Tuesday, August 16, 2011

TFF YAUFYATA MKIA KWA SIMBA KUHUSU SUALA LA KAGO.


DAR ES SALAAM, Tanzania
SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF) limeruhusu mchezaji Gervais Arnold Kago kutoka klabu ya Olympic Real de Bangui ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) kuichezea timu ya Simba katika mchezo wa wa ngao ya jamii dhidi ya Yanga unaotarajiwa kupigwa kesho katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za wachezaji, Alex Mgongolwa alisema wamemruhusu mchezaji huyo huswa ikizingatiwa mchezo wa Ngao Jamii sio mchezo wa mashindano ni wakuzindua msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Alisema Simba imeingia mkataba na mchezaji huyo kwa ajili ya kuichezea timu hiyo kwenye ligi kuu na michuano ya kimataifa hivyo mchezaji huyo itabidi apate Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kupitia mfumo wa Transfer Matching System (TMS) ili aweze kushiriki ligi kuu na mashindano ya kimataifa.

Alisema ni ukweli kuwa Simba imeingia mkataba na Kago kama mchezaji wa kulipwa ambaye uhamisho wake ni lazima ufanywe kwa TMS na si ITC ya karatasi ambayo inatumika kwa wachezaji wa ridhaa.



Mgongolwa alisema kwa mujibu wa Ibara ya 2(2) ya Kanuni za Uhamisho wa Wachezaji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), mchezaji wa kulipwa ni yule ambaye ana mkataba wa maandishi na klabu na analipwa kutokana na shughuli ya kucheza mpira.
 
Alisema pia si kweli kuwa CAR hawamo kwenye TMS. Nchi hiyo inatumia mfumo huo wa mtandao na Meneja wao wa TMS ni Elie-Delphin Feidangamo.
 
Alisema kwa mujibu wa annexe 3(5) ya Kanuni hizo za FIFA kuhusu uhamisho wa wachezaji, utumiaji wa mfumo wa TMS kwa uhamisho wa wachezaji wa kiume wa kimataifa ni lazima.

No comments:

Post a Comment