Saturday, August 20, 2011
FIFA YARUHUSU ITC YA KAGO.
DAR ES SALAAM, Tanzania
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) limeruhusu Shirikisho la Mpira wa Miguu Jamhuri ya Afrika ya Kati kutoa Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Gervais Anold Kago aliyejiunga na timu ya Simba kutoka Olympic Real de Bangui ya huko.
FIFA imeruhusu ITC itolewe baada ya kubaini kuwa Simba ilituma maombi ya kuomba hati hiyo ndani ya muda uliopangwa, lakini CAR ilishindwa kufanyia kazi. Hivyo kinachosubiriwa sasa ni CAR kutuma ITC hiyo.
Licha ya FIFA kuagiza hivyo, TFF imeitaka Simba kukata jina moja kati ya sita ya wachezaji wa kigeni ilionao katika orodha yake. Kanuni ya Ligi Kuu ya Vodacom inaruhusu timu kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi watano.
Wachezaji wa kigeni ambao Simba ina mikataba yao ni Derrick Walulya, Emmanuel Okwi, Felix Sunzu, Gervais Kago, Patrick Mafisango na Jerry Santo.
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji wakati ikipitia usajili iliagiza kuwa Walulya ambaye Simba ilisema imemuacha ni mchezaji wake kwa vile bado ina mkataba nayo. Hivyo inachotakiwa kufanya Simba ni kuvunja mkataba wa mchezaji mmoja ili kubaki na watano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment