Wednesday, May 30, 2012

KIKOSI CHA UJERUMANI KUTEMBELEA KAMBI YA NAZI NCHINI POLAND.

KIKOSI cha timu ya taifa ya Ujerumani pamoja na kocha wao Joachim Loew na nahodha Philipp Lahm wanatarajiwa kutembelea kambi kubwa ya watu wa Nazi waliofariki kipindi cha vita kuu ya pili ya dunia iliyopo katika mji wa Auschwitz nchini Poland kabla ya kuanza kwa michuano ya Ulaya. Zaidi ya watu milioni 1.5 wengi wao wakiwa wayahudi walikufa katika kambi hiyo katika kipindi cha kati ya mwaka 1940 na 1945, wengine kwa kuwekewa hewa ya sumu katika vyumba maalumu, baridi kali, njaa, magonjwa na wengine kutumikishwa kazi ngumu. Mbali na rais wa Shirikisho la Soka Ujerumani-DFB, mwenyekiti wa ligi ya Ujerumani Reinhard Rauball na meneja wa kikosi hicho Oliver Bierhoff katika msafara huo pia watakuwepo wachezaji ambao ni wazaliwa wa Poland ambao ni Miroslav Klose na Lukas Podolski. Ujerumani imepangwa kundi moja na timu za Ureno, Uholanzi na Denmark katika michuano hiyo ambayo imeandaliwa kwa pamoja kati ya Poland na Ukraine itakayoanza kutimua vumbi June 8 mpaka Julai 1 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment