Monday, May 28, 2012

MAANDALIZI YA ITALIA EURO 2012 YAINGIA DOSARI.


Stefano Mauri.



MAANDALIZI ya timu ya Taifa ya Italia kwa ajili ya michuano ya Ulaya 2012 yameingia doa baada ya habari kuwa baadhi ya wachezaji wakutegemewa wa timu hiyo wako katika uchunguzi kufuatia tuhuma za upangaji wa matokeo. Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini humo imesema kuwa polisi wa nchi hiyo wamemkamata nahodha wa klabu ya Lazio, Stefano Mauri ambaye ameichezea Italia mechi 11 kwa ajili ya tuhuma hizo za upangaji wa matokeo wakati kiungo wa zamani wa klabu ya Genoa Omar Milanetto nae ni mmoja watu 19 waliokamatwa. Watu wote hao wanaoshikiliwa na polisi wanahisiwa kushiriki katika genge haramu la kimataifa la michezo ya kamari ambalo linaongozwa na raia wa Singapore Tan Seet Eng ambaye alikamatwa mwishoni mwa mwaka jana. Mbali na wachezaji hao waliokamatwa pia beki wa klabu ya Zenit St Petersburg Domenico Criscito nae pia alichunguzwa na maofisa wa polisi ambao walienda katika kambi ya timu ya taifa ya nchi hiyo iliyopo jijini Coverciano pamoja na kocha wa Juventus Antonio Conte ambaye alisachiwa nyumbani kwake kuhusiana na tuhuma hizohizo. Wachezaji wa zamani wa kimataifa wa Italia ambao ni Cristiano Doni na Giuseppe Signori tayari wameshafungiwa kujishughulisha na masuala ya mpira kutokana na tuhuma kama hizo.

No comments:

Post a Comment