Friday, August 18, 2017

FINIDI GEORGE ATAFUTA KIBARUA NFF.

NGULI wa zamani wa soka wa kimataifa wa Nigeria, Finidi George ni miongoni mwa makocha 59 walioitwa kwenye usajili na Shirikisho la Soka la nchi hiy0-NFF kwa ajili ya kuziba nafasi mbalimbali kwenye timu za taifa. NFF ilithibitisha kuwa Finidi anatarajiwa kufanyiwa usaili huo Jumanne ijayo chini ya jopo la shirikisho hilo litakalokutana jijini Abuja. Haikuwekwa wazi ni nafasi gani haswa ambayo Finidi ameomba NFF, kwani nafasi zilizopo ni nyingi ikiwemo kocha wa timu za taifa za vijana chini ya 17, 20 na 23, makocha wasaidizi na makocha wa makipa. Finidi amekuwa akifanya kazi kama kocha wa timu ya vijana ya umri wa miaka 16 ya klabu ya Real Mallorca na ana leseni daraja A inayotambuliwa na Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA.

No comments:

Post a Comment