Friday, August 18, 2017

SPURS YAKARIBIA KUFANYA USAJILI WAKE WA KWANZA

KLABU ya Tottenham Hotspurs inadaiwa kukaribia kukamilisha usajili wake wa kwanza kipindi hiki cha majira ya kiangazi baada ya kukubali dili la kumsajili beki wa kati wa Ajax Amsterdam Davinson Sanchez. Spurs inatarajia kuvunja rekodi yao kwa kutoa kitita cha paundi milioni 42 kwa ajili ya chipukizi huyo mwneye umri wa miaka 21, ambaye amefunga mabao sita kwenye mechi 32 alizoichezea Ajax msimu uliopita na kupewa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa klabu. Kama Spurs wakifanikiwa kumsajili watakuwa wamewatuliza mashabiki wao ambao walikuwa na wasiwasi kufuatia kuona juhudi zozote za usajili zinazofanyika. Spurs ambao walimaliza nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu msimu uliopita, ndio timu pekee ambayo haijafanya usajili mpaka sasa.

No comments:

Post a Comment