Friday, August 4, 2017

NEYMAR ATUA PARIS, AELEZA SABABU ZILIZOMUONDOA BARCELONA.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Brazil, Neymar amesema alikuwa akihitajia changamoto mpya kufuatia kujiunga na Paris Saint-Germain-PSG akitokea Barcelona kwa kitita kilichovunja rekodi ya dunia cha euro milioni 222 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 573,204,000,000. 
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 ameshinda mataji makubwa saba katika kipindi cha miaka minne aliyokaa Camp Nou, ikiwemo taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mara moja na La Liga mara mbili. Neymar amesema baba yake Naymar Sr alikuwa akimtaka abaki Barcelona. 
Neymar ambaye atakuwa akikunja kitita cha euro milioni 45 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 116,190,000,000 kwa mwaka kwenye mkataba wa miaka mitano, amesema ameshashinda kila kitu mchezaji anachoweza kushinda. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa anachotaka sasa ni changamoto mpya na kwa mara ya pili katika maisha yake amepishana kauli na baba yake.

No comments:

Post a Comment