, mwenyekiti wa ligi ya Ujerumani Reinhard Rauball na meneja wa kikosi hicho Oliver Bierhoff katika msafara huo pia watakuwepo wachezaji ambao ni wazaliwa wa Poland ambao ni Miroslav Klose na Lukas Podolski. Ujerumani imepangwa kundi moja na timu za Ureno, Uholanzi na Denmark katika michuano hiyo ambayo imeandaliwa kwa pamoja kati ya Poland na Ukraine itakayoanza kutimua vumbi June 8 mpaka Julai 1 mwaka huu.

WAZIRI MKUU WA ITALIA ASHAMBULIWA KWA KAULI YAKE.

Maurizio Zamparini.
WAZO lililotolewa na Waziri Mkuu wa Italia, Mario Monti la kusimamisha Ligi Kuu ya nchi hiyo kwa miaka kadhaa kutokana na sakata ya rushwa linaloikabili limepingwa vikali na viongozi wa vilabu pamoja na viongozi wa Shirikisho la Soka nchini humo. Vyombo vya habari nchini humo vilimnukuu rais wa klabu ya Palermo, Maurizio Zamparini akimshambulia Monti kuwa natakiwa kuona haya kwa kauli yake alitoa. Zamparini ambaye alikataa kuingia katika masuala ya kisiasa baada ya kuombwa kufanya hivyo ni mmoja wa waanzilishi wa chama cha kulinda haki za raia nchini humo. Kauli hiyo ya Zamparini imekuja kufuatia Monti kukaririwa akisema kuwa ligi hiyo inastahili kusimamishwa kwa muda wa miaka miwili au mitatu kutokana na tuhuma za rushwa na masuala ya upangaji matokeo unaoiandama ligi hiyo toka mwaka jana. Mamia ya wachezaji na viongozi wa vilabu wamekamatwa katika awamu ya tatu ya msako wa watu wanaotuhumiwa na masuala ya rushwa na upangaji matokeo shughuli ambayo imefanyika wiki hii. Zamparini amesema kuwa kauli ya Monti ni upuuzi na anaonekana kama anatapatapa kutokana na kuingilia mambo yasiyomhusu akisahau suala muhimu la kushughulikia mdororo wa kiuchumi unaolikabili taifa hilo hivi sasa.

VIKOSI VYA TIMU ZOTE 16 ZITAKAZOSHIRIKI MICHUANO YA EURO 2012.


HIVI ndio vikosi vya mwisho vya wachezaji 23 kwa nchi 16 zinazoshiriki michuano ya Ulaya inayotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao nchini Poland na Ukraine.

Group A

Czech Republic

MAKIPA: Petr Cech (Chelsea/ENG), Jan Lastuvka (Dnepropetrovsk/UKR), Jaroslav Drobny (Hamburg/GER) MABEKI: Frantisek Rajtoral (Plzen), Roman Hubnik (Hertha/GER), Tomas Sivok (Besiktas/TUR), Michal Kadlec (Leverkusen/GER), Theodor Gebre Selassie (Liberec), David Limbersky (Plzen), Marek Suchy (Spartak Moscow/RUS) VIUNGO: Tomas Rosicky (Arsenal/ENG), Jaroslav Plasil (Bordeaux/FRA), Jan Rezek (Famagusta/CYP), Daniel Kolar (Plzen), Vladimir Darida (Plzen), Petr Jiracek (Wolfsburg/GER), Milan Petrzela (Plzen), Vaclav Pilar (Plzen), Tomas Hubschman (Donetsk/UKR) WASHAMBULIAJI: Milan Baros (Galatasaray/TUR), David Lafata (Jablonec), Tomas Pekhart (Nuremberg/GER), Tomas Necid (CSKA Moscow/RUS)

Greece

MAKIPA: Costas Chalkias (PAOK), Michalis Sifakis (Aris), Alexandros Tzorvas (Palermo/ITA) MABEKI: Vasilis Torosidis (Olympiakos), Avraam Papadopoulos (Olympiakos), Kyriakos Papadopoulos (Schalke/GER), Stelios Malezas (PAOK), Jose Holebas (Olympiakos), Giorgos Tzavellas (Monaco/FRA), Sokratis Papastathopoulos (Werder Bremen/GER) VIUNGO: Grigoris Makos (AEK), Giannis Maniatis (Olympiakos), Kostas Katsouranis (Panathinaikos), Giorgos Karagounis (Panathinaikos), Giorgos Fotakis (PAOK), Kostas Fortounis (Kaiserslautern/GER), Sotiris Ninis (Panathinaikos), Giannis Fetfatzidis (Olympiakos) WASHAMBULIAJI: Giorgos Samaras (Celtic/SCO), Dimitris Salpigidis (PAOK), Fanis Gekas (Samsunspor/TUR), Nikos Limberopoulos (AEK), Kostas Mitroglou (Atromitos)

Poland

MAKIPA: Wojciech Szczesny (Arsenal/ENG), Przemyslaw Tyton (PSV Eindhoven/NED), Grzegorz Sandomierski (Genk/BEL) MAKIPA: Sebastian Boenisch (Werder Bremen/GER), Marcin Kaminski (Lech Poznan), Damien Perquis (Sochaux/FRA), Lukasz Piszczek (Borussia Dortmund/GER), Marcin Wasilewski (Anderlecht/BEL), Jakub Wawrzyniak (Legia Warsaw), Grzegorz Wojtkowiak (Lech Poznan) VIUNGO: Kuba Blaszczykowski (Borussia Dortmund/GER), Dariusz Dudka (Auxerre/FRA), Kamil Grosicki (Sivasspor/TUR), Adam Matuszczyk (Fortuna Duesseldorf/GER), Adrian Mierzejewski (Trabzonspor/TUR), Rafal Murawski (Lech Poznan), Ludovic Obraniak (Bordeaux/FRA), Eugen Polanski (Mainz/GER), Maciej Rybus (Terek Grozny/RUS), Rafal Wolski (Legia Warsaw) WASHAMBULIAJI: Pawel Brozek (Celtic/SCO), Robert Lewandowski (Borussia Dortmund/GER), Artur Sobiech (Hannover 96/GER)

Russia

MAKIPA: Igor Akinfeyev (CSKA Moscow), Vyacheslav Malafeyev (Zenit St Petersburg), Anton Shinin (Dynamo Moscow) MABEKI: Alexander Anyukov (Zenit St Petersburg), Alexei Berezutsky, Sergei Ignashevich, Kirill Nababkin (all CSKA Moscow), Vladimir Granat (Dynamo Moscow), Yury Zhirkov (Anzhi Makhachkala), Dmitry Kombarov (Spartak Moscow), Roman Sharonov (Rubin Kazan) VIUNGO: Igor Denisov, Roman Shirokov, Konstantin Zyryanov (all Zenit St Petersburg), Denis Glushakov (Lokomotiv Moscow), Igor Semshov (Dynamo Moscow), Alan Dzagoyev (CSKA Moscow), Marat Izmailov (Sporting/POR) WASHAMBULIAJI: Andrei Arshavin, Alexander Kerzhakov (both Zenit St Petersburg), Alexander Kokorin (Dynamo Moscow), Roman Pavlyuchenko (Lokomotiv Moscow), Pavel Pogrebnyak (Fulham/ENG)

Group B

Denmark:

MAKIPA: Kasper Schmeichel (Leicester City/ENG), Stephan Andersen (Evian/FRA), Anders Lindegaard (Manchester United/ENG). MABEKI: Lars Jacobsen (FC Copenhagen), Simon Busk Poulsen (AZ Alkmaar/NED), Daniel Wass (Evian/FRA), Simon Kjaer (AS Roma/ITA), Daniel Agger (Liverpool/ENG), Andreas Bjelland (FC Nordsjaelland). VIUNGO: Michael Silberbauer (Young Boys Berne/SUI), William Kvist (VfB Stuttgart/GER), Christian Poulsen (Evian/FRA), Niki Zimling (Bruges/BEL), Jakob Poulsen (FC Midtjylland), Lasse Schone (NEC Nijmegen/NED), Christian Eriksen (Ajax/NED), Thomas Kahlenberg (Evian/FRA). WASHAMBULIAJI: Dennis Rommedahl (Brondby), Michael Krohn-Dehli (Brondby), Nicklas Bendtner (Sunderland/ENG), Tobias P. Mikkelsen (FC Nordsjaelland)

Germany

MAKIPA: Manuel Neuer (Bayern Munich), Tim Wiese (Werder Bremen), Ron-Robert Zieler (Hanover) MABEKI: Holger Badstuber (Bayern Munich), Jerome Boateng (Bayern Munich), Benedikt Hoewedes (Schalke 04), Mats Hummels (Borussia Dortmund), Philipp Lahm (Bayern Munich), Marcel Schmelzer (Borussia Dortmund), Per Mertesacker (Arsenal/ENG) VIUNGO: Lars Bender (Bayer Leverkusen), Toni Kroos (Bayern Munich), Thomas Mueller (Bayern Munich), Mesut Oezil (Real Madrid/ESP), Andre Schuerrle (Bayer Leverkusen), Sami Khedira (Real Madrid/ESP), Bastian Schweinsteiger (Bayern Munich), Mario Goetze (Borussia Dortmund), Ilkay Guendogan (Borussia Dortmund) WASHAMBULIAJI: Mario Gomez (Bayern Munich), Miroslav Klose (Lazio/ITA), Lukas Podolski (Arsenal/ENG), Marco Reus (Borussia Moenchengladbach)

Netherlands

MAKIPA: Tim Krul (Newcastle United/ENG), Maarten Stekelenburg (AS Roma/ITA), Michel Vorm (Swansea City/ENG) MABEKI: Khalid Boulahrouz (VfB Stuttgart/GER), Wilfred Bouma (PSV Eindhoven), John Heitinga (Everton/ENG), Joris Mathijsen (Malaga/ESP), Ron Vlaar (Feyenoord), Gregory van der Wiel (Ajax), Jetro Willems (PSV) VIUNGO: Mark van Bommel (AC Milan/ITA), Nigel de Jong (Manchester City/ENG), Stijn Schaars (Sporting Lisbon/POR), Wesley Sneijder (Inter Milan/ITA), Kevin Strootman (PSV Eindhoven), Rafael van der Vaart (Tottenham Hotspur/ENG) WASHAMBULIAJI: Ibrahim Afellay (Barcelona/ESP), Klaas-Jan Huntelaar (Schalke 04/GER), Luuk de Jong (FC Twente), Dirk Kuyt (Liverpool/ENG), Luciano Narsingh (SC Heerenveen), Robin van Persie (Arsenal/ENG), Arjen Robben (Bayern Munich/GER)

Portugal

MAKIPA: Rui Patricio (Sporting Lisbon), Eduardo (Benfica), Beto (CFR-Cluj/ROM) MABEKI: Bruno Alves (Zenit Saint-Petersburg/RUS), Fabio Coentrao (Real Madrid/ESP), Joao Pereira (Sporting Lisbon), Pepe (Real Madrid/ESP), Ricardo Costa (Valencia/ESP), Rolando (FC Porto), Miguel Lopes (Sporting Braga) VIUNGO: Carlos Martins (Granada/ESP), Joao Moutinho (FC Porto), Custodio (Sporting Braga), Miguel Veloso (Genoa/ITA), Raul Meireles (Chelsea/ENG), Ruben Micael (Real Zaragoza/ESP) WASHAMBULIAJI: Cristiano Ronaldo (Real Madrid/ESP), Hugo Almeida (Besiktas/TUR), Helder Postiga (Real Zaragoza/ESP), Nani (Manchester United/ENG), Nelson Oliveira (Benfica), Ricardo Quaresma (Besiktas/TUR), Silvestre Varela (FC Porto)

Group C

Croatia

MAKIPA: Stipe Pletikosa (Rostov/RUS), Danijel Subasic (Monaco/FRA), Ivan Kelava (Dinamo Zagreb) MABEKI: Vedran Corluka (Bayer Leverkusen/GER), Jurica Buljat (Maccabi Haifa/ISR), Domagoj Vida (Dinamo Zagreb), Josip Simunic (Dinamo Zagreb), Ivan Strinic (Dnepropetrovsk/UKR), Gordon Schildenfeld (Eintracht Frankfurt/GER) VIUNGO: Danijel Pranjic (Bayern Munich/GER), Tomislav Dujmovic (Real Zaragoza/ESP), Niko Kranjcar (Tottenham/ENG), Luka Modric (Tottenham/ENG), Milan Badelj (Dinamo Zagreb), Darijo Srna (Shakhtar Donetsk/UKR), Ivo Ilicevic (Hamburg/GER), Ivan Perisic (Borussia Dortmund/GER), Ognjen Vukojevic (Dynamo Kiev/UKR), Ivan Rakitic (Sevilla/ESP) WASHAMBULIAJI: Mario Mandzukic (Wolfsburg/GER), Ivica Olic (Bayern Munich/GER), Eduardo da Silva (Shakhtar Donetsk/UKR), Nikica Jelavic (Everton/ENG)

Ireland

MAKIPA: Shay Given (Aston Villa), Keiren Westwood (Sunderland), David Forde (Millwall) MABEKI: John O'Shea (Sunderland), Richard Dunne (Aston Villa), Sean St Ledger (Leicester City), Stephen Ward (Wolverhampton Wanderers), Paul McShane (Hull City), Stephen Kelly (Fulham), Darren O'Dea (Celtic) VIUNGO: Keith Andrews (West Bromwich Albion), Glenn Whelan (Stoke City), Darron Gibson (Everton), Damien Duff (Fulham), Aiden McGeady (Spartak Moscow), Stephen Hunt (Wolverhampton Wanderers), Paul Green (Derby County) James McClean (Sunderland) WASHAMBULIAJI: Robbie Keane (LA Galaxy), Kevin Doyle (Wolverhampton Wanderers), Simon Cox (West Bromwich Albion), Jonathan Walters (Stoke City), Shane Long (West Bromwich Albion)

Italy

MAKIPA: Gianluigi Buffon (Juventus), Salvatore Sirigu (Paris Saint-Germain/FRA), Morgan De Sanctis (Napoli) MABEKI: Cristian Maggio (Napoli), Ignazio Abate (AC Milan), Federico Balzaretti (Palermo), Leonardo Bonucci (Juventus), Andrea Barzagli (Juventus), Giorgio Chiellini (Juventus), Angelo Ogbonna (Torino) VIUNGO: Andrea Pirlo (Juventus), Claudio Marchisio (Juventus), Emanuele Giaccherini (Juventus), Daniele De Rossi (Roma), Thiago Motta (Paris Saint-Germain/FRA), Antonio Nocerino (AC Milan), Riccardo Montolivo (Fiorentina), Alessandro Diamanti (Bologna) WASHAMBULIAJI: Antonio Cassano (AC Milan), Mario Balotelli (Manchester City/ENG), Sebastian Giovinco (Parma), Antonio Di Natale (Udinese), Fabio Borini (Roma)

Spain

MAKIPA: Iker Casillas (Real Madrid), Jose Reina (Liverpool/ENG), Victor Valdes (Barcelona). MABEKI: Juanfran (Atletico Madrid), Alvaro Arbeloa, Raul Albiol, Sergio Ramos (all Real Madrid), Jordi Alba (Valencia), Gerard Pique (Barcelona), Javi Martinez (Athletic Bilbao). VIUNGO: Xabi Alonso (Real Madrid), Santi Cazorla (Malaga), Xavi Hernandez, Cesc Fabregas, Andres Iniesta, Sergio Busquets (all Barcelona). WASHAMBULIAJI: David Silva (Manchester City/ENG), Jesus Navas, Alvaro Negredo (both Sevilla), Fernando Torres, Juan Mata (both Chelsea/ENG), Pedro (Barcelona), Fernando Llorente (Athletic Bilbao)

Group D

England

MAKIPA: Joe Hart (Man City), Rob Green (West Ham), Jack Butland (Birmingham) MABEKI: Glen Johnson (Liverpool), Phil Jones (Man United), John Terry (Chelsea), Joleon Lescott (Man City), Gary Cahill (Chelsea), Ashley Cole (Chelsea), Leighton Baines (Everton), Phil Jagielka (Everton) VIUNGO: Theo Walcott (Arsenal), Stewart Downing (Liverpool), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Steven Gerrard (Liverpool), Frank Lampard (Chelsea), Scott Parker (Tottenham), Ashley Young (Man United), James Milner (Man City) WASHAMBULIAJI: Wayne Rooney (Man United), Danny Welbeck (Man United), Andy Carroll (Liverpool), Jermain Defoe (Tottenham)

France

MAKIPA: Cedric Carrasso (Bordeaux), Hugo Lloris (Lyon), Steve Mandanda (Marseille)

MABEKI: Gael Clichy (Manchester City/ENG), Mathieu Debuchy (Lille), Patrice Evra (Manchester United/ENG), Laurent Koscielny (Arsenal/ENG), Philippe Mexes (AC Milan/ITA), Adil Rami (Valencia/ESP), Anthony Reveillere (Lyon) VIUNGO: Yohan Cabaye (Newcastle United/ENG), Alou Diarra (Marseille), Florent Malouda (Chelsea/ENG), Marvin Martin (Sochaux), Blaise Matuidi (Paris Saint-Germain), Yann M'vila (Rennes), Samir Nasri (Manchester City/ENG) WASHAMBULIAJI: Hatem Ben Arfa (Newcastle United/ENG), Karim Benzema (Real Madrid/ESP), Olivier Giroud (Montpellier), Jeremy Menez (Paris Saint-Germain), Franck Ribery (Bayern Munich/GER), Mathieu Valbuena (Marseille)

Sweden

MAKIPA: Andreas Isaksson (PSV Eindhoven/NED), Johan Wiland (FC Copenhagen/DEN), Par Hansson (Helsingborg) MABEKI: Mikael Antonsson (Bologna/ITA), Andreas Granqvist (Genoa/ITA), Mikael Lustig (Celtic/SCO), Olof Mellberg (Olympiakos/GRE), Jonas Olsson (West Bromwich Albion/ENG), Martin Olsson (Blackburn Rovers/ENG), Behrang Safari (Anderlecht/BEL) VIUNGO: Emir Bajrami (Twente/NED), Rasmus Elm (AZ Alkmaar/NED), Samuel Holmen (Istanbul BB/TUR), Kim Kallstrom (Lyon/FRA), Sebastian Larsson (Sunderland/ENG), Anders Svensson (IF Elfsborg), Pontus Wernbloom (CSKA Moscow/RUS), Christian Wilhelmsson (Al-Hilal/KSA) WASHAMBULIAJI: Zlatan Ibrahimovic (AC Milan/ITA), Johan Elmander (Galatasaray/TUR), Tobias Hysen (Gothenburg), Ola Toivonen (PSV Eindhoven/NED), Marcus Rosenberg (Werder Bremen/GER)

Ukraine

MAKIPA: Andrei Pyatov (Shakhtar Donetsk), Alexander Goryainov (Metalist Kharkiv), Maxim Koval (Dynamo Kiev) MABEKI: Taras Mykhalik, Yevgeny Khacheridi (both Dynamo Kiev), Yaroslav Rakytsky, Alexander Kucher, Vyacheslav Shevchuk (all Shakhtar Donetsk), Yevgeny Selin (Vorskla Poltava), Bogdan Butko (Mariupol) VIUNGO: Anatoly Tymoshchuk (Bayern/GER), Oleg Gusev, Denis Garmash, Alexander Aliev, Andrei Yarmolenko (all Dynamo Kiev), Ruslan Rotan, Yevgeny Konoplyanka (both Dnepropetrovsk), Sergei Nazarenko (Tavria Simferopol) WASHAMBULIAJI: Andrei Shevchenko, Artem Milevsky (both Dynamo Kiev), Andrei Voronin (Dynamo Moscow/RUS), Yevgeny Seleznov, Marko Devic (both Shakhtar Donetsk)

"ALL IN ONE RHYTHM" NEW SLOGAN FOR BRAZIL 2014.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limetangaza kauli mbiu inayoitwa Sauti Moja kwa Wote au kwa lugha ya kigeni All in one rhythm itakayotumika katika michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil 2014. Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke amesema kuwa kazi ya kutafuta kauli mbiu hiyo ambayo inawakilisha ladha tofauti imefanywa kwa pamoja kati ya serikali ya Brazil na shirikisho hilo na kutangazwa rasmi kwenye sherehe zilizofanyika jijini Rio de Jenairo. Naye Waziri wa Michezo wan chi hiyo, Aldo Rebelo amesema kuwa kauli mbiu hiyo ni mwaliko wa wenyeji na wageni ambao watakuja Brazil kuungana pamoja na kushangilia michuano hiyo ya kihistoria. Hiyo ni safari ya kwanza ya Valcke kwenda nchini Brazil toka alipokwaruzana na serikali ya nchi hiyo Machi mwaka huu kuhusiana na maandalizi ya michuano hiyo kitendo ambacho yeye na rais wa FIFA Sepp Blatter waliomba radhi. Serikali ya Brazil ilipanga kutumia kiasi cha dola bilioni 13 katika miradi 101 ya kujenga na kukarabati viwanja, kukarabati viwanja vya ndege, barabara na usafiri wa jumuia lakini ni miradi 60 kati ya hiyo ndio imeanza mpka sasa.

BARCELONA KUFANYA ZIARA MOROCCO.

KLABU ya Barcelona inatarajiwa kufanya ziara ya kimichezo nchini Morocco Julai 28 mwaka huu ambapo wakiwa nchini humo watacheza mchezo wa kirafiki na moja vilabu vya nchi hiyo jijini Tanger. Wizara ya michezo nchini humo ilithibitisha ziara hiyo ambapo wanatarajia kuwalipa kiasi cha euro milioni moja Barcelona ambao ni mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya 2011. Ofisa Habari wa wizara hiyo Hamid Faridi amesema kuwa mji wa Tangier ambao uko Kaskanini mwa nchi hiyo ndio utakuwa mwenyeji wa timu hiyo ambayo itakwenda huko na nyota wao wote akiwemo Lionel Messi. Mchezo huo wa kirafiki umeandaliwa na kamati iliyoteuliwa na wizara ya michezo ya nchi hiyo pamoja na shirika la kitaifa la utekelezaji na usimamizi wa viwanja.

Tuesday, May 29, 2012

EURO 2012.

KIKOSI CHA IRELAND KASKAZINI.
MAKIPA: Shay Given (Aston Villa), Keiren Westwood (Sunderland), David Forde (Millwall) MABEKI: John O'Shea (Sunderland), Richard Dunne (Aston Villa), Sean St Ledger (Leicester City), Stephen Ward (Wolverhampton Wanderers), Paul McShane (Hull City), Stephen Kelly (Fulham), Darren O'Dea (Celtic) VIUNGO: Keith Andrews (West Bromwich Albion), Glenn Whelan (Stoke City), Darron Gibson (Everton), Damien Duff (Fulham), Aiden McGeady (Spartak Moscow), Stephen Hunt (Wolverhampton Wanderers), Paul Green (Derby County) James McClean (Sunderland) WASHAMBULIAJI: Robbie Keane (LA Galaxy), Kevin Doyle (Wolverhampton Wanderers), Simon Cox (West Bromwich Albion), Jonathan Walters (Stoke City), Shane Long (West Bromwich Albion)

KIKOSI CHA UKRAINE.
MAKIPA: Andriy Pyatov (Shakhtar Donetsk), Olexandr Horyainov (FC Metalist Kharkiv), Maxym Koval (FC Dynamo Kiev). MABEKI: Olexandr Kucher (Shakhtar Donetsk), Yaroslav Rakitskiy (Shakhtar Donetsk), Vyacheslav Shevchuk (Shakhtar Donetsk), Evhen Khacheridi (Dynamo Kiev), Taras Mykhalyk (Dynamo Kiev), Evhen Selin (Vorskla), Bogdan Butko (Illichivets). VIUNGO: Olexandr Aliev (Dynamo Kiev), Denys Garmash (Dynamo Kiev), Oleh Gusiev (Dynamo Kiev), Andriy Yarmolenko (Dynamo Kiev), Evhen Konoplyanka (Dnipro Dnipropetrovsk), Ruslan Rotan (Dnipro), Serhiy Nazarenko (Tavriya), Anatoliy Tymoshchuk (Bayern Munich). WASHAMBULIAJI: Artem Milevskiy (Dynamo Kiev), Andriy Shevchenko (Dynamo Kiev), Marco Devic (FC Metalist Kharkiv), Andriy Voronin (Dynamo Moscow), Evhen Seleznyov (Shakhtar Donetsk).

MAN UNITED MBIONI KUMNYAKUWA KAGAWA.

KLABU ya Manchester United iko karibuni kumsajili kiungo nyota wa kimataifa wa Japan na klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani, Shinji Kagawa kwa ada ya euro milioni 15. Mkurugenzi wa michezo wa Dortmund Michael Zorc alikiri kuwepo kwa suala la uhamisho wa mchezaji huyo lakini amesema kuwa kuna baadhi ya vitu havijamaliziwa hivyo mchezaji huyo bado ni mali ya klabu hiyo mpaka hapo vitakapokamilika. Mapema mwezi huu kocha wa United Sir Alex Ferguson alisafiri kwenda jijini Berlin kumwangalia Kagawa ambaye alishinda bao moja kwenye mchezo wa fainali ya kombe la ligi la nchi hiyo dhidi ya Bayern Munich ambapo Dortmund walishinda mabao 5-2. Dortmund ilimsajili Kagawa kwa ada ya euro 350,000 akitokea katika klabu ya Cerezo Osaka inayoshiriki Ligi Kuu nchini Japan maarufu kama J-League ambapo amefunga mabao 21 katika michezo 49 aliyocheza msimu huu na kuiwezesha Dortmund kutetea ubingwa wa ligi kuu nchini humo.

EURO 2012: FRENCH SQUAD.

KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Hugo Lloris (Olympique Lyon), Steve Mandanda (Olympique Marseille), Cedric Carrasso (Girondins Bordeaux) MABEKI: Gael Clichy (Manchester City), Patrice Evra (Manchester United), Laurent Koscielny (Arsenal), Philippe Mexes (AC Milan), Adil Rami (Valencia), Mathieu Debuchy (Lille), Anthony Reveillere (Olympique Lyon) VIUNGO: Yohan Cabaye (Newcastle United), Florent Malouda (Chelsea), Samir Nasri (Manchester City), Alou Diarra (Olympique Marseille), Yann M'vila (Stade Rennes), Marvin Martin (Sochaux), Blaise Matuidi (Paris St Germain) WASHAMBULIAJI: Hatem Ben Arfa (Newcastle United), Karim Benzema (Real Madrid), Franck Ribery (Bayern Munich), Olivier Giroud (Montpellier), Jeremy Menez (Paris St Germain), Mathieu Valbuena (Olympique Marseille).

EURO 2012: HODGSON ATAJA KIKOSI CHA MWISHO.

KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson ametangaza kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 ambao wataiwakilisha nchi hiyo katika michuano ya Kombe la Ulaya linalotarajiwa kuanza mapema mwakani. Katika kikosi hicho ambacho hakina mabadiliko makubwa na kile alichotangaza mara ya kwanza Hodgson amewajumuisha Danny Welbeck na Glen Johnson ambao walikosa mchezo wa kirafiki baina ya timu hiyo na Norway kutokana na majeraha yaliyokuwa yakiwasumbua. Mabadiliko yaliyopo katika kikosi hicho ni kuitwa kwa beki wa Everton Phil Jagielka kuja kuziba nafasi ya Gareth Barry ambaye aliumia nyonga wakati wa mchezo dhidi ya Norway ambao Uingereza ilishinda bao 1-0 jijini Oslo. Barry ambaye amecheza mechi 50 katika kikosi hicho cha Uingereza alizimika kutolewa nje ikiwa ni dakika 30 toka alipoingia kama mchezaji wa akiba katika muda wa mapumziko wa mchezo huo. 

KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: 1. Joe Hart (Manchester City), 13. Robert Green (West Ham), 23. Jack Butland (Birmingham City). MABEKI: 12. Leighton Baines (Everton), 5. Gary Cahill (Chelsea), 3. Ashley Cole (Chelsea), 2. Glen Johnson (Liverpool), 14. Phil Jones (Manchester United), 15. Joleon Lescott (Manchester City), 6. John Terry (Chelsea), 18. Phil Jagielka (Everton). VIUNGO: 19. Stewart Downing (Liverpool), 4. Steven Gerrard (Liverpool), 8. Frank Lampard (Chelsea), 16. James Milner (Manchester City), 20. Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), 17. Scott Parker (Tottenham), 7. Theo Walcott (Arsenal), 11. Ashley Young (Manchester United). WASHAMBULIAJI: 9. Andy Carroll (Liverpool), 21. Jermain Defoe (Tottenham), 10. Wayne Rooney (Manchester United), 22. Danny Welbeck (Manchester United).

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF.

CHIPUKIZI 10 WAPITA MCHUJO ASPIRE
Wachezaji 10 wamepita katika mchakato wa kusaka vipaji kwa chipukizi wenye umri chini ya miaka 14 kupitia mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football Dream ambao uko chini ya Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliofanyika kuanzia Mei 21-26 mwaka huu. Watoto zaidi ya 1,500 walishiriki katika mchakato huo uliokuwa chini ya mng’amua vipaji (scout) Gisbert Xavier kutoka Hispania, na ulifanyika katika vituo vya Morogoro, Bagamoyo mkoani Pwani, na Kawe, Makongo, Magomeni, Tabata, Kitunda, Tandika, Ukonga na Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kwa Dar es Salaam. Kituo cha Morogoro amechaguliwa Karim Hussein wa Shule ya Sekondari Nanenane, kituo cha Magomeni ni Joseph Mushi wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere wakati kituo cha Tabata ni Martin Tangazi. Tandika ni Ismail Ngakonda (Shule ya Sekondari Uwanja wa Ndege), Kitunda ni Nicholas Lauteri (Shule ya Sekondari Ulongoni), Omari Mbwai (Shule ya Sekondari Msongola) na Hamad Omari (Shule ya Sekondari Ulongoni). Kituo cha Ukonga ni James Msuva (Shule ya Sekondari Makongo) wakati Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ni Adolf Mtasigwa (Shule ya Sekondari Loyola) na Ally Hatibu (Shule ya Sekondari Kurasini). Mng’amuzi huyo wa vipaji anatarajia kufanya mchujo wa mwingine kabla ya chipukizi hao kwenda Nairobi, Kenya kwenye mchujo wa mwisho baada ya kambi ya ya siku nne kuanzia Juni 5-9 mwaka huu.

MAKOCHA COPA COCA COLA KUSHIRIKI SEMINA YA FIFA
Makocha 35 wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kushiriki semina ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa ajili ya michuano ya vijana ya Copa Coca-Cola. Semina hiyo itafanyika kwenye ofisi za TFF jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 4-9 mwaka huu chini ya mkufunzi kutoka FIFA, Ulric Mathiot. Makocha hao wanatakiwa kuripoti Juni 3 mwaka huu kwenye ofisi za TFF. Makocha hao na mikoa yao kwenye mabano ni Englihard Livigha (Mtwara), Joseph Sehaba (Dodoma), Ramadhan Ramadhan (Mjini Magharibi), Shaha Khamis Rashid (Kaskazini Unguja), Salum Ali Haji (Kusini Unguja), Mohamed Ali Khamis (Kaskazini Pemba), Mecky Maxime (Morogoro) na George Simon (Kagera). Haruni Dudu (Iringa), Maka Mwalwisi (Mbeya), Amos Mewa (Rukwa), Athuman Kilundumya (Tabora), Charles Mayaya (Shinyanga), Fulgence Novatus (Mwanza), James George (Mara), Amani Kongoro (Kigoma), Mtoro Likere (Ilala), Evarist Katomondo (Kinondoni), Shawal Bilanga (Temeke) na Rashid Chama (Arusha). Wengine ni Francis Samatta (Ruvuma), Issac Gamba (Kilimanjaro), Aloyce Mayombo (Pwani), Jomo Puccey (Lindi), Justine Kanemela (Singida), Charles Msengi (Manyara), Mohamed Kampira (Tanga), Alfred Itael (Arusha), Nicholas Achimpota (Dodoma), Leonard Jima (Ruvuma), Leonard Malongo (Mwanza), Kesi Abdallah (Tanga), John Memba (Ilala) na Zuhura Kapama (Kigoma).

EURO 2012: UKRAINE STADIUMS.

KIEV - OLYMPIC STADIUM.
 Beginning of construction – December 2008 
 End of construction – June 2011
 Capacity – 69000 seats
 VIP boxes – 150 seats
 Business seats – 212
 Parking – 6500 places
 Construction cost – 1 000 million PLN


KHARKIV - METALIST STADIUM. 
 Beginning of reconstruction – 2007
 End of reconstruction – November 2011
 Capacity – 41111 seats
 VIP boxes – 390 seats
 Media seats – over 900
 Construction cost – 365 million hryvnia


LVIV - ARENA LVIV.
 Beginning of construction – November 2008 
 End of construction – October 2011
 Capacity – 33000 seats
 VIP boxes – 450 seats
 Business seats – 408
 Parking – 4500 places
 Construction cost – 287 million hryvnia


DONETSK - DONBASS ARENA.
 Beginning of construction – June 2006
 End of construction – August 2009
 Capacity – 51504 seats
 Media seats – over 1159
 Construction cost – 400 million dollars

EURO 2012: POLAND STADIUMS.


WARSAW - NATIONAL STADIUM.
 Beginning of construction – October 2008
 End of construction – November 2009
 Opening date – 14.08.2011
 Capacity – 58000 seats
 VIP boxes – 69 (800 seats)
 Business seats – over 4600
 Parking – 1765 places
 Construction cost – 1 915 million PLN


WROCLAW - MUNICIPAL STADIUM.
 Beginning of construction – April 2009
 End of construction – October 2011
 Capacity – 44300 seats
 VIP boxes – 426 seats
 Business seats – 2130
 Media seats – 150
 Parking – 1000 places
 Construction cost – 853 million PLN



POZNAN - MUNICIPAL STADIUM.
 Beginning of construction – 2002
 End of reconstruction – September 2010
 Capacity – 43 000 seats (For Euro 2012 – over 41 thousand).
 VIP boxes – 45 (480 seats)
 Business seats – 1100
 Parking spaces – 900
 Modernization cost – 746 million PLN



GDANSK - PGE ARENA GDANSK.
 Beginning of construction – May 2009
 Opening date – 14.08.2011
 Capacity – 42000 seats
 VIP boxes – 40
 Business seats – 1383
 Parking – 2171 places, coaches – 74 places
 Construction cost – 775 million PLN

EURO 2008 - Best Goals

HAZARD KUJIUNGA NA CHELSEA.

Eden Hazard.
KIUNGO nyota wa kimataifa wa Ubelgiji na klabu ya Lille ya Ufaransa, Eden Hazard amesema kuwa ameamua kujiunga na mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya timu ya Chelsea badala ya Manchester City au Manchester United. Hazard ambaye ana umri wa miaka 21 aliandika katika mtandao wake wa kijamii wa twitter kuwa anatarajia kusaini katika klabu ya Chelsea na kukomesha uvumi ambao ulikuwa umesambaa kuwa atajiunga na aidha United au City katika kipindi hiki cha usajili. Mchezaji huyo amenyakuwa tuzo za mchezaji bora wa Ligi Kuu nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1amekiongoza kikosi cha Lille kunyakuwa taji la ligi hiyo mwaka 2011 na kufunga mabao 20 msimu ambayo yameiwezesha klabu hiyo kushika nafasi ya tatu msimu huu hivyo kukata tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao. Hazard alitua Lille akiwa na umri wa miaka 16 ambapo haraka haraka alipanda kiwango na kujikuta akiwa katika kikosi cha kwanza cha Lille na alitangaza msimu wa mwisho kuwepo katika klabu hiyo Octoba mwaka jana.

Monday, May 28, 2012

Zlatan Ibrahimovic ● All 35 Goals ● 2011-2012

Robin van Persie's All 37 Goals in 2011/12 season for Arsenal

Cristiano Ronaldo 2012 All 60 Goals With Real Madrid in All Competion 20...

Lionel Messi All 73 Goals 2011-2012 Season

Top 10 goals EURO 2004

MAANDALIZI YA ITALIA EURO 2012 YAINGIA DOSARI.


Stefano Mauri.



MAANDALIZI ya timu ya Taifa ya Italia kwa ajili ya michuano ya Ulaya 2012 yameingia doa baada ya habari kuwa baadhi ya wachezaji wakutegemewa wa timu hiyo wako katika uchunguzi kufuatia tuhuma za upangaji wa matokeo. Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini humo imesema kuwa polisi wa nchi hiyo wamemkamata nahodha wa klabu ya Lazio, Stefano Mauri ambaye ameichezea Italia mechi 11 kwa ajili ya tuhuma hizo za upangaji wa matokeo wakati kiungo wa zamani wa klabu ya Genoa Omar Milanetto nae ni mmoja watu 19 waliokamatwa. Watu wote hao wanaoshikiliwa na polisi wanahisiwa kushiriki katika genge haramu la kimataifa la michezo ya kamari ambalo linaongozwa na raia wa Singapore Tan Seet Eng ambaye alikamatwa mwishoni mwa mwaka jana. Mbali na wachezaji hao waliokamatwa pia beki wa klabu ya Zenit St Petersburg Domenico Criscito nae pia alichunguzwa na maofisa wa polisi ambao walienda katika kambi ya timu ya taifa ya nchi hiyo iliyopo jijini Coverciano pamoja na kocha wa Juventus Antonio Conte ambaye alisachiwa nyumbani kwake kuhusiana na tuhuma hizohizo. Wachezaji wa zamani wa kimataifa wa Italia ambao ni Cristiano Doni na Giuseppe Signori tayari wameshafungiwa kujishughulisha na masuala ya mpira kutokana na tuhuma kama hizo.

FIFA YAIONYA KENYA KUHUSIANA NAMASULA YA VURUGU.


Patrick Naggi.



SHIRIKISHO la Soka la Kenya-FKF limepewa angalizo kuhusu suala la usalama na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kufuatia mchezo wa kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Malawi unaotarajiwa kuchezwa mwishoni mwa wiki hii. FKF wamepewa maelekezo kuwepo kwa ulinzi wa kutosha siku ya mchezo huo kwani vurugu zozote za mashabiki zitakazotokea siku zitapelekea nchi hiyo kufungiwa kuandaa mechi za kimataifa katika uwanja wake wa nyumbani. Mapema FIFA waliiadhibu Kenya kabla ya kukata rufani na kuwapa onyo kali kuhusu suala la vurugu za mashabiki kutokea katika michezo mingine katika siku zijazo. Adhabu hiyo ilikuja wakati FIFA ilipoufungia Uwanja wa Nyayo kutokana na vurugu zilizotokea ambapo baadae uliachiwa na kupewa onyo hilo baada ya kukata rufani. Lakini Mkurugenzi wa Kamati ya Ufundi ya FKF, Patrick Naggi amesema kuwa suala la ulinzi wakati wa mchezo huo halina tatizo lolote kwani wamehakikisha kutakuwa na wana usalama wa kutosha pamoja na ulinzi wa ziada kutokana na vitisho vya kundi la Al Shabaab la Somalia.