Friday, August 18, 2017

WEST BROM YAIWEKEA MTEGO MAN CITY KWA EVANS

MENEJA wa West Bromwich Albion, Tony Pulis, amesema klabu hiyo haina haja kumuuza nahodha wake Jonny Evans lakini mchezaji yeyote anaweza kuuzwa kama ofa muafaka ikitolewa. Kauli ya Pulis inakuja kufuatia West Brom kukataa ofa ya paundi milioni 18 kutoka Manchester City kwa ajili ya beki huyo mwenye umri wa miaka 29 ambaye amebakisha miaka miwili katika mkataba wake. Pulis amesema litakuwa jambo la ajabu kusema kuwa klabu hiyo haitauza mchezaji kama fedha nyingi ikitolewa. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa pamoja na kwamba hawana shida sana na fedha lakini ofa nzuri zikija mezani wanaweza kuzijadili.

No comments:

Post a Comment