Friday, August 25, 2017

SPURS YAKARIBIA KUMNASA AURIER.

KLABU ya Tottenham Hotspurs inadaiwa kukubali kumsajili Serge Aurier kutoka Paris Saint-Germain-PSG kwa kitita cha paundi milioni 23 na beki huyo amefanyiwa vipimo vya afya jijini Paris. Lakini usajili wa beki huyo wa kimataifa wa Ivory Coast hautakamilika mpaka Aurier atakapopata kiali cha kufanya kazi Uingereza. Mabingwa Serie A Juventus bado wanamtaka beki huyo kwa mkopo kama akishindwa kuhamia Ligi Kuu. Nyota huyo wa PSG alinyimwa visa ya kuingia Uingereza kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal Novemba mwaka jana kwasababu ya kuhukumiwa kwa kosa la kumshambulia polisi. Mawakili wake wanafanya kazi kutafuta suluhu la suala hilo ambalo ndio lilichangia Chelsea na Manchester United kuacha kuwania saini yake.

No comments:

Post a Comment