Friday, August 18, 2017

COSTA AENDELEA KUTOA POVU SAKATA LAKE NA CHELSEA

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Hispania, Diego Costa amesema Chelsea wanataka kiasi ambacho Atletico Madrid hawataweza kukitoa kwa ajili ya kumalisha usajili wake wa kurejea kwenye klabu yake hiyo ya zamani.  Conte mwenye umri wa miaka 28 bado yuko nchini Brazil baada ya kutumia ujumbe mfupi Juni mwaka huu na meneja Antonio Conte akimwambia kuwa hatakuwepo katika mipango yake msimu huu. Chelsea walimsajili Costa kutoka Atletico kwa kitita cha paundi milioni 32 Julai mwaka 2014. Akizungumza na wanahabari huko Brasil, Costa amesema wakati alipokwenda Chelsea walilipa kiasi kidogo kulinganisha na wanachopewa hivi sasa. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa anaona kama Chelsea wanamkomoa kwa kudai kiasi kikubwa cha fedha ili Atletico washindwe kumsajili jambo ambalo anaona sio sawa kwakuwa klabu hiyo imeshaweka wazi kuwa hawamuhitaji.

No comments:

Post a Comment