Tuesday, August 30, 2011

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF.


VIINGILIO VYA STARS NA ALGERIA
Viingilio kwa ajili ya mechi ya mchujo kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon kati ya Taifa Stars na Algeria vitakuwa kama ifuatavyo;

Viti vya kijani ni sh. 3,000, viti vya bluu sh. 5,000, viti vya rangi ya chungwa sh. 7,000, VIP C sh.10,000, VIP B sh. 20,000 na VIP A sh. 30,000. Tiketi zitaanza kuuzwa Septemba Mosi mwaka huu.

Taifa Stars tayari iko kambini tangu jana (Agosti 28 mwaka huu) na inaendelea na mazoezi Uwanja wa Karume ambapo wachezaji wote wa ndani waliripoti jana mchana na kuanza mazoezi jioni.

Wachezaji wan je waliofika jana usiku ni Abdi Kassim na Dan Mrwanda kutoka Vietnam na Mbwana Samata kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Athuman Machupa (Sweden), Henry Joseph (Norway) na Idrisa Rajab (Kenya) wanaingia leo jioni.

Nizar Khalfan wa Vancouver Whitecaps ya Canada ndiye atakayekuwa mchezaji wa mwisho kuripoti kambini. Khalfan atatua nchini kesho saa 5.15 usiku kwa ndege ya PrescisionAir akitokea Nairobi.

TWIGA STARS KUAGWA LEO
Timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twigs Stars) inayoondoka Agosti 31 mwaka huu kwenda Maputo, Msumbiji kwenye michezo ya All Africa Games itakayofanyika nchini humo kuanzia Septemba 3-18 mwaka huu itaagwa kesho (Agosti 30 mwaka huu).

Twiga Stars wataagwa saa 6 mchana kambini kwao hoteli ya Itumbi iliyopo Magomeni Mwembechai, Dar es Salaam. Wakati huo huo Kocha Mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza majina ya wachezaji 16 watakaokwenda Maputo.

Wachezaji hao ni Sophia Mwasikili, Fatuma Omary, Mwanaidi Tamba, Fatuma Bashiri, Mwajuma Abdallah, Asha Rashid, Mwanahamisi Omari, Pulkeria Charaji, Ester Chabruma, Zena Khamis, Fridian John, Fatuma Mustafa, Ettoe Mlenzi, Ftuma Khatib, Maimuna Said na Mwapewa Mtumwa.

Viongozi watakaofuatana na timu hiyo ni Mkwasa, kocha msaidizi Nasra Mohamed, daktari wa timu Dk. Gania Seif wakati Meneja wa timu hiyo ni Furaha Francis.

Mechi ya kwanza ya Twiga Stars itakuwa Septembe 5 mwaka huu dhidi ya Ghana wakati ya pili dhidi ya Afrika Kusini itachezwa Septemba 8 mwaka huu. Twiga Stars itacheza mechi yake ya mwisho katika hatua ya makundi Septemba 11 mwaka huu dhidi ya Zimbabwe.

KOCHA WA UNDER 20 AITA 30.


DAR ES SALAAM, Tanzania
KOCHA wa timu za vijana Kim Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 30 wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kwa ajili ya mazoezi mwezi ujao.

Wachezaji walioitwa ni Saleh Ally (TSA), Jackson Wandwi (Azam), Hassan Kessy (Mtibwa Sugar), Khamis Mroki (Mtibwa Sugar), Yassin Mustapha (Polisi Dodoma), Andrew Kasembe (Moro United), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Ally Teru (Simba), Said Ruhava (Kagera Sugar), Samuel Mkomola (Azam), Frank Damayo (JKT Ruvu), Omega Seme (Yanga), Atupele Green (Yanga), Thomas Ulimwengu (ABC Sweden) na Jerome Lambele (Moro United).

Wengine ni Simon Msuvan (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Alex Joseph (Majimaji), Ibrahim Rajab (Azam), Renatus Patrick (Polisi Dodoma), Abdallah Kilala (AFC), Rajab Zahir (Moro United), Amani Kyata (TSA), Edward Shija (Simba), Alfred Amede (Russia), Khelf Hassan (Kenya), Emily Mgeta (TSC Mwanza), Ramadhan Salum (Simba), Frank Sekule (Simba) na Hassan Dilunga (Ruvu Shooting).

Monday, August 29, 2011

FORLAN ATIMKIA INTER.


MILAN, Italia
Diego Forlan amethibitisha kuwa atajiunga na Inter Milan baada ya muda wake wa kubaki Atletico Madrid kuisha.

Uruguay straiker mwenye umri wa miaka 32 amefanya mkutano na waandishi wa habari na kueleza kwamba hatoendelea kuwepo ndani ya Uwanja wa Vincente Calderon kama mchezaji wa Atletico na sasa anaelekea jijini Milan kuitumikia klabu inayotumia uwanja wa Giuseppe De Maeaza.

Forlan sasa atasafiri kueleka Milan ambapo atafanyiwa vipimo vya afya na baadae kusaini mkataba wa kuitumikia Inter Milan.

“Naenda kujiunga na klabu kubwa na kuna changamoto kubwa mbele yangu.Nataka kumshukuru Massimo Moratti kwa nafasi hii.

“Nimeshaongea na Estaban Cambiasso na Diego Milito, wote ni marafiki zangu.Naifahamu Serie A kwa kuwa nimeshaangalia mechi nyingi kwenye TV na nina furaha kubwa kucheza nchini Italia baada ya Premier League na La Liga.” – Forlan

BARCELONA 5 VILLARREAL 0

Sunday, August 28, 2011

MONEY WELL SPENT.

Zaragoza Vs Real Madrid 0-6 | All Goals & Highlights | 28-8-2011 Zaragoz...

KIPIGO CHA FEDHEHA: MANCHESTER UNITED 8 ARSENAL 2MATOKEO YA MECHI NYINGINE.

Tottenham Hotspur 1-5 Manchester City


Newcastle United 2-1 Fulham


Liverpool 3-1 Bolton Wanderers


Blackburn Rovers 0-1 Everton


Chelsea 3-1 Norwich City


Swansea City 0-0 Sunderland


Wigan Athletic 2-0 Queens Park Rangers


Aston Villa 0-0 Wolverhampton Wanderers

Friday, August 26, 2011

HATIMAYE LIGI KUU NCHINI HISPANIA KUANZA JUMAMOSI HII, BAADA YA KUMALIZA MGOMO.


Spain's professional football league (LFP) and players' union (AFE) have reached an agreement to end the strike which saw the first round of Primera and Segunda Division matches called off last weekend.

Following the seventh meeting between the two parties on Thursday, an accord has finally been reached and this weekend's games will go ahead as normal, with last week's matches to be rescheduled for a later date, thought to be in May or June.

The AFE, who represent the top-two tiers of football in Spain, called the strike on August 11, after their demand that clubs pay players any outstanding monies, later revealed to be around €50 million and affecting almost 200 footballers, proved futile.

However, a sixth meeting on Wednesday was arguably the most significant en route to an agreement being found, as crucial progress was made during a 12-hour exchange, which ended at 05:30 CET. The following meeting at 10:30 CET on Thursday subsequently clinched the deal.

Both parties will give a joint press conference in due course to explain details of the agreement, which sees Spanish football restarting on Friday, as Segunda Division oufits Girona and Elche play out the curtain-raiser.

Thursday, August 25, 2011

POULSEN ATAJA KIKOSI CHA KUIVAA ALGERIA.


Jan Poulsen, Kocha Mkuu Taifa Stars.

DAR ES SALAAM, Tanzania
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi ya mchujo dhidi ya Algeria ‘Desert Warriors’ kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon
.
Wachezaji walioitwa ni makipa Shabani Dihile (JKT Ruvu Stars), Juma Kaseja (Simba) na Shabani Kado (Yanga). Mabeki wa pembeni ni nahodha Shadrack Nsajigwa (Yanga), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya) na Amir Maftah (Simba). Mabeki wa kati ni Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba) na Victor Costa (Simba).

Viungo wakabaji ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Juma Seif (Yanga) na Jabir Aziz (Azam). Viungo washambuliaji ni Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam) na Salum Machaku (Simba).

Washambuliaji ni Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Ramadhan Chombo (Azam), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden) na John Bocco (Azam).

Timu itaingia kambini Jumapili (Agosti 28 mwaka huu) mchana na jioni itaanza mazoezi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Mechi dhidi ya Algeria itachezwa Septemba 3 mwaka huu kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

UEFA Champions League Draw 2011/2012- HD 1080p

UEFA CHAMPIONS LEAGUE DRAW.


GROUP A 
Bayern Munich
Villarreal
Manchester City
Napoli

GROUP B
Inter Milan
CSKA Moscow
Lille
Trabzonspor

GROUP C 
Manchester United
Benfica
Basle
Otelul Galati

GROUP D 
Real Madrid
Lyon
Ajax
Dinamo Zagreb

GROUP E 
Chelsea
Valencia
Bayer Leverkusen
Genk

GROUP F 
Arsenal
Marseille
Olympiakos
Borussia Dortmund

GROUP G 
Porto
Shakhtar Donetsk
Zenit St Petersburg
APOEL

GROUP H 
Barcelona
AC Milan
BATE
Viktoria Plzen

Udinese Vs Arsenal 1-2 | UEFA Champions League Full Match Highlights & G...

Tuesday, August 23, 2011

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF.


RATIBA YA LIGI KUU MZUNGUKO WA KWANZA
BAADA ya Serikali kuufunga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa ajili ya marekebisho, Yanga na Simba ambazo awali zilikuwa zimeruhusiwa kutumia uwanja huo kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom zililazimika kutafuta viwanja vipya. Simba imehamia Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakati Yanga iko Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro.

Licha ya timu hizo kupata viwanja vipya ratiba itabaki kama ilivyotolewa awali. Mechi za Simba zilizokuwa zichezwe Uwanja wa Taifa sasa zitachezwa Mkwakwani wakati za Yanga zitachezwa Jamhuri. Kutokana na mabadiliko hayo ratiba inasomeka kuwa Septemba 7 mwaka huu Coastal Union v Moro United (Mkwakwani) na pia Simba v Villa Squad (Mkwakwani). Mechi ya Simba v Villa Squad imesogezwa mbele kwa siku moja ambapo sasa itachezwa Septemba 8 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.

MCHEZAJI CASTORY MUMBARA
TFF imeshindwa kumpa leseni Castory Mumbara ambaye ameombewa usajili katika timu ya Toto Africans kutokana na kutokuwa na Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) ambayo inatakiwa kutolewa kupitia mfumo wa mtandao wa Transfer Matching System (TMS).

Ikumbukwe kuwa Mumbara alikuwa akichezea timu ya Himalayan Sharpa ya Nepal ambapo alikwenda huko baada ya TFF kumpatia ITC. Hivyo ili aichezee Toto Africans, klabu hiyo ilipaswa kumuombea hati hiyo kupitia mtandao wa TMS baada ya kufanya mawasiliano na Himalayan Sharpa.

Muda wa usajili ulimalizika Julai 31 mwaka huu, hivyo Toto Africans kwa sasa haiwezi kumtumia mchezaji huyo badala yake inatakiwa kusubiri dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa tena Novemba mwaka huu. TFF iliendesha mafunzo ya kutumia mfumo wa TMS kwa watendaji wote wa klabu za Ligi Kuu ikiwemo Toto Africans.

MECHI YA STARS v ALGERIA
Mechi hiyo namba 103 ya mchujo kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani Equatorial Guinea na Gabon itachezwa nchini Septemba 3 mwaka huu.

Bado tunasubiri majibu ya ombi letu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo la kuturuhusu kutumia Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo.

ALL AFRICA GAMES
Mwamuzi msaidizi John Kanyenye wa Tanzania ni miongoni mwa waamuzi 32 (waamuzi wa kati na wasaidizi) walioteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuchezesha michezo ya All Africa Games itakayofanyika Maputo, Msumbiji kuanzia Septemba 3-18 mwaka huu. Kati ya hao, 16 ni wanaume na 16 ni wanawake.

Kanyenye ni mmoja kati ya waamuzi watatu kutoka  ukanda wa CECAFA- Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati walioteuliwa kuchezesha michezo hiyo. Wengine ni mwamuzi wa kati wa kike kutoka Uganda, Nabikko Ssemambo na mwamuzi msaidizi wa kike kutoka Ethiopia, Trhas Gebreyohanis.

Monday, August 22, 2011

RATIBA YA MZUNGUKO WA KWANZA LIGI KUU TANZANIA BARA.

PICHA ZINAONYESHA MATUKIO MBALIMBALI YA MCHEZO BAINA YA MAN UNITED VS TOTTENHAM USIKU HUU.
RAGE, SENDEU KIKAANGONI.


Ismail Aden Rage, Mwenyekiti wa Simba.

DAR ES SALAAM, Tanzania
SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF) limepeleka mashtaka mbele ya Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi dhidi ya Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage na Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu.

Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Agosti 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam pamoja na mambo mengine iliiagiza Sekretarieti kupeleka mashtaka hayo kutokana na kauli za viongozi hao kabla ya mechi ya Yanga na Simba iliyochezwa Agosti 17 mwaka huu.

Rage alikaririwa na vyombo vya habari kuwa Simba haitapeleka timu uwanjani kama mchezaji wake Gervais Kago kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati hataruhusiwa kucheza, na kuwa ofisa mmoja wa TFF ndiye kikwazo kwa uhamisho wa mchezaji huyo.

Naye Sendeu kupitia vyombo vya habari alikaririwa kuwa Yanga haitaingiza timu uwanjani hadi itakapolipwa sh. milioni 16 inazoidai TFF ingawa deni hilo halikuwa na uhusiano na mechi hiyo ya Ngao ya Jamii.

Luis Sendeu, Ofisa Habari wa Yanga.
Kauli hizo si tu zililenga kuvuruga mechi hiyo kwa kuwachanganya mashabiki, bali zilikuwa za kudhalilisha mchezo wa mpira wa mpira wa miguu.

Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi inayoongozwa na Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) mstaafu Alfred Tibaigana itakuwa na kikao Agosti 28 mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine itajadili mashtaka dhidi ya viongozi hao.

Sunday, August 21, 2011

LIGI KUU YA VODACOM: YANGA YALALA KWA JKT RUVU, SIMBA YAPETA YAIFUNGA JKT OLJORO MABAO 2-1.

Kikosi cha Yanga ambacho jioni hii kimekubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa JKT Ruvu katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

BRAZIL [U20] YATWAA KOMBE LA DUNIA KWA MARA YA TANO.

AZAM YAANZA LIGI VYEMA.


DAR ES SALAAM, Tanzania
BAO pekee la mshambuliaji John Bocco wa Azam FC katika dakika ya 45  limepelekea timu hiyo kuanza vyema mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom VPL kwa kuifunga Moro United 1-0 mchezo uliochezwa leo katika uwanja wa Azam Stadium, Chamazi, Dar es Salaam.

Mchezo huo ni moja kati ya michezo mitano iliyochezwa leo katika ufunguzi wa mechi za ligi kuu kwa msimu huu wa mwaka 2011/2012, Azam FC wameanza vema kwa kuchukua pointi tatu muhimu.

Mchezo wa leo haukuwa mzuri kwa timu zote labda ni kutokana na uoga, timu zote zilicheza kwa kutegeana na kupeleka mashambulizi langoni kwa mwenzake huku kila mchezaji akitafuta nafasi ya kufunga lakini mbinu za kupanga mashambulizi haikuwa murua.

Azam FC walipata goli hilo pekee katika mchezo huo kwa mkwaju wa penati iliyoamuliwa na mwamuzi wa David Paul baada ya walinzi wa Moro United kumwangusha mshambuliaji John Bocco wa Azam FC.

Bocco alipiga penati hiyo iliyomshinda mlinda mlango wa Moro, Lucheke Mussa na kuandika goli kwa Azam FC, goli ambalo lilidumu hadi kumalizika kwa mchezo huo.

Mchezaji Kipre Tchetche kama kawaida yake alisumbua lango la Moro lakini haikuwa bahati yake, huku Ramadhani Chombo alikosa nafasi mbili za wazi kipindi cha kwanza, upande wa Moro mshambuliaji mwenye mwili mkubwa Gaudence Mwaikimbi alikuwa tishio kwa mabeki wa Azam FC ambapo shambulizi lake la dakika ya 27 lililogonga mwamba.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko kuimarisha vikosi vyake Moro waliwatoa Sultani Kasikasi na George Mkoba nafasi zao kuchukuliwa na Jerome Lambele na Bakari Mpakala, Azam FC walifanya mabadiliko kwa kuwarudisha benchi Ibrahim Mwaipopo na Kipre Tcheche na kuwapa nafasi Salum Aboubakar na Khamis Mcha mabadiliko hayo yaliongeza kasi ya mchezo lakini hayakubadili matokeo.

Katika michezo mingine Toto Africa wameifunga Villa Squad 3-0, African Lyon imetoka suluhu na Police Dodoma huku Kagera Sugar waliocheza na Ruvu Shooting na Coastal Union walicheza na Mtibwa Sugar zote zimetoka sare ya 1-1.

Kikosi cha Azam FC kilichofungua pazia la ligi kuu: Obren Cirkovic, Agrey Moris, Erasto Nyoni, Waziri Ally, Said Morad, Mwaipopo/Salum Aboubakar, Abdulhalim Humud,Mrisho Ngassa, John Bocco, Kipre Tchetche/Mcha na Ramadhan Chombo Redondo.

Moro Utd, Lucheka Mussa, Tumba Swed, George Mkoba, Gideon Sepo, Godfrey Wambura, Rajab Zahir, Benedict Ngassa, Salum Telela, Mwaikimba na Sultan Kasikasi.

MATOKEO MENGINE YA MICHEZO ILIYOCHEZWA JANA NI KAMA IFUATAVYO.

COASTAL UNION 1:1 MTIBWA SUGAR

TOTO AFRICANS 3: 0 VILLA SQUARD

POLISI 0: 0 AFRICAN LYON
Saturday, August 20, 2011

FIFA YARUHUSU ITC YA KAGO.


DAR ES SALAAM, Tanzania
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) limeruhusu Shirikisho la Mpira wa Miguu Jamhuri ya Afrika ya Kati kutoa Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Gervais Anold Kago aliyejiunga na timu ya Simba kutoka Olympic Real de Bangui ya huko.

FIFA imeruhusu ITC itolewe baada ya kubaini kuwa Simba ilituma maombi ya kuomba hati hiyo ndani ya muda uliopangwa, lakini CAR ilishindwa kufanyia kazi. Hivyo kinachosubiriwa sasa ni CAR kutuma ITC hiyo.

Licha ya FIFA kuagiza hivyo, TFF imeitaka Simba kukata jina moja kati ya sita ya wachezaji wa kigeni ilionao katika orodha yake. Kanuni ya Ligi Kuu ya Vodacom inaruhusu timu kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi watano.

Wachezaji wa kigeni ambao Simba ina mikataba yao ni Derrick Walulya, Emmanuel Okwi, Felix Sunzu, Gervais Kago, Patrick Mafisango na Jerry Santo.

Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji wakati ikipitia usajili iliagiza kuwa Walulya ambaye Simba ilisema imemuacha ni mchezaji wake kwa vile bado ina mkataba nayo. Hivyo inachotakiwa kufanya Simba ni kuvunja mkataba wa mchezaji mmoja ili kubaki na watano.

AFRICAN LYON KUWALIPA WACHEZAJI KWA MAKATO YA MLANGONI.TIMU ya African Lyon imeomba kuwalipa kwa makato ya mlangoni wachezaji wake wawili wanaoidai; Godfrey Komba na Abdul Masenga ambao ilikatiza mikataba yao msimu uliopita. Awali Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji iliiagiza Lyon kuwalipa wachezaji hao kufikia Agosti 17 mwaka huu vinginevyo isingeruhusiwa kushiriki Ligi Kuu ya Vodacom inayoanza leo (Agosti 20 mwaka huu).

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liliitaka Lyon ithibitishe kwa maandishi kuwa itakatwa kwenye mapato yake ya mlangoni katika mechi hadi deni la wachezaji hao litakapomalizika. Lyon imetekeleza maagizo hayo, hivyo imeruhusiwa kucheza mechi yake ya leo (Agosti 20 mwaka huu) dhidi ya Polisi Dodoma kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Hivyo Lyon itakatwa katika mechi yake ya leo ili kulipa deni hilo. Kama fedha ilizopata katika mgawo hazitatosha kulipa deni hilo itakatwa sehemu iliyobaki katika mechi inayofuata.

Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji katika kikao chake cha Januari 7 mwaka huu chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa kiliiagiza Lyon iwalipe wachezaji hao baada ya kusitisha mikataba yao nje ya taratibu za kimikataba. Masenga na Komba kila mmoja anadai sh. milioni 4.3.

Wachezaji hao wataarifiwa juu ya utaratibu wa malipo yao ambapo TFF ndiyo itakayofanya makato kwa niaba yao.

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF.


MSIMU MPYA LIGI KUU YA VODACOM
Msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom 2011/2012 unaanza kesho (Agosti 20 mwaka huu) ambapo timu 10 kati ya 14 zinazoshiriki katika ligi hiyo zitakuwa viwanjani. Mechi za kesho ni Coastal Union v Mtibwa Sugar (Mkwakwani, Tanga), Kagera Sugar v Ruvu Shooting (Kaitaba, Bukoba), Toto Africans v Villa Squad (Kirumba, Mwanza) na Polisi Dodoma v African Lyon (Jamhuri, Dodoma).

Mechi nyingine ni Azam v Moro United itakayochezwa Chamazi, Dar es Salaam wakati mechi za Jumapili (Agosti 21 mwaka huu) ni Oljoro JKT v Simba (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha), na Yanga watakaokuwa wenyeji wa JKT Ruvu.

WAAMUZI WA KATI
Waamuzi wa kati (centre referees) 16 wameteuliwa kuchezesha Ligi Kuu. Waamuzi hao ni Ronald Swai (Arusha), Isihaka Shirikisho (Tanga), Peter Mujaya (Mwanza), Amon Paul (Mara), Mathew Akrama (Mwanza), Ibrahim Kidiwa (Tanga), Dominic Nyamisana (Dodoma), David Paul (Mtwara), Hashim Abdallah (Dar), Martin Saanya (Morogoro), Orden Mbaga (Dar), Kennedy Mapunda (Dar), Israel Mujuni (Dar), Alex Mahagi (Mwanza), Abdallah Kambuzi (Shinyanga) na Thomas Mkombozi (Kilimanjaro).

Pia wameteuliwa waamuzi wa akiba (reserve referees) sita ambao watatumika wakati wowote watakapohitajika. Waamuzi wasaidizi (assistant referees) walioteuliwa kuchezesha ligi ni 34. Kwa upande wa waamuzi wasaidizi wa akiba walioteuliwa ni kumi. Hivyo jumla ya waamuzi watakaotumika kwenye ligi hiyo ni 50.

MAKAMISHNA WA MECHI
Jumla ya makamishna (match commissioners) 24 wameteuliwa kusimamia mechi za ligi hiyo. Kati ya hao 20 ni wa zamani na wanne ni wapya. Makamishna wapya ni Charles Ndagala, Victor Mwandike, Godbless Kimaro na Hamis Tika.

Makamishna wa msimu uliopita walioteuliwa tena ni Hamis Kissiwa, David Lugenge, Abdallah Mitole, Charles Komba, George Komba, Jimmy Lengwe, Amri Kiula, James Mhagama, Fulgence Novatus, Pius Mashera, Michael Bundara, Gabriel Gunda, Mohamed Nyange, Mwijage Rugakingira, Arthur Mambeta, Paul Opiyo, Edward Hiza, Salim Singano, William Chibura na Omary Mwamela.

Uteuzi wa makamishna kama ilivyo kwa waamuzi ulifanyika baada ya kuhudhuria kozi na kufanya mitihani. Kwa upande wa makamishna ambao hawakufanya vizuri, watalazimika kurudia mitihani kabla ya kuteuliwa tena.

NAULI KWA TIMU ZINAZOSHIRIKI LIGI
Kila timu inayoshiriki ligi itapata jumla ya sh. milioni 26.3. Fedha hizo zitatolewa kwa awamu tano tofauti kuanzia mwezi huu. Agosti kila timu itapata sh. 4,732,142, Septemba (sh. 4,732,142), Oktoba (sh. 5,622,321), Januari (sh. 5,622,321) na Machi (sh. 5,622,321).

Jumla ya fedha kutoka kwa mdhamini wa ligi, Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ambazo zitatumika kwa ajili ya nauli kwa timu zote katika msimu mzima ni sh. 368,637,458.

MECHI YA STARS, ALGERIA
Tumeiandikia barua Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuomba iruhusu mechi ya mchujo ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani Equatorial Guinea na Gabon kati ya Taifa Stars na Algeria (Desert Warriors) ichezwe Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ombi letu limetokana na ukweli kuwa tulishaliarifu Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) miezi mitatu iliyopita kuwa mechi hiyo itachezwa katika uwanja huo. Taarifa hiyo pia tuliipa Algeria ambayo imeshatuma ujumbe wake kukagua hoteli ambayo timu yao itafikia.

Kwa upande wa CAF uamuzi wa kubadili uwanja hivi sasa maana yake kuwa itatupiga faini, lakini vilevile TFF tutalazimika kuingia gharama za kusafirisha kwa ndege timu zote mbili pamoja na waamuzi kwenda Mwanza kwa ajili ya mechi hiyo.

Friday, August 19, 2011

AZAM YAKAMILISHA MECHI ZAKE ZA KIRAFIKI KWA USHINDI.


KIGALI, Rwanda
TIMU ya Soka ya Azam jana ilifanikiwa kuifunga timu ya Ryon Sports ya Rwanda mabao 3-1 katika mfululizo wa michezo ya kirafiki ya timu hiyo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2011/12, mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro, Kigali, Rwanda.
Azam FC ilianza kushambulia tangia dakika ya kwanza ya mchezo na katika dakika ya 17, faulo ya kiufundi ya Ibrahim Mwaipopo iligonga mwamba.

Azam FC ilipata goli lake la kwanza katika dakika ya 43 baada ya Wahab Yahaya kufunga baada ya kupokea pasi ya kipre Tchetche ambaye naye alipokea krosi ya nahodha Ibrahim Shikanda.

Goli la pili la Azam FC lilifunga katika dakika ya 55 kufuatia kazi nzuri ya Ibrahim Mwaipopo ambaye aliipangua ngome ya Ryon kabla ya kutoa pasi nzuri kwa Kipre Tchetche ambaye naye alimchambua golikipa wa Ryon na kufunga kirahisi.

Baada ya hapo Azam FC ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Kipre Tchetche ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Himid Mao, Wahab Yahya ambaye alimpisha Khamis Mcha Viali, Ibrahim Mwaipopo ambaye alimpisha Jabir Aziz, Ramadhan Chombo ambaye alimpisha Salum Abubakar na Nafiu Awudu ambaye alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Said Morrad.

Azam FC iliandika goli la tatu katika dakika ya 65 baada ya gonga nzuri upande wa kushoto na mpira kumkuta Mrisho Ngasa ambaye alitoa pasi upande wa kushoto na mpira kumkuta Khamis Mcha ambaye alifunga kuifundi mkubwa na kufanya uwanja kusisimka. Kwa kufunga tena leo, Mcha kafikisha magoli nane katika mechi nane za kirafiki magoli matano kati ya hayo kayafunga Uganda na Rwanda dhidi ya timu kubwa zenye heshma kubwa Afrika Mashariki.

Ryon Sports walipata goli lao la kufutia machozi  katika dakika ya 70 lakini baada ya kufunga goli hilo hawakuonekana kuwa na uwezo wa kukabiliana na Azam FC ambayo imeacha gumzo hapa Kigali.

Azam FC, Obren, Shikanda/Erasto, Waziri, Aggrey, Nafiu/Morrad, Humud, Ngasa, Mwaipopo/Jabir, Wahab/Mcha, Redondo/Sureboy, Kipre/Himid

OWINO KUJIUNGA NA AZAM FC DIRISHA DOGO.


BEKI wa kimataifa wa Uganda Cranes Joseph Owino amejiunga rasmi na Azam Fc kwa ada ya uhamisho wa dola za kimarekani 30,000.

Owino ambaye msimu uliopita alikuwa akiitumikia Simba Sports Club kabla ya kupata majeraha ya goti yaliyomweka nje ya uwanja kwa msimu wote uliopita na mwishowe aliachwa na Simba katika usajili wa msimu huu.

Beki huyo ambaye kwa sasa anaendelea vizuri na majeraha yake ya goti baada ya kuachwa na Simba, matajiri wa Vodacom Premier League Azam FC waliamua kumchukua na kumpeleka nchini India kwa ajili ya matibabu yaliyogharimu kiasi cha pesa kinachofikia dola 15,000 na baadae wakamsainisha mkataba wa miaka 3 wenye thamani ya $30,000.

Owino anatarajiwa kujiunga rasmi na Azam na kuanza kuitumikia klabu hiyo mwezi January mwakani wakati wa dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa.

FOOTBALLERS ON TWITTER TODAY.


"Very happy for being called up, surely this is one of the best days of my life, I would like to thank all the support messages!"

Porto striker Hulk was delighted to have returned to Brazil's plans after being omitted from the side since February. (http://twitter.com/OficialHulk)

"Veeeery happy to have been called up by Mano! Thank you God for this accomplishment! There is no better feeling! #joyjoy"

Santos midfielder Danilo was thrilled to have earned his first-ever senior call up with Brazil. (http://twitter.com/daaniloluiz)

"crazy Clasico yesterday...just saw a few highlights. now that is what i call rivalry"

Villarreal's Giuseppe Rossi was surprised with the unsavoury scenes that marked the Supercopa. (http://twitter.com/GiuseppeRossi22)

"hey Guys long time ago... i just want to say that i'm very happy to be a blue :-).. First of all thank you all Anderlecht fans. You're awesome! And to The Chelsea fans one thing. We're going to be succesfull! Take care :)"

Chelsea's newest signing Romelu Lukaku expressed his delight at joining Chelsea and stated he aims high at Stamford Bridge. (http://twitter.com/romelulukaku)

Thursday, August 18, 2011

MECHI YA STARS NA ALGERIA KUCHEZWA MWANZA.


DAR ES SALAAM, Tanzania
MECHI ya mchujo ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon katika ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Algeria (Desert Warriors) itachezwa Septemba 3 mwaka huu jijini Mwanza.

Awali tulipanga mechi hiyo ichezwe Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Lakini uamuzi wa kuihamishia Mwanza umefanyika baada ya jana kupata barua kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ikitufahamisha kuwa Uwanja wa Taifa hautatumika tena kwa sasa. Kwa mujibu wa Wizara, uwanja huo utakuwa katika matengenezo baada ya kuharibika wakati wa michuano ya Kombe la Kagame iliyofanyika mwanzoni mwa mwezi uliopita.

YANGA, SIMBA NAZO KUATHIRIKA
Uamuzi huo wa uwanja kufungwa kwa ajili ya matengenezo pia umeziathiri klabu za Yanga na Simba ambazo zilikuwa zimekubaliwa timu zao zitumie kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom ambayo inaanza kutimua vumbi Agosti 20 mwaka huu.

Tayari leo (Agosti 18 mwaka huu) tumeziandikia rasmi klabu za Simba na Yanga kuzifahamisha kuhusu uamuzi huo wa Wizara, hivyo kuzitaka zitafute viwanja vingine kwa ajili ya mechi zao za ligi.

Hatua hiyo ya uwanja kufungwa, itailazimisha TFF ifanye mabadiliko kwenye ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom kwa kuzingatia viwanja ambavyo klabu za Yanga na Simba zitakuwa zimeamua kuvitumia.

Mabadiliko hayo pia yataziathiri timu za African Lyon, Azam, JKT Ruvu, Moro United na Villa Squad ambazo licha ya kutumia Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam, zilipanga mechi zao za nyumbani dhidi ya Simba na Yanga zichezwe Uwanja wa Taifa.

Kwa sasa msimamo wa wamiliki wa Uwanja wa Azam ni Yanga na Simba kutoutumia kwa vile uwezo wake wa kuchukua watazamaji ni mdogo.

FAINALI WORLD CUP UNDER 20 NI BARZIL VS PORTUGAL.


                                                                          VS


Brazil vs Mexico 2-0 All Goals & Full Highlights Semifinal U20 World Cup...

France Vs Portugal (0-2) (U20) - All Goals And Highlights

Wednesday, August 17, 2011

BARCA YAENDELEZA UTEJA KWA MADRID YAINYUKA 3-2 (AGG. 5-4) NA KUNYAKUWA SUPERCOPA.

SIMBA YATWAA NGAO YA JAMII (COMMUNITY SHIELD) KWA KUIFUNGA YANGA 2-0.

Nahodha wa Simba Juma Kaseja akinyanyua juu Ngao ya Jamii walioinyakuwa baada ya kuifunga Yanga mabao 2-0 ikiwa ndio mchezo wa uzinduki wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, usiku huu. 

Kiungo wa Simba Haruna Moshi "Boban" akiwa anagaagaa chini baada ya kukwatuliwa katika mchezo huo.

Vijana wa huduma ya kwanza Red Cross wakiwa wamembeba Boban kumpeleka nje ili akapatiwe matibabu baada ya kuumia.

Sehemu ya Mashabiki wa simba wakiwa wanashangilia baada ya timu kushinda.

Kikosi cha Simba .

Kikosi cha Yanga.

Tuesday, August 16, 2011

TFF YAUFYATA MKIA KWA SIMBA KUHUSU SUALA LA KAGO.


DAR ES SALAAM, Tanzania
SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF) limeruhusu mchezaji Gervais Arnold Kago kutoka klabu ya Olympic Real de Bangui ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) kuichezea timu ya Simba katika mchezo wa wa ngao ya jamii dhidi ya Yanga unaotarajiwa kupigwa kesho katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za wachezaji, Alex Mgongolwa alisema wamemruhusu mchezaji huyo huswa ikizingatiwa mchezo wa Ngao Jamii sio mchezo wa mashindano ni wakuzindua msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Alisema Simba imeingia mkataba na mchezaji huyo kwa ajili ya kuichezea timu hiyo kwenye ligi kuu na michuano ya kimataifa hivyo mchezaji huyo itabidi apate Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kupitia mfumo wa Transfer Matching System (TMS) ili aweze kushiriki ligi kuu na mashindano ya kimataifa.

Alisema ni ukweli kuwa Simba imeingia mkataba na Kago kama mchezaji wa kulipwa ambaye uhamisho wake ni lazima ufanywe kwa TMS na si ITC ya karatasi ambayo inatumika kwa wachezaji wa ridhaa.Mgongolwa alisema kwa mujibu wa Ibara ya 2(2) ya Kanuni za Uhamisho wa Wachezaji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), mchezaji wa kulipwa ni yule ambaye ana mkataba wa maandishi na klabu na analipwa kutokana na shughuli ya kucheza mpira.
 
Alisema pia si kweli kuwa CAR hawamo kwenye TMS. Nchi hiyo inatumia mfumo huo wa mtandao na Meneja wao wa TMS ni Elie-Delphin Feidangamo.
 
Alisema kwa mujibu wa annexe 3(5) ya Kanuni hizo za FIFA kuhusu uhamisho wa wachezaji, utumiaji wa mfumo wa TMS kwa uhamisho wa wachezaji wa kiume wa kimataifa ni lazima.

Monday, August 15, 2011

MAN CITY YAIKARIBISHA SWANSEA LIGI KUU KWA KIPIGO.

Arsene Wenger Interview for Cesc Fabregas leaves Gunners .mp4

Cesc Fabregas Signs for Barcelona: Exclusive Interview 15/08/2011

Cesc Fabregas Signs for Barcelona: Exclusive Interview 15/08/2011

Cesc Fabregas Unveiled As A Barcelona Player Today-- Kissing the badge

YANGA KIKAANGONI FIFA.


DAR ES SALAAM, Tanzania
KLABU ya soka ya Yanga imetumiwa barua ya kujileza kutoka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuhusu sakata la aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo John Njoroge.

Barua hiyo imekuja kufuatia mchezaji huyo kuishitaki Yanga FIFA kutokana na kusitisha mkataba wake bila kumlipa malipo yake mpaka leo.

John Njoroge.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile osiah alisema tayari shirikisho hilo limeshaiandikia Yanga barua pamoja na kuambatanisha kopi iliyottumwa na FIFA.

Alisema Yanga inatakiwa kuijibu FIFA sababu za kutomlipa mchezaji huyo na kama haitafanya hivyo hatua kali dhidi yao itachukuliwa na shirikisho hilo la dunia.

KUZIONA SIMBA NA YANGA NGAO YA JAMII SHS. 5,000, TFF YAMKOMALIA KAGO.


Angetile Osiah, Katibu Mkuu TFF.

DAR ES SALAAM, Tanzania
SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Ngao ya Jamii (Community Shield) utakaowakutanisha watani wa jadi Simba na Yanga Agosti 17 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema maandalizi yote kwa ajili ya mchezo huo ambao umedhaminiwa na Kampuni ya Mafuta ya Big Bon tayari yamekamilika.

Alisema katika mchezo huo viingilio vya juu kabisa yaani VIP A kitakuwa ni shilingi 50,000 wakati kiingilio cha chini kabisa jukwaa la viti vya bluu (Blue Stand) kitakuwa shilingi 5,000, viingilio vingine katika mchezo huo vitakuwa ni VIP B shs. 25,000, VIP C shs. 20,000, viti vya rangi ya chungwa mzunguko (Orange Curve) shs. 10,000 na viti vya rangi ya kijani (Green Stand) shs. 7,000.

Alisema ulinzi kwa ajili ya mchezo huo ambao utachezwa majira ya saa mbili za usiku utakuwepo ndani na nje ya uwanja katika kipindi chote cha mchezo na baada ya mchezo hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kuja kushuhudia mchezo huo pasipo hofu yoyote.

Wakati huohuo TFF imesema inasikitishwa na tuhuma anazotupiwa Mkurugenzi wa Mashindano wa shirikisho hilo Sadi Kawemba kwamba ndiye aliyemzuia mchezaji Kago wa Simba asipitishwe kuichezea timu hiyo katika mechi hiyo ya ngao ya jamii.

Angetile alisema mkataba Simba waliompa mchezaji huyo unaonyesha kuwa mchezaji huyo ni wa kulipwa tofauti na barua walioiwasilisha TFF kuwa wamemsajili mchezaji huyo kama wa ridhaa.

Alisema walichotakiwa kufanya kuja kwao (TFF) ili wapewe maelekezo na taratibu za kufuata na kufanya kama walivyofanya kutoka tuhuma ambazo hazina msingi wowote.