Friday, August 25, 2017

WEST BROM WANASA WINGA WA RB LEIPZIG.

KLABU ya West Bromwich Albion imemsajili winga wa kimataifa wa Scotland Oliver Burke kutoka RB Leipzig ya Ujerumani kwa kitita cha paundi milioni 15 na kumpa mkataba wa miaka mitano. Burke mwenye umri wa miaka 20, alikuwa mchezaji ghali zaidi kutoka Scotland wakati alipojiunga na klabu hiyo ya Bundesliga kwa kitita cha paundi milioni 13 Agosti mwaka 2016. Winga huyo amecheza mechi 25 za ligi msimu uliopita na kuisaidia Leipzig kufuzu makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Akizungumza na wanahabari baada ya uhamisho huo, Burke amesema anadhani sasa ni wakati wake wa kucheza mechi nyingi zaidi. Burke ambaye anaweza kuanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stoke City Jumapili hii, anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na West Brom kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

No comments:

Post a Comment