Friday, August 25, 2017

RATIBA YA MAKUNDI YA EUROPA LEAGUE

Kundi A: Villarreal, Maccabi Tel Aviv, Astana, Slavia Prague.
Kundi B: Dynamo Kiev, Young Boys, Partizan Belgrade, Skenderbeu.
Kundi C: Sporting Braga, Ludogorets, Hoffenheim, Istanbul Basaksehir.
Kundi D: AC Milan, Austria Vienna , Rijeka, AEK Athens.
Kundi E: Lyon, Everton, Atalanta, Apollon Limassol.
kundi F: FC Copenhagen, Lokomotiv Moscow, Sheriff Tiraspol, FC Zlin.
Kundi G: Vitoria Plzen, Steaua Bucarest, Hapoel Beer-Sheva, FC Lugano.
Kundi H:Arsenal, BATE Borisov, Cologne, Red Star Belgrade.
Kundi I: Salzburg, Marseille, Vitoria Guimaraes, Konyaspor.
Kundi J: Athletic Bilbao, Hertha Berlin, Zorya Luhansk, Ostersund.
Kundi K: Lazio, Nice, Zulte Waregem, Vitesse Arnhem.
Kundi L: Zenit St Petersburg, Real Sociedad, Rosenborg, Vardar.

RATIBA YA MAKUNDI YA CHAMPIONS LEAGUE

Kundi A: Benfica, Manchester United, Basel, CSKA Moscow
Kundi B: Bayern Munich, Paris St-Germain, Anderlecht, Celtic
Kundi C: Chelsea, Atletico Madrid, Roma, Qarabag
Kundi D: Juventus, Barcelona, Olympiakos, Sporting
Kundi E: Spartak Moscow, Sevilla, Liverpool, Maribor
Kundi F: Shakhtar Donetsk, Manchester City, Napoli, Feyenoord
Kundi G: Monaco, Porto, Besiktas, RB Leipzig
Kundi H: Real Madrid, Borussia Dortmund, Tottenham, Apoel

LIVERPOOL YAMNYATIA SANCHEZ

KLABU ya Liverpool inadaiwa kujiandaa kumuwania kiungo wa Bayern Munich Renato Sanchez. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno ambaye alitua Allianz Arena majira ya kiangazi mwaka jana, anataka kutafuta timu atakayopata nafasi ya kucheza mara kwa mara na meneja Jurgen Klopp yuko tayari kufanikisha suala hilo. Sanchez ambaye alijizolea umaarufu mkubwa kutokana na kiwnago bora alichoonyesha katika michuano ya Ulaya akiwa na kikosi cha ushindi cha Ureno kiangazi mwaka jana, kwa kipindi kirefu amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwaniwa na Manchester United. Bayern wanaweza kukubali kumuacha kwa mkopo kiungo huyo kwani bado wanamuhitaji nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 kwa siku zijazo.

SPURS YAKARIBIA KUMNASA AURIER.

KLABU ya Tottenham Hotspurs inadaiwa kukubali kumsajili Serge Aurier kutoka Paris Saint-Germain-PSG kwa kitita cha paundi milioni 23 na beki huyo amefanyiwa vipimo vya afya jijini Paris. Lakini usajili wa beki huyo wa kimataifa wa Ivory Coast hautakamilika mpaka Aurier atakapopata kiali cha kufanya kazi Uingereza. Mabingwa Serie A Juventus bado wanamtaka beki huyo kwa mkopo kama akishindwa kuhamia Ligi Kuu. Nyota huyo wa PSG alinyimwa visa ya kuingia Uingereza kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal Novemba mwaka jana kwasababu ya kuhukumiwa kwa kosa la kumshambulia polisi. Mawakili wake wanafanya kazi kutafuta suluhu la suala hilo ambalo ndio lilichangia Chelsea na Manchester United kuacha kuwania saini yake.

WEST BROM WANASA WINGA WA RB LEIPZIG.

KLABU ya West Bromwich Albion imemsajili winga wa kimataifa wa Scotland Oliver Burke kutoka RB Leipzig ya Ujerumani kwa kitita cha paundi milioni 15 na kumpa mkataba wa miaka mitano. Burke mwenye umri wa miaka 20, alikuwa mchezaji ghali zaidi kutoka Scotland wakati alipojiunga na klabu hiyo ya Bundesliga kwa kitita cha paundi milioni 13 Agosti mwaka 2016. Winga huyo amecheza mechi 25 za ligi msimu uliopita na kuisaidia Leipzig kufuzu makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Akizungumza na wanahabari baada ya uhamisho huo, Burke amesema anadhani sasa ni wakati wake wa kucheza mechi nyingi zaidi. Burke ambaye anaweza kuanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stoke City Jumapili hii, anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na West Brom kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

DORTMUND YAKANUSHA KUMALIZANA NA BARCELONA

KLABU ya Borussia Dortmund imedai mapema leo kuwa hakuna makubaliano yeyote yaliyofikiwa kwa ajili ya uhamisho wa Ousmane Dembele kwenda Barcelona. Kauli hiyo ya Dortmund inakuja kufuatia taarifa kutoka nchini Ujerumani kudai kuwa tayari makubaliano baina ya pande hizo kwa ajili ya Dembele yamekamilika. Akizungumza na wanahabari, msemaji wa Dortmund amesema wamewapa muda Barcelona hivyo kuna kitu kinaweza kikatokea au kisitokee pia. Taarifa zingine zinadai kuwa Barcelona imekubali kutoa kitita cha euro milioni 120 hivuo kumfanya kuwa mchezaji wa pili ghali zaidi duniani baada ya Neymar.

Monday, August 21, 2017

BARCELONA KUMGEUKIA DI MARIA WAKIMSHINDWA COUTINHO

KLABU ya Barcelona inatarajiwa kugeukia kwa Angel Di Maria kama wakishindwa kumsajili Philippe Coutinho kutoka Liverpool. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Catalan zimedai kuwa nafasi ya Barcelona kumsajili kiungo huyo wa Brazil imekuwa finyu hivyo kuna uwezekano klabu hiyo ikaamua kuachana naye. Kutokana na hilo Barcelona sasa inaweza kuhamishia nguvu zao kwa Di Maria ili waimarishe kikosi chao. Katika hatua nyingine, Afisa mkuu wa Borussia Dortmund, Hans-Joachim Watzke amedai kuwa nafasi ya Ousmane Dembele kujiunga na Barcelona ni chini ya asilimia 50. Watzke aliwaambia wanahabari kuwa kama Barcelona wanamtaka Osmane lazima walipe ada wanayotaka kwakuwa mchezaji huyo bado ana mkataba wa miaka minne.

ARSENAL HUENDA IKAMUUZA MUSTAFI

KLABU ya Arsenal inadaiwa kukataa ya mkopo kutoka Inter Milan kwa ajili ya beki wake wa kimataifa wa Ujerumani Shkodran Mustafi wiki iliyopita. Hata hivyo taarifa zinadai kuwa Arsenal wanaweza kukubali kumuuza beki huyo kama Inter wataweza kutoa kiasi cha milioni 35 ambacho walilipa wakati walimnyakuwa kutoka Valencia kiangazi mwaka jana. Mustafi amekuwa akipata kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal lakini amekuwa akipata tabu kidogo kuelewana na wachezaji wenzake hatua ambayo inaweza kupelekea suala la kuuzwa liwezekane. Kama Arsenal ikiamua kumuuza nyota huyo mwenye umri wa miaka 25, italazimika kutafuta mbadala wake ili kuimarisha safu yao ya ulinzi.

WEST BROM WAIKATIA RUFANI KADI NYEKUNDU YA ROBSON-KANU

KLABU ya West Bromwich Albion imekata rufani dhidi ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa Hal Robson-Kanu katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Burnley kwenye mchezo wa Ligi Kuu jana. Mshambuliaji huyo alitolewa nje dakika za mwishoni kufuatia kumchezea hovyo beki wa Burnley Matthew Lowton. Robson-Kanu ndiye aliyefunga bao pekee kwenye mchezo huo na kuifanya West Brom kuanza vyema mechi zao mbili za mwanzo za ligi. Taarifa ya West Brom imedai kuwa watatuma malalamiko yao kutokana na uamuzi huo kwenda Shirikisho la Soka la Uingereza-FA.

NEYMAR AWASHAMBULIA VIONGOZI WA BARCELONA

MSHAMBULIAJI wa Paris Saint-Germain-PSG, Neymar amewaponda wakurugenzi wa klabu yake ya zamani na kudai kuwa Barcelona inastahili viongozi bora zaidi yao. Akizungumza na wanahabari mara baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 6-2 waliopata PSG dhidi ya Toulouse, Neymar amesema viongozi wa Barcelona waliopo madarakani hawastahili kuwepo hapo. Neymar aliandelea kudai kuwa amekaa Barcelona kwa miaka minne na amekuwa na furaha wakati wote lakini sio kwa viongozi wa klabu hiyo. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil amesema Barcelona inastahili uongozi bora zaidi na dunia nzima inafahamu hilo.

Friday, August 18, 2017

LIVERPOOL YAKATAA OFA YA TATU YA BARCELONA KWA COUTINHO

KLABU ya Liverpool imekataa ofa ya tatu kutoka Barcelona inayoamikika kufikia paundi milioni 114 kwa ajili ya Philippe Coutinho. Wiki iliyopita Liverpool walikataa ofa ya paundi milioni 90 kutoka kwa klabu hiyo ya La Liga ambapo baadaye nyota huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 alituma maombi ya kuondoka. Coutinho amekosa mechi mbili za ufunguzi za Liverpool msimu huu kutokana na majeruhi ya mgongo, lakini klabu hiyo imeshaweka wazi nia yake kutotaka kumuuza kiungo huyo. Pamoja na kauli hiyo ya Liverpool, Barcelona bado wamekuwa wakidai kuwa wanakaribia kunasa saini ya kiungo huyo.

COSTA AENDELEA KUTOA POVU SAKATA LAKE NA CHELSEA

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Hispania, Diego Costa amesema Chelsea wanataka kiasi ambacho Atletico Madrid hawataweza kukitoa kwa ajili ya kumalisha usajili wake wa kurejea kwenye klabu yake hiyo ya zamani.  Conte mwenye umri wa miaka 28 bado yuko nchini Brazil baada ya kutumia ujumbe mfupi Juni mwaka huu na meneja Antonio Conte akimwambia kuwa hatakuwepo katika mipango yake msimu huu. Chelsea walimsajili Costa kutoka Atletico kwa kitita cha paundi milioni 32 Julai mwaka 2014. Akizungumza na wanahabari huko Brasil, Costa amesema wakati alipokwenda Chelsea walilipa kiasi kidogo kulinganisha na wanachopewa hivi sasa. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa anaona kama Chelsea wanamkomoa kwa kudai kiasi kikubwa cha fedha ili Atletico washindwe kumsajili jambo ambalo anaona sio sawa kwakuwa klabu hiyo imeshaweka wazi kuwa hawamuhitaji.

WEST BROM YAIWEKEA MTEGO MAN CITY KWA EVANS

MENEJA wa West Bromwich Albion, Tony Pulis, amesema klabu hiyo haina haja kumuuza nahodha wake Jonny Evans lakini mchezaji yeyote anaweza kuuzwa kama ofa muafaka ikitolewa. Kauli ya Pulis inakuja kufuatia West Brom kukataa ofa ya paundi milioni 18 kutoka Manchester City kwa ajili ya beki huyo mwenye umri wa miaka 29 ambaye amebakisha miaka miwili katika mkataba wake. Pulis amesema litakuwa jambo la ajabu kusema kuwa klabu hiyo haitauza mchezaji kama fedha nyingi ikitolewa. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa pamoja na kwamba hawana shida sana na fedha lakini ofa nzuri zikija mezani wanaweza kuzijadili.

FINIDI GEORGE ATAFUTA KIBARUA NFF.

NGULI wa zamani wa soka wa kimataifa wa Nigeria, Finidi George ni miongoni mwa makocha 59 walioitwa kwenye usajili na Shirikisho la Soka la nchi hiy0-NFF kwa ajili ya kuziba nafasi mbalimbali kwenye timu za taifa. NFF ilithibitisha kuwa Finidi anatarajiwa kufanyiwa usaili huo Jumanne ijayo chini ya jopo la shirikisho hilo litakalokutana jijini Abuja. Haikuwekwa wazi ni nafasi gani haswa ambayo Finidi ameomba NFF, kwani nafasi zilizopo ni nyingi ikiwemo kocha wa timu za taifa za vijana chini ya 17, 20 na 23, makocha wasaidizi na makocha wa makipa. Finidi amekuwa akifanya kazi kama kocha wa timu ya vijana ya umri wa miaka 16 ya klabu ya Real Mallorca na ana leseni daraja A inayotambuliwa na Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA.

SPURS YAKARIBIA KUFANYA USAJILI WAKE WA KWANZA

KLABU ya Tottenham Hotspurs inadaiwa kukaribia kukamilisha usajili wake wa kwanza kipindi hiki cha majira ya kiangazi baada ya kukubali dili la kumsajili beki wa kati wa Ajax Amsterdam Davinson Sanchez. Spurs inatarajia kuvunja rekodi yao kwa kutoa kitita cha paundi milioni 42 kwa ajili ya chipukizi huyo mwneye umri wa miaka 21, ambaye amefunga mabao sita kwenye mechi 32 alizoichezea Ajax msimu uliopita na kupewa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa klabu. Kama Spurs wakifanikiwa kumsajili watakuwa wamewatuliza mashabiki wao ambao walikuwa na wasiwasi kufuatia kuona juhudi zozote za usajili zinazofanyika. Spurs ambao walimaliza nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu msimu uliopita, ndio timu pekee ambayo haijafanya usajili mpaka sasa.

RONALDO NA MESSI WATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA TUKIO LA BARCELONA

WACHEZAJI nyota wa soka, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wameungana na nyota wenzao duniani kote kulaani shambulio la kigaidi lililotokea jijini Barcelona na kusababisha vifo vya watu 13. Mtaa maarufu wa Las Ramblas uliopo Barcelona ulikumbwa na simanzi kufuatia gari kugonga umati wa watu wengi wao wakiwa watalii. Messi mwenye umri wa miaka 30 aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kukemea tukio hilo na kuzipa pole familia za wahanga. Kwa upande wake Ronaldo yeye alituma salamu zake za rambirambi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kwenda kwa familia za waathirika. Klabu zote za La Liga na ligi daraja la pili nchini humo zinatarajiwa kukaa kimya kwa dakika moja kuwakumbuka wahanga wa tukio wakati msimu mpya ligi utakapoanza baadae leo.

Friday, August 4, 2017

COSAFA WAIPA TAIFA STARS ZAWADI ZAO

BARAZA la Mpira wa Miguu kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (Cosafa), limetoa zawadi ya dola 10,000 kwa Taifa Stars ya Tanzania baada ya kushinda na kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya Castle Cosafa yaliyofanyika mwezi uliopita nchini Afrika Kusini. Fedha hizo ni sawa na Sh. 22,000,000 ambako Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeamua fedha hizo kwa mgawanyo sawa, zitolewe kwa wachezaji wote walioshiriki fainali hizo pamoja na benchi la ufundi. Kadhalika Cosafa limetuma fedha za zawadi kwa wachezaji wa Tanzania ambao walifanya vema kwenye mchezo mmoja baada ya mwingine katika mashindano hayo ambayo yalikuwa na mvutio wa aina yake kwa mafanikio ya timu ya Tanzania. Wachezaji hao ni Shiza Kichuya aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Malawi; Muzamiru Yassin aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Angola; Erasto Nyoni aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Mauritius; Elius Maguri aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Afrika Kusini. Kipa Bora wa michuano hiyo ni Said Mohammed alyezawadiwa moja kwa moja na Cosafa. Tanzania ilishika nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa Zimbabwe na Zambia iliyoshika nafasi ya pili. Tanzania iliifunga Lesotho na kushika nafasi ya tatu.

MABADILIKO MAKUNDI LIGI DARAJA LA KWANZA TANZANIA BARA 2017/18

BODI ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefanya mabadiliko kidogo ya timu zilizo kwenye makundi ya ‘A’ na ‘B’ katika Ligi Daraja la Kwanza (FDL) Tanzania Bara iliyopangwa kuanza Septemba 16, mwaka huu. Timu ambazo zimefanyiwa mabadiliko ni Polisi Morogoro FC ya Morogoro iliyokuwa kundi ‘A’ sasa itakuwa Kundi ‘B’ wakati Mshikamano FC ya Dar es Salaam iliyokuwa Kundi ‘B’ sasa itacheza mechi mechi zake katika Kundi ‘A’. Kwa msingi huo, makundi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu yenye timu nane kila kund, zitakazochuana msimu huu wa 2017/18 kuwania nafasi tatu muhimu za kupanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2018/19 yatakuwa hivi:- Kundi ‘A’ litakuwa na timu za African Lyon, Ashati United, Friends Rangers, Mshikamano za Dar es Salaam, JKT Ruvu na Kiluvya United za Pwani, Mgambo JKT ya Tanga na Mvuvumwa ya Kigoma. Kundi ‘B’ zitakuwa timu za itakuwa na timu za Coastal Union ya Tanga; JKT Mlale ya Ruvuma; KMC ya Dar es Salam, Mbeya Kwanza ya Mbeya, Mufundi United ya Iringa, Polisi Dar za Dar es Salaam na Polisi Morogoro na Mawezi Market ya Morogoro. Kundi ‘C’ ina timu za Alliance School, Pamba na Toto African za Mwanza, Rihno Rangers ya Tabora, Polisi Mara ya Mara, Polisi Dodoma ya Dodoma, Transit Camp ya Shinyanga na JKT Oljoro ya Arusha.NEYMAR ATUA PARIS, AELEZA SABABU ZILIZOMUONDOA BARCELONA.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Brazil, Neymar amesema alikuwa akihitajia changamoto mpya kufuatia kujiunga na Paris Saint-Germain-PSG akitokea Barcelona kwa kitita kilichovunja rekodi ya dunia cha euro milioni 222 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 573,204,000,000. 
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 ameshinda mataji makubwa saba katika kipindi cha miaka minne aliyokaa Camp Nou, ikiwemo taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mara moja na La Liga mara mbili. Neymar amesema baba yake Naymar Sr alikuwa akimtaka abaki Barcelona. 
Neymar ambaye atakuwa akikunja kitita cha euro milioni 45 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 116,190,000,000 kwa mwaka kwenye mkataba wa miaka mitano, amesema ameshashinda kila kitu mchezaji anachoweza kushinda. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa anachotaka sasa ni changamoto mpya na kwa mara ya pili katika maisha yake amepishana kauli na baba yake.