Patrick Naggi. |
SHIRIKISHO la Soka la Kenya-FKF limepewa angalizo kuhusu suala la usalama na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kufuatia mchezo wa kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Malawi unaotarajiwa kuchezwa mwishoni mwa wiki hii. FKF wamepewa maelekezo kuwepo kwa ulinzi wa kutosha siku ya mchezo huo kwani vurugu zozote za mashabiki zitakazotokea siku zitapelekea nchi hiyo kufungiwa kuandaa mechi za kimataifa katika uwanja wake wa nyumbani. Mapema FIFA waliiadhibu Kenya kabla ya kukata rufani na kuwapa onyo kali kuhusu suala la vurugu za mashabiki kutokea katika michezo mingine katika siku zijazo. Adhabu hiyo ilikuja wakati FIFA ilipoufungia Uwanja wa Nyayo kutokana na vurugu zilizotokea ambapo baadae uliachiwa na kupewa onyo hilo baada ya kukata rufani. Lakini Mkurugenzi wa Kamati ya Ufundi ya FKF, Patrick Naggi amesema kuwa suala la ulinzi wakati wa mchezo huo halina tatizo lolote kwani wamehakikisha kutakuwa na wana usalama wa kutosha pamoja na ulinzi wa ziada kutokana na vitisho vya kundi la Al Shabaab la Somalia.
No comments:
Post a Comment