Friday, August 18, 2017

LIVERPOOL YAKATAA OFA YA TATU YA BARCELONA KWA COUTINHO

KLABU ya Liverpool imekataa ofa ya tatu kutoka Barcelona inayoamikika kufikia paundi milioni 114 kwa ajili ya Philippe Coutinho. Wiki iliyopita Liverpool walikataa ofa ya paundi milioni 90 kutoka kwa klabu hiyo ya La Liga ambapo baadaye nyota huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 alituma maombi ya kuondoka. Coutinho amekosa mechi mbili za ufunguzi za Liverpool msimu huu kutokana na majeruhi ya mgongo, lakini klabu hiyo imeshaweka wazi nia yake kutotaka kumuuza kiungo huyo. Pamoja na kauli hiyo ya Liverpool, Barcelona bado wamekuwa wakidai kuwa wanakaribia kunasa saini ya kiungo huyo.

No comments:

Post a Comment