Monday, August 15, 2011

YANGA KIKAANGONI FIFA.


DAR ES SALAAM, Tanzania
KLABU ya soka ya Yanga imetumiwa barua ya kujileza kutoka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuhusu sakata la aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo John Njoroge.

Barua hiyo imekuja kufuatia mchezaji huyo kuishitaki Yanga FIFA kutokana na kusitisha mkataba wake bila kumlipa malipo yake mpaka leo.

John Njoroge.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile osiah alisema tayari shirikisho hilo limeshaiandikia Yanga barua pamoja na kuambatanisha kopi iliyottumwa na FIFA.

Alisema Yanga inatakiwa kuijibu FIFA sababu za kutomlipa mchezaji huyo na kama haitafanya hivyo hatua kali dhidi yao itachukuliwa na shirikisho hilo la dunia.

No comments:

Post a Comment