Tuesday, May 29, 2012

MAN UNITED MBIONI KUMNYAKUWA KAGAWA.

KLABU ya Manchester United iko karibuni kumsajili kiungo nyota wa kimataifa wa Japan na klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani, Shinji Kagawa kwa ada ya euro milioni 15. Mkurugenzi wa michezo wa Dortmund Michael Zorc alikiri kuwepo kwa suala la uhamisho wa mchezaji huyo lakini amesema kuwa kuna baadhi ya vitu havijamaliziwa hivyo mchezaji huyo bado ni mali ya klabu hiyo mpaka hapo vitakapokamilika. Mapema mwezi huu kocha wa United Sir Alex Ferguson alisafiri kwenda jijini Berlin kumwangalia Kagawa ambaye alishinda bao moja kwenye mchezo wa fainali ya kombe la ligi la nchi hiyo dhidi ya Bayern Munich ambapo Dortmund walishinda mabao 5-2. Dortmund ilimsajili Kagawa kwa ada ya euro 350,000 akitokea katika klabu ya Cerezo Osaka inayoshiriki Ligi Kuu nchini Japan maarufu kama J-League ambapo amefunga mabao 21 katika michezo 49 aliyocheza msimu huu na kuiwezesha Dortmund kutetea ubingwa wa ligi kuu nchini humo.

No comments:

Post a Comment