Monday, August 29, 2011

FORLAN ATIMKIA INTER.


MILAN, Italia
Diego Forlan amethibitisha kuwa atajiunga na Inter Milan baada ya muda wake wa kubaki Atletico Madrid kuisha.

Uruguay straiker mwenye umri wa miaka 32 amefanya mkutano na waandishi wa habari na kueleza kwamba hatoendelea kuwepo ndani ya Uwanja wa Vincente Calderon kama mchezaji wa Atletico na sasa anaelekea jijini Milan kuitumikia klabu inayotumia uwanja wa Giuseppe De Maeaza.

Forlan sasa atasafiri kueleka Milan ambapo atafanyiwa vipimo vya afya na baadae kusaini mkataba wa kuitumikia Inter Milan.

“Naenda kujiunga na klabu kubwa na kuna changamoto kubwa mbele yangu.Nataka kumshukuru Massimo Moratti kwa nafasi hii.

“Nimeshaongea na Estaban Cambiasso na Diego Milito, wote ni marafiki zangu.Naifahamu Serie A kwa kuwa nimeshaangalia mechi nyingi kwenye TV na nina furaha kubwa kucheza nchini Italia baada ya Premier League na La Liga.” – Forlan

No comments:

Post a Comment