Friday, August 19, 2011
AZAM YAKAMILISHA MECHI ZAKE ZA KIRAFIKI KWA USHINDI.
KIGALI, Rwanda
TIMU ya Soka ya Azam jana ilifanikiwa kuifunga timu ya Ryon Sports ya Rwanda mabao 3-1 katika mfululizo wa michezo ya kirafiki ya timu hiyo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2011/12, mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro, Kigali, Rwanda.
Azam FC ilianza kushambulia tangia dakika ya kwanza ya mchezo na katika dakika ya 17, faulo ya kiufundi ya Ibrahim Mwaipopo iligonga mwamba.
Azam FC ilipata goli lake la kwanza katika dakika ya 43 baada ya Wahab Yahaya kufunga baada ya kupokea pasi ya kipre Tchetche ambaye naye alipokea krosi ya nahodha Ibrahim Shikanda.
Goli la pili la Azam FC lilifunga katika dakika ya 55 kufuatia kazi nzuri ya Ibrahim Mwaipopo ambaye aliipangua ngome ya Ryon kabla ya kutoa pasi nzuri kwa Kipre Tchetche ambaye naye alimchambua golikipa wa Ryon na kufunga kirahisi.
Baada ya hapo Azam FC ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Kipre Tchetche ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Himid Mao, Wahab Yahya ambaye alimpisha Khamis Mcha Viali, Ibrahim Mwaipopo ambaye alimpisha Jabir Aziz, Ramadhan Chombo ambaye alimpisha Salum Abubakar na Nafiu Awudu ambaye alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Said Morrad.
Azam FC iliandika goli la tatu katika dakika ya 65 baada ya gonga nzuri upande wa kushoto na mpira kumkuta Mrisho Ngasa ambaye alitoa pasi upande wa kushoto na mpira kumkuta Khamis Mcha ambaye alifunga kuifundi mkubwa na kufanya uwanja kusisimka. Kwa kufunga tena leo, Mcha kafikisha magoli nane katika mechi nane za kirafiki magoli matano kati ya hayo kayafunga Uganda na Rwanda dhidi ya timu kubwa zenye heshma kubwa Afrika Mashariki.
Ryon Sports walipata goli lao la kufutia machozi katika dakika ya 70 lakini baada ya kufunga goli hilo hawakuonekana kuwa na uwezo wa kukabiliana na Azam FC ambayo imeacha gumzo hapa Kigali.
Azam FC, Obren, Shikanda/Erasto, Waziri, Aggrey, Nafiu/Morrad, Humud, Ngasa, Mwaipopo/Jabir, Wahab/Mcha, Redondo/Sureboy, Kipre/Himid
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment