Friday, August 18, 2017

RONALDO NA MESSI WATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA TUKIO LA BARCELONA

WACHEZAJI nyota wa soka, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wameungana na nyota wenzao duniani kote kulaani shambulio la kigaidi lililotokea jijini Barcelona na kusababisha vifo vya watu 13. Mtaa maarufu wa Las Ramblas uliopo Barcelona ulikumbwa na simanzi kufuatia gari kugonga umati wa watu wengi wao wakiwa watalii. Messi mwenye umri wa miaka 30 aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kukemea tukio hilo na kuzipa pole familia za wahanga. Kwa upande wake Ronaldo yeye alituma salamu zake za rambirambi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kwenda kwa familia za waathirika. Klabu zote za La Liga na ligi daraja la pili nchini humo zinatarajiwa kukaa kimya kwa dakika moja kuwakumbuka wahanga wa tukio wakati msimu mpya ligi utakapoanza baadae leo.

No comments:

Post a Comment